Hadithi za Bukhari
Mamia ya maelfu ya hadithi (mapokeo) yanadai kuelezea mafundisho na matendo ya Muhammad na wafuasi wake wa karibu. Waislam wa kale walizichambua hadithi hizi ili kuona ni zipi kati yake ni za kweli. Kuna makundi sita ya hadithi zinazofikiriwa na Wasuni kuwa "sahihi" au halisi na zenye mamlaka ya kidini. Hadithi hizi huchukuliwa kuwa ni muhimu karibu sawa na Kurani yenyewe. Kundi refu zaidi ni Sahih al-Bukhari lenye juzuu tisa na hadithi 7,275. Mambo yafuatayo yana mvuto mkubwa kwa wasomaji wote Waislam na wasio Waislam toka kwenye hadithi za kundi la Bukhari. Dondoo hizi zimetolewa toka kwenye kitabu kiitwacho Tafsiri za Kiarabu na Kiingereza za Maana za Sahih Al-Bukhari kilichoandikwa na Dr. Muhammad Mushin Khan wa Chuo Kikuu cha Kiislam cha Medina Al-Munawwara, Saudi Arabia.
Muhammad Haabudiwi
"Baada ya hapo Abu Bakr alisema Tashah-hud (yaani hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wake)... Abu Bakr alisema, ‘Amma ba’du, yoyote miongoni mwenu aliyemwabudu Muhammad, basi Muhammad amekufa, lakini yoyote aliyemwabudu Mungu, Mungu yu hai na hatakufa kamwe. Mungu alisema: ‘Muhammad ni Mtume tu’" Bukhari juzuu ya 2 kitabu cha 23 (Kitabu cha Misiba) sura ya 3 na. 333 uk.188-189.
Hata hivyo Waislam wanamthamini sana Muhammad. "Kwa [msaada wa] Allah, Mtume wa Allah alipotema mate, mate yaliangukia kwenye mkono wa mmoja wa (yaani washiriki wa nabii) ambaye alifuta uso na ngozi vyake; alipowaamuru, washiriki wake walitimiza" maagizo yake mara moja; aliponawa walipigania kuchukua maji yaliyobakia; na walipoongea naye, walipunguza sauti zao na hawakumwangalia usoni mara kwa mara kwa ajili ya heshima." Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 50 (Masharti, ‘Conditions’) sura ya 13 na. 891 uk.564-565.
Marufuku Vinywaji Vikali
"‘Aisha [mke wa Muhammad] Nabii alisimulia akisema, ‘Vinywaji vyote vyenye kuleta ulevi ni Haram (vimezuiliwa) kunywa." Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 4 (Kitabu cha Kujitakasa) sura ya 75 na. 243 uk.153.
"Abu Huraira alisimulia: ‘Nabii alisema, ‘Mzinzi, wakati anafanya tendo la ndoa lisiloruhusiwa si muumini; na mtu yeyote, wakati anapokunywa kinywaji chenye kulevya, si muumini; na mwizi, wakati anapoiba si muumini" Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 69 (Kitabu cha Vinywaji) sura ya 1 na. 484 uk.339.
Waislam pia wamezuiliwa kuuza mvinyo, sanamu na nyama ya nguruwe. Muislam Sahih juzuu ya 3 kitabu cha 9 (Kitabu cha Biashara) sura ya 621-622 na.3835-3840 uk.828-830. Hawaruhusiwi kununua, kuuza au kubeba mvinyo. Ibn-i-Majah juzuu ya 4 kitabu cha 30 (Kitabu cha Vinywaji) namba 3380-3381 uk.493-494; juzuu ya 4 kitabu cha 30 na.3382 uk.494. Kuuza pombe kumezuliwa kwenye Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 8 (Kitabu cha Maombi) sura ya 73 na. 449 uk.267.
Je Muhammad Aliona Mwezi Ukigawanyika Vipande Viwili?
"Ombi la wapagani kwa Nabii kuwa awaonyeshe muujiza. Nabii aliwaonyesha kugawanyika kwa mwezi. ‘Abdullah bin Massud alisimulia: Wakati wa uhai wa Nabii mwezi uligawanyika vipande viwili na Nabii alisema, ‘Shuhudia (jambo hili).’" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 (Wema na Uadilifu wa Nabii na Washiriki Wake) sura ya 26 na. 830 uk. 533.
"Anas alisimulia kuwa watu wa Maka walimwomba Mtume wa Mwenyezi Mungu awaonyeshe muujiza, na kwa ajili hiyo aliwaonyesha kugawanyika kwa mwezi." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 (Wema na Uadilifu wa Nabii na Washiriki Wake) sura ya 26 na. 831 uk.533.
"Ibn ‘Abbas alisimulia: Mwezi uligawanyika vipande viwili wakati wa uhai wa Nabii." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 (Wema na uadilifu wa Nabii na Washiriki Wake) sura ya 26 na. 832 uk.534.
Nyota Zinapaswa Kuyapiga Mashetani?
"Uumbaji wa nyota ulikuwa na malengo matatu, yaani kuwa mapambo ya mawingu, kupiga mashetani, na ishara za kuongozea wasafiri. Kwa hiyo, mtu yoyote anapojaribu kutafuta tafsiri tofauti, amekosea na anapoteza nguvu zake..." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 (Mwanzo wa Uumbaji) sura ya 3 maelezo ya mwenye kutafsiri kabla ya na. 421 uk.282.





