Tuesday, March 20, 2018

UKRISTO NDIO IMANI PEKEE INAYOTHIBITISHIKA NJE (KIHISTORIA) NA NDANI YA BIBLIA

Image result for HISTORICAL JESUS
ZAIDI YA HAPO, YESU ANATHIBITISHIKA NJE NA NDANI YA BIBLIA TOFAUTI NA MUHAMMAD AMBAYE YUPE KWENYE HADITHI ZAKE TU NA QURAN YAO YA KUTENGENEZA.

Kwenye injili, kuna vianzo gani vya habari kuhusu Yesu mbali ya Biblia vilivyoandikwa kabla ya mwaka 200 BK?

Inawezekana mtu kufikiri kuwa maisha ya Yesu na Ukristo havikuelezwa, hata nje ya Biblia. Moja ya malengo ya kutoa nukuu hizi ni kusitisha madai ambayo watu wenye kushuku wanayatoa kuwa Yesu hakuwahi kuishi hapa duniani.

Cornelius Tacitus (aliyeishi karibu mwwaka 55 hadi karibu mwaka 117 BK) alikuwa mwanahistoria wa Kiroma aliyeandika kuhusu matukio ya Roma na Uingereza kuanzia mwaka 15-70 BK. Dharau aliyoionyesha inadhihirisha kuwa hakuwa rafiki wa Ukristo. Kwenye Annals 15:44 aliandika: ". . . Lakini juhudi zote za kibinadamu, zawadi zote za kifahari za Mfalme, na kuiridhisha miungu, havikuondoa imani mbaya kuwa moto mkubwa [wa Roma] ulitokana na amri [ya Mfalme]. Kwa ajili hiyo, ili kujiepusha na taarifa hiyo, Nero alikazia hatia yake na kutoa mateso makubwa zaidi kwa kundi la watu lililochukiwa kwa ajili ya mambo yake yasiyopendeza, ambalo watu wengi waliliita Wakristo. 'Christus', ambaye jina hili lilitokana naye, alipewa adhabu kubwa zaidi na mmoja wa maliwali wetu, Pontio Pilato, wakati wa utawala wa Tiberius, na ushirikina wenye kusumbua sana, ambao ulidhibitiwa kwa muda, uliibuka tena Uyahudi, mahali ulikoanzia, na hata Roma, ambako mambo yote yenye kuchukiza na kuaibisha kutoka sehemu zote za dunia hufanya makao na kupata ummarufu. Kwa ajili hiyo, kwanza kabisa watu waliobainika kuwa na hatia walikamatwa; kisha, baada ya taarifa zao, umati mkubwa ulionekana kuwa na hatia, si kwa ajili ya kuuunguza mji bali kuwachukia binadamu wengine. Vifo vyao viliandamana na dharau za kila namna. Wakiwa wamefunikwa na ngozi za wanyama, walishambuliwa na mbwa na wakaangamia, au walisublubiwa msalabani, au walihukumiwa kutupwa kwenye moto na kuunguzwa, kutumika kama mwanga wakati wa usiku, wakati mwangaza wa mchana unapokuwa umeondoka . . ."

Tacitus kwenye Histories kitabu cha 5 pia anaongelea undani wa vikosi mbalimbali vya Kiroma, cha 5, 10, 15, 12, na watu wengine kutoka vikosi vya 18 na 3 walivyozimisha maasi Uyahudi na kuuteketza mji wa Yerusalem.

Nukuu za Tacitus zimechukuliwa kutoka kwenye kitabu kiitwacho The Annals and The Histories kilichoandikwa na P. Cornelius Tacitus, Encyclopedia Britannica, Inc. 1952.

Mara Bar-Serapion alikuwa Mshamu wa kawaida aliyemwandikia mwanae, Serapion, barua baada ya mwaka 73 BK. Anamsihi kuiga mwenendo wa watu wenye hekima katika historia ambao walkufa kwa ajili ya mambo waliyoyaamini, kama vile Socrates, Pythagoras, na mfalme mwenye hekima aliyeuawa na Wayahudi. Kazi hii imo kwenye jumba la Makumbusho la Uingereza (British Museum).

Josephus alikuwa mwanazuoni wa Kiyahudi aliyezaliwa mwaka 37/38 BK, aliyeandika mambo mazuri kuhusu Kristo. Kuna vifungu viwili ambavyo anamwongelea Yesu. Kwenye kifungu cha kwanza, Josephus anaongelea maisha na huduma ya Yesu (Antiquities of the Jews 18.3.3, au 18 งง63-64), na kwenye kifungu cha pili anamtaja Yesu kama kaka yake Yakobo (Antiquities of the Jews 20.9.1, or 20 งง200-203). Kuna matoleo mbalimbali ya kifungu cha kwanza, lakini tutaongelea kwa ufupi matoleo ya Kiarabu na Kilatini. Toleo la Kilatini, ambalo limeonyeshwa hapa, na toleo la Kiarabu, ambalo liliandikwa karne ya 10, yanafanana sana isipokuwa toleo la Kiarabu halina sehemu zilizopigiwa mstari.

"Karibu na kipindi hiki, Yesu, mtu mwenye hekima, kama ni sahihi kumuita mtu, kwani alikuwa mtendaji wa mambo ya ajabu, - mwalimu wa watu kama hawa waliopokea kweli kwa furaha. Aliwavuta kwake wengi wa Wayahudi, na wengi wa mataifa. Alikuwa Kristo; na wakati Pilato, kwa mapendekezo ya wakuu wa watu miongoni mwetu, alipomhukumu asulubiwe, watu wale waliompenda tokea mwanzo hawakumuacha, kwani alitokea kwao tena akiwa hai siku ya tatu, kama ambavyo manabii wa Mungu walivyokuwa wametabiri mambo haya na kisha mambo mengine ya maajabu elfu kumi kuhusu yeye; na kabila la Wakristo, walioitwa hivyo kwa jina lake, hawajatoweka leo."

(Antiquities of the Jews 18.3.3, iliyoandikwa karibu mwaka 93-94 BK). Kifungu hiki kimetolewa kutoka Josephus: Complete Works. Kregel Publications 1960. Maneno haya ni muunganiko wa tafsiri ya William Whiston (1867) na toleo la lenye kutumika sana lililotolewa na Porter na Coates, Philadelphia, Pennsylvania).
Toleo la Kiarabu ambalo ni fupi kuliko la Kilatini huchukuliwa kuwa sahihi zaidi. Toleo lolote lililo sahihi, huu ni ushuhuda wa kuwa Yesu alikuwepo hapa duniani na kuwa alisulubiwa.

Lucian wa Samosata, (pia alifahamika kama Lucian Mgiriki) mwandishi tashtiti wa karne ya pili, aliyeandika kuhusu Kristo, ". . . mtu aliyesulubiwa Palestina kwa sababu ya kuanzisha mfumo wa kidini ulimwenguni . . . Pia, mto sheria wao wa kwanza aliwashawishi kuwa wote ni ndugu wa kila mmoja wao baada ya kukiuka kwa kukataa miungu ya Kigiriki na kwa kumwabudu mwalimu wa filisofia mwenyewe aliyesulubiwa na kuishi kwa kufuata sheria zake." (The Passing Peregrinus -pia inaitwa The Death of Peregrine 11-13).

Clement wa Roma alikuwa askofu wa Kikristo aliyeliandikia kanisa lililoko Korinto, kimsingi aliwauliza kwa nini hawakuwa wanatii mambo ambayo Paulo aliwaandikia miaka 50 iliyopita. Barua ya Clement iliandikwa mwaka 97/98 BK.

Pliny Mdogo alikuwa liwali wa of Bithynia aliyewaua Wakristo wengi kwa sababu ya imani yao. Alimwandikia Mfalme Trajan mwaka 112 BK na kumuuliza endapo aendelee kuwaua wanaume, wanawake, na watoto kwa ajili ya kutokuiabudu sanamu ya mfalme. Pliny anasema kuhusu Wakristo, "hata hivyo walithibitisha kuwa hatia yao yote ilikuwa kwamba walikuwa na mazoea ya kukutana kwenye siku moja iliyopangea kabla ya jua kuchomoza, baada ya kuimba mistari ya nyimbo kwa kupokezana wakimtukuza Kristo kama Mungu, na kuweka kiapo cha kutokufanya matendo yeyote maovu, bali kujiepusha na ulaghai, uizi, uzinzi, kutokusema uongo, kutokukataa jukumu wanapotakiwa kulitimiza (Epistles 10.96). Pamoja na hayo, Pliny pia anatupa habari kuhusu Waesene.

Papias ni askofu mwingine aliyekuwa mwanafunzi wa Mtume Yohana. Aliandika kazi nyingi sana karibu na miaka 110 hadi 130 BK. Kwa bahati mbaya maandiko yake yamepotea, isipokuwa maelezo mafupi yaliyotolewa na Eusebius wa Kaisaria (aliyeandika karibu mwaka 325 BK). Eusebius anasema kuwa pamoja na mambo mengine, Papias alisema kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa kwenye Kiebrania, Marko alikuwa mkalimani wa Petro, na kwama Papias alifundisha kuhusu kuja kwa Yesu kabla ya kipindi cha kutawala kwake duniani kwa muda wa miaka elfu moja, yaani 'premillennialism.' (Eusebius alikuwa haamini uwepo wa kipindi hicho, hivyo anaitwa 'millennialist').
Ignatius alikuwa mwanafunzi wa Mtume Yohana. Aliandika barua kwa makanisa mengi, na alikufa ama mwaka 107 au 116 BK wakati wa utawala wa Mfalme Trajan.

Polycarp askofu wa Smyrna, alikuwa mfiadini Mkristo na mwanafunzi wa Ignatius aliyeongea kuhusu Kristo. Alikufa karibu mwaka c.163 BK.

Irenaeus, askofu wa yon (Ufaransa), alikuwa mwanafunzi wa Polycarp, na mfiadini aliyeishi kutoka mwaka 120/140-202 BK. Aliandika andiko kubwa dhidi ya mafundisho ya uongo ya wakati ule kutoka mwaka 182-188 BK.

Didache (au Mafundisho ya Mitume Watakatifu) kilikuwa ni kitabu cha kiada cha mafundisho ya kanisa ambacho mtunzi wake na tarehe ya kuandikwa havifahamiki, inakisiwa kuwa karibu mwaka 380 BK.

Justin Martyr alikuwa ni mwanafilosofia Mgiriki aliyezaliwa ama mwaka 110 au 114 BK. Alibadili dini na kuwa Mkristo karibu mwaka 138 na kwa mujibu wa kazi yake, First Apology ilikuwa miaka 150 baada ya Kristo kuzaliwa. Kwenye utetezi wake wa kwanza na wa pili, na kazi yake, Dialogue with Trypho the Jew, Justin anaeleza kuwa Yesu ni Mungu. Chronicon Paschale inaeleza kuwa Justin aliuawa kwa sababu ya imani yake mwaka 165 BK.

Suetonius, mwanahistoria wa Kiroma na afisa wa mahakama aliyeandika karibu mwaka 120 BK, anasema kuwa "Wakati Wayahudi walipokuwa wanafanya vurugu zilizotokana na Krestus (Chrestus, ni tahajia nyingine ya Kristus [Christus], yaani Krsto), aliwafukuza Roma (Life of Claudius 25.4).

Theophilus, askofu wa Antiokia alikuwa mwandishi wa kwanza anayefahamika sasa kutumia neno la Kigiriki lenye kumaanisha Utatu (Triad) kwenye To Autolycus kitabu cha 2 sura ya 15, uk.101. Aliandika kati ya mwaka 168 na 181/188 BK.

Clement wa Alexandria, huyu ni tofauti na Clement wa Roma aliyeongelewa hapo awali, ambaye aliishi kutoka mwaka 193-217/220 BK. Aliandika kwa kiasi kikubwa sana ikiwa ni pamoja na wimbo wa Kristo na kazi kubwa iitwayo Miscellanies.
Hippolytus aliandika kutoka mwaka 225-235/6 BK na aliandika Refutation of All Heresies. Hippolytus alikuwa mwanafunzi wa Irenaeus.

Tatian aliishi kutoka mwaka 110-172 BK na aliandika mpangilio wa injili nne unaoweka pamoja matukio yanayofanana wenye karibu 79% ya mistari yote ya kwenye injili. Kwa bahati mbaya, baadaye aliiasi imani na kujiunga na Waenkrate (dhehebu la Kinostisia la karne ya pili waliokuwa wanazuia kuoa au kuolewa, kula nyama na kunywa mvinyo), dhehebu la mafundisho ya uongo la Kinostisia (harakati kizushi ya zama za kanisa la Kikristo la karne ya pili BK iliyokazia kuwa mada ni ovu na kuwa uhuru unapatikana kwa ufahamu).

Talmudi za Kiyahudi zinamwongelea Yesu sehemu kadhaa, ikiwa ni pamoja na Babylonian Talmud, Tol'doth Yeshu, Barailu, Amoa 'Ulla', Yeb. IV 3, na Baraita. Tazama pia Tractate Sanhedrin.

Phlegon alikuwa mwandishi wa Kigiriki kutoka Caria na mtumwa wa Mfalme Harian aliyeachwa huru. Aliandika muda mfupi baada ya mwaka 137 BK kuwa kwenye mwaka wa nne wa kipindi cha 202 cha miaka mine baina ya michezo ya Olimpiki [33 BK] kulikuwa na "kupatwa kwa jua kukubwa zaidi" na kwamba "kulitokea giza saa sita mchana [saa 6:00 kamili] hata nyota zilionekana mbinugni. Kulitokea tetemeko kubwa la ardhi huko Bithynia, na vitu vingi vilipidnuliwa huko Nikea" (Case for Christ, uk.111). Nukuu nzima kwa mujibu wa Baker Encyclopedia of Christian Apologetics, uk.384 inasomeka: "Yesu, alipokuwa hai, hakujipa msaada wowote ule, lakini alifufuka baada ya kufa na kuonyesha alama za kuteswa kwake, na kuonyesha jinsi mikono ilivyochomwa nan a misumari" na baadaye "kupatwa kwa jua wakati wa utawala wa Kaisari Tiberius, ambao unaelekea kuwa ndio muda Yesu aliposulubiwa, na tetemeko kubwa lililotokea wakati huo" kwenye Origen Against Celsus kitabu cha 2 sura ya 33, uk.455 kwenye Ante-Nicene Fathers juzuu ya 4, na Julius Africanus Events in Persia sura ya 18, uk.136. Tazama pia Origen Against Celsus kitabu cha 2 sura ya 59, uk.455.

Thales (au Thallus) alikuwa mwanahistoria wa Kipalestina aliyetajwa na Julius Africanus (aliyeandika mwaka 232-245 BK) Julius anaongea kuhusu giza lililotkea wakati wa Kristo, "Giza hili Thallus, kwenye kitabu cha tatu cha historia yake, analiita, kama inavyoonekana kwangu bila sababu, kupatwa kwa jua" (The Ante-Nicene Fathers juzuu ya 6 kipande cha 18, uk.136).

Muktadha ni Julius anapoongelea jinsi muda kuanzia amri ya Ahasuero hadi kusulubiwa kwa Kristo, ulivyotimiza Danieli 9.
Mwanahistoria wa Samaria, Thallus, ambaye ni tofauti na mwanahistoria wa Kigiriki, Thales, alikuwa anafahamika sana. Kazi zifuatazo zinamtaja Thallus.

Justin Martyr's Hortatory Address to the Greeks kitabu cha 9, uk.277 inawataja Thallus, Philo, Josephus, na wengineo.

Theophilus to Autolychus sura ya 29, uk.120 anamtaja Thallus, pia kabla ya hapo Berosus ambaye ni mwanahistoria Mkaldayo aliyeongea kwenye uk.121.

Octavius wa Minucius Felix sura ya 22, uk.186
Tertullian's Apology sura ya 19, uk.33 inawataja Thallus na Josephus.

Julius Africanus kipande cha 18, uk.136.

The Shepherd of Hermas ni kazi ya Kikristo ambayo mwandishi wake hafahamiki iliandikwa karibu mwaka 160 BK.

Athenagoras alimwandikia mfalme wa Roma utetezi wa Ukristo karibu mwaka 177 BK.

Aristides wa Athens na Quadratus pia wanafahamika kuandika utetezi wa Ukristo, lakini tuna baadhi tu ya maandiko yao yaliyohifadhiwa.

Shalom.

Max Shimba mtumwa wa Yesy Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13.

KWANINI KUNA INJILI NNE KWENYE BIBLIA TAKATIFU?

Image result for four gospels

Injili nne zina malengo tofauti na kwa kiasi fulani watu tofauti walioandikiwa.

Mathayo:
Iliandikwa kwa mara ya kwanza kwenye lugha za Kiebrania (Kiaramu?) kwa mujibu wa Papias. Injili hii inatilia mkazo ufalme wa Mungu, tofauti na Injili ya Yohana inayotilia mkazo jinsi ya kuupata wokovu. Injili ya Mathayo inanukuu nabii nyini za Agano la Kale, na inaonyehsa jinsi ambavyo maisha ya Yesu yanavyofanana na maisha ya Israel kwenye Agano la Kale. Watu wanaichukulia Injili ya Mathayo kuwa kama "simba" kwani inamsistiza Kristo kuwa Mfalme. Irenaeus (mwaka 182-188 BK) kwenye kipande cha 28 cha kazi yake anasema kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa kwa Wayahudi, ikisistizia kuwa Kristo ni wa ukoo wa Daudi.
Marko:
Inasistizia matendo ya Kristo. Watu wengi wanaichukulia Injili ya Marko kuwa kama "maksai", yenye kumsistiza Kristo kuwa mtumishi.
Luka:
Injili ndefu zaidi, iliandikwa na daktari na mshiriki wa safari za kimisheni za Mtume Paulo. Luka anaonekana kuwa mwanahistoria mkubwa zaidi wa ulimwengu wa kale. Watu wengi wanaichukulia Injili ya Luka kuwa kama "binadamu", ikisistizia uanadamu wa Kristo.

Yohana:
Hii inaweza kuwa Injili ya maana zaidi, kwani inasistizia maisha ya Kristo kwa kiasi kidogo lakini maneno na mafundisho yake kwa kiasi kikubwa. Watu wengi wanaichukulia Injili ya Yohana kuwa kama "tai", ikisistizia uungu wa Kristo.

Kwenye Agano la Kale, Masihi anaitwa ". . . Chipukizi . . . mfalme" wa nyumba ya Daudi (Yer 23:5, 6), "mtumishi wangu, aitwaye Chipukizi" (Zek 3:8), "huyu ndiye . . . Chipukizi" (Zek 6:12), na "chipukizi la Bwana" (Isa 4:2).

Hapakuwa na injili zaidi ambazo Wakristo walizikubali kwa ujumla. Irenaeus, aliyeandika karibu mwaka 182-188 BK, alisema palikuwa na Injili nne (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 11.8, uk.428).

Shalom

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13

Monday, March 19, 2018

KUTO KUWEPO "NOTHING" HAKUWEZI KUUMBA KITU

Image result for creation ex nihilo
Kwanza, ifuatayo ni njia rahisi na yenye mantiki rahisi yenye kuelezea.
Haya, tuanze kufikicha akilia na Max Shimba.

Huwezi kupata kitu bila kuwa na kitu (kingine). Kila kitu kilichoumbwa kilihitajika kuumbwa. Hata vitu vya kwanza kuumbwa vilihitajikwa kuumbwa na kitu/mtu mwingine ambaye aliisha kuwepo. Kwa hiyo, panatakiwa kuwa na kitu au mtu ambaye hajaumbwa na anaishi milele.
Yafuatayo ni maelezo makali; maana ni zangu mwenyewe.
Tunadhani kuwa kila mtu anaufahamu wa kutosha kuweza kuwa na maana inayofaa ya mantiki, kupingana na kutopingana, tukio, mchakato, "ndani ya", kitu, mkusanyiko, muda, mada, nishati, roho, chanzo, kilichosababishwa na, na matokeo.

Uwepo halisi kunafafanuliwa, katika makala hii, kuwa ni kuwepo kwenye ulimwengu huu, kuwa na uwezo wa kuathiriwa na kitu mojawapo hapa ulimwenguni, au kuwa na uwezo wa kuathiri kitu kimojawapo hapa ulimwenguni. Huu ni ufafanuzi mfinyu sana wa kuwepo/kuishi, kwani unashindwa kuhusisha mawazo, mienendo, na mambo mengine. Kwa hiyo, hebu na tuuite uwepo "halisi" na tufanye majadiliano yetu hapa yakomee kwenye uwepo halisi.

Kitu halisi kinafafanuliwa hapa kuwa ni kitu au mkusanyiko au mada, nishati, roho, au mchanganyiko wenye kuwa na uwepo halisi. Ukweli wa kimantiki, ukinzani wa kimantiki, na ushahidi wa kihesabu havichukuliwa kuwa vitu hapa.

Uwepo wa kimelea, kama kitu cha ndani, unfafanuliwa kuwa ni uwepo halisi wa vitu ambavyo si vitu halisi. Mashimo, giza, upungufu, kutokuwa sahihi, na maovu si mada, nishati, au roho, lakini kama ambavyo kivuli kinaweza kuua mimea ambayo inahitaji jua, au upungufu ea chakula unavyoweza kuua mtu, vivuli na upungufu wa chakula vina uwepo halisi licha ya kutokuwa vitu halisi.

Ulimwengu unafafanuliwa hapa kuwa ni mkusanyiko wa vitu halisi ambavyo vipo kiuhalisi. Tazama kuwa katika ufafanuzi huu, ulimwengu unajitisheleza, na Mungu (tuchulie kuwa Mungu yupo, ni roho na anaweza akaathiri vitu) yupo ulimwenguni.

Kutokwepo (nothing) kunafafanuliwa kuwa ni kitu ambacho hakijawahi kabisa kuwepo, au ambacho hakijawahi kuwa na uwepo wa kweli/kihalisi wakati wowote ule. Kwa maneno mengine, kabla hakijaumbwa [au baaday ya kuharibiwa], kitu halisi hakipo ulimwenguni, hakiuathiri ulimwengu, na hakiathiriki na ulimwengu.

Uumbaji unafafanuliwa hapa kuwa ni tukio au mchakato wa kufanya kitu halisi kipya. Kuumba kunatofautishwa na "kubadilisha", ambako hakuhitaji chanzo chochote mbali ya kitu chenyewe. Kuumba kitu halisi kipya kunaweza kuhusisha kubadilisha au kuharibu kitu halisi kilichowahi kuwepo, lakini hakulazimiki kufanya hivyo. Hata hivyo, angalia sehemu inayofuata.

Hakuna kitu kinachoweza kuwepo kutokana na kitu kisichokwepo. Kitu chochote halisi kilichoumbwa kinahitaji chanzo cha kuumbwa kwake. Kwa maneno mengine, hakuna kitu kinachoweza kuumbwa isipokuwa kitu/vitu vinginie vimekiumba.

Hakuna kitu kinachoweza kujiumba chenyewe. Hakuna kitu kinachoweza kujiumba chenyewe. Ingawa vitu halisi vinaweza kujibadilisha wakati mwingine, au kujiharibu vyenyewe, hakuna kitu kinachoweza kuwa chanzo cha kuumbwa kwake.

Chanzo cha kwanza. Ingawa vitu halisi vilivyoumbwa vinaweza kuumba vitu vingine halisi vilivyombwa, mwisho wa siku patahitajika kuwa na chanzo cha kwanza. Kwa maneno mengine, kwenye mlolongo wa vyanzo, chanzo walau kimoja kinatakiwa kuvitangulia vyanzo vingine vyote.

Kisichoumbwa. Kwa vile chanzo walau kimoja hakitakiwa kuwa na chanzo kilichokitangulia, na kila kiumbe kinahitaji chanzo, kuna kitu halisi walau kimoja ambacho hakijaumbwa na kimekuwepo toka milele iliyopita, kwa sababu kuna kitu halisi walau kimoja ambacho hakijaumbwa.

Mhutasari: Kila kitu halisi ambacho kinaishi ama kina wakati au kipindi fulana=i ambacho kiliwahikuishi, vinginevyo hakijawahi kuishi. Kama kimewahi kuishi, basi kuna kitu halisi ambacho ni chanzo cha kuwepo kwake.

Mipaka: Hoja hii haithibitishi kwamba chanzo cha kwanza ni kitu chenye uhai, au kwamba kuna chanzo kimoja tu ambacho hakijaumbwa, au kwamba vyanzo vyovyote ambavyo havijaumbwa bado vinaishi. Kitu ambacho hoja hii inasema ni kwamba kuna walau kitu kimoja halisi (nafsi iliyo hai au kitu kisichokuwa nafsi) ambacho kimekuwepo milele bila kuumbwa.
Moja ya waandishi wa kwanza aliyeiona hoja ya muundo na umbo la ulimwengu na kusema kuwa Mungu ni chanzo cha kwanza alikuwa Philo, Myahudi aliyeishi Alexandria, Misri, toka mwaka 15/20 KK hadi mwaka 50BK. R. C. Sproul na Norm Geisler wameandika kazi nyingi na nzuri kuhusiana na hoja ya muundo na umbo la ulimwengu.

Je, kuto kuwepo kunaweza kutengeneza au umba uwepo?
If nothing ever existed, nothing would exist now. Nothingness has no capacities or being.

Shalom,

Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13.

SHETANI NI NANI NA AMETOKA WAPI?

Image result for WHO IS SATAN
Hivi shetani ni nani? Biblia humwita “mungu wa ulimwengu huu.” Lakini alitoka wapi? Je Mungu alimuumba kama alivyo? Je, yeye ni roho aliyeanguka? Haya hapa ni majibu kutoka katika Neno la Mungu!

Mwanzoni Mungu aliumba makerubi watatu: Lusifa au Nyota ya Alfajiri (aliyegeuka kuwa Shetani), Mikaeli na Gabrieli. Kila mmoja alitawala theluthi ya mamia ya mamilioni ya malaika (Ufunuo 5:11). Nyota ya Alfajiri na theluthi yake walitawala ulimwengu uliokuwa kabla ya Adamu. Yeye, pamoja na malaika zake, waliasi serikali ya Mungu, na leo anawaongoza malaika hawa walioanguka, au mapepo, kama mungu wa dunia hii.

Shetani amekuwa somo lenye shauku kubwa kwa maelfu ya miaka. Amedhaniwa kuwa kama jini, mzuka, na zimwi. Ama kama mtu mwenye sura nzuri ya “kishetani” aliyevalia suti nyekundu, mwenye pembe na uma ya nyasi. Shetani hata amesimuliwa kuwa kama kitu kisicho dhahiri “aliye muhtasari wa maovu yote.” Au kama chanzo cha kila kitu kibaya watendacho watu. Huenda wengi wanaufahamu usemi “shetani alinifanya nitende.” Ingawa fikira hizi ni za kawaida, zote SI SAHIHI! Hata zinapojumuishwa pamoja, kwa kiwango kikubwa zinamwakilisha isivyo roho huyu mkuu aliyeanguka!

Shetani yuko hai na halisi. Biblia inamuita “mungu wa ulimwengu huu” (2 Korintho 4:4). Ufunuo 12:9 husema kwamba “audanganyaye ulimwengu wote.” Kwa hakika hii hujumuisha ukweli juu ya utambulisho wake. Lakini je wakati wote amekuwa shetani? Wakati wote amekuwa yule mwovu, muuaji, mwongo, mkuu wa giza mharabu? Je aliumbwa jinsi hiyo?

Ufunuo 12 husema juu ya Shetani na pepo wake wabaya “walitupwa katika nchi” (fu. 13). Kwa hakika sura hii imepachikwa katikati ya kitabu cha Ufunuo, na ni muhtasari mfupi wa historia ya Kanisa la Agano Jipya.

Fungu la 3 linamwelezea Shetani kama “joka” aliye “kokota theluthi ya nyota za mbinguni na kuziangusha katika nchi” (fu. 4). Kumbuka kwamba “nyota” hizi zilikuwa ni theluthi ya malaika wote waliokuwa chini ya Nyota ya alfajiri kabla hajaasi.

2 Petro 2:4 hutoa kiashiria kingine juu ya huku “kutupwa chini” kwa Shetani na malaika zake “aliowakokota pamoja” naye. Angalia: “Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa [Shetani hakuwa malaika pekee aliyeasi], bali aliwatupa shimoni.” (Neno la Kigiriki hapa ni tartaros na linamaanisha aidha “gerezani” ama “kizuizini”—hii ni dunia yenyewe.) Pepo hawa wabaya pamoja na Shetani “wanalindwa hata ije hukumu,” wakiisha “kutiwa…katika vifungo vya giza.” Hii inafunua kwamba Mungu aliwatia katika gereza hili la giza pepo wengine wengi walioanguka waungane na “mkuu wa giza.”

Ufunuo 12:7-9 hueleza, kwa undani, lini Shetani na pepo wake wabaya watatupwa hata nchi kwa mara ya mwisho wasipate tena kibali cha kuingia mbinguni. Mafungu ya 12-14 yanaonyesha kwamba mwitikio wa ibilisi ni hasira kuu. Wakati huu wa kutisha unakuja kwa ulimwengu mzima hapo mbeleni kidogo!

Hatima ya Shetani
Lakini kitatokea nini kwa Shetani mara baada ya Kurudi kwa Kristo? Je, ataachwa huru kurandaranda duniani, akiendelea “kudanganya” (Ufu. 12:9) na “kudhoofisha” (Isa. 14:12) mataifa? Je, ataruhusiwa kubakia kuwa “mungu wa ulimwengu huu” (2 Kor. 4:4) milele? Hatima yake ni nini?

Ufunuo 20 huelezea Kristo akisimamisha utawala wa milenia kwa miaka-1000 (fu. 4) na kuzileta “sura za mwisho” katika kisa cha Shetani. Fungu la 2 husema kwamba malaika mwenye nguvu (fu. 1) anamfunga hakika kwa “miaka elfu” na “kumtupa katika kuzimu,” mahali “anapofungwa.” Kisha malaika huyu “[hu]tia muhuri juu yake, kwamba asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie: na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.”

Paulo alitaja wakati wa Shetani kufungwa aliposema, “naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi” (Rum. 16:20). Hii ni ahadi ya Mungu kwa Wakristo wote wa kweli na wanadamu wote, kwa sababu Shetani amewatesa Wakristo na kawadanganya wanadamu kwa maelfu ya miaka!

Mtume Yuda alisema kwamba Shetani na pepo wake wabaya watatupwa nje ya mifumo ya sayari kwenda mahali ambapo Biblia hupafafanua kuwa hapana nuru. Fungu la 13 huwaongelea viumbe hawa wenye kudhalilika kama “nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliyowekewa milele.” Yule “mkuu wa giza” na malaika zake watapata kile wanachostahili—kile walichojiletea wao wenyewe. Yule ambaye hapo awali alijulikana kama “aletaye nuru” alichagua giza. Mungu atampatia giza kamili kwa muda wote utakaofuata!

“Kwa hiyo Mungu HAKUUMBA ibilisi. Aliumba kerubi, Nyota ya alfajiri—mkamilifu katika njia zake, lakini akiwa na nguvu ya uchaguzi huru—na Nyota ya alfajiri alijigeuza mwenyewe akawa shetani kwa kuasi Serikali ya Mungu!’



Shalom

KAMA MUNGU NI WA UPENDO, KWANINI KUNA MAJANGA NA UOVU?

Related image
Kwenye Mwanzo 1, kwa kuwa Mungu aliumba kila kitu kikiwa kizuri, kwa nini radi, milipuko ya magonjwa na majanga mengine hutokea?

Kila kitu kilikuwa kizuri mwanzoni. Lakini katika Warumi 8:20-22 inaonyesha kuwa tokea wakati wa anguko, dunia "ilitiishwa chini ya ubatili" pia. Ulimwengu wote upo chini ya utawala wa mwovu (1 Yohana 5:19), na mkuu wa dunia hii ni Shetani kwa mujibu wa Yohana 12:31; 14:30.

Mungu wa kwenye Biblia hakuumba uovu, wala mwovu wala shetani. Kwamaana. Biblia inasema hivi: Mtume Paulo aliandika, “Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu” (1 Korintho 14:33). Wakati MKANGANYIKO mkubwa umegubika utambulisho wa shetani, huhitaji kukanganyikiwa!

Paulo pia aliandika, “JARIBUNI mambo yote; lishikeni lililo jema” (1 The. 5:21), na “MPATE KUJUA hakika mapenzi ya Mungu, yaliyo mema, yakumpendeza, na ukamilifu” (Warumi 12:2).

Mungu hakuumba uovu, lakini uruhusu uovu uwepo. Kama Mungu hangeruhusu nafasi ya uovu, wote mwanadamu na malaika wengemtumikia Mungu kwa lazima, bali si kwa kuchagua. Mungu hakutaka “miigizo” kwa ufupi yenye ingefanya chenye aliwataka wafanye kwa sababu ya “ratiba” yao. Mungu aliruhusu jukumu la uovu ili tuwe na nia njema ya kweli na kuchagua ikiwa ama hatukutaka kumtumikia.

Shalom,



Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13.

VINASABA (DNA) NDANI YA BIBLIA

Image result for DNA NI NINI?
VINASABA (DNA) NI NINI?
DNA Ni kifupi cha neno (Deoxyribonucleic Acid). Hizi ni chembechembe asili za urithi au viini tete ambavyo hupatikana katika kila kiumbe hai.

Nasaba hupatikana katika kiini cha seli hai na huwa na taarifa za urithi kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto. Taarifa za nasaba ndizo pekee zenye kutoa ukweli usiopingika kuhusu uzao wa mtoto.

Msingi wa Uchunguzi wa DNA (Vinasaba) Kila Binadamu ana mpangilio wa chembechembe asili za urithi aliyorithi kutoka kwa wazazi wote wawili (Baba na Mama). Mpangilio wa chembechembe asili za urithi hurithiwa nusu kutoka kwa baba na nusu kutoka kwa mama. Hivyo basi ili kutambua uhalali wa mzazi kwa mtoto ni lazima mtoto awe na chembechembe asili za urithi nusu zinazooana na za baba na nusu nyingine zinazooana na za mama.

ZIMEANDIKWA KWA NJIA AMBAYO TUNAWEZA KUELEWA


Bila shaka! Ikiwa Mungu ndiye aliyeumba uhai, basi Mungu ndiye anayestahili kusifiwa wala si mageuzi. (Ufunuo 4:11) Pia, ikiwa sisi tumeumbwa na Muumba mwenye hekima, basi tupo hapa kwa kusudi fulani. Hali isingekuwa hivyo ikiwa uhai ulijitokeza wenyewe.
Habari yoyote iwe ni picha, sauti, au maandishi, inaweza kuhifadhiwa na kushughulikiwa kwa njia nyingi. Kwa mfano, kompyuta hufanya hivyo kielektroniki. Kwa kutumia DNA, chembe hai huhifadhi na kushughulikia habari kwa njia ya kikemikali. DNA hupitishwa wakati chembe zinapogawanyika na viumbe vinapozaliana—uwezo unaoaminika kwamba ndiyo unaofafanua maana ya uhai.
Chembe hutumia habari jinsi gani? Hebu wazia kwamba DNA ni kama kitabu cha mapishi chenye maelekezo na hatua mbalimbali, na kila hatua imeandikwa kwa umakini na utaratibu maalumu. Hata hivyo, badala 
Habari zilizo kwenye chembe ya urithi huhifadhiwa mpaka zitakapohitajiwa, labda ili kubadili chembe zilizochakaa au zilizo na ugonjwa kwa kutokeza chembe mpya au kupitisha tabia kwa mtoto.
Kufafanua habari zilizo katika DNA kama “lugha ya molekuli ya chembe za urithi hakutoshi,” anasema Küppers. Anaendelea kusema hivi: “Kama tu ilivyo katika lugha za wanadamu, lugha ya molekuli ya chembe za urithi ina utaratibu maalumu.” Kwa ufupi, DNA ina “sarufi,” au kanuni, zinazoongoza kikamili jinsi maagizo yanavyotolewa na kutekelezwa.
“Maneno” na “sentensi” katika DNA huunda “maagizo” mbalimbali ambayo huongoza kutokezwa kwa protini na viini vingine vinavyojenga chembe mbalimbali zinazounda mwili. Kwa mfano, “maagizo” hayo yanaweza kuongoza kufanyizwa kwa chembe za mifupa, misuli, neva, au chembe za ngozi. Mwanabiolojia wa mageuzi, Matt Ridley aliandika hivi: “Uzi wa DNA una habari au ujumbe ulioandikwa kikemikali, na kila herufi moja inawakilisha kemikali moja.” Akaongezea hivi: “Ni jambo la kushangaza kwamba alama hizo au utaratibu huo hubadilika na kuwa maandishi tunayoweza kuelewa.”
Mwandikaji wa Biblia Daudi alisali kwa Mungu hivi: “Macho yako yalikiona kiini-tete changu, na katika kitabu chako sehemu zake zote zilikuwa zimeandikwa.” Zaburi 139:16) Daudi alitumia lugha ya kishairi. Hata hivyo, kulingana na kanuni, alikuwa sahihi kabisa akiwa mwandishi wa Biblia. Hakuna mwandishi yeyote wa Biblia aliyeathiriwa hata kidogo na hekaya au mapokeo ya watu wa kale.—2 Samuel 23:1,2; 2 Timotheo 3:16.
Wanasayansi wengi husema nini? 
Wanabiolojia wengi na wanasayansi fulani hufikiri kwamba DNA pamoja na maagizo yake yaliyopangwa vilitokana na matukio yaliyojitokeza yenyewe ambayo yalifanyika kwa kipindi cha mamilioni ya miaka. Wanasema kwamba hakuna uthibitisho wa ubuni katika maumbile ya molekuli hiyo wala katika habari inayobeba na kuituma wala jinsi inavyofanya kazi.
Biblia inasema nini? 
Biblia inasema kwamba kufanyizwa kwa sehemu mbalimbali za mwili wetu—hata wakati zitakapofanyizwa—kunahusisha kitabu cha mfano ambacho chanzo chake ni Mungu. Ona jinsi Mfalme Daudi alivyoongozwa na roho kueleza mambo, akisema hivi kumhusu Mungu: “Macho yako yalikiona kiini-tete changu, na katika kitabu chako sehemu zake zote zilikuwa zimeandikwa, kuhusiana na siku ambazo zilifanyizwa na hakukuwako hata moja kati ya hizo.”—Zaburi 139:16. 
Uthibitisho unafunua nini?
Ikiwa fundisho la mageuzi ni la kweli, basi inapaswa angalau kuonekana kwamba huenda DNA ilijitokeza yenyewe kupitia mfuatano wa matukio. Ikiwa Biblia inasema kweli, basi DNA inapaswa kutoa uthibitisho wenye kusadikisha kwamba inatokana na Muumba mwenye utaratibu na akili.
Shalom
Max Shimba Ministries 

TRENDING NOW