Thursday, February 3, 2022

GAIDI WA KIKUNDI CHA KIISLAM CHA ISIS ABU IBRAHIM AL HASHEMI AMEJILIPUA

 



Rais wa Marekani Joe Biden amesema Kiongozi wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, Abu Ibrahim al-Hashemi al-Quraishi amejilipua mwenyewe katika operesheni iliyofanyika leo kaskazini-magahribi mwa Syria.

Afisa wa Marekani amesema al-Qurayshi alijilipua mwenyewe wakati wa operesheni hiyo, Al-Quraishi alirithi nafasi ya Abu Bakr al-Baghdad alieliongoza kundi hilo wakati lilipochukuwa udhibiti wa maeneo makubwa nchini Syria na Iraq.

Baghdad aliuawa Oktoba 2019 na Wanajeshi wa Marekani katika operesheni nchini Syria baada ya wapiganaji wa Dola la Kiislamu kushindwa katika uwanja wa vita.

Operesheni ya leo imekuja wakati IS ikijaribu kurejesha makali yake kwa kufanya msururu wa mashambulizi kwenye kanda hiyo yakiwemo ya siku 10 ya mwezi uliyopita yaliyolenga kuliteka gereza.


No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW