Wednesday, September 23, 2020

Asili ya Uislamu

 


IJUE DINI YA UISLAMU NA ASILI YAKE

Na Mwalimu Eleutary H. Kobelo.

Utangulizi

Kwa miaka mingi waislamu duniani, wanatuhimiza sana sisi Wakristo tuache imani na dini yetu, ili tuingie katika dini yao ya uislamu. Waislamu wanasema dini yao ndio ya haki, mbele ya Mwenyezi Mungu, na tena wasema manabii wote walikuwa waislamu, wanaendelea kusema kuwa hata Bwana Yesu naye alikuwa mwislamu, waislamu wanaendelea kusema kwamba dini ya Islamu haikuchukua au kurithi hata chembe (kidogo) ya tabia ya mafundisho ya ibada za kikafiri, kushirikina na ujahili (yaani ujinga), kwani wanasema Uislamu ni dini safi kuliko zote. Swali la muhimu ni hili. Je, ni kweli kwamba dini ya uislamu haikuchua tabia na mafundisho ya ibada za kikafiri, kushirikina na ujahilia? Ili kujua yote hayo fuatilia kwa makini somo hili lililoandikwa na Mwalimu wangu Mwinjilisti Kobelo na kupitiwa upya nami Mwalimu Chaka.


Sehemu kuu tano za somo

  1. Je, manabii wote walikuwa waislamu?
  2. Maana ya neno Islam.
  3. Nani aliyekuja na dini ya kiislamu?
  4. Je, dini ya kiislamu imechua ibada za waarabu za zama ujahilia (yaani ujinga)?
  5. Wajibu wa mkristo baada ya kujua Uislamu.

1. Je, Manabii wote walikuwa waislamu?

Hoja kubwa ya waislamu ni kule kutuhimiza wakristo tukubali kuwa waislamu kwa kusema kwamba manabii wote wa Mungu walikuwa waislamu, hivyo wanataka tuache imani yetu tuwe waislamu. Lakini inafaa kwanza kuvichunguza vitabu vya kiislamu kuhusu ujio wa Qurani inafundisha nini? Na je, ni nani aliyeleta dini hiyo? Qurani ya Allah Mungu kama wanavyoamini waislamu inasimulia hivi;

Qurani 6:14 Suratul An-Am (Wanyama)

Sema: hakika nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu.

Katika aya hii tunaona Muhammad ndiye mtu wa kwanza kuamrishwa asilimu.

Imesimuliwa pia ya kwamba Muhammad S.A.W. alisema, “Sisi waislamu ndiyo wa mwisho kuja” hayo tunayasoma katika Sahih Al-Bukhari vol. ix Hadithi na 587.


Muhammad vilevile aliwaambia wafuasi wake wafuate njia ya waliowatangulia. “nchi kwa nchi, hatua kwa hatua hata kama ikiwa waliingia katika shimoni mwa mjusi” masahaba zake wakauliza “Layahud waal Na-swara? Yaani wayahudi na wakristo? Akawajibu Farman? Yaani nani zaidi? Hayo tunayaona katika Sahih Muslim vol. iv katika Al-lim, hadithi na 6448. Kutokana na jibu hili la Muhammad (S.A.W.) ni dhihiri kuwa dini ya Uislamu ilitanguliwa na dini yetu Wakristo na hata ile dini ya Kiyaudi.

  1. Manabii wa Mungu Yehova walifuata dini (njia) hii.

Tunaposoma maandiko matakatifu ya Biblia yanatufundisha kuwa manabii waliongozwa na huyu.

1 Petro1:10-11

katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta tafuta na kuchunguza chunguza ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. Wakati upi na wakati wa namna gani ulioonywa na roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao.

1 wakorintho 10:1-4

kwa maana ndugu zangu,sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu. Wote wakapita kati ya bahari,wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingi na katika bahari; wote wakala chakula kilekile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata na mwamba ule ulikuwa ni kristo.

Katika aya hizi tunaona wazi wazi kuwa manabii wote waliongozwa na roho wa Kristo Yesu ambaye alikuwa ndani yao. Musa pamoja na watu wake pia walifuatwa na kristo naye aliwalisha na kuwanywesha. Wote waliongozwa na Bwana Yesu yeye mwenyewe aliwaita “watu wa Kristo” Soma Marko 9:38-41 hii ni kwasababu Bwana Yesu ndiye kiongozi wetu. Tazama Mathayo 23:9, tena Bwana Yesu ndiye njia (dini) ya kweli na uzima Yohana 14:6 hivyo manabii wote walikuwa ni watu wa Kristo kwasababu roho yake Yesu ulikuwa ndani yao ikiwaongoza.

  1. Maana ya neno Islam

Neno islam ni la lugha ya Kiarabu. Maana yake ni “Utii” au “Amani” katika Qurani neno Islam limetajwa mara 38. ijapokuwa neno Islam limetajwa mara nyingi lakini neno hilo ni tofauti na dini ya uislamu hii ni kwasababu dini a Uislamu maana yake ni kujisalimisha chini ya amri za Allah au amani chini ya sheria za Allah. Qurani ya Allah Mungu kama wanavyoamini waislamu inasimulia kumhusu Muhammad (s.a.w.) hivi.

Qurani 6:163 Suratul Al-An-Am (Wanyama)

Na haya ndiyo nilivyoamrishwa na mimi ni wa kwanza wa wanaojisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu).

Qurani 39:12 Suratul Az-zumar (Makundi/Vikosi)

“Na pia nimearishwa niwe wa kwanza wa (viumbe) wanaojisalimisha kwa Mwenyezi Mungu.”

  1. Nani aliyekuja na dini ya kiislamu?

Tunaposoma katika ufafanuzi wa aya ya 19-20 kati ka suratul Yusuf ulio ndani ya Qurani juzuu ya 12 chapa ya tatu ya kiswahili ukurasa wa 311 kuna maneno ambayo yanaelezea mtu aliyekuja na dini ya kiislamu hapa duniani na maneno yenyewe ni haya…

Unaona kwanza kulikuwako zaidi ya miaka 4000 kabla ya kuja dini ya kiislamu aliyokuja nayo Nabii Muhammad khalafu wakausingizia Uislamu kuwa ndio ulikuja na kuuza watu.

Kadiri ya ufafanuzi huu uliomo ndani ya qurani, na ushahidi wa vitabu maarufu vya hadithi za muhammad katika sahih Al-Bukhari na sahih muslim. Na vitabu mbalimbali vilivyoandikwa na masheikh wa dini ya kiislamu, inathihirika waziwazi kuwa dini ya uislamu imeletwa na kuanzishwa na Muhammad (s.a.w.) mfano mzuri wa mwanzo wa dini ya uislamu tunauona katika kitabu kiitwacho maisha ya nabii muhammad (s.a.w.) kilichotungwa na aliyekuwa kadhi mkuu wa zanzibar na baadaye nchi ya kenya marehemu sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy. Katika ukursa wa 18 kuna maneno yanayo husu mke wa muhammad aliyeitwa khadija binti khuweylid nayo yanatuhadithia hivi…

Akarejea kwa mkewe bibi khadija, akamsimulia habari hii. Palepale bibi huyu akamwamini, akawa ndiye mtu wa awali kabisa kushehedusha shahada ya uislamu. Basi mwislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke.

Katika kitabu hicho hicho cha maisha ya nabii muhammad ukurasa wa 18 kifungu c. wametajwa waislamu wa awali kabisa nao ni hawa…

(i) Mwislamu wa kwanza

Bibi Khadija bint Khuweylid

Mtume aliamrishwa kufundisha dini siku ya jumatatu na bibi huyu alisilimu siku hiyo hiyo akafanya ibada na mtume usiku ule ule kabla ya mtu yeyote ulimwenguni huyu ndiye aliyefuzu kwelikweli.

(ii) Mwislamu wa pili

Sayyidina Ali bin Abi Talib bin Abdul Muttalib

Alipomwana mtume na bibi Khadija usiku ule wanafanya mpya aliwauliza, “hii ni ibada gani?” mtume alimfahamisha na akamtaka awe pamoja nao lakini yeye alikataa kwanza akasema mpaka niende nikamshauri baba yangu”. Mtume akamkataza kuitoa siri ile nje. Mara asubuhi ya usiku ule ule, kijana huyu akaja kwa mtume akampa habari kuwa yeye yu pamoja nao. Akawa ndiye islamu wa pili duniani. Aliposilimu alikuwa kijana wa miaka 10 hivi.

(iii) Mwislamu wa tatu na wa nne.

Zayd bin Haritha Al Ka’bi na Bibi Aymana.

Huru wa mtume na mwanawe wa kupanga alikuwa akikaa pamoja na mtume na akasilimu kama sayyidina Ali mchana wa jumane. Alisilimu yeye na mkewe, bibi ummu Aymana yaya wa mtume.

Hawa wote ndio waislamu wa awali kabisa ambao walisilimu mara baada ya muhammad s.a.w. kuleta dini ya uislamu ambayo alianzisha rasmi hapa duniani jumatatu ya siku ya 17 ya mwezi wa ramadhani sawa sawa na 27th december ya mwaka wa 610 baada ya kristo. Kabla ya muhammad dini ya kiislamu haikuwepo kabisa duniani.

  1. Je, dini ya uislamu imechukua ibada za waarabu wa zama za ujahilia (yaani ujinga)?

Wakati wa ujahilia (ujinga) kabla ya dini ya uislamu makureshi ambalo ni kabila la muhammad s.a.w. na waarabu wenzao, walikuwa wakiabudu miungu mingi yapata 360 hivi. Kawaida hiyo ya kuabudu kwao miungu mingi kumesimuliwa waziwazi katika quarani na vitabu mbalimbali vya kiislamu. Vitabu hivyo vimeandikwa na masheikh na wanachuoni wengi, nitawataja baadhi yao nazo ni hawa…

(i) Maulamaa sayyid Abul A’la Maududi

Katika kitabu chake kiitwocho katika kuufahamu uislamu ukurasa wa 42-44 kuna maneno haya…”Bara Arabu mwina wa kiza wafanya biashara waarabu walijikokota masafa marefu ilikuwa vigumu kwao kupata hata chembe ya elimu wachache waliojua kusoma na kuandika walikuwa wakiabudu mawe, miti, masanamu, nyota na pepo, kwa ufupi kila kilichowapitia akilini mwao, hawakujua hata kidogo mafunzo ya mitume waliowatangulia. Walikua na dhana kuwa ibrahimu na ismail walikuwa babu zao, lakini walikuwa hawajui kitu kuhusu mafunzo yao ya dini na Mungu waliyemwabudu.

(ii) Sheik Abdullah saleh Al-Farsy ambaye alikuwa kadhi mkuu zanzibar na baadaye nchini Kenya

Katika kitabu chake kiitwacho maisha ya nabii muhammad s.a.w. ukurasa wa 6 kuna maneno haya… “Hata ilipokuwa karibu atadhihiri mtume mapadiri wa kinasara na makuhani wa kiyahudi waliokuwa wakikaa bara arabu walikuwa wakiwataharisha majirani zao wa kiarabu waliokuwa wakiabudu masanamu;

Qurani imetaja miungu mbalimbali iliyoabudiwa na makureshi na waarabu wenzao zama za ujahilia

(i) Waliabudu maandazi.

Qurani 25:43-44 Suratul Al;- furqan (Qurani)

Je umemuona yule aliyefanya matamanio yake (kile alichokipenda). Kuwa mungu wake? Basi je, utaweza kuwa mlinzi wake (ukamhifadhi) na haya, na hali ya kuwa hataki?) au je, unafikiri ya kwamba wengi katika wao wanasikia au wanafahamu? Hawa kuwa hao ila ni kama wanyama bali wao wanapotea zaidi njia.

Ufafanuzi wa aya ya 43 ulio katika qurani juzuu ya 19 ni huu, “waarabu kwa ujinga wao wa kuabudu chungu ya miungu walikuwa baadhi yao wakiona chochote kile kikawapwndeza hukiabudu hata andazi lililokaa kwa sura nzuri.

Hapa tunaona kuwa qurani inasimulia wazi wazi kwamba waarabu waliabudu hata andazi na tena ni wajinga “yaani majahalia”

(ii) kuabuduwa kwa miungu ya sanamu.

Qurani 71 22-23 Suratul Nuh (Nuhu)

Na walifanya hila kubwa kubwa za (kubatilisha dini). Na waliwaambia (wafuasi wao): “Msiache miungu yenu wala msiwaache waddi wala suwa’a wala yaghuta wala ya’uqa wala Nasra”. (Majina ya waungu wao wa kisamu).

Hii ni miungu ya uongo ya sanamu ambayo iliabudiwa na waarabu mungu waddi alikuwa na umbo la mwanamke yaghuta umbo la simba, ya’uga umbo la farasi hayo yanapatikana katika kitabu kiitwacho “history of Islam kilichoandikwa na Pro. Masudul Hassan ukurasa wa 43

(iii) kuabudiwa kwa miungu iitwayo lata, uzza na manata

Qurani 53:18-20,23 suratul An-najm

kwa yakini aliona nabii muhammad mambo makubwa kabisa katika alama (Qudra) za mola wake.je mume waona lata na uzza? Na manata mungu wenu mwingine wa tatu, kuwa ndio waungu hao badala ya mwenyezi mungu? Hayakuwa hayo majina ya lata mungu mwanamke, na uzza mungu mwanamke mwenye enzi na manata, mungu mwanamke anaye neemesha ila ni majina tu mliwapa nyinyi na baba zenu…

(iv) kuabudiwa kwa Allah (s.w.) na majahilia (wajinga)

makureshi pamoja na waarabu wenzao ambao walikuwa wakabudu miungu mingi kama tulivyoona huko juu. Vilevile miongoni mwa hiyo miungu walimuabudu Allah (S.W.) ambaye ndiye aliyekuwa mungu mkubwa, na miungu ya hata na uzza na manata wakawaitakadi kuwa mi waungu wanawake ama wake zake Allah au watoto wake. Hayo tunayaona katika ufafanuzi wa aya ya 180 katika Qurani suratul Al- A’raf na pia katika kitabu kiitwacho history of isalmu kilichoandikwa na pro masudul hasan ukurasa 43. ushahidi wa wazi zaidi wa kuonyesha kuwa waarabu majahilia walimuabudu Allah tunaupata katika vitabu vifuatavyo…

(i) kuzaliwa kwa Muhammad S.A.W. mtume wa waislamu

maombi na dua ya abdul mutalib kwa Allah.

Tunaposoma kitabu cha maisha ya Muhammad S.A.W. kilitangwa na sheikh Farsy ukurasa wa 5 kuna maneno hayo…


Pale pale alfajiri alipokwisha kuzaliwa mtume alikwenda kuitwa babu yake kuja kumwona mjukuu wake. Babu huyu alifurahi sama na akamfunika manguo mjukuu wake, na akamfunika manguo mjukuu wake, akajikongoja naye mpaka kwenye Al-ka’ba akafungua mlango akaingia ndani, akasimama, akamwombea dua kwa mashairi mazuri ya kiarabu aliyoyatunga mwenyewe wakati ule ule, kisha akarejea naye na jua bado halikuchomoza.

Ushahidi wa wazi unaothibitisha kuwa baba yake Muhammad Abdul muttalib aliomba dua kwa Allah tunaupata tunaposoma utangulizi wa suratul al-fyl ulio katika juzuu ya ukurada wa 946 Qurani iliyotafsiriwa kwa kiswahili chapa ya nane tunasoma maneno hayo. “chifu mkuu wa makka zama hizo alikuwa Abdul muttalib, alikwenda al ka’ba pamoja na baadhi ya machifu wa kikuraish na akilishika komeo la chuma la mlango wa al-ka’ba, akamwambia Allah (S.W.0 kuilinda nyumba yake pamoja na wahudumu wake. Zama hizo kulikuwa na masanamu 360 ndani na kando ya Al- ka’ba.”

(v) imani ya Abdul muttalib ilikuwa hii.

Katika kitabu kilichoandikwa na mwanachuoni maarufu wa kiislamu aitwae ale muhsin barwani ukurasa wa 153 tunasoma maneno haya; “hapakutokea mwarabu ambaye alipewa jina hilo na babu yake tangu kuzaliwa kwake, na huyo babu hakuwa mkristo bali alikuwa akifuata mila za kishirikina.” Na wala hakujua taurati wala injili.

(vi) himizo la Muhammad (S.A.W.) kwa makureshi wenzie kuhusu mungu aitwae Allah.

Katika kitabu kiitwacho mkweli mwaminifu kilichotungwa na sheikh said moosa muhamed al kindy juzuu ya mwanzo na pili chapa ya kumi ukurasa wa 130 tunadoma maneno haya: “katika wakati wa ujaahiliya kabla mtume (S.A.W.) kupata utume alikuwa akiwaambia waru “enyi watu semeni laa ilaha illah laah mtafuzu” yaani hana mola ila Allah mtafuzu.

Huu ni ushahidi wa wazi kabisa ya kwamba Allah aliabudiwa na makureshi ma waarabu wenzao hao watu walikuwa washikina , wapagni na majahilia (wajinga). Kumbuka Muhammad alikuwa ni mkureshi naye aliposema “hapana mola ila Allh” alikuwa yupo za ujahilia na hakuwa anajua kitabu wala imani tazama Qurani 42:52 Suratul shuraa.

(vii) je, mungu anayeabudiwa ba waislamu jina lake ni nani?

Qurani 17:110 suratul ban israil wana wa Israel

sema: “mwombeni mwenyezi mungu kwa jina la Allah au muombeni kwa jina la rahman kwa jina lolote mtakalo mwita katika hayo itaifaa: kwani ana majina mazuri mazuri,” wala usiiseme sala yako kwa sauti kubwa wala usiseme kwa sauti ndogo, bali shika njia baina ya hizo katikati si kwa kelele wala kimya.

Katika aya hii tunaona jina la mungu anayeabudiwa ba waislamu anaitwa Allah. Katika qurani jina hilo limetjwa mara 2,866 kumbuka kuwa makureshi na waarabu wenzao waliokuwa washirikina wapagani na majahilia wajinga kabla ya uislamu walimuabudu mungu huyo aitwae allah swali muhimu je, waislamu hawakutithi mungu wa makureshi? Tafakari kwa makini.

(viii) mji mkuu wa makureshi na waarabu wenzao zama za ujahilia ambako walikuwa wanaenda kuhiji ni huu

Tunaposoma utangulizi wa suratul Quraysh katika juzuu ya 30 ukurasa wa 950-951 chapa ya nane ya Qurani ya kiswahili kuna maneno haya…kabila la kureshi lilikuwa limetawanyika kote hijaz hadi zama za Qusayy bin kilaab mmoja wa mababu wa mababu wa mtume (S.A.W.). kwanza kabisa Qusayy aliwakusanya makureshi pamoja huko makka, na hivyo kabila hili likawa wadhamini wa Al-ka’ba kwa msingi huo, Qusayy alikuwa akiitwa mujammi mkusanyaji wa wartu wa habila lake. Mtu huyu kwa busara yake aliweza kuasisi serikali katika mji wa makka, na akaweka mipango mizuri kwa ajili ya mahujaji wajao toka kote arabuni, na matokea yake ni kuwa makureshi walipata umaarufu mkubwa miongoni mwa makabila ya kiarabu.

Hapa tunaona kuwa zama za ujahilia na upagani kabla ya dini ya uislamu waarabu wote walienda kuhiji katika mji wa makka kwenye nyumba ya Al-ka’ba inayoitwa “Bait-ullah” yaani nyumba ya allah. Kumbuka nyumba hiyo hiyo wapagani wa kiarabu zama za ujahilia (ujinga) waliabudu miungu 360 na Allah ndiye mungu wao mkuu.

Mji mkuu wa hija kwa waislamu ni huu.

Qurani 3:96 suratul Al-aal-imran (watu wa imran)

kwayakini nyumba ya kwanza iliyewekwa kwa ajili ya watu kufanya ibada ni iloe iliyoko makka, na yenye baraka na uongozi kwa ajili ya walimwengu wote.

Qurani 22:27-29 suratul Al-Hajj. (Hijja)

Na (tukamwambia “utangaze kwa watu habari ya Hijja, watakujia, (wengine) kwa miguu na (wengine) juu ya kila mnyama aliyekonda kwa machofu ya njiani wakija kutoka katika kila njia ua mbali; ili washuhudee manufaa yao na ili wakushirishe kulitaja jina la mwenyezi mungu katika diku zinazojulikana fadhila zake na juu ya yale aliyowaruzuku, nao mi wanyana wenye miguu mine. Na kuleni katika wanyama hao na mlisheni mwenye shida na fakiri. Kasha wajisafishe toka zao, na watimize hadhiri zao na waizunguke nyumba ya kale (nyumba kongwe Al-ka’ba.)

Tunaposoma ufafanuzi wa aya ya 29 ulio ndani ya Qurani katika juzuu ya 17 kuna maneno haya; “kabla ya uislamu waarabu walikuwa wakiitukuza Al-ka’ba. Na kwa ilivyokuwa ni jingo la zamani sana waliita Al-Baytul’Atiq yaani nyumba ya kale.”

Kama vile waarabu wapagani, makafiri na majahilia mji mkuu wa Hijja ni makka kule Saudi Arabia ndivyo ilivyo kwa waislamu nao mji wao mkuu ambao wanaenda kuhiji ni makka. Isitoshe Qurani inasimulia kuwa makka ni mama wa miji soma hayo katika Qurani 6:92 suratul Al- An-Am (wanyama) waislamu popote walipo duniani wanaambiwa wanaposali waelekeze nyuso zao mahali maalumu,

Qurani inasimulia hivi

Qurani 7:29Suratul Al- Araf

Sema: mola wangu ameamrisha uadilifu, na ameniambia nikuambieni elekezeni nyuso zenu kwake wakati wa kila sala…

Je mola huyo ambaye anasema kuwaambia wenye kufuata Qurani waelekeze nyuso alipo huko ni wapi?

Qurani 27:91 suratul An-Naml

Bila shaka nimeamrishwa nimwabudu mola wa nji huu wa makka ambaye akadiri ya aya hizi tunaona kuwa qurani inasimulia kuwa mola huyo ni wa mji wa makka ambaye…

Katika ibada zao waislamu huelekeza nyuso zao kibla nako ni katika msikiti wa Al' ka’ba iliyoko makka Qurani 2:144-150 mola wa mji wa makka ndiye Allah ambaye aliabudiwa na waarabu washirikina zama za ujahilia, na ndiye huyo huyo anoyeabudiwqa na waislamu.

(ix) kuzunguka Al- ka’ba wakiwa uchi wakati wa ibada.

Kabla ya dini ya uislamu makureshi na waarabu wenzao walikuwa wakiizunguka Al-ka’ba “bait ullah’ yaani nyumba ya Allah wakiwa uchi wake kwa waume walikuwa wakiitikadi nguo ni kitu kinachopata uchafu kwa hivyo hakistahiki kuvaliwa wakati wa ibada hayo tunayaona katika kitabu cha maisha ya Muhammad ukura wa 4 kilichotungwa na shikh Abdullah saleh Al Farsy ambaye alikuwa kadhi mkuu wa Zanzibar baadaye nchini Kenya. Siyo Farsy peke yake ambaye aliyeandika hayo bali na mwanachuoni maarufu aitwae Abul A’la maududi katika kitabu chake kiitwacho katika kuufahamu uislamu ukurasa wa 43 aliwaelezea waarabu hivi: maisha yao yalikuwa ya kishenzi. Mambo yao yalikuwa ya kishenzi na wakati wote walisherekea uzinzi kamari na ulevi. Kuteka nyara na kunyang’anya ulilokuwa useni wao, kuu na kutwaa wanawake kwa nguvu ndizo zilikuwa tabia zao halisi. Wakiweza kukao tupu uchi mbele za wenzao pasina haya wala hata kuona wamefanya jambo lolote la fedheha. Hata wake zao walikuwa wakiizunguka al-ka’ba uchi. Kwa ajili ya fikira za ujinga mtupu ati wa kuchunga heshima zao, waliwaua mabinti zao ili asije mtu akawa mkwa wao. Walikuwa wakiwaoa mama zao wa kambo baada ya kufa baba zao. Walikuwa wajinga hata wa mambo madogo ya kula, kuvaa na kunawa. Ama katika imani zao za kidini, walikuwa na ugonjwa ule ule uliotokana na uovu uliokuwa ukipoteza ulimwengu mzima.

Kumbuka Allah ndiye mungu waliomuabudu waarabu hao na nyumba yao ya ibada ni Al-ka’ba jambo la kushangaza maulamaa Abul A’la maududi ana sema kuwa waarabu hao walikuwa na uovu ulioupoteza ulimwengu mzima. Swalli je, kuzunguka Al-ka’ba na kumwabudu Allah ndio kuupoteza ulimwengu?

Je, waislamu wanapoenda Hijja wanaizunguka Al-ka’ba?

Kabla ya kujua mambo wanayoyafanya waislamu kule Al-ka’ba inafaa tujue jinsi Al- ka'ba ilivyo. Neno ka'aba ni la kiarabu lina maanisha kitu cha mirabo sita iliya sawa, ka’ba ni la kiarabu linamaanisha kitu cha miraba sita iliya sawa. Ka’aba ni jingo lenye ureru wa meta 12 upana meta 10 na urefu kwenda juu meta 15 jengo hilo lipo makka kule daudi Arabia. Jingo hilo limefunikwa na na mapazia meusi yaliyotariziwa aya za Qurani kwa herufi za kiarabu kwa kutumia uzi wa dhahabu halisi. Katika pembe ya mashariki ya ka’aba kuna jiwe jeusi katika kiarabu jiwe hili linaitwa “hajarul Aswad”.

Qurani inawaagiza waislamu wafanye ibada zao za Hija hivi…

(i) kuzunguka Al-ka’aba

qurani 22:29 suratul al-Hajj

Na kasha wajisafishe taka zao na watimize nadhitri zao na waizunguke nyumba ya kale (nyumba kongwe ya Al-ka’ba)

kadiri ya aya hii tunaona kuwa Allah anawaagiza waislamu waizunguke Al- ka’ba huko nyumba tuliona kuwa waarabu wapagani waliizunguka Al-ka’ba wakiwa uchi bila nguo je waislamu wao wanaizunguka Al-ka’ba wakiwa vipi?

Tunaposoma kitabu kiitwacho vipi uhiji kilichoandikwa na mwanachuoni wa kiislamu aitwae A. sulemani ukurasa wa 16 kuna maneno hayo: “ni haramu kuvaa nguo zilizoshonwa kwa mwanamume muhrim anayekwenda kuhiji makka kwenye Al-ka’ba (msikiti). Kushona hapa ina maana kushona kwa ajili ya kuvaliwa siyo kama kiraka, vazi linalozunguka mwili kama shati, suruali na kadhalika anaruhusiwa kufunga kwa pini au mkanda nguo za hiramu ili zisivuke yaani nguo mbili kama mgolole.

Kadiri ya maneno haya waislamu katika hija yao kule ka’ba wazunguka ka’ba wakiwa wanavaa nguo sisizo shonwa zinaitwa “ihram” yaani mashuka mawili meupe.

(x) ibada ya kuomba kubusu na kuliheshimu jiwa jeusi “hajarul Aswad” katika Al-ka,aba msikiti wa makka.

Makureshi pamoja na waarabu wenzao kabla ya uislamu walikuwa wakiheshimu sana nyumba ya allah al-ka’ba pamoja na jiwe jeusi liitwalo kwa kiarabu “hajaral Aswad” wakati huo wakiendeleza ibada zao za kishiriki kipagani na zilizojaa ukafiri. Jambo linalotuthibitia kuwa makureshi waliheshimu al kaba na jiwa jeusi tulipata katika kitabu cha maisha ya Muhammad (s.a.w) kilitungwa na sheikh Abdullah saleh Al-Farsy ukurasa wa 15-16 kuna maneno haya: “kujengwa kwa Al- ka’ba mtume alipokuwa na miaka 35 Al-ka’ba mtume alipokuwa na miaka 35 Al-kaba ilifanya nyufa kubwa, na ikakaribia kuvunjika, makureshi wakafanya shauri ya kuivunja na kujenga yote upya, Al-ka’ba ilikuwa haina sakafu…lakini Hajarul Aswad lilipokuwa likitaka kuwekwa mahali pake baina ya ukuta wa kusini na mashariki. Hapo ndipo walipogombana kilaukoo ukitaka mkubwa wao aliweke. Ugomvi ukashika nguvu. Kazi ikazuilika kwa muda wa siku tano, panangojewa vita tu, tumbo litakalo shinda ndilo liweke jiwe la Hajarul Aswad…mara kwa bahati nzuri aliingia mtume, alikuwa hakupata utume bado. Na hapo wote wakasema kwa umoja wao: “Hadhal Amin huyu yule mwaminifu na sote tumekubali” mtume akalichukua lile jiwe akalitia katila shali yake, akamwita kila mkubwa na ukoo; kisha akawaamrisha walichukue kiti mpaka mahjali pake. Hapo mtume akapokea akaliweka yeye kwa mikono wake na kwa radhi yao wote.

Huu ni ushahidi kuwa makureshi na waarabu wenzao kabla ya dini ya uislamu kuja walikuwa wanaihwshimu sana Al-ka’aba na jiwe jeusi lililokuwa ndabi ya msikiti huoj wa la’aba. Ambamo ndiyo sehemu waliokuwe wakizunguka wakiwa uchi wake kea waume, na hata Muhammad tunaoma alishiriki katika Al-ka’ba hiyo kwani na yeye aliweka hilo jiwe keusi na makureshi wote walikubali afanye hivyo. Swali la muhimu la kujuuliza je waislamu hawakurithi ibads hizo za ujahilia? Endelea…

Je, waislamu wanafanya ibada ya kuomba, kugusa, kubusu na kuliheshimu jiwe jeusi “Hajarul aswad”

Tunaposoma vitabu mbalimbali vya kiislamu tunaona namna ambavyo waislamu wanavyo fanya ibada ya kuliheshimu jiwe jeusi lililo katika msikiti mkuu wa makka uitwao Al-ka’ba unaofahamikakuwa ni “bait ullah” yaani nyumba ya Allah. Baadhi ya vitabu hivyo ni hivi…

  1. kitabu kiitwacho mkweli mwaminifu mtungaji sheikh said moosa muhamed al-kindy ya 3-4 chapa ya 14 ukurasa wa 75 kuna maneno haya; kasema mtume (S.a.W.) ya mwenyezi mungu katika Ardhi. Basi atakaye ligusa basi kafungamana na wenyezi.
  2. katika kitabu cha hadithi za Muhammad cha sahih al-bukhari vol. Ii ukurasa wa 397 hadithi na 682. kastika hadithi hii tunaambiwa kwamba “kila wakati mtume saw alikuja kwenye jiwe jeusi akalielekezea kikdolw na kusema Takbirt maana yake Allah ni mkuu.
  3. swahaba kwa mtume aliyeitwa umar bin khattab alilibusu jiwe jeusi al Al-ka’ba kasha akadema: “bila shaka nafahamu wewe ujiwe lisiloweza kumfaidia wala kumdhuru mtu yeyote. Kama nisingalikuwa nimemwons mtume )S>A.W.) akibusu mimi nisingalikubusuu” kiarabu chepesi cha maneno hayojni hivi; inna alamu annakha hajarul atadhura wala tanalwau. Walaula annahu tahiyyatu rasul Allah (S.A.W.) yakabalka makabul atukha.”
  4. kitabu kiitwacho vipi uhiji kilichoandikdwa na A-sulelman ukurasa wa 29-30 kuna maneno haya: Hajar-al Aswad (jiwe jeusi) “kabla ya kuanza kuzu\nguka Al-ka’ba ni uzuri kwanza kuliendea hajar-Al Aswad lililoko Al-ka’aba hapo husogea karibi ikiea inayumkinika kikaribia bila ya kuumiza watu unalikabili Hajar-Al Aswad una lieekea mkona na bila ya kusema unalikabili Hajar-Al Aswad unaliweka mkono na bila ya kusema unalibusu mara tatu na kuligusisha kipaji chako cha uso mara tatu kwa wawake kufanya hivi ni suna ikiwa hapana zogo la dwaru, ikiwa hulifikiri liashire kea mkono. Tena mtu hurudi kwenye Hajar-al Aswad na kuligusa, kulibusu mara tatu na kugusisha kipaji cha uso mara tatu kama vile mwanzo tena utasema Allahu Akbaaar mara tatu (huku ukilashiria hajar kea mikono yote miwili ikisha utaongeza “Alla humma iimana bika wartaddika bikitabika wafaa biahdika wattibaa lisunnat nabiyyika salla ila hu Alayhi wassalim.” Kiwsaili. “ewe mola kwa imani yengu juu yako na kuthibitisha kitabu chako na kutekeliza ahadi yako uya kufuata mwendo wa mtume. Tena hapo utapita kulipita Hajar-Al Aswad ukilielikea huku ukiendelea kuzunguka Al-ka’aba yote nzima.
  5. kumbuka tendo la kuzunguka Al-ka’aba lilifanya washirikina na dwapagani wa kiarabu zama za ujahilia kabla ya dini ya uislamu kuanza. Na waislamu noo huizunguka Al-ka’aba swali je, waislamu hawakurithi eneo la ibada za ujahilia tafakari.

Mungu wetu yehova anavyotufundisha kuhusu ibada ya jiwe.

Mambo ya walawi 26:1

Msifanye sanamu yeyote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jifee lolote lililochorwa katika nchi yenu ili kilisujudia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana mungu wenu.

Kadiri ya mafundisho ya mungu wet yehova ambaye wakristo tumuabudu ni kakosa makubwa kuchukua jiwe na kulisujudu. Tafakari kuhusu waislamu na matendo yao katika jiwe la jeusi “Hajarul Aswad.”

(xi) ibada ya kuzunguka majabali (vilimo) vya safaa na marwa huko makka kabla ya uislamu.

Qurani 2:158 suratul Al-Baaraqh (Ng’ombe jike) hakika safaa na marwa (majabali mawili yana yofanyiwa ibada ya kusai huko makka) ni katika alma za kuadhimisha dini ya mwenyezi mungu basi anayehiji kwenyu nyumba hiyo ar kufanya umra. Si kosa kwake kuvizunguka (vilima) hivyo viwili na anayefanya wema (atalipwa) kwani mwenyezi mungu ni mwenye shukrani na mjuzi wa kila jambo.

Ufafanuzi wa aya hiii ya 158 ulio katika qurani ni huu katika ibada ambazo hazisihi kufanywa ila makka ni hizi (a) Hijja na (b) umra. Na takriba zote mbili hizi ni sawa sawa ila zinakhitalifiana. Kidogo to. Moja katika hitilafu zao ni kuwa Hijja haifanyi ila miezi makhususi: na mwisho wa miezi ya Hijja ni kumi la mwanzo la mfungo tatu…ama mengine bi sawa. Nayo ni: (1) kuzunguka Al-ka’aba mara 7 (2) kwenda matiti mara 7 baina ya majabali hayo mawili ambalo moja linaitwa safaa na moja linaitwa marwa (3) kunyoa nywele au kuzikata. Majabali hayo kabla ya uislamu yalikuweka yamewekwa juu yake madanamu na makafiri wakiyaabudu. Basi ulipokuja uislamu. Waislamu wengine waliona labda si vizuri kufanya ibada haopo penye majabali hayo. Basi wakaambiwa kuwa si vibaya.

Maelezo ya aya hii yanafanana na yle yaiyo katika saqhih Al-Bukhari volii ukurasa wa 415-416 hadith no. 710 pale Asim alipomuuliza Anas bin maliki (A.S.) hivi: je, ulikuwa ukichukia kufanya tawaf (yaani kuzunguka) kati ya safaa na marwa? Akasema ndiyo kwaqsababu ni matendo ya kwaida (sherehe) iliyofanyofanyika wakati wa ujinga kutajua kabla ya uislamu kuja. Imesimuliwa pia kuwa Muhammad alifanjya tawwaf ya ka’aba na sa’I ya safa na marwa ili kuonyesha nguvu zake kwa safa na marwa. Hayo yamesimuliwa katika sahih Al Bukhari vol ii hadithi no.711. jambo linaloshangaza ni kuwa ibada hiyo ilifanywa na makafiri zama za ujahilia (ujinga) na waislamu nao wazunguka vilima hivyo isitoshe insshangaza kuona Allah mungu anayeabudiwa ba wislamu anayaita majabali hayo minshahilillah yaani alama za mungu au kwa kiingereza “symbols of Allah” hii ni ajabu kuona vilima vinaitwa hivyo.

Bwana yesu anatufundisha nini kuhusu ibada ya milima? Yohana 4:19-22

Yule mwanamke akamwambia bwana naona ya kuwa unabii, baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko yerusalemu ni mahali patupa sapo kuabudjiwa. Yesu akamwambia mama, unisadiki saa ubajyha ambayi gamtamwabudu baba katika mlima huu, wala kule yersalemu, ninyi mnaabudu msichokijua sisu tunaabudu tukijuacho kwa kuwa wokovu watoka kwa wayahudi.

Katika aya hizi Bwana Yesu anatuambia kuwa wale wanaofanya ibada katika mlima hawajui wachokiabudu. Ndugu tafakqari ibada ya waislamu katika vilima je, wanajua wanachokiabudu?

(xii) mwezi wa ramadhani.

Tunaposoma katika kitabu cha maisha ya muhammaf ukurasa wa 32 kilichotungwa na sheikh Farsy tunaona kuwa miezi iliyotumiwa na waarabu kabla yo dini ya uislamu ndiyo inayotumiwa ba waislamu. Kitabu hicho kinasomeka hivi…”Makka tangu kabla ya uislamu, ilikuwa ni mahali patakatifu kwa waarabu wote. Kila mwaka walikuwa wakija kuhiji miezi hii hii wanayoitumia sasa waislamu katika kuhiju kwao.

Waarabu walikuwa washirikina na wapagani majahilia. Walikuwa na mwezi wa ramadhan nalo ndio mwezi ambao dwaislamu wana amini kuwa Muhammad alipata utume. Tazama kitabu cha maisha ya Muhammad ukurasa 16-17.

Ibada ya kufunga katika mwezi wa Ramadhan kwa waislamu

Qurani 2:183 suratul Al-Baarah (Ng’ombe jike)

Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga (saumu) kama walivyoiazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha mungu.

Imeelezwa katika sahih Bukhari volii Hadith 662 vol. Iii Hadith no. 219 na 220 pia vol vi Hadith no.31 ya kuwa Muhammad aliamuru waislamu wafunge siku ya Ashura siku ya 10 ya mwezi kwanza katika mwaka wa kiislamu yaani mweziuitwalo muharram) kufunga huko kaqbla ya uislamu ilikuwa ni desturi katika dini ya Hums na uislamu ukaichukua.

(xiii) kumpiga mawe shetani katika bonde la wadah muhassir.

Miongoni mwa tendo moja kubwa linalofanya na waislamu wanapofika hija huko makka ni kumpinga mawe shetani. Kitabu kiitwacho vipi uhiji ukurasa wa54,55,61 kuna maneno haya…”Mahujaji wanapofika bonde liitwalo wadi ah muhasisi karibu na mina ni suna kunyapuka hao huelikea jamrat al a quba (shetani mkubwa) na hupiga yale mawe saba waliyoyaokota muzdelifa baada ya kupiga mawe jamarati Al-Aqaba hufuatiwa na kuchinja.

Kwa sisi wakristo tunajua shetani ni roho ya uasi waefeso 2:1-5 na ni roho ya udanganyifu 1 Timotheo 4:1-2. Hivyo huwezi kumshinda shetani kwa kumpiga kwa mawe maana ni roho tu. Roho ni upepo au pumzi. Biblia inatufundisha kuwa tunamshinda shetani kwa njia ya imani sahihi ya mungu, kushika neon la mungu, dala, na maombi, hivyo tutamshinda shetani soma waefeso 6:11-18.

  1. Wajibu wa Mkristo baada ya kuujua uislamu.

Ninaamini kuwa imejifunza mengi kuhusu dini ya uislamu, na umeona mambo mengi yuanayotendeka na waislamu kule makka wakati wa hija. Mambo hayo yalifanywa na makureshi na waarabu wenzao kabla ya dini ya uislamu kuja, na tena umeona kuwa mungu tunayemwabudu wakristo hataki ibada zinazoshirikisha mawe na milima. Basi wajibu wako mkristo kuwafikishia injili waislamu na watu wa dini nyingine zisizomuamini Bwana Yesu, ili wamdwamini na wapate kuokolewa. Kumbuka injili ndio uweza wa mungu uletao wokovu Warumi 1:16. na tena injili ndilo neon la kweli Wakolosai 1:5. bwana akubariki sana ni mimi katika utumishi wa Bwana Yesu Mwalimu;

Eleutary H. Kobelo.

JE ISA BIN MARYAMU NDIYE YESU KRISTO?

 


JE , ISA BIN MARYAMU NDIYE YESU KRISTO?

Utangulizi

Kwa miaka mingi sasa imekuwa ni kawaida kuwasikia Waislamu wakifundisha jamii kuwa Isa bin Maryamu” kama Qurani inavyofundisha ndiye “Yesu Kristo”. Mafundisho haya Hivi sasa yanaendeshwa kwa mtindo wa kulinganisha aya za Biblia na Qurani. Wahadhiri wa dini ya kiislamu wanaendesha Mihadhara ambayo imeenea sana duniani na hasa zaidi katika nchi za Africa ya Mashariki na Kati (East and Central Africa). Wahadhiri hao pia huchapisha vijarinda na kurekodi kanda(Cassette) za Audio na Video, ambazo zimesababisha baadhi ya Wakristo waamini kuwa Isa Bin Maryamu ndiye Yesu Kristo. Swali la msingi kwa Wakristo wote; Je, ni kweli kuwa Isa bin Maryamu ndiye Yesu Kristo? Nakusihi fuatilia somo hili ili kujua ukweli.

SEHEMU KUU NANE ZA SOMO HILI

  1. Hoja zinazotumika na Waislamu kusema Isa ndiye Yesu.
  2. Je,Mama wa Isa ndiye wa Yesu?
  3. Maana ya jina Isa

4. Maana ya jina Yesu

  1. Je,kuzaliwa kwa Yesu ni sawa na Isa?

6. Je,Isa bin Mariam ni Mwana wa Mungu?

7. Je,Mamlaka ya Isa na Yesu ni sawa

8. Ikiwa Yesu ndiye Isa je, Isa alikufa?

9. Ujue umuhimu wa kumuamini Bwana Yesu


1.Hoja zinazotumika na waislamu kusema Isa ndiye Yesu.


1.Hoja ya kwanza – Mama wa Isa jina lake Maryamu

Qurani 3:45 Suratul Aal-Imran (watu wa Imran)

(Kumbukeni)waliposema malaika, “Ewe Maryamu Mwenyenzi Mungu anakupa habari njema za (kumzaa mtoto bila mume bali kwa kutamka] Neno tu litokalo kwake (la kumwambia zaa ukazaa pasina kuingiliwa) jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na ahera na miongoni mwa waliopelekwa mbele na Mwenyenzi Mungu

Marko 6:3-4

Huyo si yule seremala, mwana wa Mariamu na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. Yesu akawaambia “Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake na nyumbani mwake.

Hapa Waislamu wanasema kama vile Qurani inavyofundisha jina la Mama wa Isa ni Mariamu kadharika Biblia inafundisha jina la Mama yake Yesu ni Maryamu. Hivyo wanasema kuwa Yesu ndiye Isa. Soma pia Mathayo 1: 18-21 na Yohana 2:1

2.Hoja ya pili Isa ni Mtume wa Allah kwa Waisraeli

Quran 4:171 Suratul An Nisaa (Wanawake)

Enyi watu wa kitabu msipindukie mipaka katika dini yenu, wala msiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila yaliyo kweli. Masihi Isa bin Maryamu ni mtume wa Mwenyenzi Mungu…

Hapa tunaona kuwa Qurani imemtaja Isa kuwa ni Mtume, je, mtume kwa akina nani? Endelea kusoma aya hii katika Qurani.

Quran 61:6 Suratul As Saff [Msitari wa vita/Wajipangao safusafu]

Na (wakumbushe) aliposema (Nabii) Isa bin Maryamu (kuwaambia mayahudi) enyi wana wa Israili! mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu. Nisadikishaye yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati. Na kutoa habari njema ya mtume atakayewajia nyuma yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad...Soma pia katika Quran 3:49 Suratul Aal Imran

Aya hii inathibitisha kuwa Isa ni mtume kwa Waisraeli. Je, Yesu ni mtume kwa akina nani?

Waislamu wanaoendesha mihadhara pia husoma aya hizi za Biblia

Waebrania 3:1

Kwa hiyo ndugu watakatifu wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtakafarini sana mtume na kuhani mkuu wa maungamo yetu Yesu.

Mathayo 15:24

Akajibu, akasema, “Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli”

Kwa hivyo kama Quran inavyofundisha kuwa Isa mwana wa Maryamu ni mtume kwa Waisraeli ndivyo Biblia inafundisha kuwa Yesu ni mtume kwa waisraeli hivyo basi Isa ndiye Yesu. Hivi ndivyo wahadhiri wa dini ya Uislamu wanavyoifundisha jamii. Je, hoja hii ni sahihi nitajibu huko mbele:-

3.Hoja ya tatu

Isa bin Maryamu alifanya miujiza

Qurani 5:110 Suratul Al Maidah (Meza)

(kumbukani tena) mwenyenzi Mungu atakaposema ,Ewe Isa mwan wa MaryamuKumbukeni neema yangu juu ya mama yako.Nilipokusaidia kwa [kukupa kuwa na wewe ]Roho takatifu[Jibrili],ukazungumza na watu [maneno ya nafuu]katika utoto[wako] na katika utu-uzima [wako].Na [kumbuka].Nilipokufundisha kuandika na [nikakupa] hikima,Taurati na Injli na ulipotengeneza kwa udongo sura za ndege kwa idhini yangu,na ulipo waponesha vipofu na wenye mbalanga kwa idhini yangu,na ulipowatoa [baadhi ya] wafu [makaburi mwao] kwa idhini yangu,na Nilipokuzuilia wana wa Israili [wasikudhuru] ulipowafikia kwa hoja zilizo wazi;wale walio kufuru miongoni mwao wakasema:Haya si chochote ila ni uchawi dhahiri.

Waislamu wanasema huu ni ushahidi wakutosha kwani Allah anasema Isa alifanya miujiza mingi hii.

Isa aliponyesha vipovu ndiye …………….. Yesu aliponyesha vipovu Marko 10:46-52

Aliwafufua wafu makaburi ndiye………….. Yesu alifufua wafu Marko 5:21-43

Aliwaponyesha wenye mbalanga Ndiye…... Yesu aliponya Ukoma Luka 17:1

Wahadhiri wa kiislamu wanasema kama vile Qurani inavyosimulia kuwa Isa amefanya miujiza mingi, ndivyo Biblia inavyofundisha hivyo Yesu ndiye Isa isitoshe wanasema hivi:-

Isa bin Maryamu ni Nabii, Suratul An- Nisaa 4;171, kadhalika Biblia inafundisha kuwa Yesu ni Nabii, Yohana 6:14, Yohana 7:40, Luka 13:33,Luka 24:19, Marko 6:4 na Mathayo 13:57. kwa wastani Biblia inafundisha kuwa Yesu ni Nabii mara 12. Vile vile wahadhiri wa Kiislamu wanafundisha ya kwamba Isa ni Neno la Kiarabu ,katika kiingereza Jesus na kwa Kiswahili niYesu.Kupita vigezo hivi baadhi ya Wakristo wameshawishika kuamini kuwa Isa ndiye Yesu. Lakini, lazima tuzichunguze hizi hoja moja baada ya nyingine ili tujue ukweli.

2.Je,Mama wa Isa ndiye wa Yesu Kristo?

Hapo awali tumeona kuwa Mama wa Isa anaitwa Maryamu, Suratul Al Imran 3:45 na pia Mama wa Yesu anaitwa Mariamu Mathayo 1:18-21, Marko 6:3-4 lakini kufanana kwa majina hakuwezi kamwe kumaanisha kuwa ni mtu mmoja. kwani walio na Jina hilo ni wengi. Biblia inatufundisha hivi.

Yohana 19:25

Na penye Msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama, Mamaye, na umbu la Mamaye M ariamu wa Klopa na Mariamu Magdalena.

Hapa tunaona Mariamu watatu. Ili kutambua tofauti baina ya Mariamu Mama wa Isa na Mama wa Yesu, lazima tulinganishe ujumbe wa Qurani na Biblia. Qurani inasimulia kuhusu Baba na Kaka wa Mariamu Mama wa Isa hivi.

Suratul Al Tahrym 66:12 [kuharimisha]

Na Maryamu mtoto wa Imrani aliyejihifadhi nafsi yake na tukampuliza humo roho yetu, (inayotokana na sisi) na akayasadikisha maneno ya mola wake, na vitabu vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu (wakubwa)

Surah Al-Maryam 19:28

Ewe dada yake Haruni. Baba yako hakuwa mtu mbaya. Wala mama yako hakuwa hasharati.

Hapa tunaona kuwa Maryam Mama wa Isa Baba yake ni Imrani na Kaka yake aliitwa Haruni.

Tusomapo Biblia inatueleza kuwa Amrani aliwazaa hawa.

Hesabu 26:59

Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi binti wa lawi ,ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri;na huyo Yokebedi akamzalia Amram Haruni,na Musa,na Miriamu umbu lao.

Soma pia 1 Nyakati 6:1-3 na Kutoka 6:20

Huyo Amrani aliishi miaka mingi Kabla ya Yesu na, tena ametokana na kizazi cha Lawi mtoto wa tatu wa mzee Yakobo. Mwanzo 29:34 Kut. 2:1-10. Ikiwa Mariamu wa Qurami Baba yake ni Imrani basi atakuwa ameishi miaka 1500 kabla Mama yake Yesu hajazaliwa!

Je, Mariamu mama wa Yesu ametokana na kizazi gani?

Tunaposoma Biblia tunaona kwamba Yesu anaitwa mwana wa Daudi Mathayo 1:1 Marko 10:47 na Luka 1:27,32 ndio maana pia Yesu anaitwa Simba wa Yuda Ufunuo 5:5. Hivyo basi ukoo aliyetoka Yusufu na Mariamu Mama wa Yesu ni mmoja.

3.Maana ya Jina Isa.

Ni jambo la kawaida sana jina au majina kuwa na maana. Mfano majina haya ya kiarabu yana maana hizi. Muhammad linaamanisha mwenye kushukuriwa, Abdallah ni Mtumwa wa Allah Abu-Bakar maana yake ni Baba wa bikira, Abu Huraira ni Baba wa mapaka.

Aidha majina ya Kiebrania nayo pia yana maana. Malaki ni mtumishi au Mjumbe wa Yehova, Isaya ni Wokovu wa Yehova, Ezekiel inaamanisha Mungu hutia nguvu, Daniel Mungu ni Hakimu wangu.

Jina Isa maana yake ni hii.

Katika Qurani yenye jumla ya juzuu 30 Surah 114 aya 6236 maneno yenye kutamkika 76,440 herufi 322,373 jina Isa linatamkwa lisa au Aysi limetajwa mara 25. Isa pia ameitwa masihi mara 93. Lakini tunaposoma Qurani iliofarsiriwa na Imam Baidawi voI.1 ukurasa wa 160 ameeleza kuwa Isa jina la Kiarabu maana yake ni Wekundu unaozidiana na weupe.

4.Maana ya jina Yesu

Jina Yesu linatokana na lugha ya Kiebrania ‘Yehoshua’ katika lugha ya Kigiriki wanasema ‘Iesous’ inatamka ‘Yesous’ yaani Yesu. Katika lugha ya Kiarabu wanasema “ Yasu.”kwa kiingereza ni ‘’Jesus’’ Maana yake “Bwana anaokoa au Bwana ni Mwokozi”Soma aya hizi..

Mathayo 1:18-21 na Luka 2:8-11. Bwana maana yake Mungu ndiye mwokozi Isaya 43:6, 10-11. Katika Biblia ambayo ina jumla ya Surah 1189 aya 31,102 vitabu 66 39, Agano la kale na 27 agano jipya neno Mwokozi kiiengereza wanasema Saviour limetajwa mara 55. ikumbuke kwamba katika agano jipya jina Yesu au kiebrania Yehoshua kiarabu Yashua au Yasu limetajwa mara 1275 katika aya zipatazo 1226. zingatia pia kuwa agano jipya lina jumla ya aya 7930 na Sura 260 hivyo hapa tunaona jina Yesu maana yake ni Mwokozi na jina Isa ni wekundu uliozidiana na weupe. Kwa kuwa maana ya haya majina tofauti bila shaka Isa siyo Bwana Yesu.

5Je,kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni sawa na Isa?

1.Taarifa za Malaika kabla ya kuzaliwa kwao, kadiri ya Qurani na Biblia.

Jibrili alivyomtokea Mama wa Isa

Gabrieli alivyomtokea Mama wa Yesu

Alienda kwa Mariamu aliyekuwa msikitini Qurani 19:16-17 Saratul Mariam

  1. Alienda kwa Mariamu aliyekuwa Nyumbani kwake .Luka 1:26-28

  1. Mariamu Mama wa Isa haijulikani aliishi kijiji gani wala mji gani wala hata nchi haijulikani. Isitoshe Qurani inasema kuwa Jibrili ndiye aliyemleta utume Muhammed asiwapelekee Mayahudi (hana kosa),Soma Qurani 2:97 Suratul Al-Baqarah

  1. lakini Mariamu Mama yake Yesu alitokewa na malaika Gabrieli akiwa katika kijiji cha Nazareti mji wa Galilaya nchi ya Israel Luka 1:26

Mariamu Mama wa Yesu ni Myahudi.

2.Jibrili hakutoa salamu kwa Mariamu Mama wa Isa ila alijimithilisha kwa umbo la binadamu aliye kamili Qurani 19:7 Suratul Mariam

  1. Malaika Gabrieli alimsalimia Mariamu Mama wa Yesu Luka 1:28.

  1. Jibrili alimwambia Mariamu kwamba mimi ni mjumbe wa mola wako ili nikupe Mwana Mtakatifu Qurani 19:19 Suratul Mariam

  1. Jibrili alisema kwa Mariamu kuwa ili tumfanye mtoto muujiza kwa wanadamu QuranI 19:21Suratul Mariam. Isitoshe Jibrili hakutaja jina la Mwana kwa Mariamu. Bali alisema ili nikupe Mwana Mtakatifu.

  1. Lakini malaika Gabrieli alimwambia Mama waYesu kuwa utachukua mimba Luka 1:31

5. Malaika Gabrieli alisema kwa Mariamu Mama wa Yesu kuwa mtoto jina lake utamwita Yesu Luka 1:31, 2:21 Gabrieli hakusema kuwa atampa Mwana Mariamu. Bali alisema Roho mtakatifu atakujilia juu yako, yaani mtoto atazaliwa kwa uwezo wa Mungu.

2.Tofauti ya kuzaliwa kwa Isa na Yesu ni hii.

Isa bin Mariam.

Yesu Kristo.

  1. Isa alizaliwa katika shina la mtende Qurani 19:23 Suratul Mariam.

  1. Yesu kazaliwa katika hori la kulishia ng’ombe Luka 2:7

  1. Kuzaliwa kwa Isa haijulikani kama mimba ya mama yake ilichua muda gani maana malaika Jibrili alisema nikupe mwana mtakatifu mara akachukua mimba na kuzaa Qurani 19:22-23 Suratul Mariam.

  1. Lakini Mariamu Mama wa Yesu siku zake za kuzaa zilitimia Luka 2:6-7

3.Qurani haionyeshi kama Isa alitabiriwa na manabii kuwa atazaliwa

  1. Lakini Biblia inatuthibitishia kuwa manabii walitabili kuzaliwa kwa Yesu, Isaya 7:14, 9:6 utabili huu ulitolewa na Nabii Isaya miaka 750 kabla ya Yesu kuja kuzaliwa nao ulitimia Mathayo 1:18-23

  1. Isa haijulikani alizaliwa katika kijiji gani wala mji, wala nchi aliyozaliwa Qurani haikueleza.

4. Biblia inatujulisha kuwa Yesu alizaliwa Bethelehemu ya Uyahudi katika Mji wa Daudi umbali wa maili 5 toka kusini mwa Yerusalemu nchi ya israel Tazama Luka 2:8-16. Kuzaliwa kwake mahali hapo pia ni kutimiza unabii uliotowe na Nabii Mika miaka 750-686 kabla ya kristo kuja wakati wa wafalme – hawa wakitawala – Jotham, Ahaz na Hezekia wafalme wa Yuda. Yesu mwenyewe alizaliwa kama mwaka wa 4 wakati wa Mfalme Herode Mkuu akitawala Yuda tangu

  1. Isa aliongea na watu akiwa mtoto mchanga, na kusema kuwa yeye ni mja wa Mungu amepewa kitabu na amefanywa Nabii Qurani 19:30-33 Suratul Mariam.

  1. Yesu hakuongea na mtu akiwa mtoto mchanga. Alianza kuwauliza maswali na kutoa majibu akiwa na wazee Hekaluni akiwa na miaka 12 Luka 2:42-49.

Hivyo tunaona kwamba kuna tofauti nyingi tu kati ya Bwana Yesu na Isa.Swali kwako mfuatiliaji je, Isa bin Maryamu ndiye Bwana Yesu Mwokozi? Tafakari.

6.Je,Isa bin Mariam ni Mwana wa Mungu

Kama kuna jambo ambalo Allah Mungu anayeabudiwa na waislamu analikataa sana kupitia Qurani basi jambo hilo si lingine bali ni uwana wa Mungu. Allah anasema hivi.

Quani 6:101 Suratul Al-An-am [Wanyama]

Yeye ndiye Mwumba wa mbingu na ardhi. inamkinikanaje awe na mwana, hali hana mke. Naye ndiye aliye umba kila kitu (sio baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu.

Qurani 9:30 Suratul At-Tawba [Kutubu]

Na mayahudi wanasema “uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu;”na “Wakristo wanasema Masihi ni Mwana wa Mwenyezi Mungu” Haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasina na kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla yao, Mwenyenzi Mungu uwaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa!

Hili ni agizo la kutisha kwamba Wakristo na Wayahudi tuangamizwe kwa kuwa tumaamini Mungu ana Mwana au wana, lakini Wakristo tunaoamini hivyo kwa sababu Mungu wetu

1.Yehova alifundisha kuhusu Bwana Yesu hivi:

Kutoka 4:22 … Israeli ni mwanangu mimi...

Mathayo 17:5 ….Huyu ni mwanangu mpendwa wangu…

2.Malaika wa Mungu alisema hivi.

Luka 1:30-31,35

Malaika akamwambia usiogope Mariamu,kwa maana umepata neema kwa Mungu.Tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume;na jina lake utamwita Yesu. Malaika akajibu akamwambia,Roho Mtakatifu atakujilia juu yako,na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli;kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu Mwana wa Mungu.

Hivyo Isa siyo Mwana Mungu lakini Yesu ni mwana wa Mungu. Kwa hivyo Yesu siyo Isa.

7.Je,Mamlaka ya Yesu ni sawa Isa? .

1.Qurani inasimulia kuhusu Isa bin Maryamu hivi.

Qurani 5;75 Suratul Al Maidah (Meza)

Masihi bin Maryamu “si chochote ila mtume (tu).” (Na) bila shaka mitume wengi wamepita kabla yake (Hawajaona?) na mamake ni mwanamke mkweli (na) wote wawili walikuwa wakila chakula (na kwenda choo. Basi waungu gani wanaokula na kwenda choo?) Tazama jinsi tunavyo wabainishia aya, kisha tazama jinsi wanavyogeuzwa (kuacha haki).

Hapa tunaona Qurani inasimulia kuwa masihi Isa si chochote ila mtume tu.Hivyo hana Mamlaka. .

2.Mamlaka ya Bwana Yesu ni haya.

Mathayo 28:18

Yesu akaja kwao akasema nao akawambia, “nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.

Malaika Gabrieli alisema hivi.

Luka 1:30-33

Malaika akamwambia, “Usiogope Mariamu kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama utachukuwa mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyu atakuwa mkuu ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. Atamiliki nyumba ya Yakobo hata milele na ufalme wake utakuwa hauna mwisho

Bwana Yesu mwenye alisema hivi.

Yohana 17:1-2

Maneno hayo aliyasema Yesu;akainua mikono yake kuelekea mbinguni,akasema,Baba saa imekwisha kufika Mtukuze mwanao,ili Mwana wako naye akutukuze wewe;kama vile ulivyompa Mamlaka juu ya wote wenye mwili,ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele

Warumi 14:9

Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii awamiliki waliokufa na walio hai pia.

Hivyo basi Yesu ana mamlaka kwa watu wote wenye mwili na pia ni mfalme wa milele.

8.Ikiwa Yesu ndiye Isa je,Isa alikufa?

Jambo moja lenye kuleta utata miongoni mwa waislamu ni kuhusu kufa kwa Isa .Waislamu wa jumuiya ya Ahamadia wao wana amini kuwa Isa alikufa kifo cha kawaida kule India na siyo msalabani. lakini waislamu wa madhehebu ya Suni,Shia,Shafi, na mengineyo wanaamini kuwa Isa bin Maryamu hajakufa wakinukuu aya hii…

Qurani 4:157-158 Suratul An-Nisaa (Wanawake)

Na kwa (ajili ya )kusema kwao sisi tumemuua masihi Isa mwana wa Maryamu, mtume wa Mungu. Hali hawakumuua wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa (mtu mwingine wakamdhani nabii Isa.) Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika (hakika)hiyo (ya kumuua nabii Isa) wamo katika shaka nalo (jambo hilo kusema kauwawa]. Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo)hili (la kuwa kweli wamemuua nabii isa) isipokuwa wanafuata dhana tu.Na kwa yakini hawakumuua. Bali mwenyenzi Mungu alimnyanyua kwake. Na mwenyenzi Mungu ni mwenye nguvu (na)mwenye hikima.

Aya hii inasimilia kuwa Isa hawakumuua wala hawakumsulubu lakini ukianza kusoma aya ya

156 inasimulia hiv...

Qurani 4:156 Suratul AnNisaa (Wanawake]

Na kwa sababu ya kufukuru zao na kumzingizia Maryamu uwongo mkubwa (kuwa kamzaa nabii Isa kwa kuzini)

Hiki ni kisa cha kuhusu kuzaliwa kwa Isa, yaani dhama za utotoni ndio maana aya zinazofuatia zinasema hawakumua. lakini tukiendelea kusoma aya nyingine inasimulia hivi.

Qurani 21:7-8 Suratul Al Anbiyaa (Manabii)

Hatukuwatuma (hatuwapa utume) kabla yako ila wanaume (wa kibinadamu, si malaika) tiliowafunulia (tuliowaletea wahyi). Basi waulizeni wenye kumbukumbu (ya mambo ya zamani) ikiwa nyinyi hamjui. Wala hatukuwajalia (hao mitume kuwa] miili isiyo kula chakula, wala hawakuwa wenye kukaa milele(wasife).

Qurani 21:34 Suratul Al Anbiyaa

Nasi hatukumfanya mwanadamu yeyote kabla yako aishi milele.Basi ukifa wewe, wao wataishi milele?

Aidha Qurani inasema mitume waliokuja na hoja zilizo wazi wazi waliuwa Qurani 3:183 kadiri ya Qurani hiyo hiyo Isa alikuja na hoja waziwazi tazama Qurani 5:110

Isa mwenyewe alitabili mambo makuu matatu haya...

Qurani 19:33 Suratul maryamu

Na amani iko juu yangu siku niliyozaliwa na siku nitakayo kufa na siku nitakayofufuka kuwa hai.

Lipo fundisho kuwa Isa atarudi tena duniani aoe, azae watoto,ndipo afe harafu afufuliwe. Lakini fundisho hili ni dhana tu. Hakuna aya yoyote katika Qurani inayofundisha hivyo. Kumbuka Qurani inasema, “hatukufanya mwanadamu yeyote kabla ya Muhammad aishi milele asife kufa. Swali Je, Isa ni mwanadamu au la? Na je, ikiwa ndivyo aliishi kabla ya Muhammad au baada ya Muhammad? Vyovyote ilivyo iwe Isa amekufa au hakufa bado Isa siyo Yesu.

Bwana Yesu alisulubiwa na kufa na kufufuka siku ya tatu.

Yohana 19:18,33

Wakamsulibisha huko,na wengine wawili pamoja,mmoja huku na mmoja huku, naYesu katikati. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa,hawakumvunja miguu.

Mathayo 28:5-6

Malaika akajibu,akawaambia wale wanawake,Msiogope ninyi;kwa maana najua yakuwa mnamtafuta Yesu aliyesubiwa. Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema.Njoni,mpatazame mahali alipolazwa.

Aya hizi zote zinatudhibitishia kuwa Bwana Yesu alikufa na kufufuka.Hivyo Isa siyo Yesu.

9. Ujue umuhimu wa kumwamini Bwana Yesu

Baada ya kujifunza kwa urefu kuhusu tofauti kubwa kati ya Isa na Bwana Yesu. Na kugundua kuwa Isa siyo Bwana Yesu hata kidogo. Pengine sasa unaweza kubaki na mawazo kuwa huyu Isa mbona Qurani inamwita Nabii! tena inasema ni mtume. Tazama Qurani 19:33 na 61:6. Pia Isa kapewa injli Qurani 57:27.Je, kwa nini nisimwamini? Tukisoma Biblia inayotuongoza Wakristo haitupasi kushtuuka na kuamini tu ili mradi mtu ameitwa mtume au nabii, jambo kubwa ni kupima huo utume wake au huo unabii wake, je umetokana na nani? Tukiongozwa na aya hii…

1Yohana 4:1

wapenzi misiiamini kila roho bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na Mungu. Kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.

Bwana Yesu alituonya kuwa watatokea manabii wa uongo Mathayo 24:24. Nao tutawatambua kwa matunda yaoYaani mafundisho.

kuhusu Mitume Biblia inatufundisha hivi...

2 Wakorintho 11:13-14

Maana watu kama hao ni mitume wa uongo watendao kazi kwa hila,wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.Wala si ajabu.Maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

Majibu kuhusu hoja ya kusema Isa kapewa injili ni haya…

Wagalatia 1:6-9

nastaajabu kwa kuwa mmemwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kuigeukia injili ya namna nyingine.Wala si nyingine;lakini wapo watu wawatabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. Lakini ijapokuwa ni sisi au Malaika wa mbinguni akiwahubiria ninyi injili yeyote isipokuwa hiyo mliyoipokea na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiria ninyi injili yeyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.

Kadiri ya Biblia injili ya kweli ni ile inayofundisha ya kuwa.Yesu alikufa,na kufufuka ili atuokoe.Injili isiofundisha hivyo ni ya uongo.Tafakari kuhusu Isa!

Kumfuata Yesu kuna umuhimu mkubwa maana Yesu mwenyewe anasema hivi…

Yohana 14:6

Yesu akamwambia,Mimi ndimi njia,na kweli,na uzima mtu haji kwa Baba,ila kwa njia ya mimi.

Isitoshe Bwana Yesu ndiye atakayemlipa kila mtu.

2 Wakorintho 5:10

kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyoyatenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mabaya au mema.

Ikumbukwe kuwa Isa bin Maryamu hana sifa hizi hata moja kadiri ya Qurani. Hivyo basi ninategemea umeweza kujua kuwa, Isa bin Maryamu siyo Bwana Yesu hata kidogo.

Nimatuimaini yangu kuwa utafikisha ujumbe huu kwa watu wa mataifa ili wamwamini Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo,ili waokolewe. Bwana akubariki sana.

Ni mimi katika utumishi wa Bwana Yesu

MWALIMU

Saturday, September 5, 2020

Seventh Day Adventism is Fatally Flawed!

 

Seventh Day Adventism is Fatally Flawed!

Seventh Day Adventism is a religious group founded by Ellen G. White, whom they consider a prophetess. They especially magnify the Saturday Sabbath command given to Israel. Regarding the Lord Jesus Christ, they wrongly teach Jesus is Michael the archangel (like Jehovah's Witnesses do), but the Seventh Day Adventists believe in his deity, unlike the JWs who wrongly deny the deity of Jesus Christ! In other words, the Seventh Day Adventists believe Michael the archangel is God!

seventh day adventistThe writings of Ellen G. White, their prophetess, are of extreme importance to them. Those same writings display her heretical and dangerous views of the mark of the beast and distort the atonement.

Strange as it might sound to Christians, Seventh Day Adventists think Sunday worship is the mark of the beast in the bible! The sinister effects of that single doctrinal error will not be manifested until the real mark of the beast is revealed, but its identity will be hidden from them because they have been taught the mark of the beast is something totally different!

Furthermore, they imply from their errant doctrinal view that if someone takes the mark of the beast, he can afterwards repent and be saved. That too is dangerous, for that is NOT the message of God delivered through the third angel in Revelation.


seventh day adventism Did The Early Christians Observe a Saturday Sabbath Until Constantine?

Over the years, zealous Saturday Sabbatarians, especially Seventh Day Adventists, have contacted our ministry about early Christianity and their alleged observance of the Saturday Sabbath until it was changed by the Catholic church under Constantine in the fourth century.
sabbath commandseventh day adventism Isa. 66:22,23 is Not a Solid Argument for Saturday Sabbath Keeping
The Isa. 66:22,23 argument for Saturday Sabbath keeping is common in Saturday Sabbath Keeping circles, but not a solid argument.
seventh day adventism Ellen G. White Fact Sheet
In Seventh-Day Adventist (SDA) circles, a vision that Ellen G. White (EGW) had in 1847 is important to their exaltation of the Sabbath command:
seventh day adventism Who Is Michael The Archangel
The SDA people have been WRONGLY taught Jesus is Michael the archangel!
seventh day adventism Seventh Day Adventism and The Mark of The Beast
Probably the strangest view of the mark of the beast can be found among the Seventh Day Adventists.
sabbatarians
seventh day adventism The Wicked Dead - Will They Experience Annihilation or Eternal Torment?
As with any point of doctrine, one must carefully search the Scriptures for an answer to this important question (2 Tim. 3:16, 17). This cannot be stressed too much, for it is only in the Scriptures that we can learn God's truths.
seventh day adventism Six Facts For Saturday Sabbatarians To Ponder | Print this as a tract in pdf format (change your printer settings to legal and landscape).

seventh day adventism Ecclesiastes -- Almost Everything Is Vanity and Meaningless

Ecclesiastes is a book that Seven Day Adventists like to use when trying to teach soul sleep. You'll find out much in this review of that book.
seventh day adventism Seventh Day Adventists Think The Mark of The Beast Is Sunday Worship!
For a Saturday Sabbatarian to say Sunday worship is the mark of the beast is a GRAND and GLARING scriptural error. Read why this is so here.
seventh day adventism
OTHER TOPICS:

Messianic Jews Have Reintroduced DEADLY Galatianism

Find Peace With God

Plan Of Salvation

Angels, Demons and Satan

Former Roman Catholic

Evangelical Outreach Alphabetical Map

Contact Us Or Join Our Internet Church

Evangelical Outreach
PO Box 265
Washington, PA 15301

www.EvangelicalOutreach.org
www.EternalLifeBlog.com

Neuroplasticity, Spiritual Formation, and Holistic Redemption in Christ

Neuroplasticity, Spiritual Formation, and Holistic Redemption in Christ By Dr. Maxwell Shimba, Shimba Theological Institute Introduction ...

TRENDING NOW