Wednesday, April 16, 2014

PASAKA NI NINI NA MAANA YAKE


Pasaka ni sikuku iliyoamriwa na Mungu tangu siku za kale kwa wayahudi kuifanya katika mwezi wa Abibu au Nisani katika “kalenda ya kiebrania” yaani mwezi wa 3 au 4 katika kalenda ya kirumi, kwa lengo la kumbuka njisi Mungu alivyowakomboa kutoka utumwani Misri; Twasoma: “Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka BWANA, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA; Mungu wako. Nawe umchinjie pasaka BWANA, Mungu wako katika kundi la kondoo na la ng’ombe, mahali atakapochagua BWANA apakalishe jina lake.” (Kumbukumbu 16:1-2) Soma pia: (Kutoka 12:14) Kama tulivyoona katika pasaka wayahudi waliamriwa kuchinja mnyama mmoja katika kundi, lakini tunapoendela kusoma tunaona jinsia Mungu alivyoamuru mnyama huyo aokwe na kuliwa; Twasoma:

“Usimle pamoja na mikate iliyotiwa chachu; siku saba utakula naye mikate isiyotiwa chachu, nayo ni mikate ya mateso; kwa maana ulitoka nchi ya Misri kwa haraka; ili upate kukumbuka siku uliyotoa nchi ya Misri, siku zote za maisha yako. Wala isionekane kwako chachu muda wa siku saba katika mipaka yako yote; wala katika hiyo nyama uchinjayo siku ya kwanza jioni, kisilale cho chote usiku kucha hata asubuhi. Usimchinje pasaka ndani ya malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako; ila mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako apakalishe jina lake, ndipo mtakapomchinjia pasaka jioni, katika machweo ya jua, kwa wakati kama uliotoka Misri.” (Kumbukumbu 16:3-6); Soma pia: (Kut 12:3-13) Katika mwezi huo wa abibu ambao Mungu aliufanya kuwa mwezi wa kwanza kwako, Wayahudi walifanya karamu ya Pasaka kuwa kumbukumbu la jinsi Mungu alivyowaokoa kutoka Misri (Kutoka 12:1-51; Walawi. 23:5).

Pasaka maana yake ni "kupita Juu", maana Mungu alipita juu ya nyumba zao asiwaangamize wazaliwa wao wa kwanza; Twasoma: “Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazo kuwapo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu nitakapoipiga nchi ya Misri.” (Kutoka 12:13); Soma pia:(Kutoka 12:27)

JE WAKRISTO TUNA PASAKA LEO?
Ni kweli wakristo tuna pasaka leo, walakini si katika utaratibu ule Uliotumika katika siku za waisraeli, kama tulivyoshuudia maandiko yaneleza wazi ya kuwa sikukuu hizo zilikomeshwa; Basi hebu tuone utaratibu wa Pasaka ya wakristo leo ni upi;

Zingatia: Kama tulivyoona hapo juu, waisraeli waliokolewa na damu ya mnyama walio ipaka katika miimo na miisho ya milango yao na ndipo malaika wa Bwana alipotambua na kupita juu; Soma tena: (Kutoka 12:13, 27); lakini wakristo tunaambiwa pasaka wetu ni Yesu mwenyewe aliyetuokoa kwa damu yake; Twasoma:

“Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” (Yohana 1:29); Soma pia: (Yohana 1:36) “Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa milioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.” (1 Petro 1-18-19) “Basi jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mapate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;” (1 Wakoritho 5:7) Basi kama tulivyoona Neno la Mungu linatuthibitishia ya kuwa kwa sasa wakristo tunaokolewa na damu ya Yesu ambaye ndiye Pasaka wetu na si kwa damu ya mnyama aliyekuwa Pasaka wa kale. Basi kiwa hivyo ndivyo, ni dhahiri hata utratibu wa kusherehekea pasaka kwa wakristo ni tofauti, Basi hebu tuone wakristo tunasherehekeaje pasaka yetu leo.

Yesu alipokuwa akila Pasaka ya mwisho pamoja na wanafunzi wake, aligeuza Pasaka. Aliwaambia kwamba, kuanza siku ile, watakapokula mikate wangekumbuka mwili wake uliotolewa kwa ajili yao badala ya kukumbuka kuokolewa kutoka utumwani nchini Misri; Twasoma: “Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega akawapa wanafunzi wake, akisema, Twaeni mle; huu ndio mwili wangu Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.” (Mathayo 26:26-28) “Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa ninyi, ya kuwa usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, na ye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kwa kila mywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.” (1 Wakorintho 11:23-26).

JE WANAOSHEREHEKEA PASAKA YA KALE WAMEPOTEA?
Ni kweli karibu ulimwengu mzima unasherehekea pasaka kama walivyokuwa wakisherehekea wayahidi nyakati zile, wakidhani ndivyo ilivyo agizwa, basi na tuzingatie maneno yafuatayo; Twasoma: “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti” (Mithali 14:12) “Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa. Waacheni hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.” (Mathayo 15:13-14) “Si kila aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.” (Mathayo 7:21-23) “Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe.” (1 Wakorintho 4:6) Basi kama tulivyoona, upotofu uliopo katika sikukuu hii ya pasaka na jinsi Mungu anavyo tuonya kuwa makini na mafundisho ya uongo, ni dhahiri tunawajibu wa kujifunza neno la Mungu kwa bidii ili tupate kujua yaliyo mapenzi yake tukayafanye; Soma: (Yakobo 1:22-25)

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW