Wednesday, July 1, 2015

UISLAM UNADHARAU WAAFRIKA

Si MWEUSI wala MWAFRIKA
Na Abdullah Al Araby
Rangi ya ngozi ya mtu mara imekuwa kigezo cha dini. Wakereketwa wa uislam wamekuwa wakijaribu kuwashawishi Waamerika wenye asili ya Kiafrika kuwa uislam ni dini ya mtu mweusi, kwamba uislam ni dini ya kiafrika na kwamba Muhammad alikuwa mweusi. Hatuhitaji kusema kwamba Waislam wamekuwa wakitoa madai haya kwa watu weusi tu; lakini kwa wazungu hutumia njia tofauti!
Kwa kujua kuwa haya ni mawazo potofu yaliyofikiriwa kwa umakini mkubwa sana, yaliyokusudiwa kuwavuta watu weusi kwenda kwenye uislam, nimejisikia kuuweka ukweli wazi. Hakuna kitu chochote kwenye makala hii kinachoafikiana na mtazamo huu wa ubaguzi wa rangi. Kama tukiupokea au kuukataa uislam, basi iwe ni kwa sababu za sifa halisi za uislam wenyewe na si rangi ya ngozi ya mtu au chimbuko lake.
Chanzo change kikuu cha taarifa za makala hii, licha ya Koran, ni Maandiko matakatifu ya Waislam "Hadithi", ambazo ni matendo na maneno ya Mtume Muhammad wa uislam kama yalivyonukuriwa na "Sahih al Bukhary" na "Sahih "Muislam."

AFRIKA HAIKUWA CHIMBUKO LA UISLAM
Uislamu ulizaliwa katika karne ya 7, katika rasi ya Arabia, ambayo ilikuwa sehemu ya bara la Asia. Asia ya njano na Afrika nyeusi vimetengwa na bahari ya Shamu [Red Sea]. Hapa tunazungumzia mabara mawili tofauti na rangi mbili tofuati.
Uislamu ulikwenda Afrika muda si mrefu sana uliopita, na hii si dini inayotawala Afrika. Kuna uwezekano mkubwa kuwa Waamerika wenye asili ya Kiafrika walikuwa ama Wakristo ama waumini wa dini za jadi wakati walipoletwa Amerika.
Ukristo umekuwapo Afrika tangu nusu ya kwanza ya karne ya kwanza. Mtakatifu Marko, mwandishi wa Injili ya Marko, alikuwa Myahudi wa Afrika kaskazini aliyeihubiri Injili kule Misri. Kutokea kule, ukristo ulisambaa Afrika ya kaskazini yote, na kusini mwa mipaka ya Misri. Kanisa la mashariki liliwapa weusi wengi hadhi ya utakatifu [sainthood]. Kwa mfano Mtakatifu Musa mweusi, Mtakatifu Tekla Himanote, mwethiopia na wengineo. Mmojawapo wa walimu na manabii katika kanisa la kwanza alikuwa "Simoni Niger", na Ninger inamaanisha mtu mweusi kwa Kilatini (Matendo 13:1). Upande wa mashariki mwa Afrika ulifanywa kuwa wa kikristo kutokana na huduma ya mjumbe wa bunge la Malkia Kandake wa Ethiopia aliyebatizwa na mwinjisti Filipo (Matendo 8:6-40).


MUHAMMAD HAKUWA MWEUSI
Muhammad alikuwa Mwarabu wa Kiasia. Huwezi ukachanganya kati ya Mwarabu wa Kiasia na mtu mweusi. Kuna vithibitisho vingi kuwa Muhammad alikuwa mweupe. Ufinyu wa nafasi ndio utatufanya tutaje vithibitisho vichache tu.
Katika Sahih Al Bukhary juzuu ya 1 na. 63, tunasoma "wakati tukiwa tumekaa na Nabii, mtu mmoja alikuja na kusema, ‘yupi kati yenu ni Muhammad?’ Tukajibu, ‘huyu mtu mweupe anayeegemea mkono wake…"
Katika juzuu ya 2 Hadithi na. 122 inamzungumzia Muhammad kama "mtu mweupe" na katika juzuu ya 2 Hadithi na. 141 tunaambiwa kuwa Muhammad wakati aliinua mikono yake, "ueupe wa kwapa zake ulikuwa bayana."
MUHAMMADI ALIMILIKI WATUMWA WEUSI
Muhammad aliwachukulia watu weusi kama watumwa. Hata alikuwa akimiliki watumwa weusi kadhaa. Bilal, Abu Hurairah, Usama Ebn Zayyed, na "Ghulaam" (kijana) aliyeitwa Rabbah, walikuwa miongoni mwa watumwa wa Muhammad.
Hata sasa, nchini Saudi Arabia, nchi mama ya uislamu, neno la kawaida kwa "mtu mweusi" ni "Abd" likiwa na maana ya mtumwa.

Muhammad alikuwa na maoni gani kuhusu kuwaachia huru watumwa?
Kuna tukio mojawapo ambapo mtu alimwacha huru mtumwa ambaye alikuwa mwenziwe kingono. Wakati Muhammad aliposikia kitu kilichotokea, alimpiga mnada huyo mvulana na kumuuza kwa derhamu 800 kwa Na-eem Ebn Abdullah Al-Nahham. (Sahih Muislamu juzuu ya 7, uk.83).
Kwa mujibu wa Muhammad, adhabu ya ugoni ni tofauti kati ya mwanaume aliyehuru, mwanamke aliyehuru, na mwanamke mtumwa. Mwanaume alipaswa kupigwa mijeredi mia moja na kufukuzwa kutoka kwenye jamii kwa mwaka moja. Mwanamke alipaswa kupondwa mawe hadi kufa. Lakini mwanamke mtumwa, mjakazi, (kwa kuwa alikuwa na thamani kifedha) hakufukuzwa wala kuuawa ila alipigwa mijeredi mia moja. Ikiwa kosa hilo litarudiwa, mjakazi huyo aliuzwa (Sahih Al Bukhary juzuu ya 8:821, 822).

UISLAMU ULIWADHARAU WEUSI
Uislamu ni dini, ambayo Maandiko yake matakatifu yana maneno yanayowadhalilisha watu weusi wazi wazi.
Muhammad aliwaita watu weusi "vitita vya mizabibu" [raisin heads]. (Sahih Al Bukhary juzuu ya 1, na. 662 and juzuu ya 9 na. 256).
Katika Hadhithi ambayo imethibitishwa kuwa kweli, Muhammad amenukuriwa akisema, "Watu weusi huiba wakiwa na njaa; wakishiba huzini" (Sahih Mwislamu).
Katika Hadith nyingine Muhammad amenukuriwa akisema, "ni lazima umtii Imam (kiongozi) hata kama ni mtumwa mwenye pua iliyobonyea" (ikimaanisha mtu mweusi). Angalia Sahih Muislam juzuu ya 9 uk.46 na 47.

UISLAMU SI MAHALI SALAMA PENYE UHURU NA USAWA
Hata tukidhani kimakosa kuwa uislam ulianzia Afrika na kwamba Nabii wake alikuwa mweusi, hii pekee yake haitakuwa sababu nzuri kwa weusi kuasiri uislam.

Hata haitakuwa sababu nzuri kwa wazungu kuasiri uislamu kwasababu tu Muhammad alikuwa mweupe. Tunapaswa kuuangalia uislamu wenyewe.
Nisingependa niwe Muislam kwa sababu uislam hupingana na uhuru, kitu ambacho kipo karibu sana na mioyo na nia za Waamerika wenye asili ya Kiafrika, ukizingatia dhuluma waliyoipata hapo zamani.
Kitu kimoja ambacho uislam hauamini ni uhuru wa kidini. Ikiwa uislam utaichukua Amerika hapatakuwa na uhuru wa kidini. Koran inasema, "Ikiwa mtu yeyote ataka dini nyingine licha ya uislam, jambo hili halitakubaliwa kwake kamwe; na katika maisha yajayo mtu huyu atakuwa katika kundi la waliopotea (Sura 3:85).
Mafundisho mengi ya uislam hayaendani na na maendeleo na nyakati. Na pia hayaendani na haki za binadamu, haki za kiraia au haki za kikatiba.
Ifuatayo ni mifano michache ya uislam
  • Wanaume ni bora kuliko wanawake (Sura 2:228)
  • Wanawake wana haki nusu ya zile za wanaume:
  1. haki za kutoa ushahidi mahakamani (Sura 2:282)
  2. haki za mirathi (Sura 4:11)
  • Mwanaume aweza kumpiga mkewe (Sura 4:34)
  • Mwanaume aweza kuoa wake hadi wanne kwa wakati mmoja (Sura 4:3)
  • Waislam lazima wapigane mpaka wapinzani wao wajisalimishe kwenye uislam (Sura 9:5)
  • Muislam asiwe na rafiki Myahudi wala Mkristo (Sura 5:54)
  • Mtu anayeasi uislamu lazima auawe (Sura 9:12)
  • Wizi huadhibiwa kwa kukata mikono (Sura 5:41)
  • Ugoni huadhibiwa kwa kupigwa mijeredi hadharani (Sura 24:2)
  • Hakuna utengano kati ya kanisa [dini] na serikali. (Sura 2:193)
  • Hakuna upinzani utakaoruhusiwa hata kidogo (Sura 4:59)
Mwamerika mwenzangu mwenye asili ya Kiafrika
Kwa kusema kuwa uislam ni dini ya mtu mweusi, wakereketwa wa uislam wanaonyesha tu chuki yao halisi na ubaguzi wa rangi. Usiliache hili likakurubuni.
Waislam hawajali rangi ya ngozi yako, wanatumia usemi huo tu ili wapate kukuteka. Maana kama Waislam wangelikuwa wanajali watu weusi, kwa nini Waislam weusi wanawateka ndugu zao Wakristo weusi huko Sudan siku hizi, wakiwachinja wanyonge na kuwauza wenye afya kama watumwa (angalia taarifa ya Idara ya Taifa [State Dept]: Habari za Mtandao wa Kimataifa; Mei 26, 1993).
Zingatia, upande mwingine, kuwa Yesu Kristo alikuja kutupa uzima wa milele, ambapo kila mmoja ni sawa mbele za Mungu.
"Hapana Myahudi wala Myunani. Hakuna mtumwa wala aliyehuru. Hakuna mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu" (Wagalatia 3:28).

Tofauti kati ya mafundisho ya kiislam na mafundisho ya Yesu Kristo ni kubwa. Uchaguzi uko wazi, na uchaguzi huu ni wako mwenyewe.

IJUE KWELI
IFUATE KWELI
ISAMBAZE KWELI
"Mtaifahamu kweli, na hiyo kweli itawaweka huru" (Yohana 8:32).
"Kwa hiyo simameni, msinaswe tena na utumwa" (Wagalatia 5:1, 2). 

TENGENEZA NAKALA ZA KIPEPERUSHI HIKI NA UWAPATIE WATU WENGINE 

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW