Saturday, November 16, 2013
MUNGU ANASEMA KUWA HAUNA HATIA TENA
Warumi 5:8-9
Tunawezaje kusema kwamba Bwana ametutangazia kuwa" hatuna hatia " ya dhambi zetu? Jambo la kwanza la kuelewa ni kwamba katika kitendo hiki cha kututangazia kuwa hatuna hatia ya dhambi ilikuwa ni kazi ya Mungu Mwenyewe. Sisi kama binadamu hatuna uwezo wowote ule wa kuondoa hata doa dogo la dhambi zetu wenyewe. Ni kwa sababu hii Mungu Baba alimtuma Mwanae Yesu Kristo ulimwenguni.
Biblia inatuambia kuwa, moja ya malipo ya dhambi ni mauti (Rum 6:23), na kwa sababu Mungu alitaka kutuokoa kutoka adhabu hiyo ya mauti, basi, alitutengenezea njia pekee ya wokovu. Alitoa sadaka kamili: Mwana wake, Yesu Kristo (Rum. 5:08 ) ili afe kwa ajili ya dhambi zetu.
Je, hili tendo la upendo lilikamilisha nini? Lilituwezesha sisi kumwendea Mungu kupitia njia iliyo safi na takatifu, Biblia inasema kuwa Yesu Ndie Njia na Kweli na Uzima, Mtu haji kwa Baba ila kupitia Yeye. Usafi wetu ambao unatuwezesha kwende mbele za Mungu, hauna uhusiano na kitu chochote kila ambacho sisi tumefanya, bali unahusiana na unatokana na ukweli kwamba tumetakaswa na damu ya Yesu. Hivyo basi, tunaweza kusema kwamba " Tumeoshwa na damu ya Yesu" ambayo ndio njia pekee ya kuondoa doa la dhambi zetu.
Hivyo basi, tunapokwenda Mbele za Mwenyezi Mungu kwa kupitia Njia ya Yesu Kristo, kitu kinacho tokea hapo ni kuwa, mbele za Mungu tunaonekana kuwa hatuna Hatia ya dhambi- [kwa maneno mengine, Mungu anatangaza kwetu kuwa "Hatuna hatia dhambi]." Hii ina maana kwamba kama waumini/walio kombolewa na damu ya Yesu, tunaweza kusimama mbele ya Mungu Mtakatifu kwa ukamilifu, kwa sababu sasa Mungu anatuona sisi ni Watoto wake mwenyewe.
Je, damu ya Yesu inatufanya tusitende dhambi tena? Hapana. Hata hivyo, sisi kwa imani yetu katika Yesu Kristo kama Mwokozi tumepewa msamaha wa dhambi zetu kupitia damu yake pale tunalipo tubu na tunakuwa tumeokolewa kutoka hukumu ya Mungu (Warumi 8:01).
Tumshukuru Baba yetu aliye Mbiguni hii leo, si tu kwa ajili ya kutusamehe dhambi zetu, lakini pia kwa ajili ya kutukomboa kutoka mzigo “wa hatia” kupitia Mwanawe wa Pekee Yesu Kristo.
Mungu awabariki sana
Max Shimba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?
Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...
TRENDING NOW
-
Baba umenipa funguo muhimu katika Mathayo 16:19 za kufunga na kufungua. Ninatumia funguo hizo kufunga na kufungua, kuvunja na kubamiza kil...
-
Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaid...
-
Adui anakuja kuiba, kuua na kuharibu kila kitu chetu, ni lazima kuwa tayari kupambana na maadui, tujue silaha zetu, na kutumia neno la Mun...
-
Twakusalimu kwa mara ingine katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo Bwana wetu. Twazidi pia kukushukuru kwa ajili ...
No comments:
Post a Comment