Pasaka ni sikuku iliyoamriwa na Mungu tangu siku za kale kwa wayahudi
kuifanya katika mwezi wa Abibu au Nisani katika “kalenda ya kiebrania”
yaani mwezi wa 3 au 4 katika kalenda ya kirumi, kwa lengo la kumbuka
njisi Mungu alivyowakomboa kutoka utumwani Misri; Twasoma: “Utunze mwezi
wa Abibu, ukamfanyie pasaka BWANA, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni
mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA; Mungu wako. Nawe umchinjie
pasaka BWANA, Mungu wako katika kundi la kondoo na la ng’ombe, mahali
atakapochagua BWANA apakalishe jina lake.” (Kumbukumbu 16:1-2) Soma pia:
(Kutoka 12:14) Kama tulivyoona katika pasaka wayahudi waliamriwa
kuchinja mnyama mmoja katika kundi, lakini tunapoendela kusoma tunaona
jinsia Mungu alivyoamuru mnyama huyo aokwe na kuliwa; Twasoma:
“Usimle pamoja na mikate iliyotiwa chachu; siku saba utakula naye mikate
isiyotiwa chachu, nayo ni mikate ya mateso; kwa maana ulitoka nchi ya
Misri kwa haraka; ili upate kukumbuka siku uliyotoa nchi ya Misri, siku
zote za maisha yako. Wala isionekane kwako chachu muda wa siku saba
katika mipaka yako yote; wala katika hiyo nyama uchinjayo siku ya kwanza
jioni, kisilale cho chote usiku kucha hata asubuhi. Usimchinje pasaka
ndani ya malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako; ila mahali
atakapochagua BWANA, Mungu wako apakalishe jina lake, ndipo
mtakapomchinjia pasaka jioni, katika machweo ya jua, kwa wakati kama
uliotoka Misri.” (Kumbukumbu 16:3-6); Soma pia: (Kut 12:3-13) Katika
mwezi huo wa abibu ambao Mungu aliufanya kuwa mwezi wa kwanza kwako,
Wayahudi walifanya karamu ya Pasaka kuwa kumbukumbu la jinsi Mungu
alivyowaokoa kutoka Misri (Kutoka 12:1-51; Walawi. 23:5).
Pasaka
maana yake ni "kupita Juu", maana Mungu alipita juu ya nyumba zao
asiwaangamize wazaliwa wao wa kwanza; Twasoma: “Na ile damu itakuwa
ishara kwenu katika zile nyumba mtakazo kuwapo; nami nitakapoiona ile
damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu
nitakapoipiga nchi ya Misri.” (Kutoka 12:13); Soma pia:(Kutoka 12:27)
JE WAKRISTO TUNA PASAKA LEO?
Ni kweli wakristo tuna pasaka leo, walakini si katika utaratibu ule
Uliotumika katika siku za waisraeli, kama tulivyoshuudia maandiko
yaneleza wazi ya kuwa sikukuu hizo zilikomeshwa; Basi hebu tuone
utaratibu wa Pasaka ya wakristo leo ni upi;
Zingatia: Kama
tulivyoona hapo juu, waisraeli waliokolewa na damu ya mnyama walio ipaka
katika miimo na miisho ya milango yao na ndipo malaika wa Bwana
alipotambua na kupita juu; Soma tena: (Kutoka 12:13, 27); lakini
wakristo tunaambiwa pasaka wetu ni Yesu mwenyewe aliyetuokoa kwa damu
yake; Twasoma:
“Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake,
akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”
(Yohana 1:29); Soma pia: (Yohana 1:36) “Nanyi mfahamu kwamba
mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate
kutoka katika mwenendo wenu usiofaa milioupokea kwa baba zenu; bali
kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa,
yaani, ya Kristo.” (1 Petro 1-18-19) “Basi jisafisheni, mkatoe ile
chachu ya kale, mapate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa
chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;” (1 Wakoritho 5:7) Basi kama tulivyoona Neno la Mungu linatuthibitishia ya kuwa kwa sasa
wakristo tunaokolewa na damu ya Yesu ambaye ndiye Pasaka wetu na si kwa
damu ya mnyama aliyekuwa Pasaka wa kale. Basi kiwa hivyo ndivyo, ni
dhahiri hata utratibu wa kusherehekea pasaka kwa wakristo ni tofauti,
Basi hebu tuone wakristo tunasherehekeaje pasaka yetu leo.
Yesu
alipokuwa akila Pasaka ya mwisho pamoja na wanafunzi wake, aligeuza
Pasaka. Aliwaambia kwamba, kuanza siku ile, watakapokula mikate
wangekumbuka mwili wake uliotolewa kwa ajili yao badala ya kukumbuka
kuokolewa kutoka utumwani nchini Misri; Twasoma: “Nao walipokuwa wakila
Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega akawapa wanafunzi wake, akisema,
Twaeni mle; huu ndio mwili wangu Akatwaa kikombe, akashukuru,
akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu
yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.”
(Mathayo 26:26-28) “Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa ninyi,
ya kuwa usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, na ye akiisha kushukuru
akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni
hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa
kikombe, akisema, kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni
hivi kwa kila mywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu
na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.” (1
Wakorintho 11:23-26).
JE WANAOSHEREHEKEA PASAKA YA KALE WAMEPOTEA?
Ni kweli karibu ulimwengu mzima unasherehekea pasaka kama walivyokuwa
wakisherehekea wayahidi nyakati zile, wakidhani ndivyo ilivyo agizwa,
basi na tuzingatie maneno yafuatayo; Twasoma: “Iko njia ionekanayo kuwa
sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti” (Mithali
14:12) “Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni
litang’olewa. Waacheni hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu
akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.” (Mathayo
15:13-14) “Si kila aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika
ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu
aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya
unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako
kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe;
ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.” (Mathayo 7:21-23) “Basi
ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu
ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale
yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe.” (1 Wakorintho 4:6) Basi kama tulivyoona, upotofu uliopo katika sikukuu hii ya pasaka na
jinsi Mungu anavyo tuonya kuwa makini na mafundisho ya uongo, ni dhahiri
tunawajibu wa kujifunza neno la Mungu kwa bidii ili tupate kujua yaliyo
mapenzi yake tukayafanye; Soma: (Yakobo 1:22-25)