Thursday, April 12, 2018

YESU ALIDHIHIRISHWA KWA MIUJIZA NA AJABU NA ISHARA

Tuanze kusoma aya:
Matendo 2: 22 Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;
Siku hizi kume kuwa na tabia ya watumishi kui\pinga hili andiko. Neno linatukumbusha kuwa, Yesu Kristo alidhihirishwa kwa miujiza, na ajabu na ishara. Je, kuna miujiza na ajabu na ishara kwenye Kanisa lako?
Mpendwa, kama Kanisani kwako hakuna hii miujiza na ishara na ajabu, basi elewa kuna tatizo hapo.
Bwana Yesu kabla ya kuondoka alituambia hivi:
Marko 16: 17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
19 Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.
Je, mnatoa pepo Kanisani kwenu? Mnazungumza kwa lugha mpya? Naam, bado tuna mwendo mrefu sana, lakini, ukweli unabakia pale pale.
Sasa kama hakuna hii miujiza Kanisani kwenu, je, nyie mna tofauti gani na waislam na wapagani nk?
Mathayo 10: 7 “Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu”
Leo hii watu wanataka waaminiwe kwa maneno matupu bila kufanya matendo. Huwezi kufanya matendo ya Baba yako kama humwamini Baba yako. Yesu alipooza wagonjwa akaturuhusu sisi tukimwamini tunaweza kutenda kama yeye alivyotenda na zaidi ya yale aliyoyafanya.
Waefeso 3:20 “Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu”
Kuna nguvu itendayo kazi ndani yetu. Unapompokea Roho Mtakatifu nguvu inaingia ndani yako ambayo hauombi ili uwe nayo sababu tayari ipo ndani yako.
Yesu alifufua wafu, alipooza wagonjwa, alitakasa wenye ukoma, alitoa pepo na sisi tumwaminiye tunafanya kama yeye alivyofanya halafu alisema tutafanya zaidi yake kama tukimwamini.
Shalom
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13

Image result for miujiza na ajabu

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW