Thursday, November 7, 2013

KUMBE MALAIKA WANA AKILI KULIKO ALLAH WA ISLAM!

Malaika Watabiri Mwenendo wa Binadamu kabla ya kuumbwa. Allah atumia hila kuficha udhaifu wake.

Katika somo letu la leo, tutajifunza kuwa Malaika wa Allah wana Akili na ufahamu wa mambo ya baadae kuliko Allah wa Islam.

Quran Surah 2:
30. Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua. ***

KATIKA AYA YA 30. Tunasoma kuwa Malaika wanampa  darsah Allah, jinsi gani Mtu atakuwa kabla ya uumbaji wake. Malaika wameonyesha upeo mkubwa kwa kufahamu maisha ya baada ya Adam/binadamu kabla ya hata kuumbwa.

31. Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli. ***

Kwenye aya 31 hapo juu, tunasoma kuwa Allah anamfundisha kwa siri Adam ili aweze kuwazima mdomo Malaika. Kitendo cha Allah kumfudisha Adam ili kushindana na Malaika haikuwa haki kwani Malaika walimpa changamoto Allah, Je, Allah ni mwenye ufahamu wa yote?

32. Wakasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyo tufunza Wewe. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hikima. ***

Je, Allah alipo tumia udanganyifu na uongo ili kujitetea mwenyewe dhidi ya mashtaka kwa Adamu kama yalivyo letwa na Malaika (mashtaka ambayo aligeuka kuwa ni sahihi) ni sahihi?  

33. Akasema: Ewe Adam! Waambie majina yake. Basi alipo waambia majina yake alisema: Sikukwambieni kwamba Mimi ninajua siri za mbinguni na za duniani, na ninayajua mnayo yadhihirisha na mliyo kuwa mnayaficha? ***


34. Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipo kuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri. ***


35. Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani, na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa katika wale walio dhulumu. ***


36. Lakini Shet'ani aliwatelezesha hao wawili na akawatoa katika waliyo kuwamo, na tukasema: Shukeni, nanyi ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Katika ardhi yatakuwa makaazi yenu na starehe kwa muda. ***


37. Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na Mwenye kurehemu. ***


38. Tukasema: Shukeni nyote; na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu, basi watakao fuata uwongofu wangu huo haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. ***

Katika vifungu hapo juu, tumesoma kuwa Malaika wanaufahamu kama Mungu (Omniscient) na ua wa Kimungu. Malaika waliweza kufahamu maisha ya Mwandamu kabla ya hata kuumbwa. Jambo ambalo Allah wa Islam hakulifahamu na hakuwa na ufahamu huo.

Kwanza, jinsi gani Malaika walijua hali ya mtu itakuwa kabla ya uumbaji wake? Malaika walifahamuje kabla ya uumbaji kuwa, binadamu watakuwa na vurugu? Nani aliwaambia? Nakala haisemi chochote juu ya Allah kuwapa kipande hiki cha habari. Je, Malaika anayajua yote kama Mungu (Omniscient)?

Pili, Mwenyezi Mungu kwa siri anafundisha Adam majina yasiyojulikana ili kuwanyamazisha Malaika kwa kulalamika dhidi ya mtu. Je, hii ni haki? Kwa nini Allah anatumia hila na hujmah, ili kuwafanya Malaika waonekane hawana ufahamu?

Je, Allah alipo tumia udanganyifu na uongo ili kujitetea mwenyewe dhidi ya mashtaka kwa Adamu kama yalivyo letwa na Malaika (mashtaka ambayo aligeuka kuwa ni sahihi) ni sahihi?  

Je, si dhahiri kwamba Adamu angekuwa na ufahamu wakawaida kama Malaika kwasababu Allah alikuwa bado hajawafundisha kuhusu uumbaji wake?

Kwanini Allah wa Islam anatumia udanganyifu ili kuficha udhaifu wake katika uumbaji?

Ndugu zanguni, leo tumejifunza kuwa Allah si msema ukweli na Allah hana ufahamu wa mambo yote kama alivyo Yehova ambaye ni Mungu aliye semwa ndani ya Biblia.

Kama unataka kufahamu kweli, basi nakusihi umpokee Yesu aliye hai, yeye ndie Njia, Kweli na Uzima. Katika Yesu, hakuna udanganyifu wa Allah. Mpokee leo ili upate uzima wa milele.

Katika huduma yake.

Max Shimba

For Max Shimba Ministries



Copyright © Max Shimba Ministries 2013

MUHAMMAD ANADAI KUWA ALIMUONA ALLAH: AISHA ANASEMA YEYOTE YULE ASEMAYE MUHAMMAD ALIMUONA ALLAH NI MUONGO

Kama kawaida, naendelea kufunua uongo na vituko vilivyo jaa kwenye Koran na Hadith. Katika somo letu la leo, tutajifunza uongo ulio semwa na Muhammad, eti, alimuoana Allah. Soma aya ifuatayo kutoka Koran iliyo shushwa na Jibril.

Quran 81:15. Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma, ***16. Zinazo kwenda, kisha zikajificha, ***17. Na kwa usiku unapo pungua, ***18. Na kwa asubuhi inapo pambazuka, ***19. Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu, ***20. Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi, ***21. Anaye t'iiwa, tena muaminifu. *** 22. Na wala huyu mwenzenu hana wazimu. ***23. Na hakika yeye alimwona Mwenyezi Mungu kwenye upeo wa macho ulio safi. ***24. Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu. ***25. Wala hii si kauli ya Shetani maluuni. ***26. Basi mnakwenda wapi? ***27. Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. ***28. Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa. ***29. Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.  *** 

Katika aya ya 23, Koran inatuambia kuwa Muhammad alimwona Bwana wake/Allah kwenye upeo wa macho ulio safi. Lakini Maswahiba wa Allah walipo Muuliza mke wake Aisha kama ni kweli Muhammad alimuona Allah, Aisha alikana na kusema asemaye kuwa Muhammad alimwona Allah ni MUONGO. Pata ushaidi hapa chini:

(Sahih al-Bukhari, Volume 9, Book 93, Number 477)
Amehadithia Masruq:
Mimi nilimuuliza 'Aisha, "O Mama! Je Mtume Muhammad aliwai kumuona Bwana wake?" Aisha akasema, "Kile umesema hufanya nywele yangu kusimama juu ya mwisho kujua kwamba kama mtu atakwambia moja ya mambo matatu yafuataho, HUYO NI MUONGO!. Yeyote atakayekwambia kwamba Muhammad alimwona Bwana wake, NI MWONGO"

Ndugu zanguni, leo tumejifunza kuwa, kumbe Muhammad alikuwa MUONGO, pale alipo dai kuwa eti, alimwona Bwana wake. Aisha amesema kuwa YEYOTE YULE ATAKAYE SEMA KUWA MUHAMMAD ALIMWONA BWANA WAKE NI MUONGO.

Je, Maneno ya Aisha yanaukweli, Hebu tuangalie Biblia inasema nini. Katika Injili ya Yohana Biblia inasema kuwa, HAKUNA ALIYE MUONA MUNGU, ISIPOKUWA MWANA(YESU).

Yohana 1: 18Hakuna mtu ye yote aliyemwona Mungu wakati wo wote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba ndiye ambaye memdhihirisha.

Biblia ipo wazi kuwa, Mwenye uwezo wa kumwona Baba ni Mungu Mwana. Leo tumejifunza kuwa Yesu ni Mungu Mwana. Mtu wa kawaida hawezi kumuona Mungu na akaishi. Zaidi ya Hapo leo tumejifunza kuwa Mtume wa Allah ni MUONGO.

Nakukaribisha kwa Mungu Mwana ambaye yeye yupo Upande wa Kulia wa Baba. Mwamini Yesu hii leo ili upate uzima wa milele.

Katika huduma yake.

Max Shimba

For Max Shimba Ministries


Copyright © Max Shimba Ministries 2013

KORAN INADAI KUWA YESU ALIZEEKEA HAPA DUNIANI.

VIOJA NDANI YA KORAN.

KORAN INADAI KUWA YESU ALIZEEKEA HAPA DUNIANI.

Leo tunajifunza Vioja vya Allah na Koran. Koran kupitia Allah na Mtume wake Muhammad inaleta UTATA pale ilipo sema eti Yesu alizeeka.

Soma kwanza hii aya.

QURAN 5:110. Na pale Mwenyezi Mungu atapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipo kutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu katika utoto na uzeeni. Na nilivyo kufunza kuandika na hikima na Taurati na Injili. Na ulipo tengeneza udongo sura ya ndege, kwa idhini yangu, kisha ukapuliza ikawa ndege kwa idhini yangu; na ulipo waponesha vipofu na wakoma kwa idhini yangu; na ulipo wafufua wafu kwa idhini yangu; na nilipo kukinga na Wana wa Israili ulipo wajia na hoja zilizo wazi, na wakasema walio kufuru miongoni mwao: Haya si lolote ila ni uchawi mtupu!

Leo tumesoma kutoka Quran kuwa Yesu alizeeka. Sasa angalia UTATA huu hapa:

Huduma ya Yesu ilidumu hadi alipokuwa na miaka 33. Hii ni aya ilikubalika na Yusuf Ali katika maoni yak. 388 juu ya Sura 3:46.

Sasa leo tumejifunza tena Vioja na Utata ndani ya Koran.

Je, kweli Allah anaweza kufanya makosa ya namna hii? You Judge if Allah is God.

Katika Huduma yake.

Max Shimba

For Max Shimba Ministries

UTATA NDANI YA KORAN: NINI KITAKUWA CHAKULA CHA WATU JEHANNAM

Leo Allah ameamua kutueleza kuwa, watu watakuwa wanakula nini huko Jehannam. Soma aya hapa chini:

Quran 88:6. Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba. 

Quran 69: 36. Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni. 


Sasa angalia UTATA UNAPO INGIA: Quran 39: 62-69

62. Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum? ***63. Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu. ***64. Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu. ***65. Mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani. ***66. Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo. ***67. Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji yamoto yaliyo chemka. ***68. Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu. ***

Ndugu zanguni, Koran ni kitabu cha ajabu sana, maana kinapingana kila sehemu.  Leo tumesoma nini watu watakula Jehannam. Hivyo, kuhusu mada hii moja peke yake, Qur'ani ina utata tatu:

"Kula matunda ya mti wa Zaqqum" (37:66) inapingana na "kula tu Dhari" (88:6).
"Kula matunda ya mti wa Zaqqum" (37:66) inapingana na "kula tu pus mchafu" (69:36).
"Kula tu Dhari" (88:6) inapingana na "kula tu pus mchafu" (69:36).

Koran imejaa UATATA na si kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba

For Max Shimba Ministries

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

Wednesday, November 6, 2013

KUTOKANA NA KORAN: YESU ANAUMBA, ANAPONYA, ANAFUFUA WATU, LAKINI MUHAMMAD HAKUWA NA UWEZO HUO

Koran leo imekiri kuwa Yesu ni zaidi ya Mtume. Ukisoma hii aya hapa chini utaona kuwa Yesu aliumba, hii sifa ya kuumba ni ya Mungu Pekee. Yesu alifufua watu, Yesu Aliponya watu. n.k. Lakini hatusomi kuwa Muhammad alifanya hayo.  Hebu soma Koran.

Quran 5: 110. Na pale Mwenyezi Mungu atapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipo kutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu katika utoto na utuuzimani. Na nilivyo kufunza kuandika na hikima na Taurati na Injili. Na ulipo tengeneza udongo sura ya ndege, kwa idhini yangu, kisha ukapuliza ikawa ndege kwa idhini yangu; na ulipo waponesha vipofu na wakoma kwa idhini yangu; na ulipo wafufua wafu kwa idhini yangu; na nilipo kukinga na Wana wa Israili ulipo wajia na hoja zilizo wazi, na wakasema walio kufuru miongoni mwao: Haya si lolote ila ni uchawi mtupu!

Ndugu zanguni, leo tumejifunza kuwa Yesu hakuwa mtu wa kawaida. Alikuwa anafanya mambo ambayo ni Mungu pekee mwenye uwezo wa kufanya hao. Ushaidi huu umewekwa kwenye Koran. Madai ya kuwa Yesu alikuwa Mtume/Nabii kama wengine, yanashindwa nguvu, baada ya kusoma hii aya ambayo imetuonyesha adhama ya Mungu ndani ya Yesu. Je, kuna Nabii au Mtume yeyote Yule aliye wai kuumba?

Hebu tusome hadith ifuatayo kutoka kwa Al Bukhar.

Ibn 'Abbas akasema, "Hiyo ilionyesha kifo cha Mtume wa Allah ambacho Allah alimtaarifu." 'Umar alisema, "Sielewi haya isipokuwa kile wewe unakielewa." 'Aisha: Mtume katika maradhi yake ambayo yalimuua, Alikuwa akisema, "O' Aisha bado nahisi maumivu yanayosababishwa na chakula nilicho kula nilipo kuwa Khaibar, na kwa wakati huu, Najisikia kama aorta   yangu inakatwa kutoka sumu niliyo kula. "(Sahih al-Bukhari, Volume 5, Kitabu 59, Namba 713)

Kwenye Hadith tuliyo soma tunaona kuwa Mtume wa Allah alikuwa anasumbuliwa na Sumu aliyo lishwa kwa Mtego na Yule Mama wa Kiyahudi. Hadithi hii inatupa ushaidi kuwa Mtume wa Allah alikuwa akiomba uponyaji kutoka kwa Allah. Swali la kujiuliza, Je, Muhammad alipo baada ya maombi haya  kwa Allah?

Endelea kupata somo:

Kwenye hadith ifuatayo hapa chini, tunasoma kuwa Jibril nayeye amekuja kumuombea uzima Mtume wa Allah, lakini maombi hayo hayakumponya Mtume wa Allah.

Kutoka kwa Ibn Sad ukurasa 265
Mtume wa Mwenyezi Mungu aliugua na yeye yaani Gabriel, alimuombea juu yake, akasema, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu mimi nakuombea uzima na nazuia kutoka kwenu kila kitu kibaya na madhara yeyote (kuizuia kwako wewe) dhidi ya hasidi kila na kutoka kila uovu na Allah atakuponya.

Je, Baada ya haya Maombi, Mtume wa Allah alipona? Kutokana na Hadith yetu ya kwanza, Mtume wa Allah hakupona licha ya kupata Maombi kutoka Malaika Jibri. Lakini katika Koran tunasoma kuwa Yesu alikuwa na uwezo wa kuponya watu, kufufua watu, kuumba, jambo ambalo Jibril na Mtume wa Allah, Muhammad hawakuwa nalo.

Ndugu zanguni,

Kwanini mfuate Mtume ambaye hakuwa na uwezo wa kuponya?

Kwanini mumsikilize, Malaika ambaye hakuwa na Nguvu za kuponya, licha ya kuwa alitumwa na Allah?

Kwanini Allah amtume Jibril kwenda kumwombea Mtume Muhammad, huku akifahamu fika kuwa Muhammad hato pona?

Hayo ni maswali machache tu ambayo unaweza jiuliza. Je, Allah ni Mungu? Kama ni Mungu, kwanini alishindwa kuponya Mtume wake Muhammad (Pbuh)?

Biblia inasema yafuato kupitia Injili kutokana na Marko.

Marko 16: 17“Nazo ishara hizi zitafuatana na wale waaminio: Kwa Jina Langu watatoa pepo wachafu, watasema kwa lugha mpya, 18watashika nyoka kwa mikono yao na hata wakinywa kitu cho chote cha kuua, hakitawadhuru kamwe, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa,
nao watapona.”
Wakristo wamepewa uwezo wa kuombea wagonjwa katika Jina la Yesu, jamba ambalo halipo kwenye Uislam. Biblia inasema kwa Jina la Yesu, tutatoa Pepo Wachafu, n.k. Haya mamlaka tumepewa na Yesu. Yesu ametupa Jina lake ambalo lipo juu ya majina yote. Ndio jina pekee linaloweza kutoa pepo, kuponya, kufufua na kufanya mengi. Yesu hakuwa Nabii au Mtu wa Kawaida. Matendo yake yanajidhihiriza kila siku kupitia wafuasi wake.

Nawasihi mumpokee Yesu ambaye alikuwa na uwezo wa kufufua watu, kuponya watu na kuumba. Haya maneno yamesemwa na Allah kwenye Koran na Biblia inakiri hayo.


Kama kweli Allah ni Mungu, kwanini alimtuma Jibril kumwombea Muhammad wakati akifahamu kuwa Muhammad atakufa?

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba

For Max Shimba Ministries

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

Tuesday, November 5, 2013

UTATA NDANI YA KORAN: NANI ALIKUWA MTEREMSHAJI WA KWANZA WA QURAN KWA MTUME MUHAMMAD?

Adui wa Jibril au Roho Takatifu?

Somo letu la leo tutazungumzia utata ulio jaa ndani ya Koran. Leo hii tutajinfunza kuhusu nani alikuwa wa kwanza kuteremsha Koran kwa Mtume wa Allah. 

Katika Qura 2:97 tunasoma kuwa, Jibril ndie aliye kuwa wa kwanza kushusha aya za Quran kwa Mtume wa Allah. Soma kifungu hiki hapa:

Quran 2:97. Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini.

Hiyo aya hapo juu ipo wazi kabisa kuwa, aliye kuwa adui wa Jibril ndie aliye kuwa mshushaji wa Quran kwa Mtume wa Allah ajulikanaye kwa jina la Muham'mad. Hebu tuendelee kusoma Quran hiyo hiyo na tuone kama ni kweli adui wa Jibril alikuwa wa kwanza kufanya hiyo kazi au kulikuwa na mtu mwingine aliye kuwa anafanya kazi hiyo hiyo ya kushusha Quran kwa Mtume wa Allah.

Rejea hapa:

Quran 16:102. Sema: Ameiteremsha hii Roho takatifu kutokana na Mola wako Mlezi kwa haki, ili awathibitishe wale walio amini, na kuwa ni uwongofu, na ni bishara kwa Waislamu.

103. Na Sisi hakika tunajua kwamba wanasema: Yuko mtu anaye mfundisha. Lugha ya huyo wanaye muelekezea ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu mbayana.

Katika aya tulizo zisoma hapo juu, tunagundua kuwa Allah alimtumia Roho Takatifu kushusha Aya kwa Mtume wake na si Jibril kama wanavyo dai Waislam na tulivyo soma kwenye Surah 2 aya 97 ni Adui wa Jibril ndie aliye shusha Quran.

Katika Surah 2:97 tunasoma kuwa Mteremshaji wa Quran ni adui wa Jibril.

Katika Surah 16:102-103 tunasoma kuwa Roho Takatifi ndie anateremsha Quran.

Ndugu zanguni. Hivi kwanini Koran inamakosa namna hii? Nani alikuwa mteremshaji wa Koran? Ni Adui wa Jibril au Roho Takatifu?

Nimategemeo yangu kuwa, hili soma litawafungua macho na kufahamu ukweli kuhusu Quran. Kama kweli Allah ni Mungu na yeye ndie aliye kuwa anaishusha Quran kupita Jibril, basi asinge fanya kosa la kumsingizia Roho Takatifu kuwa na yeye alikuwa anashusha Quran au Adui wa Jibril.

Kama kweli Allah ni Mungu, kwanini afanye makosa makubwa namna hii?

Je, Roho Takatifu ni adui wa Jibril?

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba

For Max Shimba Ministries

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

UTATA NDANI YA KORAN: JE, INJIL ILIKUWEPO WAKATI WA MUSA



Ndugu zanguni, 

Leo nitazungumzia makosa na utata ndani ya Koran. Katika somo letu la leo, mtaona utata na makosa kutoka kwa Allah, alipo kuwa anamjibu Musa maombi yake. Allah anamjibu Musa na kumweleza kuwa eti Nabii asiye fahamu kusoma na kuandika yupo ndani ya Injili, huku ikifaamika kuwa Injili ilikuwa bado haikushushwa.

Aya nyingi katika Qur'ani zipo wazi kwamba Injil ilitolewa kwa Yesu ambaye alizaliwa miaka mia kadhaa [1400 BC] baada ya Musa.

Lakini cha kushangza, eti Musa aliye ishi miaka 1400 kabla ya YESU kuzaliwa na yeye anajibiwa na Allah kuhusu Injili ya Yesu kama vile yeye Musa alizaliwa baada ya Yesu. Soma majibu ya Allah kwa Musa hapa chini. 

Quran 7: 155. Na Musa akawateuwa watu sabiini katika kaumu yake kwa miadi yetu. Na ulipo fika mtetemeko mkubwa alisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ungeli taka ungeli wahiliki wao na mimi zamani! Unatuhiliki kwa waliyo yafanya wajinga katika sisi? Haya si chochote ila ni mtihani wako, umpoteze umtakaye na umhidi umtakaye. Wewe ndiye Rafiki Mlinzi wetu. Basi tughufirie na uturehemu. Na Wewe ndiye mbora wa kughufiria. ***

156. Na utuandikie mema katika dunia hii na katika Akhera. Sisi tumerejea kwako. (Mwenyezi Mungu) akasema: Adhabu yangu nitamsibu nayo nimtakaye. Na rehema yangu imeenea kila kitu. Lakini nitawaandikia khasa wanao mchamngu, na wanao toa Zaka, na wale ambao wanaziamini Ishara zetu, ***

157. Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa. ***

Koran imejaa mashaka kila sehemu. Leo tunaona Allah anamjimu Musa kuhusu Injili ambayo ilishushwa mika 1400BC. Hivi huyu Allah alipitiwa na kuanza kuzumguzia Isa Bin Maryama kwa Musa au ni kufichuka kwa siri kwamba Quran si kitabu cha Mungu? 

Kama kweli Allah ni Mungu, kwanini afanye makosa makubwa namna hii?

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba

For Max Shimba Ministries

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

Monday, November 4, 2013

UISLAM NDIO DINI PEKEE YENYE MTUME MWENYE WAZIMU


Ndugu zanguni.

Biblia inasema kuwa, mtawafahamu kwa matunda yao, hayo yalikuwa maneno kutoka Injili ya [Mathayo 7:16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? 17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya].

Mtume Muhammad alishindwa kuonyesha uadilifu katika kazi yake. Kazi aliyo dai katumwa na Mungu, ilijaa maswali mengi ambayo yaliwafanya watu wamuite yeye, Muhammad, “Mwendawazimu”. Kitendo cha Mtume kuoa Mtoto wa miaka 6, kulileta kizungumkuti, kwasabau kitendo hicho si cha kibinadamu na hakikufanywa na Mitume walio kuja kabla yake. Hapa chini ni aya kutoka Koran iliyo teremshwa na mungu wa Islam kupitia msaada wa Gibril.

Quran 15: 6. Na walisema: Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu.

Muhammad anaitwa mwendawazimu mbele ya kadamnasi. Hayo madai ya uwendawazimu hayakukataliwa na mtume wa Allah. Alicho fanya Muhammad ni kukaa kimya, jambo ambalo ni jibu tosha kuwa alikubali kuwa yeye ni Mwendawazimu. Uhakikisho wa uwendawazimu wake upo kimaandishi.

Hebu tusome Simulizi zake kidogo: "Kitab al-Tabaqat al-Kabir", (Kitabu cha Madarasa Meja), na Ibn Sad, kutafsiriwa na S. Moinal Haq, [4], ukurasa wa 225; Muhammad akisema:

O Khadija, Ninaona Mwanga, na nasikia Masautisauti, nina hofu kuwa mimi nina Wazimu. 

Kwenye hiyo simulizi yake, hapo juu, Mtume wa Allah anakiri kuwa yeye ni mwendawazimu. Kukiri huko, kunatuletea maswali mengi, ambayo nategemea mengi ya maswali hayo, yatakosa majibu. Lakini ni vyema tujiulize maswali. Kwanini Allah aliteremsha aya inayo muita Mtume wake Mwendawazimu? Kwanini Muhammad hakukataa kuitwa Mwendawazimu? Utume wa huyu Muhammad umejaa shaka, pale alipo kubali kuwa yeye ni mwendawazimu. Rejea kwenye simulizi yake hapo juu. Nita nukuu sehemu fupi ya kukubali kwake “O Khadija, …….nina hofu kuwa mimi nina Wazimu”.

Hatujawai soma kwenye vitabu vingine vitakatifu kuwa Mitume wa Mungu wa Biblia walikubali kuwa wao ni Wendawazimu, lakini leo hii tumejifunza kuwa Muhammad mtume Allah, anakubali kuwa yeye ni Mwendawazimu.

Hivi, kwanini tufuate mtume aliye kubali kuwa yeye ni Mwendawazimu? Hilo ni swali la msingi. Allah anasema kuwa watu wa Kitabu ambao ni Wayahudi na Wakristo ndio wenye elimu na muwaulize wao, mtakapo kuwa na maswali.

Allah amesha jibu. Wakristo ndio wenye majibu katika hii duni.

MUHAM-MAD ANASEMA: "Nina hofu kuwa mimi nina Wazimu"

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

Hell pictures_ A Trip To Hell (Full version) / 지옥그림_지옥을 견학하다 (Full version)

http://www.youtube.com/watch?v=dWXkBBIaiVc

http://www.youtube.com/v/dWXkBBIaiVc?version=3&autohide=1&feature=share&showinfo=1&autohide=1&attribution_tag=hY2elLNSMwttZSEiiRSDCA&autoplay=1

ALLAH ANASEMA KATIKA KORAN KUWA WAISLAM WOTE WATAINGIA JEHANNAM

Jamani huu ni Msiba katika taifa la Islam kwa kushindwa kusoma aya hii ambayo ipo wazi (Quran 40:60).

Katika mada hii, nitawawekea aya kutoka Koran na simulizi za Muhammad ambazo zinatushuhudia kuwa, Waislam wote wataingia Jehanamu.

Hebu tumsome kwanza Allah katika aya aliyo iteremsha kwa Mtume wake Muhammad (Pbuh).

Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.

Mungu wa Waislam ajulikanaye kwa Jina la Allah amesema kiuwazi kabisa kuwa “wale wote ambao wanajivunia Uislam na kumuabudu Allah wataingia Motoni”


Ndugu zanguni, huu ni Msiba, tena msiba mkubwa sana katika dini na taifa la Kiislam. Allah amesha toa hukumu kwa wamfuatao na inafahamika fika kuwa, Wale wote waingiao Jehannam, hao walikuwa hawafanyi Mapenzi ya Mungu wa Biblia.  Allah anasema kuwa, ukifanya mapenzi yake, basi wewe utaingia Jehannam. Huu ushaidi ndio tulio usoma katika Quran 40:60.


Sasa tuwasikilize na maswahiba wa Mtume Muhammad.

Simulizi:
Pia imesimuliwa na Ibn Jarir, iliyosimuliwa na Abu Kurayb, imesimuliwa na Ibn Yaman, imesimuliwa na Ibn Malik Maghul, imesimuliwa na Ibn Ishaq ambaye alisema, "Kila mara Abu Maysarah anapo kwenda kulala na akiwa kitandani kwake yeye husema, 'Mimi nasikia Uchungu kuzaliwa na Mama yangu. 'na kisha anaanza kulia kwa Machozi. Alipoulizwa kwa nini alikuwa akilia, alijibu ayafuatayo,' Tuliambiwa kwamba SISI WAISLAMU tutaingia Jehannamu, LAKINI HATUKUAMBIWA kwamba TUTATOLEWA HUKO JEHANNAMU NA HATUKUAMBIWA NI KIVIPI TUTATOKA HUKO'"

Mfuasi huyu wa Muhammad anaoneka kupatwa na mshtuko mkubwa, pale alipo ambiwa kuwa, Waislam wote wataingia Jehannam. Mshtuko huu umemfanya ailaani siku ambayo alizaliwa. Kitu cha kujiuliza, kwanini Allah ambaye ni mungu wa Waislam anatoa ahadi ya Jehannam na si Akhera kama wafundishavyo Waislam?

Ndugu zanguni, ningependa mfahamu kuwa, utakapo ingia Jehannam, kutakuwa hakuna tena njia nyingine ya kutoka huko. Pale Jehannam ndio mwisho wa maisha ya walio tenda dhanb. Allah anasema kuwa, ukifanya mapenzi yake, basi wewe utaingia Jehannam. Je, kufanya mapenzi ya Allah ni sawa na kutenda dhanb? Je, Uislam ni dini ya haki, kama wanavyo sema wafundishaji wa dini hiyo? Jiulize tena, kwanini Allah anatoa ahadi ya Jehannam kwa wafuatayo mafundisho yake?


Lakini Yesu anasema haya:
Yohana 14: 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. 

Ndugu zanguni, mwamini Yesu ili uwe na uzima wa milele. Yesu anakupenda. Yesu Ndie Njia Pekee. Yesu Ndie Uzima. Dini haita kupeleka kwa Baba aliye Mbingu, lakini Yesu anasema Yeye NDIE NJIA.

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba

For Max Shimba Ministries


Copyright © Max Shimba Ministries 2013

BREAKING VIDEO: IDF pounding Hezbollah training compounds

  BREAKING VIDEO: IDF pounding Hezbollah training compounds. The targets included a Radwan Force training facility used for weapons drills ...

TRENDING NOW