Sunday, September 10, 2017

UNAFAHAMU KUWA SABATO "JUMAMOSI" ILIKUWA NI SIKU YA SAYARI ZOHALI "DIES SATURNI" NA ILIABUDIWA NA WAPAGANI WA KIRUMI?

Image may contain: one or more people and text
Wapinga Ukriso na dini zingine kama Waislam wanaihusisha siku ya Jumapili na waabudu JUA, kwa kufanya tafsiri ya neno la Kiingereza ‘Sunday’ – WANALIGAWA NENO “SUNDAY” KWA KUTENGANISHA SUN AND DAY, SUN = JUA NA DAY = SIKU Na kuja na jibu kuwa wale wote wanao abudu Jumapili basi wao wanamwabudu Mungu JUA, ingawa tuna uthibitisho tosha kuwa Wakristo wa kwanza walimwabudu Yesu ambaye alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na SIO MUNGU JUA kama wanavyo dai. Ili kufahamu kwanini kuna siku hizi za wiki na maana yake, ni vyema kuangalia msingi wa hizi siku na jinsi walivyo ziweka.
MFANO: Tuiangalie siku ya JUMAMOSI ambayo kwa Kiingereza ni SATURDAY, je, hili jina walilipataje? Kutokana na Warumi siku hii ya SATURDAY iliitwa kutokana na SAYARI YA ZOHALI yaani (dies Saturni) kwa sababu Warumi wa wakati huo waliheshimu sayari Zohali. SASA KAMA TUKITUMIA UTAALAMU HUO HUO WA KUHUSISHA SIKU NA IMANI AU DINI, JE, INAMAANISHA KUWA WASABATO “SDA” WAO WANAAMINI NA AU ABUDU SAYARI YA ZOHALI?
Ndugu msomaji, nimeamua kufundisha hili somo kwa kujibu maswali mengi sana yanayo ulizwa na Wasabato kwanini tunaabudu Jumapili na kutuhukumu kuwa tunavunja sheria za Musa. “Mosaic covenant/laws”
Hivyobasi, leo nakuacha hapa kwa kukukumbusha kuwa Wakristo wa kwanza waliabudu siku ya Jumapili na hakuna aya yeyote ile kutoka Biblia inayosema kiuwazi kuwa WAKRISTO WALIKUSANYIKA SIKU YA JUMAMOSI.
Sasa soma aya hizi hapa chini kwa ufasaha:
Warumi 14.5 Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. 6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.
Ndugu zanguni, kutokana na Warumi 14, tumewekwa huru kuchagua siku ya kuabudu, na nini tule au tusile, hivyo hivyo ni kuadhimisha kwa Bwana. Hivyo basi, hakuna kosa lolote lile mtu anapo sali Jumamosi au Jumapili au Jumatatu, au siku yeyote ile ya wiki. Mungu wetu yupo kila siku na siku zote alizumba yeye.
Matendo ya Mitume 2: 46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,
Unaona hiyo aya hapo juu inavyo sema? Je, Jumatatu imekosekana kwenye hiyo aya, vipi kuhusu Jumanne? Ndio maana nilisema sisi tumewekwa huru kutokana laana ya sheria na sasa tupo huru kuabudu Mungu siku yeyote ile. Mungu si wa Jumamosi tu au Jumapili tu au Ijumaa tu. Mungu ni wa kila siku.
KWANINI UNAPENDA MAFUNZO AMBAYO NI DHAIFU?
Wagalatia 4:8 Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu. 9 Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? 10 Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka.
Mtume Paulo anatukumbusha kuwa, mafunzo ambayo tulikuwa tunayafuata kabla ya kukombolewa na Yesu yalikuwa dhaifu. Sasa tumejazwa na Roho Mtakatifu ambaye ndie Mwalimu wetu Mkuu. Basi tushikamane naye na tujifunze kutoka kwake.
USIKOSE SEHEMU YA PILI ……………………………… “Kwanini Bwana Yesu aliingia kwenye Sinagogi siku ya Jumamosi “SABATO”? …………………….
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
© Copyright 1998-2016 Max Shimba Ministries - All Rights Reserved.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW