Sunday, September 10, 2017

WAKRISTO WA KWANZA WALIKUTANA JUMAPILI NA SIO SABATO DHAIFU

No automatic alt text available.
Ni siku gani ya Sabato, Jumamosi au Jumapili? Je, Wakristo wastahili kuitunza hii siku?
Sabato (kwa Kiebrania: שבת, shabbāt, yaani pumziko kwa Kiswahili) ni siku ya pumziko ya kila juma katika Uyahudi kwa ujumla na hasa katika nchi ya Israeli.
Kumekuwa na maswali mengi sana kutoka imani tofauti kuhusu hii siku ya Jumamosi. Wafuasi wa dini na imani zote wanao fuata Torati wanajiuliza kuhusu Sabato, je, Mwenyezi Mungu anaikubali Jumamosi tu kama siku ya ibada? Katika Agano Jipya, tunajifunza kuwa siku ya Jumapili inaitwa siku ya kwanza ya juma na walio amini walikusanyika katika siku hii ya Jumapili. Matendo 20: 7 Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.
Siku ya kwanza ya juma ni Jumapili na hii ni siku ambayo walio mwamini Yesu walikusanyika na kuabudu. Huu ni ushaidi wa kuonekana kwa macho ambao Wakristo wanaabudu Jumapili tokea Karne ya kwanza.
“Hata sabato ilipokwisha, kupambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.” (Mathayo 28:1). “Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma…”. (Marko 16:9).
Bwana Yesu alifufuka kutoka wafu katika siku ya kwanza ya Juma. Zaidi ya hapo, tumesoma nyaraka za Mtume Paulo zikionyesha kuwa kuwa Wakristo wa kwanza walikuwa walikusanyika siku ya kwanza ya Juma, yaani Jumapili. “Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kuumega mkate, Paulo akawahutubu…” (Matendo 20:7). “Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja…” (1 Wakor.16:2).
Zaidi ya hapo, hatusomi na wala hakuna amrisho ndani ya Agano Jipya kuhusu wauminia yaani Wakristo ni lazima wakutane kwenye hii siku ya kwanza ya Juma, “Jumapili”, lakini tunao mfano wa siku ambayo Wakristo wa kwanza “Kanisa la Kwanza wakati wa Pentekoste”, na utamaduni huo wa kuabudu Jumapili unaendelea mpaka sasa. Zaidi ya hapo, ukisoma Agano Jipya kwa umakini utaona kuwa WAKRISTO WA KWANZA HAWAKUKUSANYIKA SIKU YA SABATO, nikimaanisha kuwa, hakuna aya ambayo inasema moja kwa moja kuwa Wakristo walikusanyika siku ya Sabato au kulikuwa na utamaduni au desturi au mila au sheria inayo walazimisha kukutana siku ya Sabato.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

SINAGOGI SIO MSIKITI SEHEMU YA PILI

Image may contain: outdoor and text
TUNAZIDI KUCHAMBUA HOJA ZA MIHADHARA ya Kiislamu
LEO TUANGALIE SINAGOGI!!
Kama tulivyosema Neno SInagogi linatokana na Kigiriki συναγωγή sinagoge likimaanisha "mkutano"; ni tafsiri ya Kiebrania בית כנסת beit knesset yaani "nyumba ya mkutano".
Wayahudi hutumia pia neno la Kiyiddish "shul" (=shule) kutajia sinagogi.
Katika lugha ya kiebrania neno “ beit ” linamaana “ nyumba” ndio maana hata ukisoma bethsaida “ Nyumba ya mvuvi” au bethsania-Nyumba ya masikini. Bethlehemu, nyumba ya mkate. (Soma injili imetajwa sana majina haya )
Katika Israeli ya Kale (kabla ya maangamizi ya Yerusalemu mwaka 587 KK) inaonekana hakukuwa na Sinagogi: walau halitajwi kabisa katika Agano la Kale.
Inaonekana ya kwamba masinagogi yalianzishwa baada ya hekalu ya Yerusalemu kubomolewa pamoja na kuanza uhamisho wa Wayahudi kwenda nchi mbalimbali.
Tangu kuharibiwa kwa Hekalu la Pili mwaka 70 Wayahudi wana masinagogi tu kufanyia ibada.
Neno hilo limetumiwa katika maana hiyo ya mukutano kwenye Septuajinti, yaani, tafsiri ya Kigiriki ya Maandiko ya Kiebrania. Lakini, baada ya muda neno hilo lilitumiwa kurejelea jengo ambapo watu walikutana kuabudu. Kufikia karne ya kwanza W.K., karibu kila mji ambao Yesu alitembelea ulikuwa na Sinagogi; majiji yalikuwa na masinagogi kadhaa; jiji la Yerusalemu lilikuwa na masinagogi mengi.
Ukumbi wa sala huwa na sehemu zifuatazo:
• sanduku la Torati ni kabati au sanduku ambako hati za kuviringisha zenye mwandiko wa Biblia ya Kiebrania hutunzwa;
• taa inayoendelea kuwaka muda wote;
• meza ya msomaji ambako hati za torati hufunguliwa na kusomwa;
• mimbari ya mafundisho;
• kinara cha menorah chenye mishumaa 7 au 9.
Karibu na sanduku hilo, kulikuwa na viti vya mbele vilivyopangwa kuelekea kutaniko, navyo vilikaliwa na maofisa-wasimamizi wa Sinagogi pamoja na wageni wowote waheshimiwa. (Mathayo 23:5, 6)
Hii ni tofauti ni Misikiti ya kiislamu isiyokuwa na Viti karibu na eneo la katikati la sinagogi palikuwa na jukwaa lililokuwa na kinara na kiti cha msemaji . Kwenye upande wa mbele, wa kushoto, na wa kulia wa jukwaa hilo, kulikuwa na viti vya washiriki wa kutaniko .
• Kwa kawaida, gharama za kuendesha shughuli za sinagogi zililipiwa na kutaniko. Michango ya hiari iliyotolewa na wote, matajiri kwa maskini, ilitumiwa kurekebisha na kudumisha jengo hilo
Bwana Yesu alipenda sana kufundisha kwenye hekalu na katika masinagogi walimokusanyika wayahudi.
“Sikuzote nilifundisha katika sinagogi na katika hekalu, ambapo Wayahudi wote hukusanyika.”—Yohana 18:20.
Hekalu katika Jerusalemu ( hekalu katika Uyahudi )
Kulikuwa na mahekalu mawili yaliyojengwa katika nyakati tofauti tofauti na watu tofauti tofauti ndani ya Yerusalemu.
Hekalu la kwanza lilijengwa na mtoto wa mfalme Daudi,Mfalme Suleimani. Lilijengwa mnamo mwaka 957 KK.
Hekalu hili likabomolewa na mfalme Nebukadreza II mnamo 586 KK.
Hekalu la pili,
Lilijengwa 536 KK -515KK baada ya uhamisho wa Babeli.
Uhamisho wa Babeli ni kipindi ambacho Wayahudi walilazimishwa kuishi Babuloni. ( kwa lugha nyingine ni kwamba Wayahudi walilazimishwa kuishi Babeli,ambayo kwa sasa tunaweza kusema walipelekwa Iraq,sababu magofu ya Babeli yapo katika mji wa kisasa wa Al-Hillah,kando ya mto flati kama 90km kusini mwa Baghdadi)
Hekalu hili la pili linajulikana pia kwa jina la hekalu la Herode mkuu kwa sababu herode alihusika pia katika upanuzi,na kuliwekea nakshi katika Hekalu hili. Wataalamu wa mambo ya kale wanasema kwamba liliwekewa wakfu na Yuda Mmakabayo.
Hekalu hili la pili likabomolewa na Warumi mwaka wa 70. Tangu hapo halikujengwa hekalu la tatu,bali Wayahudi waliendelea kukusanyika katika mikutano yaani sinagogi na sio katika hekalu tena mpaka leo hii.
Tangu hapo halijajengwa tena, hivi kwamba sadaka zinazodaiwa na Torati hadi sasa haziwezi kutolewa kwa muda wa miaka 2000 hivi.
TOFAUTI KATI YA HEKALU NA SINAGOGI NI KAMA IFUATAVYO.
~ Hekalu huwa ni jengo kubwa lenye sehemu mbali mbali za ibada,wakati sinagogi huwa ni mkutano tu wa watu katika jengo lisilokuwa na mgawanyo mkubwa.
~ Hekalu lina sehemu ya patakatifu pa patakatifu,sinagogi halina sehemu hiyo.
~Hekalu lilikuwa kuanzia agano la kale mpaka agano jipya mfano kuanzia kitabu cha 1 Samweli 1:9,mpaka Ufunuo 21:22- Wakati Sinagogi lenyewe halitajwi katika agano la kale bali agano jipya tu.
Swali:
MBONA BIBLIA INASEMA KUWA SINAGOGI NI MSIKITI WA WAYAHUDI?
UFAHAMU
Katika tafsiri ya Biblia Union Version yapo maneno kadha wa kadha yenye asili ya lugha ya Kiarabu na Kiswahili cha kimvita hii ina tokana na mfasili(Mmisionary) wa kwanza aliye tafsiri biblia kumshirikisha mzee (Shekhe) ili aweze kusaidiana naye katika kazi hiyo iliyo onekana kuwa ngumu kwake kutokana na kutojua vizuri Kiswahili hivyo ndiyo maana utakuta maneno mengi yenye asili ya Kiarabu ndani ya Biblia (Tazama Mifano). Mashekhe kwa maana ya wazee, Kadhi kwa maana ya hakimu, Iddi kwa maana ya Sikukuu, kutawadha kwa maana ya kunawa miguu na kadhalika
Pamoja na hayo alipo tafsiri neno hili Sinagogi kuwa ni msikiti haku tafsiri kwa kuzingatia utalaamu wa lugha bali alifananisha mambo Fulani Fulani yanayo tendeka katika majengo hayo mawili yaani Sinagogi na Msikiti na ndipo akafasiri kuwa Sinagogi ni Msikiti wa Wayahudi kwa kulinganisha baadhi ya matendo yanayo fanana baina ya majengo hayo mawili.
Ni sawasawa na leo mtu kumwambia babu yake kuwa Computer ni Runinga ya kisasa wala kamwe hana maana ya Computer ni TV ila amechukua anachokifahamu mhusika ili kumweleza kitu au jambo Fulani. Hivi na sawa na mjaluo wa ugenya kusilimu kisha akirudi huku nyarigunga kavaa kanzu yake akiulizwa vipi kulikoni? Anasema “Siku hizi mimi naenda ile kanisa ya Waislamu” .
Hieleweke pia lugha yeyote ile iliyohai uzidi kuimalika . Ndivyo ilivyo na Kiswahili pia. mathalani leo tunayo maneno mengi yamezalishwa ambayo kimsingi miaka michache hayakuwepo kwenye kiswahili
Aina ya tafsiri iliyotumika kitaaluma
Kwa kadri ya taaluma ya Kiutafsiri mtafsiri huyo wa Biblia ametumia moja kati ya aina kuu mbili za kiutafsiri ambapo aina ya kwanza ni ile ya tafsiri “Shabihifu” na ya pili ni tafsiri “Maanifu”.
Hivyo kimsingi katika kutoa maana hiyo ya Sinagogi- Msikiti wa Wayahudi. msaidizi huyu katika utafsiri wa Biblia alionekana kukosa namna ya kulieleza neno hilo sinagogi na ndipo akaadhimu kutoa tafsiri hiyo ambayo kitaaluma siyo tafsiri “Maanifu” (haiendani na asili ya neno katika lugha husika) bali alitumia tafsiri “Shabihifu” inayozingatia mambo machache yanayofanana baina ya vitu viwili ndiyo maana alisema ni Msikiti wa Wayahudi hivyo kamwe hakusema kuwa ni Msikiti wa Waislam maana alitambua kuwa katika wakati huo bado uislam haukuwa umeanzishwa.
Lakini pia nimeelezea kuwa mtu anaweza akamwelezea mzazi wake kuhusu kumputa kuwa ni Runinga ya siku hizi, hii aina maana kuwa computer ni TV ila unafananisha anachokijua mhusika ili japo kumweleza.
Hivyo basi kwa kuwa wenyeji wa pwani walikuwa wana ufahamu wa misikiti, basi mfasiri akaamua kutumia kauli hii.
Ebu fikiria kwa Kiswahili mara nyingi huwa twafasiri neno Pharmacy kwa maana ya Duka la dawa!!! Lakini je ni sawa?
HEBU SASA TUANGALIE MAANA NA MAJINA YA MAJENGO YA IBADA ILI TUONE UKWELI WA NENO HILI SINAGOGI KATIKA UTAALAMU WA WA LUGHA
Je Sinagogi laweza kuwa ni Msikiti katika uasili wa lugha?
Qur-an Surat 22:40
Andiko hili linataja majina ya majengo mbalimbali ya ibada ikiwemo na sinagogi ingawa halikuwekwa kwenye tafsiri ya Qur-an ya Kiswahili ila tutalichunguza kwa watafsiri wengine wa Qur-an hususani tafsiri ya kingereza iliyotolewa na Mwanazuoni wa Kislam ndugu Yusufu Ally.
Qur-an ya Sura ya 22 :40 katika tafsiri ya kiingereza inaeleza yafuatayo
Those who have been expelled from their homes unjustly but only because they say our Lord is Allahfor had it not been that Allah checks one by means of another have been pulled down Monasteries Churches Sinagogues and Mosques …….
Tafsiri ya aya hiyo katika Kiswahili
Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nymba za wat'awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu. Al barwani
Ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki ila kwasababu wanasema mola wetu ni Mwenyezi Mungu, na kama Mwenyezi Mungu asingeliwakinga watu baadhi yao kwa wengine bila shaka yangelivunjwa Mahekalu, Makanisa, Masinagogi na Misikiti…………. Al farsy
Katika sehemu hii tafsiri hiyo ya Qur-an iliyotolewa kwa lugha ya kingereza inataja wazi kuwepo kwa majengo mawili kati ya manne ambayo kwahakika ndiyo yanayosumbua watu wengi hata hivyo Qur-an inaonekana tena kwa uwazi ikiyatofautisha majengo hayo ambayo ni Masinagogi na Misikiti. Hilo linaonekana siyo tu katika tafsiri bali hata katika maandishi ya lugha ya Kiarabu.
Fuatilia majina ya majengo hayo katika matamshi ya kiarabu na maana zake hapo chini.
BILASHAKA YANGELIVUNJWA
KISWAHILI = KIARABU
1) Mahekalu = Swawamiyu
1. Hekalu = Swawaamiu
2. Kanisa = Biyaun
3. Msikiti = Masjid
4. Sinagogi = Swalawaatun au Kanis "كنيس".
Katika ushahidi huu yametajwa majengo manne lakini mwishoni tunakuta majengo mawili na jengo la kwanza linaitwa “Swalawatuni” yaani Sinagogi na la pili “Masjid” yaani “Msikiti” hivyo haya ni majengo yaliyotofauti kabisa maana sinagogi ingekuwa ni msikiti lisinge itwa Swalawatuni kwa kiarabu bali lingeitwa Masjid hivyo hii inadhihilisha kuwa katika maana halisi ya lugha sinagogi kamwe haliwezi kuwa ni msikiti hivyo ni kama nilivyoeleza mwanzo kuwa neno sinagogi lilimaanisha kikutanisho au kukutanika.
KIGEZO CHA YESU KUINGIA KATIKA SINAGOGI SIYO KIGEZO SAHIHI CHA KUFUNDISHA LA KUWA YESU NI MUISLAM.
Hebu fuatilia fungu hili la Biblia
MATENDO YA MITUME 17:1
Akiisha kupita kati ya amfipoli na Aporonia akafika Thesalonike ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi na Paulo akaingia mle walimo akahojiana nao kwa maandiko sabato tatu.
Endapo umefuatilia fungu hilo kwa makini unaweza kujiuliza swali lifuatalo ………….
Ikiwa kuingia tu kwenye sinagogi kulimaanisha Yesu ni Muislam je Paulo naye kwa tendo hilo lakuingia humo alikuwa Muislam?
Jambo la kushangaza hata wale wanaotoa fundisho hili humkataa Paulo kwa kadri ya imani yao na huku wakijivisha kitanzi kwa madai hayo kuwa mtu huwa muislam kwa kuingia katika Sinagogi.
Alichofanya Yesu katika Sinagogi hakiwiani na Misikiti ya Waislam
Luka 4:16 – 17 Yesu apewa chuo cha nabii Isaya je Waislam leo hii wanachuo cha nabii Isaya Msikitini? (La Hasha ) hii inaonyesha utofauti mkubwa uliopo baina ya Masinagogi na Msikiti ingawa ni vitu vichache tu vianavyolingana baina ya majengo hayo mawili.
Pamoja na hayo chuo hicho Nabii Isaya humtaja Yesu kama Mungu mwenye nguvu Isaya 9:6-10 tendo ambalo linapingwa na Umma wa Kiislam hivi leo hivyo kamwe Sinagogi na Misikiti si Majengo yanayowiana katika tafsiri na pia hata katika matendo kadhaa makuu ya kiimani pamoja na kufanana kwa machache kama yale yahusuyo mavazi n.k.
KUMFANYA YESU NI MUISLAM NI MAKOSA
Yesu alipaa kwenda mbinguni mwaka wa 33 kabla ya kuzaliwa kwa Mtume Muhamadi mwaka 570 (BK) ambaye ndiye muanzilizi wa Uislam.
Yesu hakufuata kamwe nguzo tano za Uislam na hata hivyo bado hapakuwa na nguzo hizo kwa kuwa muasisi wa imani ya Uislam yaani Muhamadi (SAW) hakuwepo.
Hebu sasa tuchunguze nguzo hizo tano za uislam na kisha upime mwenyewe endapo Yesu alizitekeleza hizo ili kuwepo na usahihi kwa wanaofundisha na kudai kuwa Yesu alikuwa Muislam.
NGUZO (5) ZA UISLAM
1) Shahadat - kushahadia- hili ni tendo la kukili kuwa
Mungu ni mmoja na Muhammad ni Mtume wake.
2) Ikhamu Swalat - Kusimamisha swala- hili ni tendo la kufuata
utaratibu wa kusali swala mara tano kwa siku.
3) Ita-U Zhakhati - Kutoa zaka- kutoa mali kwaajili ya Masikini.
4) Swaum Shar Ramadhani - Kufunga – hili ni tendo la kufunga kwa kuangalia mwezi linalochukua muda wa siku 29,30.
5) Hijat ila Baitu Llah - Kuhiji Maka- hili ni tendo la ibada ya
kwenda mji wa Makka linalo ambatana na matukio mbalimbali kama vile kupiga mawe Shetani na kuheshimu jiwe jeusi n.k
Je Yesu alifanya hayo ili aitwe Muislam?
Yesu kamwe hakuwa Muislam (Yasuu Laysa Muslimuna).
Barikiwani; Maswali yanakaribishwa
Na Mwalimu Chaka
For Max Shimba Ministries

OMBA KWA JINA LA YESU SEHEMU YA TATU

Image may contain: text
Mafanikio haya tuliyapata kwa sababu tulipatana na kuomba kwa JINA LA YESU KRISTO !
Naamini wakristo wengi waliowahi kufanya maombi ya mapatano namna hii kwa Jina la Yesu Kristo, wanakubaliana name nikisema maombi ya jinsi hii yana mafanikio makubwa.
Mke wangu, Diana, alikuwa ananishuhudia siku moja juu ya matendo makuu ya Jina La Yesu Kristo yaliyofanyika kwa mama mmoja aliyekuwa mjamzito. Alisema, mama huyo alikuwa amefanyiwa operesheni alipojifungua mtoto wa kwanza, lakini kwa mimba ya pili alitaka asijifungue kwa operesheni, bali ajifungue kwa njia ya kawaida.
Mke wangu alisema, katika kikundi chao cha maombi cha akina mama walipatana kama alivyosema huyo mama kuwa wamuombe Mungu kwa Jina la Yesu Kristo ili (huyo mama) ajifungue kwa njia ya kawaida. Kwa hiyo wakaomba hivyo.
Siku za kujifungua zilipowadia yule mama likwenda hospitalini na akalazwa kwa muda usiopungua wiki mbili bila kupata uchungu wowote wa kuzaa. Mara kwa mara daktari alimwambia kuwa anataka kumfanyia operesheni, lakini mara zote aliahirisha bila kutoa sababu za kuridhisha. Lakini yule mama alijua ni sababu ya maombi – maana walipoomba walikataa asifanyiwe operesheni.
Baada ya wiki mbili hizo kupita siku moja ghafla alianza kusikia uchungu wa kuzaa na kisha akajifungua mtoto kwa njia ya kawaida kama walivyopatana katika maombi yao! Jina la Bwana libarikiwe kwa uweza wake mkuu. Lakini nataka ujue ya kuwa kufanyiwa operesheni si upungufu wa imani, na wala sina maana hiyo. Ila yule mama alitaka ajifungue kwa njia ya kawaida! Na akapata alichoomba!
Siku zote ukiomba, omba kwa jina la Yesu Kristo ukiwa na uhakika ya kuwa uatpewa ulichoomba. Ukiweza kumpata mkristo mwenzako wa kupatana naye kwenye maombi hayo ni vizuri pia.
Kumbuka Yesu Kristo alisema, “Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao. ” (mathayo 18:19-20)
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

UNAFAHAMU KUWA SABATO "JUMAMOSI" ILIKUWA NI SIKU YA SAYARI ZOHALI "DIES SATURNI" NA ILIABUDIWA NA WAPAGANI WA KIRUMI?

Image may contain: one or more people and text
Wapinga Ukriso na dini zingine kama Waislam wanaihusisha siku ya Jumapili na waabudu JUA, kwa kufanya tafsiri ya neno la Kiingereza ‘Sunday’ – WANALIGAWA NENO “SUNDAY” KWA KUTENGANISHA SUN AND DAY, SUN = JUA NA DAY = SIKU Na kuja na jibu kuwa wale wote wanao abudu Jumapili basi wao wanamwabudu Mungu JUA, ingawa tuna uthibitisho tosha kuwa Wakristo wa kwanza walimwabudu Yesu ambaye alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na SIO MUNGU JUA kama wanavyo dai. Ili kufahamu kwanini kuna siku hizi za wiki na maana yake, ni vyema kuangalia msingi wa hizi siku na jinsi walivyo ziweka.
MFANO: Tuiangalie siku ya JUMAMOSI ambayo kwa Kiingereza ni SATURDAY, je, hili jina walilipataje? Kutokana na Warumi siku hii ya SATURDAY iliitwa kutokana na SAYARI YA ZOHALI yaani (dies Saturni) kwa sababu Warumi wa wakati huo waliheshimu sayari Zohali. SASA KAMA TUKITUMIA UTAALAMU HUO HUO WA KUHUSISHA SIKU NA IMANI AU DINI, JE, INAMAANISHA KUWA WASABATO “SDA” WAO WANAAMINI NA AU ABUDU SAYARI YA ZOHALI?
Ndugu msomaji, nimeamua kufundisha hili somo kwa kujibu maswali mengi sana yanayo ulizwa na Wasabato kwanini tunaabudu Jumapili na kutuhukumu kuwa tunavunja sheria za Musa. “Mosaic covenant/laws”
Hivyobasi, leo nakuacha hapa kwa kukukumbusha kuwa Wakristo wa kwanza waliabudu siku ya Jumapili na hakuna aya yeyote ile kutoka Biblia inayosema kiuwazi kuwa WAKRISTO WALIKUSANYIKA SIKU YA JUMAMOSI.
Sasa soma aya hizi hapa chini kwa ufasaha:
Warumi 14.5 Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. 6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.
Ndugu zanguni, kutokana na Warumi 14, tumewekwa huru kuchagua siku ya kuabudu, na nini tule au tusile, hivyo hivyo ni kuadhimisha kwa Bwana. Hivyo basi, hakuna kosa lolote lile mtu anapo sali Jumamosi au Jumapili au Jumatatu, au siku yeyote ile ya wiki. Mungu wetu yupo kila siku na siku zote alizumba yeye.
Matendo ya Mitume 2: 46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,
Unaona hiyo aya hapo juu inavyo sema? Je, Jumatatu imekosekana kwenye hiyo aya, vipi kuhusu Jumanne? Ndio maana nilisema sisi tumewekwa huru kutokana laana ya sheria na sasa tupo huru kuabudu Mungu siku yeyote ile. Mungu si wa Jumamosi tu au Jumapili tu au Ijumaa tu. Mungu ni wa kila siku.
KWANINI UNAPENDA MAFUNZO AMBAYO NI DHAIFU?
Wagalatia 4:8 Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu. 9 Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? 10 Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka.
Mtume Paulo anatukumbusha kuwa, mafunzo ambayo tulikuwa tunayafuata kabla ya kukombolewa na Yesu yalikuwa dhaifu. Sasa tumejazwa na Roho Mtakatifu ambaye ndie Mwalimu wetu Mkuu. Basi tushikamane naye na tujifunze kutoka kwake.
USIKOSE SEHEMU YA PILI ……………………………… “Kwanini Bwana Yesu aliingia kwenye Sinagogi siku ya Jumamosi “SABATO”? …………………….
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
© Copyright 1998-2016 Max Shimba Ministries - All Rights Reserved.

KAMA ALLAH NI MUNGU, KWANINI ALIUMWA MACHO MPAKA YAKAWA MEKUNDU?

No automatic alt text available.


Allah (s.w) aliumwa macho na pia wakati wa mafuriko ya Nabii Nuhu (a.s) alilia mpaka macho yakawa mekundu.
“Wakati mmoja macho ya Allah yalikuwa yanauma, na Malaika walikwenda kumuona, na kwamba Allah alitokwa na Machozi, kwaajili ya Mafuriko ya Nabii Nuhu mpaka macho yake yakawa mekundu (Al Milal Wannihal J.1 uk.141)
Msiba mzito sana tunapo soma ushahid kuwa:
1. Allah ana macho kama viumbe.
2. Allah analia kama viumbe ambavyo ni kafiri.
3. Allah ana sifa za kibinadamu ikiwa ni pamoja na kutokwa machozi.
MKRISTO MWENYE KUJITAMBUA HAWEZI KUMFUATA ALLAH ANAYE UGUA MACHO KAMA VIUMBE
ALLAH ANA MACHO Na tunaamini kuwa Allah Anayo macho mawili kikweli, na hii inatokana na kauli Yake Subhaanahu wa Ta’ala Aliposema kumwambia Nuuh (‘Alayhis-Salaam):
وَاصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا
"Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu."
Huud – 37
Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
"Pazia yake ni nuru, na lau kama Ataiondoa basi nuru ya Wajihi Wake ingeunguza kila kilichokifikia."
Na alipokuwa akihadithia juu ya Ad-Dajjaal alisema:
"Dajjaal ana chongo na Mola wenu Hana chongo."
Na tunaamini kuwa macho yetu hayamfikii kumuona Allaah.
Allaah Anasema:
لاَّ تُدْرِكُهُ الأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الأَبْصَارَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ
"Macho hayamfikilii, bali Yeye anayafikilia macho. Naye ni Mjuzi, Mwenye khabari."
Al-An’aam – 103
Ndugu wasomaji, teyari mmesha elewa kuwa Allah ni kiumbe kama binadamu kwasabau ana macho na zaidi ya hapo aliugua macho.
Mungu awabariki sana.
Katika Huduma yake,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

UK Muslim leader says celebrating Christmas is punishable by death according to the Koran

He tells the story of Khaled from the Koran to explain why Muslims are not allowed to celebrate Christmas because “Christmas is infidel (kufr)”


https://youtu.be/sqOfTpms2wE

NAKALA ZA QURAN ZATUPWA KWENYE JALALA NA UBALOZI WA SAUDIA MOROCCO

Image may contain: outdoor, water and nature
Waislamu katika mitandao ya kijamii wamebainisha ghadhabu na hasira zao dhidi ya Utawala wa Saudia kufuatia kitendo cha wanadiplomasia wake kuonyesha kutoheshimu hata kidogo nakala za Qur'ani Tukufu.
Gazeti la Ajel la Saudi toleo la Jumapili limeandika kuwa, kufuatia mvua kali na kuharibika mahala panapowekwa nakala za Qur'ani na vitabu vingine vya kidini, wakuu wa ubalozi waliwaamuru wafanyakazi wachukue vitabu vyote hapo na kuvipeleka sehemu maalumu kwa ajili ya kuviteketeza moto.
Imearifiwa kuwa, vibarua katika ubalozi huo walivipeleka vitabu hivyo, ikiwemo Misahafu, katika eneo la kutupa takataka lakini wakakaidi amri ya wanadiplomasia wa Saudia ya kuviteketeza moto. Ubalozi wa Saudia umewatuhumu wafanyakazi hao kuwa walilenga kuiharibia Saudia jina kwa kusambaza picha hizo katika mitandao ya kijamii.
Tukio hilo la Ubalozi wa Saudia nchini Morocco kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu linaajiri katika hali ambayo nchi hiyo ni mwenezaji mkuu wa itikadi potovu za Kiwahhabi, Kitakfiri na kigaidi duniani. Uwahhabi ni dini rasmi Saudia na kawaida hueneza tafsiri potovu za Uislamu jambo ambalo limepelekea Saudia kuchukiwa na Waislamu wengi duniani.
Mwezi Agosti, zaidi ya wasomi na maulamaa 100 wa Kiislamu kutoka maeneo yote ya dunia walikutana Grozny, mji mkuu wa Jamhuri ya Chechenia na kutangaza kuwa, pote la Uwahhabi si la Kiislamu kama linavodai.
Kikao hicho kilidhudhuriwa na wanazuoni wa ngazi za juu wa Ahul Sunna akiwemo mkuu wa Chuo cha Al Azhar cha Misri Sheikh Ahmad Tayyib, Mufti wa Misri Sheikh Shouqi Alam.
Mkutano huo uliowachukiza sana watawala wa Saudia pia ulihudhuriwa na Maulamaa wa Ahul Sunna kutoka nchi kama vile Syria, Jordan, Sudan, Pakistan, Indonesia, Malaysia na nchi kadhaa za Ulaya.

ROHO MTAKATIFU YUPO KILA MAHALI

Image may contain: sky, ocean, cloud, text and nature
Hebu tuangalie kama Roho Mtakatifu ana adhama za Mungu aliye hai. Sifa, moja ya Mungu ni kuwa, yeye yupo kila Mahali. Je, Roho Mtakatifu anayo hii sifa ya kuwa kila mahali? Fungua Zaburi 139:7-8, “nitaenda wapi nijifiche na Roho? ama nitakimbilia wapi mbali na uwepo wako? Nikipanda juu mbinguni, huko uko; nikifanya malazi yangu kuzimu, tazama uko huko,” Daudi anatuambia kwa kupitia Zaburi kuwa, huwezi kumkimbia Mungu.
Daudi anamtaja Mungu na au anamwita Mungu kuwa ni Roho. Hii sifa ya kuwa kila mahali ni ya Mungu pekee, na katika Zaburi 139: 7-8, tumesoma kuwa, Roho Mtakatifu yupo kila mahali. Tuendele na ushahidi zaidi wa kuwa kila mahali; katika Wakorintho wa Kwanza, hapa Mtume Paulo anasema yafuatayo 1 Wakorintho 2 aya ya 10 Lakini Mungu ameyajulisha kwetu kupitia Roho wake mtakatifu.
Kwa kuwa Roho huyachunguza mambo yote, naam, mambo ya siri ya Mungu. Kwa maana ni nani ayajuaye ya mwanadamu isipokuwa roho ya mwanadamu inayokaa ndani yake?
Vivyo hivyo, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.” Kama Roho Mtakatifu anafahamu kila kitu kilicho ndani ya Binadamu, ambao wametapakaa Duniani kote, basi kitendo cha kuwa kila mahali kwa wakati mmoja ni Mungu pekee ndie aliye na huo uwezo. Tuendelee kwa Ushihidi mwingine katika aya hiyo hiyo ya 10 ya Wakorintho wa kwanza Sura ya 2. Roho Mtakatifu ni Mungu kwasababu ana akili, hisia, na mapenzi yake. Katika Wakorintho wa kwanza 2:10 tumesoma kuwa Roho Mtakatifu hufikiria na hujua siri iliyo ndani yako. Hii sifa ya kufikiria na kujua, inavunja hoja ya Mashahidi wa Yehova kuwa Roho Mtakatifu ni “Nguvu”. Nguvu haina uwezo wa kufikiria wala kufanya maamuzi.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

JE WEWE UNAISHI KWA NEEMA YA YESU KRISTO AU SHERIA ZA MUSA NA SABATO?

Image may contain: text


SABATO SI SIKU
Upo ushahidi wa kutosha katika Biblia unaoonyesha kwamba sabato si siku katika juma. Bwana anapoongelea kuhusu safari ya wana wa Israeli anasema:
Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki, nikasema, Siku zote ni watu waliopotoka mioyo hawa ... hawataingia rahani mwangu. (Ebr. 3:10-11).
Pia imeandikwa: Maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote; na hapa napo, Hawataingia rahani mwangu. (Ebr. 4:4-5).
Katika maandiko haya Mungu anasema kwamba, kutokana na kukasirishwa na uasi wa wana wa Israeli kule jangwani, alimua kwambahawataingia kwenye raha aliyokuwa amewaandalia. Neno rahani hapa, au kwa Kiingereza rest, ndilo hilohilo sabato. Ndiyo maana hapo juu katika Waebrania 4:4-5, anahusisha siku ya saba na kuingia rahani.
Lakini hebu tujiulize maswali yafuatayo ili tuweze kupiga hatua zaidi.
• Je, Israeli walipokuwa jangwani kwani hawakuwa wakitunza Sabato kama siku? Jibu ni ndiyo, waliitunza. Biblia inasema:Basi ikawa siku ya sita wakaokota kile chakula sehemu mara dufu, kila mtu pishi mbili; na wazee wote wa mkutano wakaenda na kumwambia Musa. Akawaambia, Ndilo neno alilonena BWANA, Kesho ni starehe takatifu, Sabato takatifu kwa BWANA ... (Kutoka 16:22-23).
• Kama basi waliitunza sabato, iweje tena Mungu aseme, ‘Hawataingia rahani mwangu’? Kama ingekuwa ni kumwuliza Mungu, mtu ungesema, “Bwana, unasemaje hawataingia rahani mwako wakati kila siku ya saba wanapumzika?” Hii ni ishara ya wazi kwamba sabato hasa si kupumzika au kutofanya kazi kimwili katika siku ya saba. Sabato ni jambo jingine tofauti na siku ya saba. Iko sabato halisi ambayo siku ya saba na kupumzika kwake vilikuwa ni kivuli chake tu.
• Jambo jingine la kujiuliza ni kwamba, japo ni kweli kwamba wale ambao Mungu alisema hawataingia rahani mwake walifia wote jangwani, lakini walikuwapo wengine wengi walioingia, yaani watoto wao. Sasa je, hao walioingia waliipata hiyo raha (Sabato)?
Mtu anaweza kujibu, Ndiyo, maana sote tunajua kuwa hata wakati alipokuja Bwana Yesu, alikuwa akifundisha mara nyingi kwenye masinagogi 'siku ya Sabato'. Kwa hiyo, mtu anaweza kusema, ‘Ndiyo, waliingia kwenye raha au kwenye sabato.’
Hebu sasa tumsome Mtume Paulo:
Kwa hiyo mtume Paulo anafundisha kuwa ni jambo la udanganyifu kuwafundisha watu washike siku ya Sabato. Kwa sababu ya wokovu wetu ndani ya Kristo (Wakolosai 2:11-15) Paulo anasema, “Basi, MTU ASIWAHUKUMU ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.” (mstari wa 16).
Paulo anaanzisha mstari huo na neno hili, “Basi.” Kwa nini? Kwa sababu ya mistari 14 na15, “(Yesu) akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.”
Walikuwepo watu wa dini – kama tunavyojua kwa kusoma hasa Matendo na Wagalatia – waliotaka wakristo waishi chini ya sheria, yaani, kushika mambo ya nje ya torati; kwa mfano watahiriwe au washike ‘siku’ ya torati. Paulo anafundisha hapo kama mtu akisema, “Lazima ushike sabato ili kumpendeza Mungu au kuokoka ‘kweli’, usimruhusu akuvute chini ya sheria hiyo na humjali kama anakuhukumu! Tunasoma kwenye Matendo 15 na Wagalaia juu ya watu waliojaribu kupotosha njia ya Ukweli kwa kuwalazimisha waumini wayarejee mambo ya torati ya Musa. Ni vivyo hivyo siku hizi. Wasabato wanawahukumu wakristo kwa sababu hawashiki siku ya sabato! Paulo aliwaonya wakristo juu ya watu wa dini kama hao hao!
Hayo ni mafundisho ya Agano Jipya. Hatuwezi kusema au kufundisha kwamba ni lazima tukusanyike siku ya Sabato (jumamosi). Kama fulani akifundisha hivyo anawadanganya watu, sawasawa na maneno ya Paulo. Au je, tunataka kusema Paulo alifundisha uongo? Au tunataka kutumia mstari mmoja dhidi ya mstari mwingine kana kwamba Biblia siyo neno la Mungu? Mistari yote ina muktadha (mazingira) yake! Nani aliyekupa wewe ruhusa na mamlaka kupendelea mstari mmoja na kuudharau mstari mwingine au kutokujali kabisa? Hakika hiyo haitokani na Mungu.
Ndugu msomaji, ningependa ufahamu kuwa wokovu wetu sisi Wakristo upo ndani ya Yesu Kristo, siyo kwa kushika Torati ya Musa kama ambavyo WASABATO “SDA" wanavyo amini, SIKU HAINA UWEZO WOWOTE ULE KATIKA MAISHA YAKO, LAKINI YESU NDIE MUWEZA WA KILA KITU NA YEYE NDIE ALIYEIUMBA HIYO SIKU YA SABA YA JUMA.
Wasabato hutumia hii aya kumhukumu Mtume Paulo kuwa alifundisha uongo Kwa mfano wananukuu, ‘Imeandikwa katika Kutoka 20:8-11 lazima tushiike sabato!’ Sasa, inamaana Mtume Paulo alikuwa anafundisha uongo alipo sema tuna haki ya kumtukuza na kumwabudu Mungu siku yeyote ile?
Mtume Paulo anatueleza kiuwazi kuwa, ni vigumu sana kumfuata Yesu kwa asilimia 100 na wakati huo huo unafuata sheria za Musa. Hebu tusome jinsi Mtume Paulo alivyo ianza baruka yake kwa Wagalatia “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya kristo. Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.”
Hapa ni wazi kuwa Mtume Paulo alikuwa anaongea juu ya waumini ambao walikuwa wanataka kufuata sheria ya Musa. Ndio maana tunamsoma Mtume Paulo akitumia lugha au maneno makali kwa Wagalatia.
Hii tabia ya watu kupenda kushika sheria za Musa tunaiona kwa kanisa la SDA ambalo wanafuata sheria za Musa na kusahau kuishi kwa Imani kama jinsi ambayo Biblia inatufundisha katika Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Paulo alihuzunishwa sana, kwa sababu anasema wazi hivi “…..sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini KUYAREJEA TENA MAFUNDISHO YA KWANZA yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? MNASHIKA SIKU, na miezi, na nyakati, na miaka.”(Wagalatia 4:9,10).
“Maana yale YASIYOWEZEKANA kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa DHAIFU kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma “YESU KRISTO” Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; ILI HAKI YA TORATI YATIMIZWE NDANI YETU sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.” (Warumi 8:3,4).
Kwa hiyo, mtume Paulo anasisitiza, “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO.”
Ningependa ufahamu kuwa kiwango cha haki ya Injili ya Yesu Kristo KIPO JUU ZAIDI ya kiwango cha Torati ya Musa. Imeandikwa, “torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.” Yohana 1:17:
SWALI KWAKO MSOMAJI, wewe unaishi kwa uongozi wa NEEMA YA YESU KRISTO AU UONGOZI WA TORATI YA MUSA?
Kumbuka kuwa sheria ambayo ipo nje yako haiwezi kuishinda neema ya Yesu ambayo inaishi ndani yako.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na mwokozi wetu.

SHIRIKA LA UCHAPISHAJI QURAN SAUDI ARABIA LAFILISIKA

No automatic alt text available.
LASHINDWA KUWALIPA MISHAHARA WAFANYAKAZI WAKE 1300 KWA ZAIDI YA MIEZI SITA.
WOTE SASA WAMEFUKUZWA KAZI
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wafanyakazi hao wamefanya maandamano hayo kulalamikia kitendo cha kutolipwa mishahara yao kwa miezi sita sasa. Wakati huo huo, Shirika la Kuchapisha Qur'ani nchini Saudia nalo limewafuta kazi wafanyakazi wake 1300 kwa kufilisika.
Wafanyakazi hao waliokuwa wakijishughulisha katika kituo kikubwa cha uchapishaji wa Qur'ani Tukufu cha Mfalme Fahd huko mjini Madina, walikuwa hawajalipwa mishahara yao kwa kipindi cha miezi tisa kabla ya kufutwa kazini. Awali watu hao sanjari na kutakiwa kuwasiliana na idara ya uajiri ya Shirika laOger la nchi hiyo, walitakiwa pia kusaini mkataba wa kuacha kazi.
Kushuka kwa bei ya mafuta, uungaji mkono kifedha kwa makundi ya kigaidi na kitakfiri huko Saudia na Iraq na kadhalika vita vya muda mrefu nchini Yemen ambavyo hadi sasa vimeigharimu Saudia kiasi kikubwa cha fedha, ni mambo ambayo yameufanya utawala wa Aal-Saud, kukabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha. Hii ni katika hali ambayo, Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud ametoa amri ya kukatwa mishahara ya wafanyakazi wote wa serikali kwa ajili ya kuokoa bajeti ya serikali.
Itafahamika kuwa, Saudia ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa ukandamizaji wa wafanyakazi, na kwa mara kadhaa mashirika ya kutetea haki za binaadamu yamekuwa yakiilalamikia serikali ya kifalme ya nchi hiyo na kuitaka iheshimu haki za binaadamu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wafanyakazi hao wamefanya maandamano hayo kulalamikia kitendo cha kutolipwa mishahara yao kwa miezi sita sasa. Wakati huo huo, Shirika la Kuchapisha Qur'ani nchini Saudia nalo limewafuta kazi wafanyakazi wake 1300 kwa kufilisika.
Wafanyakazi hao waliokuwa wakijishughulisha katika kituo kikubwa cha uchapishaji wa Qur'ani Tukufu cha Mfalme Fahd huko mjini Madina, walikuwa hawajalipwa mishahara yao kwa kipindi cha miezi tisa kabla ya kufutwa kazini. Awali watu hao sanjari na kutakiwa kuwasiliana na idara ya uajiri ya Shirika laOger la nchi hiyo, walitakiwa pia kusaini mkataba wa kuacha kazi.
Kushuka kwa bei ya mafuta, uungaji mkono kifedha kwa makundi ya kigaidi na kitakfiri huko Saudia na Iraq na kadhalika vita vya muda mrefu nchini Yemen ambavyo hadi sasa vimeigharimu Saudia kiasi kikubwa cha fedha, ni mambo ambayo yameufanya utawala wa Aal-Saud, kukabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha. Hii ni katika hali ambayo, Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud ametoa amri ya kukatwa mishahara ya wafanyakazi wote wa serikali kwa ajili ya kuokoa bajeti ya serikali.
Itafahamika kuwa, Saudia ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa ukandamizaji wa wafanyakazi, na kwa mara kadhaa mashirika ya kutetea haki za binaadamu yamekuwa yakiilalamikia serikali ya kifalme ya nchi hiyo na kuitaka iheshimu haki za binaadamu.
Suala linalozidisha matatizo ya kiuchumi ya Saudia mbali na matumizi ya ndani zaidi linahusiana na gharama kubwa za masuala ya kijeshi na sera za vita za watawala wa Riyadh. Kwa sasa Saudi Arabia inashika nafasi ya tatu baada ya Marekani na China katika orodha ya nchi zenye bajeti kubwa zaidi ya masuala ya kijeshi duniani. Mwaka 2014 Saudia ilishika nafasi ya kwanza kati ya nchi zinazonunuasilaha kwa wingi kutoka nje ya nchi. Mwaka huo Watawala wa kifalme wa Saudia walinunua silaha zenye thamani ya dola bilioni 604 kiwango ambacho kiliongezeka kwa asilimia 54 ukilinganisha na mwaka wa kabla yake. Wakati huo huo India ambayo ni miongoni mwa nchi kubwa muhimu duniani iliagiza silaha zenye thamani ya dola bilioni 57.5.

TRENDING NOW