Wednesday, November 27, 2013

YESU HAKUWA MUISLAM


USHAIDI WA KIBIBLIA NA KORAN

Waumini wa dini ya Kiislam wamekuwa na tabia ya kuseka kuwa, eti, Yesu alikuwa ni Muislam. Madai haya ya Waislam yamekuwa yakisemwa katika mihadhara yao ya kidini bila ya kuwa na ushaidi yakinifu kusaidia madai yao.
Leo nitajibu madai haya kwa kutumia Biblia na Koran kama ifuatavyo:

YESU HAKUWAI SEMA SHAHADA
Kufuatana na sharia za Kiislam, ili mtu awe Muislam lazima aseme na au afanya shahada. Yesu hakusema SHAHADA (La ilaha illallah) na hakuna ushaidi wa Kibiblia au Koran unao sema kuwa Yesu alisema SHAHADA. Hivyo basi, Yesu hakuwa Muislam.  

YESU HAKUWAI KUMWABUDU ALLAH
Yesu hakuwai kuomba na au kumwabudu “Allah”, lakini kutokana na Biblia, Yesu aliomba kwa Baba yake, Yohana 17:1 Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe. Koran na Uislam unakiri kuwa Allah si Baba na hakuna hata aya moja inayo mwita Allah Baba. Yesu hakuwa Muislam.

YESU HAKUWAI KUOMBA HUKU AKIANGALIA MAKKAH
Yesu hakuwai kusujudu huku akiangalia Makkah, jambo ambalo ni moja ya masharti katika kumwomba na au abudu “ALLAH”. Quran 2:149. Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na hiyo ndiyo Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yatenda. 150. Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande huo ili watu wasiwe na hoja juu yenu, isipokuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Basi msiwaogope wao, lakini niogopeni Mimi - na ili nikutimizieni neema yangu, na ili mpate kuongoka.

Sasa tumsome Yesu katika Biblia, wapi aliangalia wakati akiomba.
Yesu aliomba huku akiangalia Mbinguni soma: Marko 6: 41 Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akashukuru, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; na wale samaki wawili akawagawia wote. 
Katika aya tuliyo isoma hapo juu, imetupa ushaidi kuwa Yesu aliangalia Juu Mbinguni ambapo Baba yake alipo na si Makkah.

YESU HAKUFUNDISHA KUHUSU KAABA
Yesu hakuwai sema na au fundisha wanafunzi wake kuhusu “KAABA”. Jambo ambalo tunaona linafanywa na Waislam na lilifundishwa na Muhammad mtume wa Allah.

YESU HAKUFUNGA SWAUMU KILA MWAKA
Yesu hakuwa anafunga Ramadhani/Saumu kila mwaka, jambo ambalo ni sehemu ya Uislam kufunga ramadhani kila Mwaka. Quran 2:183, Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.

Hakuna hata sehemu moja katika Biblia ambayo tunasoma kuwa Yesu alitoa amri kwa wafuasi wake kuwa ni lazima wafunge swaumu kila mwaka, lakini tunasoma kuwa Mathayo 6:16-18: Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. 17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; 
18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. 

YESU HAKUFANYA JIHAD
Yesu hakufanya Jihad kama ilivyo amri ya kila Muislam kufanya Jihad. Quran 2:216. Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinachusha kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui. Lakini Yesu alisema yafuatayo kuhusu kupigana: Yohana 18: 36 Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa. 

Katika aya hapo juu, Yesu anatufundisha kuwa Ufalme wake si wa hapa Duniani bali Mbinguni, hivyo basi hawezi kufanya Jihad kama Allah alivyo waamrisha Waislam. Yesu hakuwa Muislam na hakufanya Jihad.

YESU ALISEMA PENDENI ADUI ZENU, WAKATI ALLAH ANASEMA WACHUKIENI WAKRISTO NA WAYAHUDI
Yesu hakuwachukia watu ambao walikuwa wanampinga, lakini aliwapenda na kuwaombea, kinyume na maamrisho ya Allah kwa Waislam wote. Soma Mathayo 5:44.  lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.

Sasa Msome Allah anavyo panda chuki kwa wafuasi wake. Quran 5:51. Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.

YESU HAKUFUNDISHA KUPIGA WAZINZI MAWE
Yesu hakupiga watu Mawe na wala hakufundisha kuwa Wazinzi wapigwe Mawe kama ambayo inafundishwa kwenye dini ya Uislam. Msome Yesu hapa: Yohana 8: 6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi. 7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. 

Lakini katika Uislam tunamsoma Muhammad akitoa amri ya kupigwa mawe mdhinifu: Volume 2, Kitabu 23, Namba 413:
Alisimulia 'Abdullah bin' Umar:
Myahudi kuleta kwa Mtume Muhammad watu wawili Mwanaume na mwanamke ambao walikamatwa wakifanya uzinzi kinyume cha sheria za ngono. Mtume Muhammad aliamrisha wote wawili wapigwe mawe mpaka kifo, karibu na mahali pa sadaka ya sala ya mazishi iliyopo kando ya msikiti.

Hivyo basi Yesu hakuwa Muislam na hakupiga wazinzi mawe lakini tunamsoma Muhammad akipiga watu mawe na akifundisha kupigwa mawe kwa Wazinzi katika Uislam.

YESU HAKUFUNDISHA WATU WATAWADHE KABLA YA KUOMBA
Yesu hakufanya na au fuata sharia za kuosha na au kutawadha kama ambavyo Waislam wanafanya kila siku. Msome Yesu katika Mathayo 15:2-11. Lakini Allah anafanya mila za kuosha na au kutawadha mwili kabla ya kumwabudu. Quran 5:6. Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi tayamamuni vumbi lilio safi, na mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.

Yesu hakuwa anatawadha kabla ya kumwomba Baba yake kama ilivyo katika Uislam. Yesu hakuwa Muislam.

YESU HAKUWAI TUMIA MANENO “SAW” AU “PBUH”
Yesu hakuwai waambia watu waandike vifupisho “SAW” na “PBUH” baada ya kutaja majina yao, kinyume chake Allah na Mtume wake wanafundisha kusema hivyo katika Uislam baada ya kutaja majina ya Mitume na Manabii.
Ndugu wasomaji, leo tumemsoma Yesu na tumesoma tabia yake  na mafundisho yake machahe ambayo yote yanapinga sheria na mila za kiislam.
Ni mategemeo yangu kuwa, kijarida hiki kitakusaidia kuelewa kuwa Yesu hakufuata mila za Kiislam na wala hakumwabudu Allah.

Mungu awabairiki sana


Katika Huduma Yake

Max Shimba

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW