Sunday, April 22, 2018

JE, UNATAKA THAWABU YA NABII?


Mathayo 10: 40-41 Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma. Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki.
Nabii anapoongea maneno ya baraka kwenye maisha yako, thawabu ni kwamba maneno hayo yatatokea, na matokeo yake ni unabarikiwa. Kama mtu wa Mungu akisema kwako "Mungu Akubariki", umebarikiwa haswaa! Hatahivyo, hii haitokei kwa kuwa tu yeye ni mtu wa Mungu. Inatokea kwasababu umempokea kama mtu wa Mungu.
Katika Marko 6, Biblia inaonyesha kuwa Yesu Alienda kwa Wayahudi na hawakumpokea. Madhara yake yalikuwa ni nini? Baraka zake hazikukaa nao. Biblia inasema hakuweza kufanya kazi yoyote kubwa kati yao; sio kwa sababu nguvu Zake zilishindwa, lakini ni kwa sababu hawakumpokea kama nabii. Walimdharau, wakisema, "Je, si huyu seremala, mwana wa Maria, kaka wa Yakobo, na Yose, na Yuda na Saimoni?na hawa si dada zake pamoja nasi hapa?na walikwazika naye" (Marko 6:3).
Usiwe hivyo. Amini na upokee Neno ambalo kutoka kwa ambaye Mungu Amemuweka juu yako. 2 Mambo ya Nyakati 20:20 inasema, "...mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa."
Shalom

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW