Sunday, June 21, 2020

IDRIS WA QURAN SIO اينوك aynuk HENOKO WA KWENYE BIBLIA



IDRIS WA QURAN SIO اينوك aynuk HENOKO WA KWENYE BIBLIA
Mwanzo 5:21-24
“ Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. Henoko akaenda pamoja na Mungu, baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana waume na wake. Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu Alimtwaa”.
Waraka wa Yuda 1:14-16
“Na Henoko mtu wa saba baada ya Adamu, aitoa maneno ya Unabii juu ya hao, akisema, angalia Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu, maelfu, ili afanye hukumu juu ya watu wote na kuwaadhibisha wote, wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda, bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote, ambayo hao wenye dhambi, wasiomcha Mungu wameyanena juu yake. Watu hawa ni wenye kunung’unika wenye kulalamika, waendao kwa tama zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno ya kiburi, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida”.
Mwisho wa ajabu wa maisha yake ulisababisha mapokeo ya kwamba alitwaliwa mbinguni (Ebrania 11:5). Kwa sababu hiyo alitumiwa kama mhusika mkuu katika maandishi mbalimbali ya kabla ya Kristo, na hata ya baada yake, hasa katika Kitabu cha Henoko. Katika Uislamu anaheshimiwa kama nabii kwa jina la Idris ingawa hili ni bandia na halipo kwenye Torati.
Lakini nilipo soma Suratul Maryam aya ya 56 na 57 nilikutana na jina hilia Idris na inadaiwa eti Idris ni Henoko wa Biblia. Je haya madai ni kweli?
Henoko kwa Kiingereza ni Enock
Henoko kwa Kiarabu ni اينوك aynuk
Henoko kwa Kiebrania ni חנוך
Sasa hili jina la Idris walilitowa wapi hawa Waislam
Kwenye Biblia ya Kiarabu kuna jina la اينوك aynuk na sio Idris jina bandia la Waislam.
Kulingana na Biblia, Henoko na Eliya ndio watu wawili pekee ambao Mungu alichukua mbinguni bila kufa. Mwanzo 5:24 inatuambia, " Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa." Wafalme wa pili 2:11 inatuambia, "... ghafla kukatokea gari la moto na farasi wa moto , likawatenga wale wawili, naye Eliya akaenda mbinguni kwa kimbunga." Henoko anaelezewa kama mtu ambaye "alitembea pamoja na Mungu kwa miaka 300" (Mwanzo 5:23). Eliya labda alikuwa Nabii mkuu wa Mungu katika Agano la Kale. Pia kuna unabii wa kurudi kwa Eliya (Malaki 4: 5-6).
Kwa nini Mungu aliwachukua Henoko na Eliya? Biblia haijat upa jibu mahsusi. Wengine wanasema kuwa walichukuliwa katika maandalizi ya jukumu katika nyakati za mwisho, labda kama mashahidi wawili katika Ufunuo sura ya 11: 3-12. Hii inawezekana, lakini haijafundishwa wazi katika Biblia. Inawezekana kwamba Mungu alipendelea kuokoa Henoko na Eliya kutokana na kufa kwa sababu ya uaminifu wao mkubwa katika kumtumikia na kumtii. Kwa hali yoyote, Mungu ana lengo lake, na wakati hatujui mipango na makusudi ya Mungu, tunajua kwamba "Njia yake ni kamilifu" (Zaburi 18:30).
Swali: Ipo wapi aya ndani ya Quran inayosema Idris wa Kiislam hakufa na alichukuliwa hai kama Henoko?
Je, Idris wa Quran aliishi miaka mingapi?
Hili jina la Idris wamelitowa wapi hawa Waislam maana halipo kwenye Torati?
HAKIKA UISLAM NI DINI BANDIA NA QURAN IMEJAA SHAKA.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13


No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW