Utangulizi
Tafadhali angalia Biblia Takatifu au Fungua Bibilia Takatifu iliyo bure na tamatisho zifuatazo kutoka Taurah (Mwanzo), Zabur (Zaburi) na Ijil (Injili).
Injili inathibitisha ya kwamba Yesu alizaliwa kutoka kwa bikira, hakuwa na makosa, alipelekwa mbinguni na Mungu na atarudi tena. Kulingana na Injili Yesu ni zaidi ya nabii. Yeye ni zaidi ya mtu aliye heshimiwa zaidi, utakatifu na baraka. Umuhimu wake kwa mwanadamu ni zaidi ya mponyaji mkubwa wa wagonjwa.
Utetezi wa Yesu kuwa Mwana wa Mungu:
Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia Mimi (Yohana 5:39).
Somo la kweli na Injili sio mafundisho au filosofia, ila ni mtu: Yesu Kristo. Yesu anatupa sisi msingi wa uhusiano wa dharura na uwiano kati yetu na Mungu. Huu uhusiano unafanya kazi kama chanzo cha uhakika na ujasiri.
Kwanini mwanishutumu kwa sababu nilisema ‘Mimi ni Mwana wa Mungu? (Yohana 10:36).
Wakati Injili inazungumza juu ya Yesu kuwa mwana wa Mungu, haisemi ya kwamba Mungu na Mariamu walipata mwana kwa njia ya kibaolojia. Hii ni dhihaka. Hii haiko katika Injili. Mariamu alikuwa bikira (Mathayo 1:18, Luka 1;34-35) Yesu ni mwana wa Mungu, aliyekuwepo toka mwanzo.
Vitu vyote vimekabidhiwa mikononi Mwangu na Baba. Wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia (Luka 10:22).
Mungu Baba ni Bwana wa mbingu na dunia. Kwa hili dai kamili kama kwa ufahamu wa Baba, Yesu ana onyesha uungu wake. Mstari huu unaonyesha asili ya Yesu inayoweza kufikiwa na kwamba hatuwezi kuwa na ufahamu ulio sawa na Mungu ila ni kupitia ufunuo. Kwa hivyo tunaweza kuwa na ufahamu wa Yesu lakini hatuwezi kumjua kikamilifu
Nilitoka kwa Baba na kuja ulimwenguni, sasa naondoka ulimwenguni na kurudi kwa Baba (Yohana 16:28).


.jpg)
.jpg)