Monday, April 30, 2018

HAKUNA MABADILIKO KATIKA MANENO YA ALLAH

Image result for origin of islam

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu.

Kwanza yanipasa nimshukuru Mola wetu mlezi ambaye ametupa uwezo wa kununa na kutumia karama ya fikra na kututenganisha na viumbe wengine wote. Baada ya kuipokea na kuikubali njia ya Bwana, na mwongozo wake, matokeo yake ni makuu na yametimizwa na ahadi ya uzima wa milele mbinguni. Kutakuwa na baraka tele na furaha kwani ALLAH amesema: ‘kwa wale wafuatao imani, kutakuwa na zawadi tele zaidi ya chochote chenye kufikiriwa, zaidi ya chochote kionekanacho au kinachosikika.’

Ebu tutumaini kuwa miongoni mwa hao watao bahatika.

Mola wetu aliyetupa akili timamu na fikra safi pia atatuongoza na kutuelekeza, kuona mwanga na kweli utakaotuongoza kwa usalama. Bwana uufanye mkono wetu unyoke kufikilia uwongofu.

Mungu mkuu amefanya tangazo hili:
“Msiliongeze neno niwaamuru wala msilipunguze, mpate 
kusishika amri za BWANA, Mungu wenu mwaamuzi’ Kumb 4:2

Na mwishoni kwa injili tukufu, tunasoma onyo kali.

‘Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, mtu yeyote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki,Mungu atamwondelea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.’ Ufunuo 22:18-19.

Baada ya amri hizi nzito namna hii, Je pana mtu yeyote mwaminifu atakayeleta changamoto kwa neno la Mungu au kulibadilisha neno la BWANA?

Imefikiriwa na baadhi ya Waisilamu wengi kwamba Biblia (Yaani Taurati, Zabur na Injili) imechafuliwa na kubadilishwa mara nyingi wakati tofauti tofauti , ima kwa kuongeza jambo ndani yake au kwa kuondoa jambo humo ndani. Kwa muda mrefu watu wenye mawazo haya wamejaribu kuleta hoja dhidi ya Biblia ijapo kwa kweli bado hawajafaulu kuleta ushindi kamilifu kwao basi ni wazi kwamba wamepoteza msingi wote kwa madai yao.


Ndungu yangu Muislamu,ni jambo la ajabu kwamba watu leo hii bado wangali wanadai kwamba Biblia (Taurati, Zaburi na Injili) imefanyiwa mabadiliko ambayo yanaleta utata kati ya Biblia halisi ya awali na Quran. Ni jambo lakusikitisha kwani Quran inashuhudia Biblia, kwamba Biblia kwa kweli ni maneno ya ALLAH, Yaliyoletwa na Mola wetu mwema kuwa nuru , muongozo na rehema. Biblia kwa kweli ni neno la ALLAH ambalo halijawahii kubadilishwa au kuletewa ushindani. Qurani inashuhudia ukweli huu, kwamba hapana mabadiliko katika maneno ya ALLAH.

Ushahidi wa kuunga mkono usahihi wa Biblia ni mwingi zaidi ya uvuli wowote wa shaka. Qurani inatupa ushahidi , Ndungu yangu Muislamu , unaushuhudia ukweli kwamba , Taurati ni kitabu kilicholetwa kutoka kwa Mola wetu mlezi kwa bwana wetu Musa, kuwa muongozo na rehema kwa walimwengu.

‘Hakika sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru…
Q 5:44

Ni wazi kuwa Taurati imetoka kwa BWANA:

‘Sema : Nani aliyoteremsha kitabu alicho kuja nacho Musa, 
chenye nuru na uwongofu kwa watu.’ Q6:9


Pasi na shaka ni wazi kuwa Taurati tumepewa kutoka kwa BWANA wetu MLEZI. Mwenyezi .

‘Na hakika tulimpa Musa kitabu na tukafuatisha baada yake 
Mitume wengine” Q 2:7

Ni vyema tukumbuke kwamba Taurati aliyokabitiwa Musa:imeitwa “kitabu”

‘Na tulipo mpa Musa kitabu na pambanuo (baina ya haki na 
baatili) ili mpata kuongoka.’’ Q 2:53


Hapo pia pana kiashiria ina ukweli kwamba. Taurati alipewa Musa (kitabu na kipambanuzi) Al – Baidwawi anasema katika ufafanuzi wa aya hii: 
(Yeye ni miongoni mwa wafafanuzi wazuri na wanaokubalika) kwamba pambanuo inamaanisha kwamba Taurati iljumuisha maana ya kitabu kilicho weka utofauti bayana baina ya halali na haramu, haki na baatili.

“Na kwa yaini tuliwapa Musa na Haaruni kipambanuzi na 
mwangaza, na makumbusho kwa wachamungu” Q 21:48


Al – Baidwawi alisema katika ufafanuzi wake kwamba Taurati ni mwangaza, ni nuru ya kuwaongoza watu wafuate njia ya kheri kuwatoa kwenye kufa moyo na ujinga wa kutofahamu, kuwaongoza watu kwenye kweli ambao ndio utakaowaokoa.


MUKHUTASARI: Ni bayana kwetu , ndungu yangu Muislamu, kutokamana na ufafanuzi huu wote , kwamba Taurati ni kitabu alichopewa Musa na Mola mlezi kama mwongozo, nuru na rehema kwa ulimwengu. Kwa maana hiyo: kwa kuwa Taurati ililetwa na ALLAH.(Quran inapeana ushahidi wa kutosha). Basi ni wazi kuwa Taurati ni maneno ya ALLAH mtukufu.

“Na tulikwisha andika katika zaburi – nacho ni kitabu cha David baada ya Taurati kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema wapate kuitengeneza na kuusahilisha njia za maisha bora humo.” 
(Bali wenye upole watairithi nchi.” Zaburi 37:11 

wenye haki watairithi nchi, nao watakaa humo milele.” Zaburi 37:29


Na sasa kwako ndungu yangu Muislamu, huu hapa ushahidi wa Qurani, unaoshuhudia kwamba zaburi alipewa Nabii Daudi.


‘Na hakika tumewafadhilisha baadhi ya manabii kuliko wengine; na Daudi tulimpa zaburi.’ Q 17:55

“Na hakika tulikwisha andika katika zaburi baada ya kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema.’’21:105



MUKHTASARI: Ni wazi sasa kwako ndungu yangu Muislamu, kwamba Mwenyezi Mungu amepeana Zaburi kwa mja wake Daudi na ALLAH ( Qurani inashuhudia jambo ili) hivyo basi Zaburi ni neno la ALLAH.


Sasa ndungu yangu Muislamu, ukweli huko bayana kwamba injili pia ililetwa kutoka kwa ALLAH wa Bwana wetu Isa Massihi kuwa nuru mwongozo na mfano kwa wachamungu.

‘Na wahukumu watu wa injili kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu ndani yake.’ Q 5: 47


Na huu ndiyo ushahidi wa ukweli kwamba kila kilichomo ndani ya injili kilipeanwa na Bwana wetu.


“ Na sisi tuliwaamrisha wafuasi wa Isa yaani . Watu wa injili , wakristo, wahukumu kwa hukumu alizo teremsha mwenyezi Mungu. Na wasio hukumu kwa musibu wa alivyo teremsha Mwenyezi Mungu basi hao wameiacha sharia ya mwenyezi Mungu, ni waasi.”

“Amekuteremshia kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili Kabla yake, ziwe uwongofu kwa watu. Na akateremsha Furqani (Upambanuo)”



Kutokamana na ushahidi huu, ni bayana kuwa injili imetoka kwa Bwana kuongoza ulimwengu wote kama vile Qurani ilivyotambua Taurati na Biblia kuwa kipambanuzi. Ni vyema pia kutambua usawa uliopo baina ya Taurati , Injili na Quran 


“Enyi watu wa kitabu, mbona mnabishana juu ya Ibrahim, na hali Taurati na Injili hazikuteremshwa ila baada yake” Q3: 65


Twaweza kuona kwa uhakika, jinsi gain ilivyo bayana kwamba Taurati na Injili zote zilipeanwa na ALLAH.


“Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati , na tukampa injili ilyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayo. Sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachamungui.’’ Q 5:46


Kwa mara nyingine tena, twaona kuwa injili aliyopatiwa kwa bwana wetu Isa iwe muongozo na nuru.



‘Tena tukafuatisha nyuma yao mitume wengine, na tukamfuatisha Isa bin Mariamu, na wengine tukampa injili. Na tukajaalia katika nyoyo za waliomfuatia upole na rehema.”


Tena kwa mara nyingine Quran inatuakikishia kuwa injili imetolewa kwa Allah kwa Bwana wetu Issa


MUKHUTASARI: Kutokamana na haya yote, ni wazi kwetu sote ndungu yangu Muislamu, kwamba injili imepeanwa na ALLAH mtukufu, kwa bwana wetu Issa kama mwongozo na nuru ya ulimwengu . Na hivyo basi kwa kuwa injili ni kitabu kilichopeanwa na ALLAH.( Quran inashuhudia hili) hivyo basi injili ni neno la Allah.

Ndungu yangu Muislamu, hapa pia utapata ushahidi mwingi zaidi kuhusu uhalali na usafi wa Biblia Tkatifu ( Taurati, Zaburi na injili katika sehemu zake zote.

“Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.” Q 16:43

“ Tungependa tungeli wateremshia kutokamana na aya hizi mbili za Bwana wetu mlezi kwa yeyote yule muisilamu ni wazi kuwa:

1.Unabii wote kutoka kwa ALLAH ambao ulipewa kwa hao watu wa Mungu kabla ya Muhammad kwa kweli na bila shaka ulitoka kwake Allah. Mola wao. Zingatia neno,Kabla yako ewe Muhamad na vilevile neno ‘uliopewa wewe ewe Muhammad.

2.Kwa kuwa Musa na Daudi ni miongoni mwa manabii wakuu walioshi kabla ya Muhammad vitabu vyao vilitoka kwa Mola mlezi. Na kwa vile Musa alihubiri Taurati, Daudi Zaburi na Isa Injili , vitabu hivi vitatu vitakuwa vimetoka kwa ALLAH.

3. Neno “Alipewa” linammanisha kwamba yote waliyopewa yalikuwa ni maneno ya ALLAH kwa maana hiyo;Taurati Zaburi na Injili vyote ni maneno ya ALLAH mtukufu.


“Hakika sisi tumekuletea wahyi wewe kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Natulimpelekea wahyi Ibrahim na Ishmail na Is – haka, na Yaakub na wajukuu zake, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daudi tukampa Zaburi” Q 4 :163

Kutokamana na haya twaweza fikia hatima hii:

a. Maneno yaliyoshushwa kutoka kwa ALLAH kwa Muhamad yalikuwa sawa kama yale ya Nuhu na manabii wengine waliomfuata (kumbuka na zingatia neno uliyopewa ewe Muhammad)
b. Kwa vile Musa Daudi na Isa wote walikuja baada ya Nuhu, mafundisho yao yalitoka kwa Mola wao Mlezi .Ivyo pia vitabu vyao vyote (Taurati, Zaburi na Injili) yalitoka kwa Mola kulingana na uisilamu yalikuwa ni maneno ya ALLAH yaliyopewa kwa Musa , Daudi na Isa.


MUKHTASARI: Kutokamana na haya, ni wazi kwa Muisilamu yeyote kwamba Qurani kwa bayana inatangaza kwamba Biblia Takatifu (Taurati, Zaburi na Injili) imetoka kwa mwenyezi Mungu. Tazama (Q 26: 3:16:43, 4:163)


Ndungu yangu muisilamu haya ndiyo majina ya sifa ya Taurati na Injili kama yalivyotajwa ndani ya Qurani :

1. Qurani inavipa Taurati na Injili jina la “KITABU”

“Sema:Enyi watu wa kitabu! hamna lenu jambo mpaka muishike Taurati na Injili na yote mlio teremshiwa kutokamana na Mola wetu mlezi.” Q 5:68
“Ewe mtume! Waambie watu wa kitabu (yaani Biblia). Hakimka ninyi hamtakuwa mnafuata dini sahihi ila mtazitangaza hukumu zote za Qurani”
Q 25:63

“Wala msijadiliane na watu wa kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa.”Q 29:46


“Enyi mlio pewa kitabu ! Aminini tuliyo yateremsha yenye kusadikisha yale mliyo nayo” Q:4:47


“Watu wa kitabu wanakutaka uwateremshie kitabu kutoka mbinguni. Q 4 : 153

Kutokamana na haya twaona wazi kuwa Qurani inaipa Taurati na Injili neno ‘kitabu” ushahidi huu unaungwa mkono pale Qurani inapowatambua wayahudi na wakristo kama “Watu wa kitabu” neno ambalo limerejelewa mara 20 ndani ya Qurani.


2. Qurani inaipa Taurati na Injili sifa ya kuitwa “Dhikr”(Ujumbe wa Mungu)


“Na kabla yako hatukuwatuma watu ila wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye kumbukumbu ikiwa ninyi hamjui” Q 21:7


Nukuu hii imetajwa katika ufafanuzi wa AL-Jalaleen (uk357) akihitimiza kuwa Qurani inatambua Taurati na Injili kama ‘Al-Dhikir’


MUKHUTASARI: Maneno haya “kitabu” na “Al-Dhikir” ni majina ambayo pia Qurani inajitambua kwao.Kwa kuwa Qurani inaipa Biblia Takatifu jina lilelile lake, huu ni ushahidi tosha kwamba Taurati na Injili vimetoka kwa Bwana Mungu.


“Amekuteremshia kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyokuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili. Q 3:3


Haya yote yana dhihirisha wazi kuwa Qurani inatambua Taurati na Injili kuwa na uongozi , nuru, Rehema na Ufunuo.Qurani pia inatuhakikishia kuwa Taurati na Injili vimetoka kwa Mola wetu mlezi



UHAKIKA KUTOKA KWA QURANI:

1. Taurati, Zaburi na Injili vyote ni vitabu vya kibinguni tulivyo pewa na Mola wetu mlezi (Q5:46,17:55,3:3)
2. Taurati, Zaburi na Injili vyote ni sawa sawa na Qurani. (Q 16: 43, 4:163)
3. Qurani vilevile inatambuliwa kwa majina yaleyale ya Taurati na Injili (“kitabu” na “Al – Dhikir) Taz Q 21: 7, 20:99,113
4. Qurani inaelezea kuwa Taurati na injili ni vitabu vitakavyostahiki kuwa vitabu vya mwenyezi Mungu.

Kutokamana na haya yote, Ndungu yangu muisilamu, twaona wazi kuwa Qurani inanakiri kuwa Biblia Takatifu ( Taurati, Zaburi na Injili) ni maneno ya Mungu mkuu.

Huenda kweli utakubali kuwa Biblia Takatifu (Taurati,Zaburi na Injili) ni neno la Mola mlezi kwa kuwa Qurani inashuhudia jambo hilo. Lakini unaweza kusema kwamba baadaye imefanyiwa mageuzi na kubadilishwa. Pia waweza kuwa na fikira kama za ndungu zetu wengine kuwa kweli Taurati ni kitabu kilichotoka kwa Mola wetu kwa kuwa Qurani inashuhudia hilo, lakini Taurati ilifanyiwa mageuzi baada ya Musa na kwa sababu hiyo Mola wetu akampa Injili bwana wetu Isa mwana wa Mariamu. Hata hivyo watu hawa husema pia kwamba injili nayo imefanyiwa mageuzi na ndio maana Allah akaleta Qurani kuwa ukurasa wa Mwisho wa ufunuo wake.

Ebu nikwambie ndungu yangu muisilamu , kwamba Qurani yenyewe inashuhudia ukweli kwamba hapakuwa na mageuzi au mabadiliko yoyote katika maneno ya ALLAH baada ya kupitiwa Musa , Daudi na Isa.

“Hakika sisi ndio tulio teremsha ukumbusho huu na hakika sisi ndio tutaoulinda” Q 15:9

Nukuu hii inadhihirisha bayana kuwa Taurati na Injili vyote vimetoka kwa Allah na vimelindwa bila mabadiliko yoyote. Waweza ukadhani ndungu yangu muisillamu;kwamba Qurani ndiyo inayo ashiria kinapotajwa kitabu kitakatifu (Al – Dhikr) wala za Taurati na Injili. Lakini tukumbuke kuwa Qurani yenyewe ndio iliyo vipa kitabu hivi viwili sifa ya Al – Dhikr.”

“Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema” Q 21: 105

Ni wazi kwako sasa kwamba kitabu kitakatifu (Al – Dhikr) kinamaanisha Taurati na wala sio Qurani: ushahidi ukiwa kwamba Zaburi imekuja baada ya Taurati, wala sio baada ya Qurani.

“Na kabla yako hatukuwatuma watu ila wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye kumbukumbu ikiwa ninyi hamjui.” Q 21: 7


Wataalamu na wanavyioni akiwemo Al – Jalaleen (uk 357) na Ibn Kathir (uk 502) wanashikilia maoni kuwa watu waliotajwa katika Al – Dhikr ni wayahudi na wakristo. Sasa utakubaliana nami, ndungu yangu muisilamu, kwamba Taurati na Injili vimetolewa kwa Allah na vyote vimelindwa kutokamana na mageuzi na mabadiliko yoyote yale.

MUKHTASARI: Sote twatambua wazi kwamba Qurani inashuhudia ukweli kwamba hapajakuwa na mabadiliko katika maneno ya Allah na kwamba Biblia ( yaani Taurati, Zaburi na Injili) ni neno la ALLAH kama tulivyotibitisha kwa aya mbalimbali za Qurani.

HATIMA:

Maneno ya Allah yaliyokuja katika Biblia yamesalia bila mageuzi au mabadiliko, kama vile kila muisilamu mwenye ujuzi wa kitabu awezavyo kuona. Kwa hivyo ndungu yangu muisilamu unaposema hata sasa kuwa Biblia ( Taurati, Zaburi na Injili) vimechafuliwa na kufanyiwa mabadiliko; kwa maneno mengine unasema hivi:

1. Qurani sio sahihi

Ni wazi kuwa Qurani inatuhakikishia kuwa maneno ya Mola wetu mlezi hayabadiliki ila bado wewe washikilia kuwa Biblia Takatifu imefanyiwa mabadiiko.

2. Allah anadhunishwa

Kwa kuwa unaashilia kuwa ALLAH alishindwa kuyalinda maneno yake, ingawaje Qurani imeshuhudia kwamba hapatakuwa na mabadiliko katika maneno ya Allah.

3. Qurani imefanyiwa mabadiliko

Ikiwa Biblia Takatifu (Yaani Taurati, zaburi na Injili vimewahi kubadilishwa; waeweze kufikria kinachoweza kufanyika kuhusiana na Qurani Takatifu.

Ebu nikuuleze swali ewe ndungu yangu muisilamu , ikiwa kweli iliwezekana Biblia Takatifu kufanyiwa mabadiliko: Je mabadiliko haya yalifanywa lini? Je ilikuwa kabla au baada ya kuja uisilamu? Ikiwa undisi kwa mageuzi haya yalifanywa kabla ya uisilamu; Je inakuwaje basi kwamba Qurani inashuhudia na kuisifu Taurati na Injili? Badala ya mashambulizi kutoka kwa Qurani kuhusu Taurati na Injili hapana chochote ila sifa na kuvitakasa.

Ndungu yangu Muisilamu, sote twaweza kuona wazi kuwa ni yule mtu asiyekuwa na ujuzi wa Qurani tu awezaye kuwa na mawazo kama hayo ; kwani pamekuwepo na ushahidi mwingi wa kuthibitisha kwamba Biblia Takatifu ilikuwepo kabla na hata baada ya kuja ka uisilamu na imebakia vile vile bila mageuzi au mabadiliko.

“Na huwaje wakufanye wewe hakimu nao wanayo Taurati yenye hukumu za mwenyezi Mungu? Q 5:43

Utagundua kwamba kuna tukio la kiajabu lililotokea zamani za Nabii Muhammad ( Tazama Ibn Kathir, uk 517-518).

Inasemekana kwamba kundi la wayahudi walikuja kwa Mtume Muhammmad wakimtaka kuhukumu baina ya wawili mume na mwanamke walioshikwa katika tendo la zinaa. Mtume akawaamuru wairejelee Taurati. Walipojaribu kuificha sehemu iliyotaja kwamba adhabu ya wazinifu ni kuuwawa kwa kupigwa mawe , mtume Muhammad alitambua hiana zao na akawaingiza waifuate Taurati. Hivyo basi wale wazinifu wawili wakapigwa mawe hata kufa.Huu ni ushahidi bayana kwako ndungu yangu muisilamu, kwamba Taurati ilikuwa bado haijachafuliwa wala kufanyiwa mageuzi.

“Sema Enyi watu wa kitabu! Hamna lenu jambo mpaka muishike Taurati na Injili na yote mlioteremsiwa kutoka na Mola wenu mlezi.”Q 5:68

“Ewe mtume! Waambie watu wa kitabu (yaani Biblia) hakika nyinyi hamtakuwa mnafuata dini sahihi ila mtapo zitangaza hukumu zote za Taurati na Injili ni mkazitenda.”

Tazama Ibn Kathir, uk 535. Utaona kuwa Taurati na Injili sote zilikuwepo sawia na Qurani na bila mabadiliko yeyote.Laiti sivyo, basi Qurani isingeli wataka wayahudi na wakristo wote pamoja, waambatane, waishike na waifuate Taurati na Injili.

“Na wahukumu watu wa Injili kwa yale aliyoteremsha mwenyezi Mungu ndani yake na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha mwenyezi Mungu, basi hao ndio wapotofu.’

Tena tazama Ibn Kathir uk 523 utagundua kwamba Quraniiliwaamurisha wakristo wajihukumu kwa hukumu za Biblia maishani mwao. Litakuwa jambo lisilo wezekana kwa Qurani kuagiza jambo ili ikiwa Biblia yenyewe imefanyiwa mageuzi ya namna yeyote wakati wowote.

“Huwaoni wale waliopewa sehemu ya kitabu? Wanaitwa kukiende kitabu cha mwenyezi Mungu ili kuwahukumu baina yao; kasha baadhi yao wanageuka wanakikataa” Q3:23

Swali la muhimu hapa, ndungu yangu muisilamu ni hili: Inamkinikaje, inawezekanaje kwa Qurani kuwataka Wayahudi wairejee Taurati ili wapate hukumu ya Mumgu ? Lazima sote tukubaliane kwamba haiwezekani jambo ili ikiwa Taurati ingelikuwa kweli imegeuzwa na kwamba mabadiliko haya yalikuwepo hata zamani za uteremsho wa Qurani.

Ukweli kuwa Qurani inawaita wayahudi na wakristo kufuata hukumu za Taurati na Injili mtawalia , ni ishara na ushahidi mwingine kuonyesha kuwa Taurati na injili havijafanyiwa mabadiliko . Mwana historia Al – Badwawi amenakiri kuwa mtume Muhammad alikuwa na mazoea ya kutembelea shule za wayahudi ambamo Taurati ilifundishwa. Wakati mtufulani (Naiem bin Amir) alipomuuliza kuhusu, imani ipi aliyoishika alijibu “Mimi n ijitolea Ibrahimu na Taurati”
“Enyi mliopewa kitabu! Aminini tuliyoyateremsha yenye kusadikisha yale mlio nayo” 
Q 4:47 

Hapa utaona kuwa Ibn Kathir aliufikia ule uelekevu kwamba Qurani inaiunga mkono Taurati na injili.

“Na aminini ndiyo yateremsha ambayo yanasadikisha ndiyo nayo” Q 2: 41

“Kisha akakujieni mtume mwenye kusadikisha mliyo nayo” Q 3:81

“Na wanapo ambiwa: Yaaminini aliyo yateremsha mwenyezi Mungu. Wao husema tunaamini tuliyo teremshiwa sisi na kuyakataa yasiyo kuwa hayo. Na hali yakuwa hii ndiyo haki inayo thibitisha yale waliyo nayo wao” Q 2:91

Kwa mara nyingine Ibn Kathir uk 89, utagundua kuwa Qurani inashuhudia ukweli na usafi na usahihi wa Taurati na injili jambo ambalo lisingeli wezekana ikiwa vingekuwa vimechafuliwa.

Pia pana maelezo mengi tofauti tofauti ya mwanawachuoni Ibn Kathir akipeana matukio kadhaa yanayoonyesha jinsi gain mtume Muhammad alivyoenzi na kuvutiwa na Taurati na Injili katika zama zake duniani.

“Na ukiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao kitabu kabla yako.”

Vilevile Al – Baidhawi alihitimshwa pale Qurani iliponakiri “ Na ukiwa unayo shaka (ewe nabii Muhammad) Waulize wale wasomao kitabu kabla yake (yaani wayahudi na wakristo)

Nasi pia twafika hatima hiyo kwamba Taurati na Injili vyote viwili vilijulikana na nabii Muhammad na vilikuwa salama kutokamana na mageuzi na mapinduzi , Natumai sasa, ndungu yangu muisilamu kwamba wakubaliana nami kwamba Taurati na Injili havijawahi fanyiwa machafuko, mageuzi au mapinduzi yoyote yale wakati wowote kabla ya uisilamu, zama za nabii Muhammad wala hata baada ya kuja kwa uisilamu duniani.

HATIMA YA UTAFITI

Taurati na Injili zote zilikuwepo ulimwnguni zamani zile alipokuwa analetewa mtume Muhammad Qurani tukufu na vilikuwepo bila ya mabadiliko ushahidi wa haya ni kama ufuatavyo:

1. Nabii wa Uisilamu (Muhammad) aliwataka Wayahudi wairejeree Taurati iwe kitabu cha kuhukumu baina ya wayahudi (Tazama Q 3:23) Ni wazi kuwa mtume asingeli pendekeza watu wairejeree Taurati na Injili ambavyo vimekorogwa.
2. Qurani inawangaa wayahudi ambao licha ya kutoiamini Quarini walijaribu kuitumia kama hakimu kwao. Niwazi kuwa mtume Muhammad aliwashangaa , na kwa kuwa alikubali Taurati basi aliwataka waitumie Taurati kama hakimu wao, kwani ndani yake mna uongofu na mwelekeo. Q: 47 – 52

3. Kwa kuwa nabii wa uisilamu aliwataka watu wa injili (yaani wakristo) waamini kila kitu kilichokuja ndani yake na waifuate (Qu 5:47) Na wazi pia kuwa mtume Muhammad asingali pendekeza wakristo wakirejeree kitabu kilicho korogwa na kubadilishwa. Huu ni ushahidi tosha wa kuthibitisha kuwa injili ilikuwa safi kipindi cha kuteremshwa Qurani.

4. Wakati Nabii wa uisilamu aliposisitiza ya kwamba wayahudi na wakristo wote waishike Taurati na Injili, kwa kuzingatia hukumu zilizokuja ndani yake (Tazama 54:5 2-52. Je wadhani hata kiufupi tu, kwamba mtume Muhammad angalifanya haya ikiwa Taurati au Injili zingelikuwa zimekorogwa na kubadilishwa?

5. Ukweli ni kwamba Qurani inatupa ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa Taurati na Injili view safi na bila dosari yeyote. (Tazama Su 3:81, 5: 47 – 52, 4:47 na Qu 2: 89-91)

6. Qurani ilimshauri mtume wa uisilamu kutafuta msaada kutoka kwa watu wasomao Taurati na Injili wakati wowote akiwa na shaka yeyote katika maswali ya dini. (Ikiwa unayo shaka ewe Muhammad.)hauwezi kamwe kupendekeza kuwa Allah angemshauri mtume wake kwenda kwa watu wenye kitabu kilicho korogwa na kubadilishwa. Au jee waweza kupendekeza kinyume?Je angemrejesha katika Taurati na Injili zilizo badilishwa tayari?

7. Qurani yenyewe inawataka wayahudi na wakristo wawe na imani katika Taurati na Injili.

“Enyi mlio amini !Muaminini mwenyezi Mungu na mtume wake, na kitabu alicho kiteremsha juu ya mtume wake, na kitabu alichokiteremsha kabla yake. Na anaye mkataa mwenyezi Mungu, na malaika wake, na vita vyake, na mitume wake, na siku ya kiyama, basi huyu amekwisha potelea mbai.” Q 4: 136

Ni jambo la kushangaza na wala haliingi akilini kwamba Qurani itawataka waislamu waiamini Biblia ilyoteremshwa kabla ya Qurani kama Biblia ingelikuwa sio kitabu chenye haki. Huu ni ushahidi kamili wa usafi na ukweli na uhakika wa Biblia, kwani Qurani isingeliwataka waislamu waiamini ikiwa ingelikuwa imebadilishwa na kugeuzwa

Sasa basi ni wazi kwako ndungu yangu muisilamu, baada ya utafiti huu wote na ushahidi huu kutoka kwa Qurani; ni dhahiri na zaidi ya uvuli wowote wa shaka kwamba Taurati na Injili vilihifadhiwa katika zama za kuteremshwa Qurani (kwa kuwa Qurani imetupa ushahidi huo) mageuzi yalifanywa baadaye wakati mwingine.Wacha nikwambie ndungu yangu, kwamba Qurani yenyewe inakanusha jambo hili kwa sababu zifuatazo.

1.Katika Su 5:48 inasaema:
“Na tumekuteremshia wewe wa haki, kitabu hichi nacho sadikisha yaliyokuwa kabla yake katika vitabu na kuyalinda”

Maana ya “kuyalinda” ni kuwa maandiko ya Mungu yatasalia na kuwa salama kutokamana na mabadiliko na mageuzi na kukologwa.Inamaana wazi kuwa ikiwa Taurati au injili vimebadilishwa baada ya Muhammad au Qurani ni kusema kuwa Qurani ilishindwa katika kazi yake kama “mlinzi” juu ya Taurati na injili kwa maneno mengine ikiwa Taurati na injili vilibadilishwa baada ya kuteremshwa Qurani, basi watu wa Qurani wameshindwa kuhifadhi kulinda na kuchunga angalau nakala moja au zaidi ya Taurati na injili safi kama mlinzi juu yake.

Wakati wakristo walipotambua kwamba Taurati ina aya nyingi zilizomhusu masihi Yesu, walichukua jukumu la kuwa walinzi wake, na wakaisambaza Taurati na injili kote ulimwenguni. Imekadiliwa kuwa Taurati imetafsiriwa karibuni lugha zote zinazo julikana na wanadamu.Kwa nini basi waisilamu hawakufanya kazi kama hii kwani waliamini kuwa Taurati na Injili ilikuwa na aya nyingi tu zinazo mhusu mtume Muhammad na Qurani?

2 Kwa kuwa tayari tumethibithisha ukweli kwamba Taurati na injili vilihifadhiwa safi kutokamana na mageuzi yeyote zamani za uteremsho wa Qurani: basi ili litatupeleka kufikia hatima hii:

3a) Wakristo wa kweli – zamani za uteremsho wa Qurani walihifadhi nakala ya Taurati maana ndani yake mlikuwepo maandiko mengi yaliyomhusu Yesu na injili.Zaidi ya hayo Yesu mwenyewe alishuhudia usafi na uhaki wa Taurati. Pia imenakiriwa ndani ya Qurani:

“Natuka wafuatisha haio Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati , na tukampa injili iliyomo ndani yake uwongofu na nuru na inayo sadikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachangamfu.’ Q 5:46

Hivyo basi ikiwa kuwa vyovyote vile wayahudi wahgelijaribu kubadilisha Taurati, wakristo wangegundua hilo na kutambua mageuzo hayo mara moja kwani walihifadhi nakala halisi ya Taurati.

b) Vilevile kwa mawazo yaleyale, ikiwa wakristo nao wangeli jaribu kubadili chochote ndani ya Taurati , wayahudi wasingeli



8. Qurani yenyewe inawataka wayahudi na wakristo wawe na imani katika Taurati na Injili.

“Enyi mlio amini !Muaminini mwenyezi Mungu na mtume wake, na kitabu alicho kiteremsha juu ya mtume wake, na kitabu alichokiteremsha kabla yake. Na anaye mkataa mwenyezi Mungu, na malaika wake, na vita vyake, na mitume wake, na siku ya kiyama, basi huyu amekwisha potelea mbai.” Q 4: 136

Ni jambo la kushangaza na wala haliingi akilini kwamba Qurani itawataka waislamu waiamini Biblia ilyoteremshwa kabla ya Qurani kama Biblia ingelikuwa sio kitabu chenye haki. Huu ni ushahidi kamili wa usafi na ukweli na uhakika wa Biblia, kwani Qurani isingeliwataka waislamu waiamini ikiwa ingelikuwa imebadilishwa na kugeuzwa

Sasa basi ni wazi kwako ndungu yangu muisilamu, baada ya utafiti huu wote na ushahidi huu kutoka kwa Qurani; ni dhahiri na zaidi ya uvuli wowote wa shaka kwamba Taurati na Injili vilihifadhiwa katika zama za kuteremshwa Qurani (kwa kuwa Qurani imetupa ushahidi huo) mageuzi yalifanywa baadaye wakati mwingine.Wacha nikwambie ndungu yangu, kwamba Qurani yenyewe inakanusha jambo hili kwa sababu zifuatazo.

1.Katika Su 5:48 inasaema:
“Na tumekuteremshia wewe wa haki, kitabu hichi nacho sadikisha yaliyokuwa kabla yake katika vitabu na kuyalinda”

Maana ya “kuyalinda” ni kuwa maandiko ya Mungu yatasalia na kuwa salama kutokamana na mabadiliko na mageuzi na kukologwa.Inamaana wazi kuwa ikiwa Taurati au injili vimebadilishwa baada ya Muhammad au Qurani ni kusema kuwa Qurani ilishindwa katika kazi yake kama “mlinzi” juu ya Taurati na injili kwa maneno mengine ikiwa Taurati na injili vilibadilishwa baada ya kuteremshwa Qurani, basi watu wa Qurani wameshindwa kuhifadhi kulinda na kuchunga angalau nakala moja au zaidi ya Taurati na injili safi kama mlinzi juu yake.

Wakati wakristo walipotambua kwamba Taurati ina aya nyingi zilizomhusu masihi Yesu, walichukua jukumu la kuwa walinzi wake, na wakaisambaza Taurati na injili kote ulimwenguni. Imekadiliwa kuwa Taurati imetafsiriwa karibuni lugha zote zinazo julikana na wanadamu.Kwa nini basi waisilamu hawakufanya kazi kama hii kwani waliamini kuwa Taurati na Injili ilikuwa na aya nyingi tu zinazo mhusu mtume Muhammad na Qurani?

2 Kwa kuwa tayari tumethibithisha ukweli kwamba Taurati na injili vilihifadhiwa safi kutokamana na mageuzi yeyote zamani za uteremsho wa Qurani: basi ili litatupeleka kufikia hatima hii:

3a) Wakristo wa kweli – zamani za uteremsho wa Qurani walihifadhi nakala ya Taurati maana ndani yake mlikuwepo maandiko mengi yaliyomhusu Yesu na injili.Zaidi ya hayo Yesu mwenyewe alishuhudia usafi na uhaki wa Taurati. Pia imenakiriwa ndani ya Qurani:

“Natuka wafuatisha haio Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati , na tukampa injili iliyomo ndani yake uwongofu na nuru na inayo sadikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachangamfu.’ Q 5:46

Hivyo basi ikiwa kuwa vyovyote vile wayahudi wahgelijaribu kubadilisha Taurati, wakristo wangegundua hilo na kutambua mageuzo hayo mara moja kwani walihifadhi nakala halisi ya Taurati.

b) Vilevile kwa mawazo yaleyale, ikiwa wakristo nao wangeli jaribu kubadili chochote ndani ya Taurati , wayahudi wasingeli kubali na wangewazuia mara moja kwa tendo la kuleta nakala halisi ya Taurati.

c) Vilevile, kama wayahudi wangelijaribu kubadilisha injili, wakristo wangali wazima kwa kuileta nakala safi na halisi ya injili.

4. Ni –bayana kuwa uisilamu asilia kama ulivyo, umekuja karibuni miaka 570 baada ya ukristo. Wakati wa kabla ya uisilam, zama za ujinga, ukristo ulikuwa umezaenea takriban kote ulimwenguni ikiwemo Afrika , uabeshi, Irani, India na Uropa.

Hii ilipelekea ugumu kwa watu wa sehemu moja ulimwenguni kubadilisha injili kuwa kazi nzito na isiyo wezekana.

5. Na sasa ndungu yangu muisilamu, lazima tujiulize wenyewe basi: Ni lini ni wapi mageuzi hayo yalifanywa? Ni nani aliyeyafanya mageuzi hayo?Hakuna yeyote ambaye anaweza kutoa na kuthibithisha jina hata moja tu la mwana historia. Myahudi au mkristo anayeweza kudhihirisha jambo hilo.Tena kama basi mageuzi na mabadiliko yeyote yalifanywa kwa makubaliano ya makundi yote mawili, wayahudi na wakristo; basi itakuwa ina maana pana mgongano, kwani Qurani inashuhudia kwamba – Hapana mabadiliko katika maneno ya Allah.

“Nasoma uliyofunuliwa katika kitabu cha Mola wako mlezi. Hapana awezaye kubadilisha maneno haya.”Q 18 :27

Hapana shaka kwamba neno “kitabu” lililotajwa katika ayah ii inaashiria Qurani lakini tamko Maneno yake” Yanaashiria Biblia Takatifu (Yaani Taurati, Zaburi na injili). Vitabu hivi vyote ni maneno ya Allah na tunaamini hapana yeyote awezaye kubadilisha maneno yake.

“Hapana mabadiliko katika maneno ya mwenyeziMungu.” Q 10:64

“Na hakuna abadilishaye maneno ya mwenyezi Mungu.”

HITIMISHO:

1. Biblia (Taurati, zaburi na injili) ni neno la Allah alilopeana Allah kwa waja wake, mitume kabla yenu injili ni mwongozo, nuru na rehema kwa ulimwengu.
2. Qurani anajenga usawa baina yake na Biblia (Yaani Taurati, Zaburi na Injili) kwani zote zililetwa na Allah kwa wajumbe wake kabla yenu.
3. Qurani inajipa jina la sifa kama lile lile inaloipa Biblia – Yaani “kitabu”
4. Maneno ya Allah yaliyopeanwa kwa wajumbe wake yalisalia hivyo na wala bado hayajafanyiwa mabadiliko

“Hakika sisi ndio tulioteremsha ukumbusho huu na hakika sisi ndio tutao ulinda” Q 15 : 9
5. Biblia Takatifu ilikuwepo kipindi ambapo Qurani inateremshwa. Ushahidi ni kuwa , mtume Muhammad aliwataka wayahudi wailete Taurati kuwa hakimu katika mjadhalo baina yao.
6. Ni jambo la kustaajabisha kudhai kuwa kitabu chochote katika vitabu vitakatifu vya mwenyezi Mungu mlezi viliwahi kufanyiwa mabadiliko kwani ukweli ni kwamba Taurati na injili vilikuwa vimekwisha tapakaa kote ulimwenguni katika lugha mbali mbali.

NDUNGU YANGU MUISILAMU:

Utafiti huu wote unaungwa mkono na maandiko na dalili kutoka kwa Qurani na pia unaungwa mkono na mabingwa miongoni mwa wanavyuoni wakubwa w kiislamu kama vile Ibn Kathir, Al – Baidhwawi, Al – jalaleen na Al – Bukhari.

Nimeenda umbali huu wote ili kumfanya kila muisilamu wa kweli atosheke kuwa utafiti huu ulifanywa katika uwazi na ukweli. Nimekuwa mwangalifu kutumia Qurani kama haswa kitabu rejeshi ili kukuhakikishia kwamba, wakati utakapokuwa umehitimisha kusoma utafiti huu ,utaweza kukubaliana nami kuwa, Biblia Takatifu (Yaani Taurati, zaburi na injili) vimehifadhiwa kutokamana na mageuzo yeyote au mabadiliko yeyote. Hivi vyote ni vitabu vya Allah nani maneno yake, na tunaamini hakuna yeyote awezaye kubadilisha maneno ya mwenyezi Mungu.

“ Hapana mabadiliko katika maneno ya mwenyezi Mungu” Q 10:64

“Hakika sisi ndio tulio teremsha ukumbusho huu, na hakika sisi ndio tutaolinda.” Q 15:9

Ndungu yangu muisilamu, ikiwa una maswali yeyote kuhusu haya niliyoandika au ikiwa unatamani kupata nakala yako ya Biblia Takatifu, tafadhali niandikie kwa anwani zifuatazo:

Al Shaikh Muhammad Kamal

IJUE DINI YA UISLAMU NA ASILI YAKE

Image result for origin of islam
Utangulizi

Kwa miaka mingi waislamu duniani, wanatuhimiza sana sisi Wakristo tuache imani na dini yetu, ili tuingie katika dini yao ya uislamu. Waislamu wanasema dini yao ndio ya haki, mbele ya Mwenyezi Mungu, na tena wasema manabii wote walikuwa waislamu, wanaendelea kusema kuwa hata Bwana Yesu naye alikuwa mwislamu, waislamu wanaendelea kusema kwamba dini ya Islamu haikuchukua au kurithi hata chembe (kidogo) ya tabia ya mafundisho ya ibada za kikafiri, kushirikina na ujahili (yaani ujinga), kwani wanasema Uislamu ni dini safi kuliko zote. Swali la muhimu ni hili. Je, ni kweli kwamba dini ya uislamu haikuchua tabia na mafundisho ya ibada za kikafiri, kushirikina na ujahilia? Ilikujua yote hayo fuatilia kwa makini somo hili lililoandikwa na Mwalimu wangu Mwinjilisti Kobelo na kupitiwa upya nami Mwalimu Chaka.

Sehemu kuu tano za somo

  1. Je, manabii wote walikuwa waislamu?
  2. Maana ya neno Islam.
  3. Nani aliyekuja na dini ya kiislamu?
  4. Je, dini ya kiislamu imechua ibada za waarabu za zama ujahilia (yaani ujinga)?
  5. Wajibu wa mkristo baada ya kujua Uislamu.
1. Je, Manabii wote walikuwa waislamu?
Hoja kubwa ya waislamu ni kule kutuhimiza wakristo tukubali kuwa waislamu kwa kusema kwamba manabii wote wa Mungu walikuwa waislamu, hivyo wanataka tuache imani yetu tuwe waislamu. Lakini inafaa kwanza kuvichunguza vitabu vya kiislamu kuhusu ujio wa Qurani inafundisha nini? Na je, ni nani aliyeleta dini hiyo? Qurani ya Allah Mungu kama wanavyoamini waislamu inasimulia hivi;

Qurani 6:14 Suratul An-Am (Wanyama)
Sema: hakika nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu.
Katika aya hii tunaona Muhammad ndiye mtu wa kwanza kuamrishwa asilimu.
Imesimuliwa pia ya kwamba Muhammad S.A.W. alisema, “Sisi waislamu ndiyo wa mwisho kuja” hayo tunayasoma katika Sahih Al-Bukhari vol. ix Hadithi na 587.

Muhammad vilevile aliwaambia wafuasi wake wafuate njia ya waliowatangulia. “nchi kwa nchi, hatua kwa hatua hata kama ikiwa waliingia katika shimoni mwa mjusi” masahaba zake wakauliza “Layahud waal Na-swara? Yaani wayahudi na wakristo? Akawajibu Farman? Yaani nani zaidi? Hayo tunayaona katika Sahih Muslim vol. iv katika Al-lim, hadithi na 6448. Kutokana na jibu hili la Muhammad (S.A.W.) ni dhihiri kuwa dini ya Uislamu ilitanguliwa na dini yetu Wakristo na hata ile dini ya Kiyaudi.
  1. Manabii wa Mungu Yehova walifuata dini (njia) hii.
Tunaposoma maandiko matakatifu ya Biblia yanatufundisha kuwa manabii waliongozwa na huyu.

1 Petro1:10-11

katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta tafuta na kuchunguza chunguza ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. Wakati upi na wakati wa namna gani ulioonywa na roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao.

1 wakorintho 10:1-4
kwa maana ndugu zangu,sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu. Wote wakapita kati ya bahari,wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingi na katika bahari; wote wakala chakula kilekile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata na mwamba ule ulikuwa ni kristo.

Katika aya hizi tunaona wazi wazi kuwa manabii wote waliongozwa na roho wa Kristo Yesu ambaye alikuwa ndani yao. Musa pamoja na watu wake pia walifuatwa na kristo naye aliwalisha na kuwanywesha. Wote waliongozwa na Bwana Yesu yeye mwenyewe aliwaita “watu wa Kristo” Soma Marko 9:38-41hii ni kwasababu Bwana Yesu ndiye kiongozi wetu. Tazama Mathayo 23:9, tena Bwana Yesu ndiye njia (dini) ya kweli na uzima Yohana 14:6 hivyo manabii wote walikuwa ni watu wa Kristo kwasababu roho yake Yesu ulikuwa ndani yaoikiwaongoza.
  1. Maana ya neno Islam
Neno islam ni la lugha ya Kiarabu. Maana yake ni “Utii” au “Amani” katika Qurani neno Islam limetajwa mara 38. ijapokuwa neno Islam limetajwa mara nyingi lakini neno hilo ni tofauti na dini ya uislamu hii ni kwasababu dini a Uislamu maana yake ni kujisalimisha chini ya amri za Allah au amani chini ya sheria za Allah. Qurani ya Allah Mungu kama wanavyoamini waislamu inasimulia kumhusu Muhammad (s.a.w.) hivi.
Qurani 6:163 Suratul Al-An-Am (Wanyama)
Na haya ndiyo nilivyoamrishwa na mimi ni wa kwanza wa wanaojisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu).
Qurani 39:12 Suratul Az-zumar (Makundi/Vikosi)
“Na pia nimearishwa niwe wa kwanza wa (viumbe) wanaojisalimisha kwa Mwenyezi Mungu.”

  1. Nani aliyekuja na dini ya kiislamu?
Tunaposoma katika ufafanuzi wa aya ya 19-20 kati ka suratul Yusuf ulio ndani ya Qurani juzuu ya 12 chapa ya tatu ya kiswahili ukurasa wa 311 kuna maneno ambayo yanaelezea mtu aliyekuja na dini ya kiislamu hapa duniani na maneno yenyewe ni haya…

Unaona kwanza kulikuwako zaidi ya miaka 4000 kabla ya kuja dini ya kiislamu aliyokuja nayo Nabii Muhammad khalafu wakausingizia Uislamu kuwa ndio ulikuja na kuuza watu.

Kadiri ya ufafanuzi huu uliomo ndani ya qurani, na ushahidi wa vitabu maarufu vya hadithi za muhammad katika sahih Al-Bukhari na sahih muslim. Na vitabu mbalimbali vilivyoandikwa na masheikh wa dini ya kiislamu, inathihirika waziwazi kuwa dini ya uislamu imeletwa na kuanzishwa na Muhammad (s.a.w.) mfano mzuri wa mwanzo wa dini ya uislamu tunauona katika kitabu kiitwacho maisha ya nabii muhammad (s.a.w.) kilichotungwa na aliyekuwa kadhi mkuu wa zanzibar na baadaye nchi ya kenya marehemu sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy. Katika ukursa wa 18 kuna maneno yanayo husu mke wa muhammad aliyeitwa khadija binti khuweylid nayo yanatuhadithia hivi…

Akarejea kwa mkewe bibi khadija, akamsimulia habari hii. Palepale bibi huyu akamwamini, akawa ndiye mtu wa awali kabisa kushehedusha shahada ya uislamu. Basi mwislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke.
Katika kitabu hicho hicho cha maisha ya nabii muhammad ukurasa wa 18 kifungu c. wametajwa waislamu wa awali kabisa nao ni hawa…
(i) Mwislamu wa kwanza
Bibi Khadija bint Khuweylid
Mtume aliamrishwa kufundisha dini siku ya jumatatu na bibi huyu alisilimu siku hiyo hiyo akafanya ibada na mtume usiku ule ule kabla ya mtu yeyote ulimwenguni huyu ndiye aliyefuzu kwelikweli.
(ii) Mwislamu wa pili
Sayyidina Ali bin Abi Talib bin Abdul Muttalib
Alipomwana mtume na bibi Khadija usiku ule wanafanya mpya aliwauliza, “hii ni ibada gani?” mtume alimfahamisha na akamtaka awe pamoja nao lakini yeye alikataa kwanza akasema mpaka niende nikamshauri baba yangu”. Mtume akamkataza kuitoa siri ile nje. Mara asubuhi ya usiku ule ule, kijana huyu akaja kwa mtume akampa habari kuwa yeye yu pamoja nao. Akawa ndiye islamu wa pili duniani. Aliposilimu alikuwa kijana wa miaka 10 hivi.

(iii) Mwislamu wa tatu na wa nne.

Zayd bin Haritha Al Ka’bi na Bibi Aymana.
Huru wa mtume na mwanawe wa kupanga alikuwa akikaa pamoja na mtume na akasilimu kama sayyidina Ali mchana wa jumane. Alisilimu yeye na mkewe, bibi ummu Aymana yaya wa mtume.

Hawa wote ndio waislamu wa awali kabisa ambao walisilimu mara baada ya muhammad s.a.w. kuleta dini ya uislamu ambayo alianzisha rasmi hapa duniani jumatatu ya siku ya 17 ya mwezi wa ramadhani sawa sawa na 27th december ya mwaka wa 610 baada ya kristo. Kabla ya muhammad dini ya kiislamu haikuwepo kabisa duniani.

  1. Je, dini ya uislamu imechukua ibada za waarabu wa zama za ujahilia (yaani ujinga)?
Wakati wa ujahilia (ujinga) kabla ya dini ya uislamu makureshi ambalo ni kabila la muhammad s.a.w. na waarabu wenzao, walikuwa wakiabudu miungu mingi yapata 360 hivi. Kawaida hiyo ya kuabudu kwao miungu mingi kumesimuliwa waziwazi katika quarani na vitabu mbalimbali vya kiislamu. Vitabu hivyo vimeandikwa na masheikh na wanachuoni wengi, nitawataja baadhi yao nazo ni hawa…
(i) Maulamaa sayyid Abul A’la Maududi
Katika kitabu chake kiitwocho katika kuufahamu uislamu ukurasa wa 42-44 kuna maneno haya…”Bara Arabu mwina wa kiza wafanya biashara waarabu walijikokota masafa marefu ilikuwa vigumu kwao kupata hata chembe ya elimu wachache waliojua kusoma na kuandika walikuwa wakiabudu mawe, miti, masanamu, nyota na pepo, kwa ufupi kila kilichowapitia akilini mwao, hawakujua hata kidogo mafunzo ya mitume waliowatangulia. Walikua na dhana kuwa ibrahimu na ismail walikuwa babu zao, lakini walikuwa hawajui kitu kuhusu mafunzo yao ya dini na Mungu waliyemwabudu.

(ii) Sheik Abdullah saleh Al-Farsy ambaye alikuwa kadhi mkuu zanzibar na baadaye nchini Kenya

Katika kitabu chake kiitwacho maisha ya nabii muhammad s.a.w. ukurasa wa 6 kuna maneno haya… “Hata ilipokuwa karibu atadhihiri mtume mapadiri wa kinasara na makuhani wa kiyahudi waliokuwa wakikaa bara arabu walikuwa wakiwataharisha majirani zao wa kiarabu waliokuwa wakiabudu masanamu;
Qurani imetaja miungu mbalimbali iliyoabudiwa na makureshi na waarabu wenzao zama za ujahilia

(i) Waliabudu maandazi.

Qurani 25:43-44 Suratul Al;- furqan (Qurani)
Je umemuona yule aliyefanya matamanio yake (kile alichokipenda). Kuwa mungu wake? Basi je, utaweza kuwa mlinzi wake (ukamhifadhi) na haya, na hali ya kuwa hataki?) au je, unafikiri ya kwamba wengi katika wao wanasikia au wanafahamu? Hawa kuwa hao ila ni kama wanyama bali wao wanapotea zaidi njia.

Ufafanuzi wa aya ya 43 ulio katika qurani juzuu ya 19 ni huu, “waarabu kwa ujinga wao wa kuabudu chungu ya miungu walikuwa baadhi yao wakiona chochote kile kikawapwndeza hukiabudu hata andazi lililokaa kwa sura nzuri.
Hapa tunaona kuwa qurani inasimulia wazi wazi kwamba waarabu waliabudu hata andazi na tena ni wajinga “yaani majahalia”

(ii) kuabuduwa kwa miungu ya sanamu.
Qurani 71 22-23 Suratul Nuh (Nuhu)
Na walifanya hila kubwa kubwa za (kubatilisha dini). Na waliwaambia (wafuasi wao): “Msiache miungu yenu wala msiwaache waddi wala suwa’a wala yaghuta wala ya’uqa wala Nasra”. (Majina ya waungu wao wa kisamu).
Hii ni miungu ya uongo ya sanamu ambayo iliabudiwa na waarabu mungu waddi alikuwa na umbo la mwanamke yaghuta umbo la simba, ya’uga umbo la farasi hayo yanapatikana katika kitabu kiitwacho “history of Islam kilichoandikwa na Pro. Masudul Hassan ukurasa wa 43
(iii) kuabudiwa kwa miungu iitwayo lata, uzza na manata
Qurani 53:18-20,23 suratul An-najm
kwa yakini aliona nabii muhammad mambo makubwa kabisa katika alama (Qudra) za mola wake.je mume waona lata na uzza? Na manata mungu wenu mwingine wa tatu, kuwa ndio waungu hao badala ya mwenyezi mungu?Hayakuwa hayo majina ya lata mungu mwanamke, na uzza mungu mwanamke mwenye enzi na manata, mungu mwanamke anaye neemesha ila ni majina tu mliwapa nyinyi na baba zenu…

(iv) kuabudiwa kwa Allah (s.w.) na majahilia (wajinga)
makureshi pamoja na waarabu wenzao ambao walikuwa wakabudu miungu mingi kama tulivyoona huko juu. Vilevile miongoni mwa hiyo miungu walimuabudu Allah (S.W.) ambaye ndiye aliyekuwa mungu mkubwa, na miungu ya hata na uzza na manata wakawaitakadi kuwa mi waungu wanawake ama wake zake Allah au watoto wake. Hayo tunayaona katika ufafanuzi wa aya ya 180 katika Qurani suratul Al- A’raf na pia katika kitabu kiitwacho history of isalmu kilichoandikwa na pro masudul hasan ukurasa 43. ushahidi wa wazi zaidi wa kuonyesha kuwa waarabu majahilia walimuabudu Allah tunaupata katika vitabu vifuatavyo…

(i) kuzaliwa kwa Muhammad S.A.W. mtume wa waislamu
maombi na dua ya abdul mutalib kwa Allah.
Tunaposoma kitabu cha maisha ya Muhammad S.A.W. kilitangwa na sheikh Farsy ukurasa wa 5 kuna maneno hayo…

Pale pale alfajiri alipokwisha kuzaliwa mtume alikwenda kuitwa babu yake kuja kumwona mjukuu wake. Babu huyu alifurahi sama na akamfunika manguo mjukuu wake, na akamfunika manguo mjukuu wake, akajikongoja naye mpaka kwenye Al-ka’ba akafungua mlango akaingia ndani, akasimama, akamwombea dua kwa mashairi mazuri ya kiarabu aliyoyatunga mwenyewe wakati ule ule, kisha akarejea naye na jua bado halikuchomoza.

Ushahidi wa wazi unaothibitisha kuwa baba yake Muhammad Abdul muttalib aliomba dua kwa Allah tunaupata tunaposoma utangulizi wa suratul al-fyl ulio katika juzuu ya ukurada wa 946 Qurani iliyotafsiriwa kwa kiswahili chapa ya nane tunasoma maneno hayo. “chifu mkuu wa makka zama hizo alikuwa Abdul muttalib, alikwenda al ka’ba pamoja na baadhi ya machifu wa kikuraish na akilishika komeo la chuma la mlango wa al-ka’ba, akamwambia Allah (S.W.0 kuilinda nyumba yake pamoja na wahudumu wake. Zama hizo kulikuwa na masanamu 360 ndani na kando ya Al- ka’ba.”
(v) imani ya Abdul muttalib ilikuwa hii.

Katika kitabu kilichoandikwa na mwanachuoni maarufu wa kiislamu aitwae ale muhsin barwani ukurasa wa 153 tunasoma maneno haya; “hapakutokea mwarabu ambaye alipewa jina hilo na babu yake tangu kuzaliwa kwake, na huyo babu hakuwa mkristo bali alikuwa akifuata mila za kishirikina.” Na wala hakujua taurati wala injili.

(vi) himizo la Muhammad (S.A.W.) kwa makureshi wenzie kuhusu mungu aitwae Allah.
Katika kitabu kiitwacho mkweli mwaminifu kilichotungwa na sheikh said moosa muhamed al kindy juzuu ya mwanzo na pili chapa ya kumi ukurasa wa 130 tunadoma maneno haya: “katika wakati wa ujaahiliya kabla mtume (S.A.W.) kupata utume alikuwa akiwaambia waru “enyi watu semeni laa ilaha illah laah mtafuzu” yaani hana mola ila Allah mtafuzu.

Huu ni ushahidi wa wazi kabisa ya kwamba Allah aliabudiwa na makureshi ma waarabu wenzao hao watu walikuwa washikina , wapagni na majahilia (wajinga). Kumbuka Muhammad alikuwa ni mkureshi naye aliposema “hapana mola ila Allh” alikuwa yupo za ujahilia na hakuwa anajua kitabu wala imanitazama Qurani 42:52 Suratul shuraa.

(vii) je, mungu anayeabudiwa ba waislamu jina lake ni nani?

Qurani 17:110 suratul ban israil wana wa Israel
sema: “mwombeni mwenyezi mungu kwa jina la Allah au muombeni kwa jina la rahman kwa jina lolote mtakalo mwita katika hayo itaifaa: kwani ana majina mazuri mazuri,” wala usiiseme sala yako kwa sauti kubwa wala usiseme kwa sauti ndogo, bali shika njia baina ya hizo katikati si kwa kelele wala kimya.

Katika aya hii tunaona jina la mungu anayeabudiwa ba waislamu anaitwa Allah.Katika qurani jina hilo limetjwa mara 2,866 kumbuka kuwa makureshi na waarabu wenzao waliokuwa washirikina wapagani na majahilia wajinga kabla ya uislamu walimuabudu mungu huyo aitwae allah swali muhimu je, waislamu hawakutithi mungu wa makureshi? Tafakari kwa makini.
(viii) mji mkuu wa makureshi na waarabu wenzao zama za ujahilia ambako walikuwa wanaenda kuhiji ni huu
Tunaposoma utangulizi wa suratul Quraysh katika juzuu ya 30 ukurasa wa 950-951 chapa ya nane ya Qurani ya kiswahili kuna maneno haya…kabila la kureshi lilikuwa limetawanyika kote hijaz hadi zama za Qusayy bin kilaab mmoja wa mababu wa mababu wa mtume (S.A.W.). kwanza kabisa Qusayy aliwakusanya makureshi pamoja huko makka, na hivyo kabila hili likawa wadhamini wa Al-ka’ba kwa msingi huo, Qusayy alikuwa akiitwa mujammi mkusanyaji wa wartu wa habila lake. Mtu huyu kwa busara yake aliweza kuasisi serikali katika mji wa makka, na akaweka mipango mizuri kwa ajili ya mahujaji wajao toka kote arabuni, na matokea yake ni kuwa makureshi walipata umaarufu mkubwa miongoni mwa makabila ya kiarabu.

Hapa tunaona kuwa zama za ujahilia na upagani kabla ya dini ya uislamu waarabu wote walienda kuhiji katika mji wa makka kwenye nyumba ya Al-ka’ba inayoitwa “Bait-ullah” yaani nyumba ya allah. Kumbuka nyumba hiyo hiyo wapagani wa kiarabu zama za ujahilia (ujinga) waliabudu miungu 360 na Allah ndiye mungu wao mkuu.

Mji mkuu wa hija kwa waislamu ni huu.

Qurani 3:96 suratul Al-aal-imran (watu wa imran)
kwayakini nyumba ya kwanza iliyewekwa kwa ajili ya watu kufanya ibada ni iloe iliyoko makka, na yenye baraka na uongozi kwa ajili ya walimwengu wote.
Qurani 22:27-29 suratul Al-Hajj. (Hijja)

Na (tukamwambia “utangaze kwa watu habari ya Hijja, watakujia, (wengine) kwa miguu na (wengine) juu ya kila mnyama aliyekonda kwa machofu ya njiani wakija kutoka katika kila njia ua mbali; ili washuhudee manufaa yao na ili wakushirishe kulitaja jina la mwenyezi mungu katika diku zinazojulikana fadhila zake na juu ya yale aliyowaruzuku, nao mi wanyana wenye miguu mine. Na kuleni katika wanyama hao na mlisheni mwenye shida na fakiri. Kasha wajisafishe toka zao, na watimize hadhiri zao na waizunguke nyumba ya kale (nyumba kongwe Al-ka’ba.)
Tunaposoma ufafanuzi wa aya ya 29 ulio ndani ya Qurani katika juzuu ya 17 kuna maneno haya; “kabla ya uislamu waarabu walikuwa wakiitukuza Al-ka’ba.Na kwa ilivyokuwa ni jingo la zamani sana waliita Al-Baytul’Atiq yaani nyumba ya kale.”
Kama vile waarabu wapagani, makafiri na majahilia mji mkuu wa Hijja ni makka kule Saudi Arabia ndivyo ilivyo kwa waislamu nao mji wao mkuu ambao wanaenda kuhiji ni makka. Isitoshe Qurani inasimulia kuwa makka ni mama wa miji soma hayo katika Qurani 6:92 suratul Al- An-Am (wanyama) waislamu popote walipo duniani wanaambiwa wanaposali waelekeze nyuso zao mahali maalumu,
Qurani inasimulia hivi
Qurani 7:29Suratul Al- Araf
Sema: mola wangu ameamrisha uadilifu, na ameniambia nikuambieni elekezeni nyuso zenu kwake wakati wa kila sala…
Je mola huyo ambaye anasema kuwaambia wenye kufuata Qurani waelekeze nyuso alipo huko ni wapi?
Qurani 27:91 suratul An-Naml
Bila shaka nimeamrishwa nimwabudu mola wa nji huu wa makka ambaye akadiri ya aya hizi tunaona kuwa qurani inasimulia kuwa mola huyo ni wa mji wa makka ambaye…

Katika ibada zao waislamu huelekeza nyuso zao kibla nako ni katika msikiti wa Al' ka’ba iliyoko makka Qurani 2:144-150 mola wa mji wa makka ndiye Allah ambaye aliabudiwa na waarabu washirikina zama za ujahilia, na ndiye huyo huyo anoyeabudiwqa na waislamu.

(ix) kuzunguka Al- ka’ba wakiwa uchi wakati wa ibada.
Kabla ya dini ya uislamu makureshi na waarabu wenzao walikuwa wakiizunguka Al-ka’ba “bait ullah’ yaani nyumba ya Allah wakiwa uchi wake kwa waume walikuwa wakiitikadi nguo ni kitu kinachopata uchafu kwa hivyo hakistahiki kuvaliwa wakati wa ibada hayo tunayaona katika kitabu cha maisha ya Muhammad ukura wa 4 kilichotungwa na shikh Abdullah saleh Al Farsy ambaye alikuwa kadhi mkuu wa Zanzibar baadaye nchini Kenya. Siyo Farsy peke yake ambaye aliyeandika hayo bali na mwanachuoni maarufu aitwae Abul A’la maududi katika kitabu chake kiitwacho katika kuufahamu uislamu ukurasa wa 43 aliwaelezea waarabu hivi: maisha yao yalikuwa ya kishenzi.  Mambo yaoyalikuwa ya kishenzi na wakati wote walisherekea uzinzi kamari na ulevi. Kuteka nyara na kunyang’anya ulilokuwa useni wao, kuu na kutwaa wanawake kwa nguvu ndizo zilikuwa tabia zao halisi. Wakiweza kukao tupu uchi mbele za wenzao pasina haya wala hata kuona wamefanya jambo lolote la fedheha. Hata wake zao walikuwa wakiizunguka al-ka’ba uchi. Kwa ajili ya fikira za ujinga mtupu ati wa kuchunga heshima zao, waliwaua mabinti zao ili asije mtu akawa mkwa wao. Walikuwa wakiwaoa mama zao wa kambo baada ya kufa baba zao.Walikuwa wajinga hata wa mambo madogo ya kula, kuvaa na kunawa. Ama katika imani zao za kidini, walikuwa na ugonjwa ule ule uliotokana na uovu uliokuwa ukipoteza ulimwengu mzima.

Kumbuka Allah ndiye mungu waliomuabudu waarabu hao na nyumba yao ya ibada ni Al-ka’ba jambo la kushangaza maulamaa Abul A’la maududi ana sema kuwa waarabu hao walikuwa na uovu ulioupoteza ulimwengu mzima. Swalli je, kuzunguka Al-ka’ba na kumwabudu Allah ndio kuupoteza ulimwengu?

Je, waislamu wanapoenda Hijja wanaizunguka Al-ka’ba?
Kabla ya kujua mambo wanayoyafanya waislamu kule Al-ka’ba inafaa tujue jinsi Al- ka'ba ilivyo. Neno ka'aba ni la kiarabu lina maanisha kitu cha mirabo sita iliya sawa, ka’ba ni la kiarabu linamaanisha kitu cha miraba sita iliya sawa.Ka’aba ni jingo lenye ureru wa meta 12 upana meta 10 na urefu kwenda juu meta 15 jengo hilo lipo makka kule daudi Arabia. Jingo hilo limefunikwa na na mapazia meusi yaliyotariziwa aya za Qurani kwa herufi za kiarabu kwa kutumia uzi wa dhahabu halisi. Katika pembe ya mashariki ya ka’aba kuna jiwe jeusi katika kiarabu jiwe hili linaitwa “hajarul Aswad”.

Qurani inawaagiza waislamu wafanye ibada zao za Hija hivi…
(i) kuzunguka Al-ka’aba
qurani 22:29 suratul al-Hajj
Na kasha wajisafishe taka zao na watimize nadhitri zao na waizunguke nyumba ya kale (nyumba kongwe ya Al-ka’ba)

kadiri ya aya hii tunaona kuwa Allah anawaagiza waislamu waizunguke Al- ka’ba huko nyumba tuliona kuwa waarabu wapagani waliizunguka Al-ka’ba wakiwa uchi bila nguo je waislamu wao wanaizunguka Al-ka’ba wakiwa vipi?

Tunaposoma kitabu kiitwacho vipi uhiji kilichoandikwa na mwanachuoni wa kiislamu aitwae A. sulemani ukurasa wa 16 kuna maneno hayo: “ni haramu kuvaa nguo zilizoshonwa kwa mwanamume muhrim anayekwenda kuhiji makka kwenye Al-ka’ba (msikiti). Kushona hapa ina maana kushona kwa ajili ya kuvaliwa siyo kama kiraka, vazi linalozunguka mwili kama shati, suruali na kadhalika anaruhusiwa kufunga kwa pini au mkanda nguo za hiramu ili zisivuke yaani nguo mbili kama mgolole.

Kadiri ya maneno haya waislamu katika hija yao kule ka’ba wazunguka ka’ba wakiwa wanavaa nguo sisizo shonwa zinaitwa “ihram” yaani mashuka mawili meupe.

(x) ibada ya kuomba kubusu na kuliheshimu jiwa jeusi “hajarul Aswad” katika Al-ka,aba msikiti wa makka.
Makureshi pamoja na waarabu wenzao kabla ya uislamu walikuwa wakiheshimu sana nyumba ya allah al-ka’ba pamoja na jiwe jeusi liitwalo kwa kiarabu “hajaral Aswad” wakati huo wakiendeleza ibada zao za kishiriki kipagani na zilizojaa ukafiri. Jambo linalotuthibitia kuwa makureshi waliheshimu al kaba na jiwa jeusi tulipata katika kitabu cha maisha ya Muhammad (s.a.w) kilitungwa na sheikh Abdullah saleh Al-Farsy ukurasa wa 15-16 kuna maneno haya: “kujengwa kwa Al- ka’ba mtume alipokuwa na miaka 35 Al-ka’ba mtume alipokuwa na miaka 35 Al-kaba ilifanya nyufa kubwa, na ikakaribia kuvunjika, makureshi wakafanya shauri ya kuivunja na kujenga yote upya, Al-ka’ba ilikuwa haina sakafu…lakini Hajarul Aswad lilipokuwa likitaka kuwekwa mahali pake baina ya ukuta wa kusini na mashariki. Hapo ndipo walipogombana kilaukoo ukitaka mkubwa wao aliweke. Ugomvi ukashika nguvu. Kazi ikazuilika kwa muda wa siku tano, panangojewa vita tu, tumbo litakalo shinda ndilo liweke jiwe la Hajarul Aswad…mara kwa bahati nzuri aliingia mtume, alikuwa hakupata utume bado. Na hapo wote wakasema kwa umoja wao: “Hadhal Amin huyu yule mwaminifu na sote tumekubali” mtume akalichukua lile jiwe akalitia katila shali yake, akamwita kila mkubwa na ukoo; kisha akawaamrisha walichukue kiti mpaka mahjali pake. Hapo mtume akapokea akaliweka yeye kwa mikono wake na kwa radhi yao wote.

Huu ni ushahidi kuwa makureshi na waarabu wenzao kabla ya dini ya uislamu kuja walikuwa wanaihwshimu sana Al-ka’aba na jiwe jeusi lililokuwa ndabi ya msikiti huoj wa la’aba. Ambamo ndiyo sehemu waliokuwe wakizunguka wakiwa uchi wake kea waume, na hata Muhammad tunaoma alishiriki katika Al-ka’ba hiyo kwani na yeye aliweka hilo jiwe keusi na makureshi wote walikubali afanye hivyo. Swali la muhimu la kujuuliza je waislamu hawakurithi ibads hizo za ujahilia? Endelea…

Je, waislamu wanafanya ibada ya kuomba, kugusa, kubusu na kuliheshimu jiwe jeusi “Hajarul aswad”
Tunaposoma vitabu mbalimbali vya kiislamu tunaona namna ambavyo waislamu wanavyo fanya ibada ya kuliheshimu jiwe jeusi lililo katika msikiti mkuu wa makka uitwao Al-ka’ba unaofahamikakuwa ni “bait ullah” yaani nyumba ya Allah. Baadhi ya vitabu hivyo ni hivi…
  1. kitabu kiitwacho mkweli mwaminifu mtungaji sheikh said moosa muhamed al-kindy ya 3-4 chapa ya 14 ukurasa wa 75 kuna maneno haya; kasema mtume (S.a.W.) ya mwenyezi mungu katika Ardhi. Basi atakaye ligusa basi kafungamana na wenyezi.
  2. katika kitabu cha hadithi za Muhammad cha sahih al-bukhari vol. Ii ukurasa wa 397 hadithi na 682. kastika hadithi hii tunaambiwa kwamba “kila wakati mtume saw alikuja kwenye jiwe jeusi akalielekezea kikdolw na kusema Takbirt maana yake Allah ni mkuu.
  3. swahaba kwa mtume aliyeitwa umar bin khattab alilibusu jiwe jeusi al Al-ka’ba kasha akadema: “bila shaka nafahamu wewe ujiwe lisiloweza kumfaidia wala kumdhuru mtu yeyote. Kama nisingalikuwa nimemwons mtume )S>A.W.) akibusu mimi nisingalikubusuu” kiarabu chepesi cha maneno hayojni hivi; inna alamu annakha hajarul atadhura wala tanalwau.Walaula annahu tahiyyatu rasul Allah (S.A.W.) yakabalka makabul atukha.”
  4. kitabu kiitwacho vipi uhiji kilichoandikdwa na A-sulelman ukurasa wa 29-30 kuna maneno haya: Hajar-al Aswad (jiwe jeusi) “kabla ya kuanza kuzu\nguka Al-ka’ba ni uzuri kwanza kuliendea hajar-Al Aswad lililoko Al-ka’aba hapo husogea karibi ikiea inayumkinika kikaribia bila ya kuumiza watu unalikabili Hajar-Al Aswad una lieekea mkona na bila ya kusema unalikabili Hajar-Al Aswad unaliweka mkono na bila ya kusema unalibusu mara tatu na kuligusisha kipaji chako cha uso mara tatu kwa wawake kufanya hivi ni suna ikiwa hapana zogo la dwaru, ikiwa hulifikiri liashire kea mkono. Tena mtu hurudi kwenye Hajar-al Aswad na kuligusa, kulibusu mara tatu na kugusisha kipaji cha uso mara tatu kama vile mwanzo tena utasema Allahu Akbaaar mara tatu (huku ukilashiria hajar kea mikono yote miwili ikisha utaongeza “Alla humma iimana bika wartaddika bikitabika wafaa biahdika wattibaa lisunnat nabiyyika salla ila hu Alayhi wassalim.” Kiwsaili. “ewe mola kwa imani yengu juu yako na kuthibitisha kitabu chako na kutekeliza ahadi yako uya kufuata mwendo wa mtume. Tena hapo utapita kulipita Hajar-Al Aswad ukilielikea huku ukiendelea kuzunguka Al-ka’aba yote nzima.
  5. kumbuka tendo la kuzunguka Al-ka’aba lilifanya washirikina na dwapagani wa kiarabu zama za ujahilia kabla ya dini ya uislamu kuanza.Na waislamu noo huizunguka Al-ka’aba swali je, waislamu hawakurithi eneo la ibada za ujahilia tafakari.

Mungu wetu yehova anavyotufundisha kuhusu ibada ya jiwe.
Mambo ya walawi 26:1
Msifanye sanamu yeyote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jifee lolote lililochorwa katika nchi yenu ili kilisujudia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana mungu wenu.

Kadiri ya mafundisho ya mungu wet yehova ambaye wakristo tumuabudu ni kakosa makubwa kuchukua jiwe na kulisujudu. Tafakari kuhusu waislamu na matendo yao katika jiwe la jeusi “Hajarul Aswad.”

(xi) ibada ya kuzunguka majabali (vilimo) vya safaa na marwa huko makka kabla ya uislamu.
Qurani 2:158 suratul Al-Baaraqh (Ng’ombe jike) hakika safaa na marwa (majabali mawili yana yofanyiwa ibada ya kusai huko makka) ni katika alma za kuadhimisha dini ya mwenyezi mungu basi anayehiji kwenyu nyumba hiyo ar kufanya umra. Si kosa kwake kuvizunguka (vilima) hivyo viwili na anayefanya wema (atalipwa) kwani mwenyezi mungu ni mwenye shukrani na mjuzi wa kila jambo.

Ufafanuzi wa aya hiii ya 158 ulio katika qurani ni huu katika ibada ambazo hazisihi kufanywa ila makka ni hizi (a) Hijja na (b) umra. Na takriba zote mbili hizi ni sawa sawa ila zinakhitalifiana. Kidogo to. Moja katika hitilafu zao ni kuwa Hijja haifanyi ila miezi makhususi: na mwisho wa miezi ya Hijja ni kumi la mwanzo la mfungo tatu…ama mengine bi sawa. Nayo ni: (1) kuzunguka Al-ka’aba mara 7 (2) kwenda matiti mara 7 baina ya majabali hayo mawili ambalo moja linaitwa safaa na moja linaitwa marwa (3) kunyoa nywele au kuzikata.Majabali hayo kabla ya uislamu yalikuweka yamewekwa juu yake madanamu na makafiri wakiyaabudu. Basi ulipokuja uislamu. Waislamu wengine waliona labda si vizuri kufanya ibada haopo penye majabali hayo. Basi wakaambiwa kuwa si vibaya.

Maelezo ya aya hii yanafanana na yle yaiyo katika saqhih Al-Bukhari volii ukurasa wa 415-416 hadith no. 710 pale Asim alipomuuliza Anas bin maliki (A.S.) hivi: je, ulikuwa ukichukia kufanya tawaf (yaani kuzunguka) kati ya safaa na marwa? Akasema ndiyo kwaqsababu ni matendo ya kwaida (sherehe) iliyofanyofanyika wakati wa ujinga kutajua kabla ya uislamu kuja. Imesimuliwa pia kuwa Muhammad alifanjya tawwaf ya ka’aba na sa’I ya safa na marwa ili kuonyesha nguvu zake kwa safa na marwa. Hayo yamesimuliwa katika sahih Al Bukhari vol ii hadithi no.711. jambo linaloshangaza ni kuwa ibada hiyo ilifanywa na makafiri zama za ujahilia (ujinga) na waislamu nao wazunguka vilima hivyo isitoshe insshangaza kuona Allah mungu anayeabudiwa ba wislamu anayaita majabali hayo minshahilillah yaani alama za mungu au kwa kiingereza “symbols of Allah” hii ni ajabu kuona vilima vinaitwa hivyo.

Bwana yesu anatufundisha nini kuhusu ibada ya milima? Yohana 4:19-22
Yule mwanamke akamwambia bwana naona ya kuwa unabii, baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko yerusalemu ni mahali patupa sapo kuabudjiwa. Yesu akamwambia mama, unisadiki saa ubajyha ambayi gamtamwabudu baba katika mlima huu, wala kule yersalemu, ninyi mnaabudu msichokijua sisu tunaabudu tukijuacho kwa kuwa wokovu watoka kwa wayahudi.

Katika aya hizi Bwana Yesu anatuambia kuwa wale wanaofanya ibada katika mlima hawajui wachokiabudu. Ndugu tafakqari ibada ya waislamu katika vilima je, wanajua wanachokiabudu?

(xii) mwezi wa ramadhani.
Tunaposoma katika kitabu cha maisha ya muhammaf ukurasa wa 32 kilichotungwa na sheikh Farsy tunaona kuwa miezi iliyotumiwa na waarabu kabla yo dini ya uislamu ndiyo inayotumiwa ba waislamu. Kitabu hicho kinasomeka hivi…”Makka tangu kabla ya uislamu, ilikuwa ni mahali patakatifu kwa waarabu wote. Kila mwaka walikuwa wakija kuhiji miezi hii hii wanayoitumia sasa waislamu katika kuhiju kwao.

Waarabu walikuwa washirikina na wapagani majahilia. Walikuwa na mwezi wa ramadhan nalo ndio mwezi ambao dwaislamu wana amini kuwa Muhammad alipata utume. Tazama kitabu cha maisha ya Muhammad ukurasa 16-17.
Ibada ya kufunga katika mwezi wa Ramadhan kwa waislamu
Qurani 2:183 suratul Al-Baarah (Ng’ombe jike)

Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga (saumu) kama walivyoiazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha mungu.

Imeelezwa katika sahih Bukhari volii Hadith 662 vol. Iii Hadith no. 219 na 220 pia vol vi Hadith no.31 ya kuwa Muhammad aliamuru waislamu wafunge siku ya Ashura siku ya 10 ya mwezi kwanza katika mwaka wa kiislamu yaani mweziuitwalo muharram) kufunga huko kaqbla ya uislamu ilikuwa ni desturi katika dini ya Hums na uislamu ukaichukua.

(xiii) kumpiga mawe shetani katika bonde la wadah muhassir.
Miongoni mwa tendo moja kubwa linalofanya na waislamu wanapofika hija huko makka ni kumpinga mawe shetani. Kitabu kiitwacho vipi uhiji ukurasa wa54,55,61 kuna maneno haya…”Mahujaji wanapofika bonde liitwalo wadi ah muhasisi karibu na mina ni suna kunyapuka hao huelikea jamrat al a quba (shetani mkubwa) na hupiga yale mawe saba waliyoyaokota muzdelifa baada ya kupiga mawe jamarati Al-Aqaba hufuatiwa na kuchinja.

Kwa sisi wakristo tunajua shetani ni roho ya uasi waefeso 2:1-5 na ni roho ya udanganyifu 1 Timotheo 4:1-2. Hivyo huwezi kumshinda shetani kwa kumpiga kwa mawe maana ni roho tu. Roho ni upepo au pumzi. Biblia inatufundisha kuwa tunamshinda shetani kwa njia ya imani sahihi ya mungu, kushika neon la mungu, dala, na maombi, hivyo tutamshinda shetani soma waefeso 6:11-18.

  1. Wajibu wa Mkristo baada ya kuujua uislamu.
Ninaamini kuwa imejifunza mengi kuhusu dini ya uislamu, na umeona mambo mengi yuanayotendeka na waislamu kule makka wakati wa hija. Mambo hayo yalifanywa na makureshi na waarabu wenzao kabla ya dini ya uislamu kuja, na tena umeona kuwa mungu tunayemwabudu wakristo hataki ibada zinazoshirikisha mawe na milima. Basi wajibu wako mkristo kuwafikishia injili waislamu na watu wa dini nyingine zisizomuamini Bwana Yesu, ili wamdwamini na wapate kuokolewa. Kumbuka injili ndio uweza wa mungu uletao wokovu Warumi 1:16. na tena injili ndilo neon la kweli Wakolosai 1:5.bwana akubariki sana ni mimi katika utumishi wa Bwana Yesu Mwalimu;


Imeandikwa na Mwalimu Eleutary H. Kobelo.

TRENDING NOW