Thursday, September 19, 2013

Je, Muhammad Ametabiriwa Kwenye Biblia? – Sehemu ya II




Katika makala yaliyopita tuliona hoja za ndugu wa Kiislamu wanavyojaribu kwa juhudi nyingi kuonyesha kwamba Muhammad ametabiriwa kwenye Biblia.

Katika makala hayo niliahidi kuwa nitaeleza jinsi ambavyo hoja zao hazina ukweli wowote. Licha ya kwamba Mungu wanayemwamini amewahakikishia kwamba Muhammad ametajwa kwenye Biblia, ukweli ni kwamba hajatajwa hata kidogo!

Katika sehemu ya kwanza ya mfululizo huu, nilimalizia kwa kunukuu kile ambacho Yehova, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, anasema juu ya Neno lake. Hebu tuangalie tena baadhi ya maneno hayo. Imeandikwa:

Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho,tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.

Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. (1 Wakorintho 2:12-15).

Tatizo mojawapo kubwa ninaloliona mara nyingi kwenye Uislamu na Waislamu ni kutazama mambo kwa jinsi ya mwili. Hapo ndipo penye shida kubwa yanapokuja masuala ya rohoni.

Je, Mtume Muham-mad Yuko Wapi Hivi Leo?




Mungu hutufunulia mambo mbalimbali kupitia watumishi wake mbalimbali ili kutujulisha yale yaliyopo na hata yajayo; katika ulimwengu huu na pia ule ujao. Wapo watu wengi ambao Mungu amewatumia kutufahamisha juu ya mbingu na hata juu ya kuzimu.

Bo Ra Choi ni mchungaji kutoka Korea ya Kusini. Mchungaji huyu amekuwa akionyeshwa maono mbalimbali na Mungu kuhusu mambo ya ulimwengu wa roho. Mojawapo ya maono aliyoonyeshwa yanamhusu Muhammad, mtume wa Uislamu.

Je, Muhammad yuko wapi hivi leo? Katika video hii, mchungaji Bo Ra Choi anafikisha kwetu ujumbe kwa namna ambavyo alisikizishwa Muhammad akisema kule aliko sasa.

Kwa maana nyingine, ananukuu moja kwa moja maneno ya Muhammad ili kwamba iwe ni kama vile tunamsikia Muhammad akizungumza.

Tafadhali zikiliza kwa makini video hii, kisha utaupata ujumbe wa Mungu anaouleta kwetu kupitia mtumishi wake, Mchungaji Bo Ra Choi.

Toufik Alikuwa Mwislamu Lakini Alimwita Yesu, Leo Ameokolewa na Hajawahi Kujuta


Ufuatao ni ushuhuda wa Toufik, ambaye alikuwa ni Mwislamu lakini alikutana na injili ya Bwana Yesu na kubadili welekeo ambao hajaujutia; na hata anapoelezea neema hii ya wokovu wa Yesu aliyoipata, machozi yanamtoka. Pia machozi yanamtoka zaidi anapowafikiria ndugu zake Waislamu ambao wanapambana kwa jitihada nyingi wakijaribu kumpendeza Mungu kwa njia ya matendo yao ya kidini. Toufik analia anapotambua kuwa yote hiyo wanayofanya ni kazi bure kwa kuwa hawajagundua ziri ambayo na yeye, miaka mingi iliyopita, alikuwa hakuijua.


......................

Nilikulia kwenye familia ya Kiislamu ambayo ilikuwa inatii imani ya Uislamu. Nilipokuwa na miaka mitano nilienda shuleni. Na wakati huohuo nilihudhuria msikitini na kufundishwa kuhusu Uislamu.

Nilipokuwa nikimtafakari Allah, sikumuona kama Mungu mzuri, Muumba anayependa viumbe wake. Nilimuona kama Mungu mkubwa sana ambaye wakati wowote alikuwa tayari kuniharibu.

Hata mimi mwenyewe sikujiona kama mtu anayekwenda mbinguni. Nilipotazama matendo yangu mazuri na yale mabaya, sikuona uwezekano wa mimi kupona.

Nilijiuliza maswali mengi: Hali yangu ya kiroho ikoje? Mungu yuko wapi sasa? Hivi mimi anaponiangalia ananionaje hasa? Anawaza nini juu yangu? Hivi ndio nimetengwa kabisa naye kutokana na dhambi zote nilizofanya? Je, kuna njia ya kumrejea? Nawezaje kurejea tena kwake?

Yesu Aongea na Binti wa Kiislamu; Binti Aokoka




Sharoni hakuwa Mkristo bali alikuwa ni binti wa Kiislamu. Na wala hakuwa amewahi kujifunza habari za Yesu na Ukristo. Lakini Bwana Yesu mwenyewe alimfuata na kujidhihirisha kwake. Je, ilikuwaje, na nini kilitokea baada ya hapo? Tafadhali fuatilia ushuhuda huu wenye nguvu na unaodhihirisha upendo na uweza na uungu wa Bwana Yesu.

……………………………….

Jina langu ni Sharoni Sabina Natrajan. Kwa sehemu kubwa ya maisha yangu nilikulia Bombay. Familia yangu si Wakristo. Kwa hiyo sikuwahi kupata mafundisho yoyote ya Kikristo. Natokea kwenye familia ambayo inathamini sana elimu, na kila mtu ana elimu ya kutosha. Upande wa mama yangu, anatokea kwenye ukoo wa Zaminda. Na hata nyakati zile, wavulana na wasichana walikuwa na elimu kubwa.

Baba yangu ni injinia ambaye amesoma kwenye chuo kinachoheshimika sana, na anashikilia cheo kikubwa kwenye makampuni ya kimataifa hapo Bombay.

Sisi ni familia ndogo tu yenye mimi, dada yangu, baba na mama. Tangu nikiwa mdogo, nilikuwa ni mtu ninayependa masuala sanaa (creative arts). Nilisomea na kuhitimu katika sanaa za maonyesho na pia uchoraji. Kwa hiyo, maisha yangu yote ya utotoni yalikuwa yamejikita kwenye mambo haya.

Wazazi wangu walikuwa na upendo sana na nilipata kila nilichohitaji. Sikupungukiwa na chochote maishani mwangu.

Baba yangu alipenda sana nisomee uinjinia, licha ya kuwa wakati nikiwa sekondari ya juu nilikuwa tayari nikifanya sanaa za maonyesho kote nchini – kucheza ngoma, maigizo,n.k. Sasa, kwa kuwa alitaka niwe injinia, nilituma maombi na kupata nafasi kwenye chuo kizuri sana. Uinjinia haukuwahi kuwa jambo la moyoni mwangu, lakini nilifanya hivyo ili tu kuwafurahisha wazazi wangu. Kwa hiyo, nilienda Puna kusomea uinjinia lakini wakati huohuo nilikuwa nikifanya sanaa za maonyesho.

Mungu Amwonyesha Nabeel Njia ya Kweli Kati ya Uislamu na Ukristo - Sehemu ya 2




Katika sehemu ya kwanza ya ushuhuda huu wa Nabeel, aliyekuwa Mwislamu kisha akakutana na Bwana Yesu na kupokea wokovu, tuliona jinsi ambavyo alimwomba Mungu ampe maono yatakayomwonyesha imani ya kweli. Alionyeshwa misalaba kwenye maono lakini yeye akasema labda ni macho yake tu yamemchezea mchezo. Kwa hiyo, alimwomba tena Mungu kwamba, kama yale maono yalitoka kwake, basi ayathibitishe kwa ndoto. Je, Mungu alifanya nini? Tafadhali endelea kusoma sehemu hii ya pili.


…………………………………

Mungu alinipatia ndoto ile kwa uwazi sana kiasi kwamba sikuwa na ulazima wa kuitafsiri. Lakini ilikuwa wazi hata zaidi kuliko nilivyotarajia. Saa chache baadaye niliwasiliana na David na kumwambia kuwa nimeota hivi na hivi.

David aliniambia, “Sina ulazima wa kutoa maoni yangu juu ya hilo. Kila kitu kiko kwenye Biblia.”

Nikasema, “Unasemaje?”

Akasema, “Nenda kwenye Luka 13.”

Nilienda kwenye Luka 13 mstari wa 22 hadi 29. Niliposoma nikakuta kumeandikwa kuhusu kuingia kwenye Ufalme wa Mungu, na Kristo akasema kwamba, wengi watajaribu kuingia lakini hawataweza. Jitahidini kuingia kupitia mlango mwembamba. Na watu watakuwa wamesimama kwenye mlango huo wakibisha hodi.

Na hicho hasa ndicho kilichotokea kwenye ndoto yangu. Nilikuwa kwenye huo mlango ambao ulikuwa haujafungwa bado. Fursa ya mimi kuingia humo kwenye kushiriki sherehe ile ilikuwa bado ipo. Nilichotakiwa tu kufanya ni kukubali mwito.

Mungu Amwonyesha Nabeel Njia ya Kweli Kati ya Uislamu na Ukristo - Sehemu ya 1




Nabeel alizaliwa na kukulia kwenye familia na maisha ya kiislamu. Uislamu ulikuwa ni kila kitu kwake. Lakini wakati ulipofika wa yeye kujua jema na baya, alianza kujihoji kuhusu maisha yake, Mungu wake, na hatima yake ya milele. Hatimaye alimwomba Mungu amwonyeshe kweli. Je, nini kilitokea? Tafadhali fuatilia sehemu hii ya kwanza ya ushuhuda huu.

……………………………………

 Nilipokuwa mdogo, wazazi wangi walikuwa wacha Mungu sana. Mimi nami nilikuwa mcha Mungu sana kwa sababu yao. Wazazi wangu walinifundisha kumwomba Allah kila wakati. Niliswali sala tano kwa siku ambazo ni za lazima. Lakini pia niliswali swala zaidi ya hizo. Swala ilikuwa ni sehemu muhimu kabisa ya maisha yangu. Kila nilipoamka asubihi niliomba mara tu nilipofungua macho yangu. Kisha nilipoenda bafuni, nilikuwa nikiomba swala ya wakati wa kuosha mikono yangu. Pia niliomba swala kabla ya kusoma Quran na mara baada ya kusoma Quran, ambayo niliisoma karibu kila siku.

Uislamu ulikuwa ndani yangu kabisa. Hivyo, wazazi wangu walikuwa wananifurahia sana maana nilikuwa ni aina ya mtoto wa Kiislamu ambaye walikuwa wanajivunia kumlea. Nilitokea kwenye familia ya kimisionari. Allah na mtume Muhammad walikuwa wanaheshimiwa sana. Allah alikuwa anaabudiwa muda wote.

Uislamu kwetu haukuwa tu ni dini, bali ulikuwa ni maisha yetu kabisa. Halikuwa ni jambo tulilofuata tu, bali zaidi sana hivyo ndivyo tulivyokuwa sisi wenyewe. Kwa hiyo, Uislamu ulikuwa ndiyo sehemu kabisa ya utu wangu.

Monday, September 2, 2013

YESU NI MUNGU


Adhama ambazo zina Yahweh pekee apatiwa Yesu Kristo:

1.   Yesu aliumba Ulimwengu:
Wakolosai 1: 16-17 Inasema: 16 Yeye ndiye aliyeumba vitu vyote mbinguni na duniani; vitu vinavyoonekana na visivyoonekana; kama ni viti vya enzi au nguvu, au watawala au milki na mamlaka: vyote viliumbwa na yeye kwa ajili yake. 17 Yeye alikuwapo kabla ya vitu vingine vyote na kwa uwezo wake vitu vyote vinahusiana kwa mpango.

Jambo hili lauumbaji lazima tuliwekee msisitizo kwasababu inafahamika kuwa ni Yahweh ndie aliye umba Ulimwengu, lakini katika kitabu hiki cha Wakolosai tunaona kuwa Yesu nayeye anapewa adhama hiyo ya uumbaji.

2.   Yesu anapewa adhama ya Umilele ambayo ni sifa pekee ya Mungu.
Yohana 8:58 Inasema:  58 Yesu akawa jibu, “Nawaambia wazi, kabla Abrahamu hajazaliwa, ‘Mimi nipo.’
Katika hiyo aya, Yesu anadai na kusema kuwa Kabla ya Ibrahimu kuwepo, yeye Yesu alikuwepo!!! Hii sifa ni ya Kimungu Pekee, kwani Mungu ndie pekee alikuwepo kabla ya uumbaji.
Na kwababu hiyo, Wayahudi wakashika Mawe ili wampige nayo Yesu.
Sasa tujiulize, je hawa Wayahudi wangetaka kumpiga Mawe Yesu kama haingekuwa ya kuwa alisikikika akikufuru kwa kusema yeye ni Mungu?

Ngoja tuongeze ushaidi zaidi wa Umilele kutoka Yohana 17: 5
Na sasa Baba nipe mbele yako ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe hata kabla dunia haijaumbwa.
Katika hii aya, Yesu anadai kwamba aliishi na Baba kabla ya dunia kuumbwa. Haya maneno ni ushaidi tosha kuwa kumbe Yesu aliishi kabla ya dunia kuumbwa na alikuwepo wakati wa uumbaji wa dunia.

3.   Yesu anapewa sifa ya kuwa kila mahali: (Omnipresent)
Mathay0 18:20, na Mathayo 28:20 Inasema:
20 Kwa maana wanapokutana watu wawili au watatu katika jina langu, hapo mimi nipo pamoja nao.”
Sifa ya kuwa kila mahali kwa wakati mmoja ni ya Mungu pekee, lakini Yesu anasema yeye hiyo sifa ni yake na anayo.

4.   Yesu ana adhama ya kufahamu yote:
Mathayo 16:21
Yesu Anazungumza Juu Ya Mateso Yake
21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaeleza wanafunzi wake kwamba hana budi kwenda Yerusalemu na kupata mateso mengi kutoka kwa wazee, makuhani wakuu na walimu wa sheria; na kwamba atauawa na siku ya tatu atafufuliwa.

5.   Yesu anapewa ADHAMA YA Mungu ya MUWEZA wa Yote:
Yohana 11: 38-44
Yesu Amfufua Lazaro

38 Yesu akafika penye kaburi akiwa amefadhaika sana. Kaburi lenyewe lilikuwa katika pango ambalo mlango wake ulikuwa umezibwa kwa jiwe.39 Akasema, “Ondoeni hilo jiwe.” Dada yake mare hemu, Martha, akasema, “Bwana, patakuwa na harufu kali kwani siku nne zimepita tangu azikwe.” 40 Yesu akamjibu, “Sikukuam bia kama ungeamini ungeuona utukufu wa Mungu?” 41 Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe. Yesu akaangalia mbinguni akasema, “Baba ninakushukuru kwa kunisikia.

TRENDING NOW