Zaheed alizaliwa kwenye familia ya Kiislamu. Baba yake na kaka zake wote walikuwa viongozi wa dini ya Kiislamu. Zaheed naye alifuata mkondo uleule.
Mara baada ya kuhitimu masomo ya dini na kukabidhiwa msikiti, chuki yake na kutokuwa na uvumilivu dhidi ya Wakristo kulianza kujionyesha waziwazi.
Zaheed anasema, “Nilikuwa nawakusanya vijana kwenye msikiti wangu na kuwachochea dhidi ya Wakristo. Niliwaambia kuwa Wakristo ni makafiri. Niliwaambia waende wakawapige Wakristo kwa fimbo na kwa nondo. Niliwaambia kuwa Allah anafurahi wakifanya hivyo. Tulikuwa tukichoma moto Biblia tunazozikusanya.”
Zaheed anaendelea kusema, “Lakini siku moja, nilijisikia tu nichukue Biblia moja niende nayo nyumbani. Nilikuwa naisoma ili niweze kutafuta mambo yanayotatanisha ili niweze kuyatumia dhidi ya imani ya Kikristo. Ghafla, nuru kubwa iliangaza kwenye chumba changu. Halafu nikasikia sauti ikiita jina langu. Nuru ile ilikuwa kali sana. Iliangaza chumba kizima. Ile sauti ikauliza, ‘Zaheed, kwa nini unanitesa?’ Niliogopa. Sikujua cha kufanya. Nilidhani ninaota. Kwa hiyo nikauliza, ‘Wewe ni nani?’ Kisha nikasikia, ‘Mimi ni njia, na kweli, na uzima.’”



