Thursday, September 19, 2013

Ndoto Yamfanya Al-Haji Mohammed Ampokee YesuAl-Haji Mohammed Ahmed alikulia kwenye familia ya Kiislamu. Anaitwa al-Haji kwa sababu alishaenda Makka kuhiji.


Mohammed anasema:”Maishani mwangu mwote nilikuwa Mwislamu thabiti sana. Katika familia yangu, lengo letu kuu lilikuwa kujenga misikiti na kueneza Uislamu kila mahali.” 


Akiwa kiongozi kwenye msikiti, Mohammed alihamasiaha vikundi vya waumini vilivyoenda mitaani kusaka Wakristo waliokuwa wakienda kanisani. Kisha waliwapiga na kuchoma moto Biblia. Mohammed hata alimshambulia Mkristo mmoja kwa kisu. Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya Mohammed.


Kisha usiku mmoja aliota ndoto ya ajabu. Mohammed anasema, “Wakati nikiwa nimelala, ilikuja sauti ya namna fulani kutoka mbinguni. Ikasema, ‘Mohammed, Mohammed, toka humo na unifuate.’”


Mohammed alijua kuwa ile ilikuwa ni sauti ya Mungu wa Wakristo. Asubuhi alipomsimulia mama yake, mama huyo alikataa kusikiliza na akamfukuza nyumbani.  Lakini kwa kuwa Mohammad alikulia kwenye familia yenye Uislamu mkali, alikataa kumfuata Mungu.


Hatimaye aliota ndoto nyingine. Safari hii, Mungu alikuwa amekasirika. Mungu alimwambia amfuate. Lakini Mohammed bado alikataa. Matokeo yake aliugua sana.


Anasema, “Sikuweza kula. Sikuweza kutembea. Sikuweza kuongea. Mzigo mzito ulinielemea. Nilienda kwenye hospitali mbalimbali kutafuta matibabu, lakini sikupona!”


Ndipo Mohammed alipowakumbuka wamisionari fulani waliowahi kumweleza habari za Yesu Kristo.


Anasema, “Nilihofia kuwa rafiki zangu na ndugu zangu wangeniua. Lakini niliamua kuwaita wale wamisionari na kuzungumza nao.  Walinieleza kuhusu Biblia na wakanitia moyo. Niliamua kumpokea Yesu kama Mwokozi wangu. Siku ileile, matatizo yangu na magonjwa yangu yote yalitoweka mwilini mwangu!”


Mohammed hakuwa peke yake aliyeamua kumpokea Yesu baada ya yale maono yake.


Anasema, “Nilimweleza mama yangu na watu wote wa familia yetu kuhusiana na uponyaji niliopata na wengi wao walimpokea Yesu.”


Japokuwa alijua kuwa ameshasamehewa, Mohammed bado alijisikia hatia kutokana na matendo yote ya nyuma aliyowatendea Wakristo.


Anasema, “Bado hadi sasa naendelea kuomba msamaha kwa yale niliyotenda huko nyuma.”


Hivi sasa, yule mtu ambaye Mohammed alimshambulia kwa kisu ni rafiki yake wa karibu sana. Wote walipatiwa mafunzo kwa lengo la kueneza Injili kote Ethiopia. Mohammed anasema kuwa kitu pekee kilicholeta urafiki kati yao na kuwawezesha kufanya kazi pamoja ni nguvu ya uponyaji ya Yesu Kristo.


Anasema, “Sina shaka hata kidogo kwamba Yesu ni halisi. Yeye ni amani yangu, uponyaji wangu, huduma yangu, na Mwokozi wangu.”

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW