Tuesday, August 22, 2017

YESU ALIKUWEPO KABLA YA KUUMBWA KWA VITU VYOTE DUNIANI NA MBINGUNI



Wakolosai 1:17 “Naye amekuwako kabla ya vitu vyote; na vitu vyote hushikamana katika yeye”.

Yesu Kristo alikuwako kabla ya Ibrahimu kuwako (Yohana 8:52-58).
Watu walioambiwa maneno hayo na Yesu mwenyewe waliokota mawe ili kumpiga Yesu wakisema kuwa anakufuru. Hawa ni watu wa tabia ya mwilini wanaotumia akili kupambanua mambo ya Mungu (mambo ya kiroho huwezi kuyatambua kwa akili maana Mungu ni Roho. (Yohana 4:24).Yohana 17:5,24.Waebrania 7:3.
Yesu ni Alfa na Omega, wakwanza nawa mwisho kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu yeye alikuwako (Ufunuo 22:13).
Shalom
Dr. Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu.

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA TANO)

Image may contain: text


Madhara Yanayosababishwa na Ponografia:
Habari ya kila aina kuhusu ngono inapatikana kwa urahisi kupitia televisheni, sinema, video za muziki, na Internet. Je, ni kweli kwamba habari hizo chungu nzima za ponografia hazina madhara, kama watu wengi wanavyotaka tuamini?*
Jinsi Ponografia Inavyowaathiri Watu Wazima:
Hata watetezi waseme nini, ponografia inaathiri sana maoni ya watu kuhusu ngono na maadili. Watafiti kwenye Hazina ya Taifa ya Utafiti na Uelimishaji wa Jamii walikata kauli kwamba “kutazama ponografia kunaweza kuwafanya watazamaji wafanye ngono potovu.” Ripoti hiyo inasema “imani ya kwamba wanawake husababisha na hufurahia ubakaji, na kwamba wabakaji ni watu wa kawaida imeenea sana miongoni mwa wanaume wenye zoea la kutazama ponografia.”
Watafiti fulani wanasema kwamba kuzoea kutazama ponografia kunaweza kuathiri uwezo wa kufurahia na kufanya ngono katika ndoa. Dakt. Victor Cline, mtaalamu wa kutibu watu wanaotawaliwa na mambo ya ngono, ametambua kwamba watu wanaotazama ponografia huendelea tu bila kuacha. Mtu anayeanza kutazama ponografia kidogo-kidogo, asipoacha mwishowe anaweza kuwa na zoea la kusoma habari na kutazama picha chafu zaidi za ponografia. Cline anadai kwamba zoea hilo linaweza kuongoza kwenye matendo mapotovu ya ngono. Wanasayansi wanaochunguza tabia za wanadamu wanakubaliana na jambo hilo. Dakt. Cline anaripoti kwamba “upotovu wowote wa ngono unaweza kuanza hivyo . . . na kwamba mtu hawezi kuacha hata akisumbuliwa sana na dhamiri.” Hatimaye, huenda mtu anayetazama ponografia akajaribu kufanya mambo yasiyo ya adili aliyoona, na mara nyingi matokeo huwa mabaya.
Tatizo hilo linaweza kuanza hatua kwa hatua bila kutambuliwa, asema Cline. Aongeza: “Huongezeka na kuenea kama kansa. Kwa kawaida zoea hilo halikomi, wala haliwezi kutatuliwa kwa urahisi. Haishangazi kwamba mara nyingi wanaume waliozoea kutazama ponografia hawakubali kwamba wana tatizo, na ni kawaida kwa wenzi wa ndoa kukosana, nyakati nyingine kutalikiana, na hata mahusiano mengine ya karibu huharibika kwa sababu hiyo.”
USIKOSE SEHEMU YA SITA
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi Wetu.

ALLAH ALIPATAJE MABINTI WATATU LAT, UZZA NA MANNAT BILA YA MKE? (SEHEMU YA TATU)

No automatic alt text available.
Mapingamizi Tisa ya Kiislam na Maitikio Yake
Pingamizi la 1 la Waislam: Watu wengine mbali ya hawa kumi na moja hawajaziongelea aya za Shetani. Baadhi ya wanazuoni wa Kiislam ambao hawakundika kuhusu aya za Shetani walkuwa Imam Muslim aliyeandika Sahih Muslim, Abu Dawud, Nas’ai, Ahmad bin Hanbal, and ibn Hisham.
Itikio: Kuna vitu vingi kwenye makusaniko ya Hadithi ambavyo havimo kwenye mikusanyiko mingine. Kwa mfano, Hadithi ndefu za Bukhari hazina mafundisho kuhuu sababu za kutoa zaka, adhabu ya kujilimbikizia vitu, na malaika wawili wanao mtembelea Muislam kila asubuhi kama yanavyopatikana kwenye Sahih Muslim juzuu ya 2 sura ya 371 na.2205, uk.484. Kama mfano wa pili, tunajua kuwa Ibn Hisham aliitumia Bukhari, lakini aliiacha sehemu inayohusu aya za Shetani. Kwenye nakala ya Ibn Hisham ya Ibn Ishaq, alisema aliondoa vitu alivyoona kuwa vibaya. Kama alijisikia aibu sana hata hakuweza kuziweka, huo sio uthibitisho kuwa hazikutokea.
Pingamizi la 2 la Waislam: Aya zinazodaiwa kuwa za Shetani haziendani sawa na sehemu nyingine ya Sura 53.
Itikio: Kumbuka kuwa sehemu ya sasa haikufuatia aya za Shetani, bali ilichukua nafasi zao. Pia nyakati zingine sehemu tofauti za Sura moja zilitolewa nyakati tofauti. Upande mmmoja, al-Wahidi alisema Muhammad alisema hadi maneno ya mwisho. Kwa upande mwingine, hatujui kuwa Sura yote ya Nyota (53) baada ya aya ya 22 iliandikwa wakati mmoja. Aya za 51-53 zinaonekana kuwa hazipo mahali ake kwani zinamongelea Muhammad mwenyewe.
Pingamizi la 3 la Waislam: Sura 53:19-21 inaweza kuwa ilikuwa mapema zaidi kuliko Sura zinazoongelea kunong’ona kwa Shetani.
Itikio: Tabari na ibn Sa’ad wanasema zilifunuliwa wakati mmoja na Sura 17:73-75. Hakuna mtu leo hii anayejua kwa uhakika wakati ambapo aya nyingi za Kurani ziliandikwa. Kwa upande mwingine, hata kama iliandikwa mapema haitaweza kukanusha maneno iliyoyasema. Kama Waislam wasahilina wanaiamini kabisa Kurani, ikiwa ni pamoja na Sura 17:73-75 na 22:52, watatakiwa kuamini kwamba Shetani anaongeza vitu kwenye Kurani. John Gilchrist, kwenye Muhammed and the Religion of Islam uk.120 anasema, "Hoja nyingine ni dhaifu kwa sababu hakuna ushahidi thabiti kuwa sehemu ya kwanza ya Surah 53 inaongelea miraj [kupaa kwa Muhammad] kulikotokea baada ya kuhamia Abyssinia. Kama ilivyokwishaonyeshwa, kuna uhakika wa kiasi kikubwa sana kuwa inaongelea moja ya ziara za mwanzo za Muhammad, ambazo Kurani yenyewe inaonyesha kuwa hazizidi mbili ambazo alizifanya wakati huduma yake ilipoanza. Kwa bahati mbaya inaonekana kuwa hoja zote za Waislam za uhalisi wa vipingamizi vya habari hii ni dhaifu."
Pingamizi la 4 la Waislam: Aya za Shetani zinapingana na mafundisho ya msingi kuwa kuna Mungu mmoja ambayo Muhammad alishikilia kufundisha.
Itikio: Muhammad hajawahi kuthibitishwa kushikilia kitu chochote kile. Kumbuka, Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 10 na.490, uk.317; juzuu ya 4 kitabu cha 53 sura ya 38 kabla ya na.400, uk.266; juzuu ya 8 kitabu cha 53 sura ya 38 na.400, uk.267 inarekodi kuwa Muhammad alikuwa amerogwa na mwovu kwa kipindi fulani. Isitoshe waandishi wa maisha yake na watu wengine waliorekodi jambo hili walikuwa bado Waislam, kwa hiyo wana historia hawa wanathibitisha kuwa kulikuwa na watu kadhaa ambao walikuwa tayari kumfuata Muhammad hata kama alisema uongo.
Pingamizi la 5 la Waislam: Vifungu vingi kwenye Kurani vinasema Muhammad hakuweza kusema maneno yoyote yasiyokuwa kweli, na kwa ajili hiyo jambo hili haliendani na tafsiri kuwa Shetani anaingilia mambo. Kwa mfano,
Sura 10:15b: "Sema; Si kwa ajili yangu, kwa hiari yangu, kubadilisha hili: Sifuati kitu chochote isipokuwa kile kilichofunuliwa kwangu…"
Sura 41:42: "Hakuna uongo unaoweza kulikaribia kutokea mbele au nyuma yake: Limetumwa na Yeye Aliyejaa Hekima na Mwenye Kustahili Sifa zote."
Sura 15:9: "Tumeutuma, bila shaka, Ujumbe; na tutaulinda kwa hakika (dhidi ya uharibifu)."
Sura 60:44-46: "Kama (Mjumbe) angetunga neno lolote kwa jina letu, Tungemkamata kwa mkono wa kulia na kisha tungeikata ateri ya moyo wake"
Itikio: Kwa upande mmoja, inadaiwa kuwa Shetani, siyo Muhammad, alitunga aya za Shetani, na kulindwa kwa Kurani haukanushi kuingia kwa mafundhisho ya uongo na Mungu kuyarekebisha. Kwa upande mwingine, kama Muislam anatafsiri aya hizi kuwa zinafundisha kwamba hakuna kitu cha uongo kitakachoweza kuingia ujumbe wa nabii, hata kama aya za Shetani hazitahusishwa, jambo hili litakuwa kinyume na kunong’oneza kwa Shetani ambako kumeelezwa kwenye Kurani.
USIKOSE SEHEMU YA NNE
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

SIRI YA KUJIBIWA MAOMBI

Image may contain: one or more people, ocean, sky, cloud, text, outdoor, water and nature
Yohana 15: 7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
Tukitaka kuona matokeo makubwa zaidi ya maombi yetu, hatuna budi kukaa ndani ya Kristo, yaani kuokolewa na kuwa viumbe vipya (2 WAKORINTHO 5:17). Siyo hilo tu, maneno yake hayana budi kukaa ndani yetu kwa WINGI (WAKOLOSAI 3:16). Neno la Mungu litatuwezesha kuifahamu KWELI yenye uwezo wa kutuweka huru mbali na uongo wa Shetani.
Shalom,
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

UISLAM NI DINI YA KUTUNGA NA HAIKUWEPO KABLA YA MUHAMMAD




Hakuna mwanadamu ye yote kabla ya ujio wa Muhammad, ambaye aliwahi kuwa Muislamu, wala aliyewahi kuujua Uislamu, kama kuna Muislamu ambaye anaweza kunithibitishia kuwa, kuna mtu aliyewahi kuwa Muislamu, kabla ya Quran kuwepo, basi nitasilimu na kuwa Muislam:-
Angalizo :- Unapotoa ushahidi usitumie Quran, wala kitabu cho chote ambacho kimepatikana baada ya kuja Muhammad, bali nahitaji ushahidi katika vitabu vilivyokuwepo kabla ya Muhammad kuja na Quran, na usichukue matukio ambayo Muhammad ameyaiga kutoka kwa watu wa zamani, kama
a) Kutawadha. 
b) kusujudu 
c) Kuvaa kanzu
d) Nk.
Na kusema huo ndo uislamu, bali ukisema hivyo, basi uambatanishe na ushahidi kimaandiko, kutoka kwenye vitabu nje ya Quran, iliyokuja mwaka 610 baada ya Kristo, maandiko yasemavyo kuwa kusujudu, kuvaa kanzu, kutawadha ni uislamu, yakipatikana basi leo hii nitasilimu na kuwa muislamu!
ZINGATIA :- kama hautapata ushahidi wa uwepo uislamu au neno Uislamu (الإسلام) kwenye vitabu vilivyokuwepo kabla ya Quran, basi tambua kuwa umeongopewa kuwa, Uislamu upo tangu zamani za Adamu, maana haiwezekani, watu kama,
Adamu
Habil
Nuhu 
Ibrahimu 
Lutu 
Sara 
Ishamael - Ismail
Isaka - Is-haqa
Yakobo Yaqubu 
Yusufu
Yunusi -Yona
Musa 
Haruni 
Daudi 
Suleiman 
Eliya - Ilyasa 
Zakaria 
Yahya - Yohana
Yesu,
Wasijitambue kuwa wao walikuwa waislamu, mpaka waje kusemewa na Muhammad, mwaka wa 610. Zinduka, ujue kuwa Uislam ni dini bandia na haukuwepo kabla ya Muhammad.
#courtesy of aliyekuwa Ustadh Abel Suleiman Shiliwa ambaye sasa ni Mtumishi wa BWANA Yesu.
For Max Shimba Ministries Org

PASIPO YESU SISI HATUWEZI KUFANYA NENO LOLOTE

Image may contain: one or more people and text
Yohana 15: 4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
Ni muhimu wakati wote kukumbuka kwamba utoshelevu wetu watoka kwa Yesu (2 WAKORINTHO 3:5). Sisi ni matawi. Matawi yasipopata chakula na maji kutoka kwenye mizizi, hunyauka na kufa. Uwezo wetu wa kufanya neno lolote, unatoka kwa Yesu aliye mizizi. Bila yeye hatuwezi kufanya neno lolote. Hapa neno halisemi bila Yeye hatuwezi kufanya NENO LOLOTE KUBWA, kama kufufua watu, kuponya walio na Ukimwi n.k., neno linasema hatuwezi kufanya neno lolote hata lililo dogo. Katika yote, WAKATI WOTE, hatuna budi kuitumainia NEEMA ya Mungu na kamwe tusijitumainie wenyewe HATUWEZI! (2 WAKORINTHO 1:8-9; 12:9).
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

MUHAMMAD ALIPAGAWA NA KUWEWESEKA BAADA YA KUONA KUPATWA KWA JUA

No automatic alt text available.
Sahih Bukhar Volume II Kitabu namba 18 Namba 167. Nabii Muhammad alipagawa na kuweweseka baada ya kuona kupatwa kwa jua. Muhammad alifikiria kuwa kiyama kimefika na ameachwa na Allah. ALikimbia mpka msikitini na kuomba msamaha kwa Allah mara mia moja.
Eti huyu ndio alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, THUBUTU.
Ndio maana Muhammad aliukana utume wake:
SOMA HAPA:
MUHAMAMD ANAOMBWA AFANYE MIUJIZA ILI KUTHIBITISHA UTUME WAKE:
Surat Al Israai 90. Na walisema: Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchem katika ardhi hii
MUHAMMAD ANAJIBU KUWA YEYE SI CHOCHOTE YULE
Surat Al Israal 93. Au uwe na nyumba ya dhahabu, au upae mbinguni. Wala hatutaamini kupaa kwako mpaka ututeremshie kitabu tukisome. Sema: Subhana Rabbi, Ametakasika Mola wangu Mlezi! Kwani mimi ni nani isipo kuwa ni mwanaadamu na mtumwa tu?
Muhammad hakuwai fanya muuiza wowote ule, hakuponya watu, hakufufua wafu, hakutoa majini zaidi ya kuwaingiza watu majini. Muhammad alikuwa dhaifu.
Kama Muhammad alifikiria kuwa, kupatwa kwa jua ni KIYAMA, kwanini tumfuate mtu wa namna hii aliye ogopa kuachwa na Allah siku ya kiyama?
Kumbe Muhammad hakuwa na uhakika kwa kwenda Akhera.
Qur’an 46;9 (Surat Al-Ahqaf) Sema; mimi si kiroja (mpya) katika mitume wala sijui nitakavyofanywa, wala mtakavyofanywa ninyi, sifuati yaliyofunuliwa kwangu, sikuwa mie lolote, ila ni muonyaji tu ninayedhihirisha.
Eti tuufuate Uislamu chini ya kiongozi Muhammad ambaye hajui hatima yake kama ataenda peponi, au ataenda motoni, bila shaka kwa Mkristo anayejitambua hawezi kuwa Muislamu.
Hakika Muhammad alikuwa Mtume Bandia na Allah ni Mpinga Mungu.
Karibuni kwa Yesu aliye hai,
Shalom,
Max Shimba ntumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA SITA)

Image may contain: one or more people and text
Jinsi Vijana wanavyoathiriwa na picha za utupu:
Takwimu zinaonyesha kwamba watazamaji wengi wa ponografia ni wavulana wenye umri wa kati ya miaka 12 na 17. Kwa kweli, wengi wao hujifunza masuala ya ngono hasa kupitia ponografia. Hilo lina matokeo mabaya sana. Ripoti moja yasema kwamba “ponografia hazionyeshi kamwe mimba za matineja na magonjwa yanayoambukizwa kingono kama UKIMWI, na hilo hutokeza wazo la uwongo la kwamba mambo yanayoonyeshwa katika ponografia hayana madhara.”
Watafiti fulani husema kwamba kutazama ponografia kunaweza pia kuathiri ukuzi wa kawaida wa ubongo wa mtoto. Dakt. Judith Reisman, mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Vyombo vya Habari, akata kauli: “Uchunguzi wa athari za sauti na picha za ponografia katika utendaji wa kawaida wa ubongo unaonyesha kwamba kutazama ponografia huathiri kabisa uwezo wa kawaida wa kufikiri. Pia hudhuru ubongo wa watoto unaoathiriwa kwa urahisi kwa sababu hufanya wasione mambo kihalisi na hudhuru afya yao ya kiakili na ya kimwili, na huwazuia kupata furaha.”
Jinsi Mahusiano yanavyoathiriwa na unagaliaji wa ponografia:
Ponografia huathiri mitazamo na tabia. Ujumbe wake unavutia hasa kwa sababu si halisi na hivyo unaifanya ionekane kuwa yenye kusisimua zaidi kuliko mambo halisi. (Ona sanduku “Utakubali Ujumbe Gani?”) “Watu wanaotazama ponografia hutarajia mambo yasiyo halisi ambayo huharibu mahusiano,” yasema ripoti moja.
Ponografia inaweza kuwafanya wenzi wa ndoa wakose kuwa wanyofu na wakose kuaminiana, sifa ambazo ni muhimu katika ndoa. Kwa sababu ponografia hutazamwa hasa faraghani, mara nyingi humfanya mtu atumie hila na uwongo. Wenzi wa ndoa huhisi kwamba wamesalitiwa. Hawaelewi kwa nini mwenzi wao havutiwi nao tena.
USIKOSE SEHEMU YA SABA
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

ALLAH ALIPATAJE MABINTI WATATU LAT, UZZA NA MANNAT BILA YA MKE? (SEHEMU YA NNE)

No automatic alt text available.
Pia, hii si mara pekee aya ya Kurani "inapotea kabisa" kwa sababu ilibatilishwa. Sahih Muslim juzuu ya 1 sura ya 244 na.1433, uk.329-330 ni Hadithi muhimu kwa sababu inaonyesha kuwa aya ilibatilishwa, bali baada ya kubatilishwa ilipotea kabisa. Hivyo ama:
a) Kurani kwenye mbao zenye maandishi [mbinguni] ilikuwa na toleo la awali, na toleo lililofuata lilitofautiana na mbao hizo. Kurani ya leo inatofautiana na mbao zenye maandishi za mbinguni.
b) Kurani kwenye mbao zenye maandishi za mbinguni zina toleo la baadaye, na toleo la awali linatofautiana nalo. Kwa hiyo maneno ya kwanza yalitolewa kama kiwakilishi cha mbao zenye maandishi za mbinguni wakati ukweli ni kwamba ilikuwa ni uongo.
Kipi ni kipi? Mbao za maandishi [mbinguni] kwenye Sura 85:20-22 hazidhaniwi kutengenezwa kwa puti ya kipumbavu.
Pingamizi la 6 la Waislam: Tabari anawezakuwa hakukusanya habari kiuhakiki.
Itikio: Ingawa hatuna ushahidi wa mada haya, waandishi wengine watatu wa maisha [ya Muhammad] pia waliandika jambo hili. Wawili kati yao waliandika kabla ya Tabari, kwa hiyo hata kama Tabari alionekana kutokuwa mhakiki, jambo hilo haliwezi kuathiri kitu chochote kwa kiasi kukubwa kwani bado tuna watu wengine watatu. Muislam anaweza kupenda kuona kuwa waandishi wote wa maisha ya Muhammad wanaonekana kuwa na dosari sana, lakini vyanzo mbalimbali vinaonyesha usahihi wao.
Pamoja na hayo, Tabari hakupokea vitu vyote bila kuvihakiki. Kwa mfano, kwenye juzuu ya 1, uk.532 anasimulia tamaduni nyingi za kiislam za Adam na Hawa alizojifunza kutoka kwa watu wenye Torati. Anazinukuu nyingi zake lakini anasema kuwa ana mashaka na uhakika wa hizi Hadithi. (Kutoka kwenye kitabu cha Barbara Freye Stowasser kiitwacho Woman in the Qur’an, Tradition, and Their Interpretation uk.28).
Pingamizi la 7 la Waislam wa Madhehebu ya Suni: Hadithi zenye uhakika hazilisemi jambo hili moja kwa moja.
Itikio: Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 19 sura ya 42 na.173, uk.100; juzuu ya 3 kitabu cha 19 sura ya 43 na.176, uk.101; juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 286-287 na.385-386, uk.364-365; Abu Dawud juzuu ya 1 kitabu cha 2 sura ya 481 na.1401, uk.369 zinaeleza hali waliokuwa nayo watu wa Maka walipokuwa wanasujudu waliposikia Sura 53. Ni vigumu kueleza tofauti kitu kilichokuwepo kuhusiana na sura hii kilichowafanya wapagani wasujudu kwa ajili ya sura hii, ikiwa hawakusujudu kwa ajili ya kitu kingine. Kurani yenyewe pia inasema kuhusu "kunong’oneza" kwa Shetani.
Pingamizi la 8 la Waislam wa madhehebu ya Suni: Shaykh al-Albani, kwenye vitabu vyake vinavyohusu mtiririko wa waenezaji wa tamaduni, alisema ushahidi wa aya za Shetani una mlolongo mbaya wa ueneaji (isnad).
Itikio: http://answering-islam.org/Responses/ Saifullah/sverses.htm inasema, "Kuhusu al-Albani, nimefahamishwa kuwa siku hizi al-Albani ameelezwa vibaya sana kwa kutokuwa sahihi kuhusu isnads, hata anaandika kwenye kitabu kimoja kuwa mtu fulani ni mkweli lakini kwenye kingine anasema kwamba jambo hilo si sahihi! Kitabu kiitwacho Al-Albani Unveiled kilichoandikwa na Sayf ad-Din Ahmed Ibn Muhammad Amirul Islam kinatoa mifano mingi sana. Upande wa nyuma unasema: Kitabu hiki ni uchunguzi mchanganifu wa mmoja wa mashehe muhimu zaidi wa Hadithi(Muhammad Nasiruddeen al-Albani) wa harakati ya kisasa ya kiislam inayojulikana kama ‘Salafiya’. Mtunzi ameeleza wazi kabisa kupingana kwa Al-Albani kwa kutumia msaada wa kazi iliyoandikwa kwanza kwa Kiarabu (Tanaqadat al-Albani al-Wadihat), na mwanazuoni wa wa Hadithi wa Kijordani anayejulikana sana - Shakh Hasan ibn Ali al-Saqqaf."
Pingamizi la 9 la Waislam: Watu wasio Waislam wanampinga Muhammad na uislam.
Itikio: Tukio hili halikuundwa na watu wasiokuwa Waislam, bali liliandikwa na Waislam wenyewe. Waislam hawa wasahilina walikuwa na vyanzo vya zamani zaidi kuliko Waislam wa sasa. Kulifumbia macho jambo linalokosoa mtazamo wako kwa sababu tu linakosoa maoni yako, hakuendani na kuufuata ukweli. Kwa kuwa Wakristo wanadai kufundisha ukweli, tunao wajibu wa kumtaja nabii wa uongo. Hatufanyi hivi kwa sababu ya chuki au matakwa binafsi, bali kwa sababu ya upendo na haja ya kuwaona Waislam wanaepukana na mafundisho ya uongo, na kumgeukia Yesu wa kweli na kuwa nasi mbinguni pamoja na Mungu wa kweli.
Unakwenda wapi kutoka hapa?
Waislam wenyewe hawajakubaliana endapo maneno ya Shetani yalikuwemo kwenye Kurani mwanzoni.
Chaguo la 1: Itakuwa vipi endapo Muhammad aliongea kama nabii kuhusu maombezi ya mabinti wa Allah? Jambo hili litamfanya Muhammad kuwa nabii wa uongo kwa kipindi fulani.
Chaguo la 2: Itakuwa vipi endapo Muhammad hakuwahi kusema aya za Shetani? Waandishi wote wanne wa maisha ya Muhammad watakuwa wamekubaliana kukosea kuwa Muhammad alikuwa nabii wa uongo. Baadhi ya watu watachagua, kwa hiari yao wenyewe, kufuata kitu hata kama wanaamini kuwa kiongozi wao aliongea mambo ya Shetani. Hata kama jambo hili ni kweli, utafanya nini na aya za Kurani zinazohusu minong’ono ya Shetani ambayo Muhammad aliipata?
Kwa vyovyote vile, uislam unafundisha kuwa Allah anaruhusu maneno yake yabadilishwe kiasi kikubwa sana, na Allah anaruhusu wafuasi wake wazuri wajifunze njia za uongo kama njia ya ukweli. Hii ni kwa sababu Kurani kwenye Sura 43:44-45, inaonyesha kuwa manabii wote waliotangulia walikuwa na ujumbe mmoja. Sura 41:43 inasema kwamba hakuna kitu kilichotumwa kwa Muhammad ambacho hakikuwahi kutumwa kwa manabii waliomtangulia pia. Kwa hiyo kwa Waislam, ama
a) Allah aliruhusu ujumbe wake uliopotoshwa hapo awali,
b) Au, Kurani ndio ujumbe uliopotoka.
Kwa vyovyote vile, uislam unasema, Allah hawezi kutumainiwa kulitunza neno lake dhidi ya mabadiliko makubwa ya mafundisho.
Mwamini Mungu
Mungu Mwenye nguvu anao uwezo wa kuutunza ujumbe wake. Watu wanatakiwa kumwamini Mungu zaidi.
Mwamini Mungu kuwa amelitunza neno lake. Sura 5:46-48 inasema kwamba Yesu aliithibitisha Torati (kwa wakati wake), Mungu alituma Maandiko kwa Wayahudi na Wakristo, na hata wakati wa uhai wa Muhammad wangeweza kuupima ukweli kwa kuyatumia [Maandiko]. Sura 3:48 na 5:110-111 zinamwonyesha Yesu kuwa alikuwa na Torati na Injili. Wanafunzi wa Yesu pia walikuwa wamevuviwa. Kwenye Biblia, Isaya 59:21; 40:8; Zab. 119:89 zinaonyesha kuwa neno la Mungu hudumu milele. Neno lake halikuwa na kosa lolote hapo awali, na limetunzwa bila makosa (bila makosa makubwa) hadi leo hii. (Isa. 55:11; 1 Petro 1:23-25; Zaburi 119:89, 91, 144, 160).
Tumaini kuwa Mungu anataka uufuate ukweli na uje kwake. Mungu hataki mtu yoyote aangamie (Ezekiel 18:23, 32; 2 Petro 3:9). Watu wote wanatakiwa kuiamini Injili ya Yesu Kristo kwenye 2 Wathesalonike 1:8.
Usimtumaini mwanadamu ambaye maisha yake yana ukomo. Usiwatumaini watu wengine ambao wanakugeuzia mbali na Mungu. "Usiwe mwenye hekima machoni pako (Mithali 3:7). Badala yake, "Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako" (Mithali 3:5-6). Je unaamini kuwa Mungu anaweza kunyoosha njia zako kama ukimkiri?
Mtumaini Yesu; Yeye ametoka kwa Mungu na ujumbe wa Mungu umetunzwa. Yesu si mwizi wala mnyang’anyi (Yohana 10:8-10). Amini kuwa Yesu alitoa uhai wake kama fidia ya ukombozi (Mathayo 20:28), ili iwe sadaka ya dhambi (Warumi 8:3), kwa njia ya damu yake aliyoimwaga msalabani (Waeb. 10:19).
Mwamini Bwana Yesu nawe utaokolewa (Matendo 16:31). "… ‘Kila amwaminiye hatatahayarika’" (Warumi 10:11). Kwa hiyo mtumaini Mungu, na amini kuwa anaongoza kwa uaminifu. Hakuacha neno lake lipotoshwe, kwa hiyo Biblia inaaminika. Mpe Yesu maisha yako, na atakupa amani na furaha.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

JE, UNAYO NEEMA YA YESU KRISTO, MUNGU MKUU?

Image may contain: food
Nini basi maana ya neema? Watu wengi wamekuwa wakiimba ,”Neema, neema imefunuliwa” na kukariri na kuisema Neema ya Bwana (2 WAKORINTHO 13:14) kama Kasuku huku hawajui wayasemayo. Nini basi maana ya neema?
Neema, ni upendeleo wa kuchaguliwa, bila kustahili kutokana na matendo yoyote aliyoyafanya mtu au sifa aliyonayo mtu.
Neema pia, ni uwezo wa kushinda katika tabia na utumishi wa Mungu sawasawa na mapenzi yake, tunaopewa na Mungu bila gharama yoyote au nguvuzetu au kufanyia kazi yoyote.
1. Upendeleo wa kuchaguliwa bila kustahili- Kutokana na matendo yake, hakuna mwanadamu yeyote mwenye haki mbele za Mungu (WARUMI 3:20). Tangu kabisa amekuwa akimhuzunisha Mungu (MWANZO 6:5-7). Wakati wa Nuhu, watu waliangamizwa kwa Gharika. Wakati wa Musa, Mungu alitaka pia kufuta kabisa kizazi cha Wausraeli na kubaki na Musa tu kama siyo maombi ya Musa (HESABU 14:11-20). Wakati wote, wanadamu wote wamepotoka na kuoza (WARUMI 3:12). Ni Yesu peke yake tu ambaye siku zote alifanya yanayompendeza Mungu (YOHANA8:29).Alijaribiwa sawasawa na sisi lakini hakutenda dhambi (WAEBRANIA 4:14-15). Yesu huyu anayempendeza Mungu ndiye aliyekufa msalabani na Baraba aliyekuwa mhalifu mkubwa akafunguliwa. Kama Baraba alivyofunguliwa pamoja na ukosaji wake, kila mwanadamu amefunguliwa, akiamini tu. Mbele za Mungu kila mtu amepimwa na kuonekana amepungua (DANIELI 5:27). Sasa kwa kuamini tu kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu pale msalabani, sisi tunaokolewa. Watu wengi hawaokolewi kwa sababu hawajui tunaokolewa kwa neema tu kwa njia ya imani peke yake (WAEFESO 2:5). Kazi aliyoifanya Yesu msalabani imetupa kuirithi mbingu aliyokwenda bila sisi kuifanya. Ni kama ambavyo bondia anavyopigana ulingoni kwa shida kubwa na kasha akishinda na kupewa mamilioni ya fedha, mke wake aliyebaki nyumbani bila kupigana naye atakuwa milionea. Hii ndiyo neema.
2. Uwezo wa kushinda bila kutumia nguvu zetu- Neema ni uwezo wa kushinda dhambi na kumtumikia Mungu apendavyo. Neema ndiyo inayotufundisha (inayotuwezesha) kukataa ubaya na tama za kidunia na kuishi kwa kiasi na haki na utakatifu (TITO 2:11-12; WAGALATIA 2:8). Maisha ya wokovu siyo ya kutumia nguvu zetu au kujitahidi. Uweza wa Mungu unatimilika kwetu katika udhaifu wetu yaani kutokuweza kwetu. Hatupaswi kujitumainia wenyewe katika kufanya lolote (2 WAKORINTHO 1:8-9).
Shalom,
Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

Why is the wife of Adam not mentioned by name in the Quran?

Why is the wife of Adam not mentioned by name in the Quran? Provocative Questions on Adam’s Wife and the Quran’s Omissions Why does the Qura...

TRENDING NOW