Wednesday, July 1, 2015

MABINTI WATATU WA ALLAH


Mabinti wa Allah


Mara nyingi Waislam wamekuwa wepesi kuwaambia watu wengine kuwa Mungu ameruhusu Biblia kupotoshwa. Kitu wanachodokeza ni kuwa Kurani leo hii ni neno la Mungu lenye kuaminika wakati ambapo Biblia sivyo. Biblia ina maandiko yanayotofautiana mengi yenye tofauti ndogo, lakini ushahidi wa mabadiliko ya mafundisho hauna uzito. Kurani ina ushahidi mkubwa zaidi wa kupotoshwa kwa mujibu wa Ubai, aya zilizobatilishwa‘Uthman, na matatizo mengine ya Kurani. Hata hivyo, tofauti kubwa zaidi ya mafundisho ya Kurani, iliyoletwa na Waislam wenyewe, ni "mabinti wa Allah."

Muhtasari

Tovuti ya Kikristo http://answering-islam.org/Responses/Saifullah/sverses.htm inasema, "Moja ya matukio yenye kuaibisha zaidi kwenye maisha ya Muhammad lilitokea wakati Shetani alipoweka maneno yake kwenye mdomo wa Muhammad. Muhammad alisema maneno ya Shetani kama neno la Mungu. Tukio hili limethibitishwa kwa maandishi na waandishi kadhaa wa Kiislam wa kale na limeongelewa kwenye Hadithi na Kurani. Waislam wa miaka iliyofuata, kwa kujisikia aibu kuwa nabii wao aliyejitangaza mwenyewe amesema maneno ya Shetani, walikana kuwa tukio hili lilitokea. Visingizio na kukana kwingi vimekuwa vikitolewa na hawa Waislam wa miaka iliyofuata ili kulifunika kosa lenye kuhusisha dhambi la Muhammad.
Ni muhimu ikafahamika tena kuwa tukio la ‘Aya za Shetani’ si jambo ambalo limetungwa na watu wasiokuwa Waislam. Tukio hili limerekodiwa na vyazo vya kale zaidi vya Kiislam vilivyokuwepo wakati wa uhai wa Muhammad. Mtu yoyote asifikiri kuwa jambo hili ni hadithi iliyotungwa na watu wenye kuupinga Uislam. Ni kisa kinachopatikana moja kwa moja kwenye rekodi za kale za Kiislam.
Hili moja ya masomo yenye kubishaniwa zaidi kwenye Uislam. Shetani alimsababishia Muhammad kunena maneno yake (Shetani) kama maneno ya Mungu."

Je Kurani Ilisema Nini Mwanzoni?

Sura ya Nyota (Sura 53) mistari ya 19-20 inasema, "Je umemwona Lat, na ‘Uzza, Na mwingine, (mungu mke) wa tata, Manat?"

Allah alikuwa maarufu huko Arabia kabla ya kuja kwa uislam, kama mungu aliyekuwa na mabinti watatu: al-Lat, al-Uzza, na Manat. (Kumbuka kuwa al- inamaanisha ‘yule’, kwa Kiingereza "the".)

Waandishi wanne wa mwanzo wa maisha ya Muhammad waliandika kuwa awali aya hizi zilifuatwa na:

"Hawa ni mawinchi (wasuluhishi) ambao maombi yao yanapaswa kutumainiwa"

Tafsiri: Mabinti wa Allah walifikiriwa kuwa viumbe wa mbinguni wenye kuomba kwa ajili ya wengine. Mawinchi marefu ya Kinumidia ilikuwa ni sitiari yao. Maneno mbadala ya "inatakiwa kutumainiwa" (turtaja) ni "imekubaliwa kwa kuthibitishwa" (turtada). (Kutoka kwenye tafsiri ya Alfred Guillaume ya The Life of Mohammed, iliyoandikwa na Ibn Ishaq, uk.166.


Baadaye, kifungu hiki kiliondolewa na kifungu kifuatacho kiliwekwa badala yake:

"Nini! Kwako wewe mwenye jinsia ya kiume, Na kwake (mwanaume), mwanamke? Tazama, hakika mgawanyo huu hautakuwa wa haki kabisa." (aya za 53:21-22 leo)

Tafsiri: Wale wanaoamini kuwa Allah alikuwa na mabinti watatu hawakuntendea haki Allah, kwa sababu walipendelea watoto wa kiume ingawa walisema kuwa Allah alikuwa na wasichana tu.

Hizi ndizo ambazo zimeitwa "Aya za Shetani." Katika nyakati za sasa Salmon Rushdie alitumia msemo huu tu kwenye kichwa cha riwaya yake ya kubuniwa na isiyohusika na aya hizi, na andiko hili halikiongelei kisa hiki cha kisasa. Kwa upande wa Aya za Sheatani za asili, Muislam au mtu mwingine asiyekuwa Muislam mwenye kutazama jambo hil bila upendeleo anawezaje kujua aya ambazo zilikuwemo toka awali? Sehemu iliyobaki ya andiko hili inatoa ushahidi wa moja kwa moja na ule usio wa moja kwa moja kuwa Aya za Shetani zilikuwemo asilia, na mapingamizi tisa ya Kiislam.

Waandishi Wanne wa Maisha ya Muhammad: Ushahidi wa Moja kwa Moja

Ingawa si kila kitu Waislam wa kale walichosema kuhusu Muhammad kilikuwa kweli, wanazuoni wa kiislam wana uwezekano mkubwa zaidi wa kukubali mambo ambayo Muhammad aliyasema ambayo yameshuhudiwa na vyanzo vitatu au zaidi. Tunajua kuwa Aya za Shetani hazikutokana na vyanzo visivyokuwa vya kiislam, lakini kutoka wanazuoni wanne tofauti wa kale wa kiislam ambao walikuwa waandishi wa maisha ya Muhammad. Kumbuka kuwa watatu kati ya waandishi hawa walisimulia maisha ya Muhammad hata kabla ya mkusanyiko mashuhuri wa Hadithi ambao dhehebu la Kiisuni limejengeka juu yake.

Al-Wahidi/Wakidi (aliyekufa mwaka 207/823 BK) aliandika Asbab al-Nozul. "Kwenye siku fulani, wakuu wa Maka, walikusanyika kwenye kundi pembeni mwa Kaaba, walijadili kama ilivyo kawaida ya mambo ya mji wao; wakati Muhammad alipotokea na, kukaa karibu yao kwa namna ya kirafiki, alianza kusema sura 53 huku wakimsikia…. ‘Na usimwangalie Lat na Ozza, na Manat wa tatu zaidi?’ Alipofika kwenye aya hii, mwovu alipendekeza njia ya kujieleza mawazo yake ambayo iliitawala nafsi yake kwa siku nyingi; na aliweka mdomoni mwake maneno ya upatanisho na masikilizano, ufunuo aliokuwa anausubiri kwa hamu kubwa sana toka kwa Mungu, yaani; ‘Hawa ni wanawake waliotukuka, na hakika maombezi yao yanatakiwa kutumainiwa. ’ Wakoreish walishangazwa na kufurahishwa na kukubaliwa huku kwa miungu yao; na kama Mahomet alivyoimalizia Sura kwa maneno ya hitimisho ‘Kwa hiyo inama mbele ya Mungu, na mtumikie’ kusanyiko zima lilijiinamisha kwa moyo mmoja chini na kuabudu. … Jioni Gabriel alimtembelea; na nabii aliisema Sura hiyo kwake. Na Gabriel alisema, ‘Umefanya kitu gani? Umeyarudia mbele ya watu maneno ambayo sikuwahi kukupa’. Kwa hiyo Muhammad alisononeka zaidi …"

Ibn Sa’ad/Sa’d (aliyekufa mwaka 230/845 BK), aliifahamu kazi ya al-Wahidi lakini yeye mwenyewe alikuwa mwandishi wa habari za maisha ya watu aliyeandika kitabu chenye juzuu 15 kiitwacho Kitab al Tabaqat al Kabir.

Ibn Isaq/Ishaq (aliyekufa mwaka 145/767 au 151/773 BK) alikuwa Msuni wa mlengo wa Kishafi ambaye baadaye alianzisha shule yake mwenyewe iliyodumu kwa muda mfupi. Aliandika kitabu kiitwacho Sirat Rasullallah (Maisha ya Nabii wa Allah). "[Wahamiaji] walibakia sehemu ileile waliyokuwepo [Ethiopia] hadi waliposikia kuwa watu wa Maka wameukubali Uislam na wamejinyenyekeza. Hii ilikuwa ni kwa sababu sura ya Nyota [Sura 53] ilikuwa imetumwa kwa Muhammad na mtume aliinena. Mtu mmoja Muislam na mwenye kuamini miungu wengi alisikiliza kimya hadi alisema maneno haya ‘Je umemwona al-Lat na al-uzza?’ Walimsikiliza kwa uangalifu sana wakati waumini walimwamini [nabii wao]. Baadhi yao waliiasi imani yao walipoisikia ‘saj’ ya Shetani na kusema, ‘Kwa uwezo wa Allah tutawatumikia (mawinchi) ili kwamba watulete karibu na Allah.’ Shetani alifundisha aya hizi mbili kwa kila mtu aliyekuwa anaamini miungu wengi na ndimi zao zilizielewa kwa urahisi. Jambo hili lilimsunbua Mtume hadi Gabriel alipokuja kwake na kulalamika …." (Anaelezea mlolongo wa kuenea kuwa Yazid bin Ziyad-> Muhammad bin Ishaq -> Salama -> Ibn Hamid -> ibn Isaq

Ibn Jarir al-Tabari (aliyekufa mwaka 923 BK) alikuwa Msuni wa mlengo wa Kishati aliyeandika kitabu chenye juzuu 38 cha Kiislam cha Historia ya ulimwengu hadi mwaka 915 BK. Alipewa jina la "shehe wa wafafanuaji." Anaandika kwenye juzuu ya 6 uk.108-110, "Mjumbe wa Mungu alipoona jinsi kabila lake lilivyomkataa na kuhuzunishwa alipowaona wanauacha ujumbe aliowaletea toka kwa Mungu, alitamani moyoni mwake kuwa kitu chochote kimjie toka kwa Mungu ambacho kitampatanisha na kabila lake …. Na alipoyafikia maneno: ‘Je umewafikiria al-Lat na al-Uzza na Manat, wa tatu, Yule mwingine?’ Shetani alimlaumu, kwa sababu ya midahalo yake ya ndani na vitu alivyokusudia kupeleka kwa watu wake, maneno: ‘Haya ni mawinchi yanayopaa juu zaidi; hakika maombezi yao hupokelwa kwa kuthibitishwa [kwa mpokezano: kuhitajiwa au kutegemea].’ Waquraysh waliposikia hili, walifurahi sana na kupendezwa na namna alivyosema kuhusu muingu yao, na walimsikiliza, wakati Waislam, wakiwa wanamwamini kabisa nabii wao kuhusu ujumbe aliouleta kutoka kwa mungu, hawakumshuku kuwa amepotoka, anaota, au kafanya makosa. … Kisha [baadaye] Gabriel alikuja kwa Mjumbe wa Mungu na kusema, ‘Muhammad, umefanya nini? Umenena kwa watu kitu ambacho sikukuletea toka kwa Mungu …’"

Wanazuoni wa Kiislam wa miaka ya mbele waliosema jambo hili:
 Abu Ma’shar kutoka Chorassan (787-885 BH)
 Ibn Abi Hatim
 Ibn al-Mundhir
 Ibn Hajar from Asqalaan (773-852 BH)
 Ibn Mardauyah
 Musa ibn ‘Uqba
 Ufafanuzi mashuhuri sana wa Zamakhshari wa Sura 22:52. (1070-1143 BH)
Wanazuoni sita ni kwa mujibu wa kitabu kiitwacho The Book of the Major Classes, kilichotafsiriwa na S. Moinul ‘Haq.

Ushahidi usiokuwa wa moja kwa moja wa Aya za Shetani:
Kurani na Hadithi

Bukhari alikufa karibu na mwaka 870 BK (hata miaka mitatu baada ya vyanzo vitatu kati ya vinne vilivyoorodheshwa.) Wakati Muhammad alipoisema Sura ya Nyota, wapagani na Waislam walisujudu. (Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 19 na.173, uk.100 juzuu ya 3 kitabu cha 19, na.176, uk.101; juzuu ya 6 kitabu cha 60 na.385-386 uk.364-365; Abu Dawud juzuu ya 1 kitabu cha 2 sura ya 481 na.1401, uk.369). Wapagani hawasemekani kusujudu kwa ajili ya Muhammad kusema maneno mengine yoyote, ni kwa nini wakubaliane kiasi hiki na sura hii, hasa kwa vile Bukhari na Abu Dawud hawasemi kuwa hao wapagani waliwahi kuwa Waislam, na hii ilikuwa kabla ya vita na hawa wapagani wa Maka!

Pia, Sura 22:52 inasema, "Hatukuwahi kumtuma mtume au nabii Kabla yako, lakini, alipoumba nia, Shetani alimtupia (ubatili) kiasi kwenye nia yake: lakini Mungu atafuta kitu chochote (batili) ambacho Shetani anatupia ndani, na Mungu atafanya dhahiri (na kuthibitisha) Ishara Zake…"

Sura 17:73-75 inasema, "Na lengo lao lilikuwa kukujaribu na kukupeleka mbali na jambo tulilolifunua kwako, kuweka badala yake kitu tofauti kabisa kwa kutumia jina letu: (Kwa ajili hiyo), tazama! Watakuwa wamekufanya kuwa rafiki (yao)! Na je hatujakupa wewe, ungeweza kuelekea upande wao kiasi. Katika hali hiyo tulipaswa kukufanya uonje mara mbili (ya adhabu) kwenye maisha haya, na kiasi kama hichohicho mautini: na zaidi ya hapo usingepata mtu wa kukusaidia dhidi yetu!"

Kumbuka kwamba ingawa baadhi ya watu wanadai kuwa Sura 17:73-75 ilifunuliwa wakati wa "Kupaa kwa Nabii", Tabari na Ibn Sa’d waliandika kuwa Sura 17:73-75 ilifunuliwa karibu na wakati wa aya za Shetani. Waislam hata wana neno maalum la kunong’oneza kwa Shetani, ambalo matamshi yake yanafanana na "wiswas".

Mapingamizi Tisa ya Kiislam na Maitikio Yake

Pingamizi la 1 la Waislam: Watu wengine mbali ya hawa kumi na moja hawajaziongelea aya za Shetani. Baadhi ya wanazuoni wa Kiislam ambao hawakundika kuhusu aya za Shetani walkuwa Imam Muslim aliyeandika Sahih Muslim, Abu Dawud, Nas’ai, Ahmad bin Hanbal, and ibn Hisham.
Itikio: Kuna vitu vingi kwenye makusaniko ya Hadithi ambavyo havimo kwenye mikusanyiko mingine. Kwa mfano, Hadithi ndefu za Bukhari hazina mafundisho kuhuu sababu za kutoa zaka, adhabu ya kujilimbikizia vitu, na malaika wawili wanaomtembelea Muislam kila asubuhi kama yanavyopatikana kwenye Sahih Muslim juzuu ya 2 sura ya 371 na.2205, uk.484. Kama mfano wa pili, tunajua kuwa Ibn Hisham aliitumia Bukhari, lakini aliiacha sehemu inayohusu aya za Shetani. Kwenye nakala ya Ibn Hisham ya Ibn Ishaq, alisema aliondoa vitu alivyoona kuwa vibaya. Kama alijisikia aibu sana hata hakuweza kuziweka, huo sio uthibitisho kuwa hazikutokea.

Pingamizi la 2 la Waislam: Aya zinazodaiwa kuwa za Shetani haziendani sawa na sehemu nyingine ya Sura 53.
Itikio: Kumbuka kuwa sehemu ya sasa haikufuatia aya za Shetani, bali ilichukua nafasi zao. Pia nyakati zingine sehemu tofauti za Sura moja zilitolewa nyakati tofauti. Upande mmmoja, al-Wahidi alisema Muhammad alisema hadi maneno ya mwisho. Kwa upande mwingine, hatujui kuwa Sura yote ya Nyota (53) baada ya aya ya 22 iliandikwa wakati mmoja. Aya za 51-53 zinaonekana kuwa hazipo mahali ake kwani zinamongelea Muhammad mwenyewe.

Pingamizi la 3 la Waislam: Sura 53:19-21 inaweza kuwa ilikuwa mapema zaidi kuliko Sura zinazoongelea kunong’ona kwa Shetani.
Itikio: Tabari na ibn Sa’ad wanasema zilifunuliwa wakati mmoja na Sura 17:73-75. Hakuna mtu leo hii anayejua kwa uhakika wakati ambapo aya nyingi za Kurani ziliandikwa. Kwa upande mwingine, hata kama iliandikwa mapema haitaweza kukanusha maneno iliyoyasema. Kama Waislam wasahilina wanaiamini kabisa Kurani, ikiwa ni pamoja na Sura 17:73-75 na 22:52, watatakiwa kuamini kwamba Shetani anaongeza vitu kwenye Kurani. John Gilchrist, kwenye Muhammed and the Religion of Islam uk.120 anasema, "Hoja nyingine ni dhaifu kwa sababu hakuna ushahidi thabiti kuwa sehemu ya kwanza ya Surah 53 inaongelea miraj [kupaa kwa Muhammad] kulikotokea baada ya kuhamia Abyssinia. Kama ilivyokwishaonyeshwa, kuna uhakika wa kiasi kikubwa sana kuwa inaongelea moja ya ziara za mwanzo za Muhammad, ambazo Kurani yenyewe inaonyesha kuwa hazizidi mbili ambazo alizifanya wakati huduma yake ilipoanza. Kwa bahati mbaya inaonekana kuwa hoja zote za Waislam za uhalisi wa vipingamizi vya habari hii ni dhaifu."

Pingamizi la 4 la Waislam: Aya za Shetani zinapingana na mafundisho ya msingi kuwa kuna Mungu mmoja ambayo Muhammad alishikilia kufundisha.
Itikio: Muhammad hajawahi kuthibitishwa kushikilia kitu chochote kile. Kumbuka, Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 10 na.490, uk.317; juzuu ya 4 kitabu cha 53 sura ya 38 kabla ya na.400, uk.266; juzuu ya 8 kitabu cha 53 sura ya 38 na.400, uk.267 inarekodi kuwa Muhammad alikuwa amerogwa na mwovu kwa kipindi fulani. Isitoshe waandishi wa maisha yake na watu wengine waliorekodi jambo hili walikuwa bado Waislam, kwa hiyo wana historia hawa wanathibitisha kuwa kulikuwa na watu kadhaa ambao walikuwa tayari kumfuata Muhammad hata kama alisema uongo.

Pingamizi la 5 la Waislam: Vifungu vingi kwenye Kurani vinasema Muhammad hakuweza kusema maneno yoyote yasiyokuwa kweli, na kwa ajili hiyo jambo hili haliendani na tafsiri kuwa Shetani anaingilia mambo. Kwa mfano,
Sura 10:15b: "Sema; Si kwa ajili yangu, kwa hiari yangu, kubadilisha hili: Sifuati kitu chochote isipokuwa kile kilichofunuliwa kwangu…"
Sura 41:42: "Hakuna uongo unaoweza kulikaribia kutokea mbele au nyuma yake: Limetumwa na Yeye Aliyejaa Hekima na Mwenye Kustahili Sifa zote."
Sura 15:9: "Tumeutuma, bila shaka, Ujumbe; na tutaulinda kwa hakika (dhidi ya uharibifu)."
Sura 60:44-46: "Kama (Mjumbe) angetunga neno lolote kwa jina letu, Tungemkamata kwa mkono wa kulia na kisha tungeikata ateri ya moyo wake"
Itikio: Kwa upande mmoja, inadaiwa kuwa Shetani, siyo Muhammad, alitunga aya za Shetani, na kulindwa kwa Kurani haukanushi kuingia kwa mafundhisho ya uongo na Mungu kuyarekebisha. Kwa upande mwingine, kama Muislam anatafsiri aya hizi kuwa zinafundisha kwamba hakuna kitu cha uongo kitakachoweza kuingia ujumbe wa nabii, hata kama aya za Shetani hazitahusishwa, jambo hili litakuwa kinyume na kunong’oneza kwa Shetani ambako kumeelezwa kwenye Kurani.
Pia, hii si mara pekee aya ya Kurani "inapotea kabisa" kwa sababu ilibatilishwa. Sahih Muslim juzuu ya 1 sura ya 244 na.1433, uk.329-330 ni Hadithi muhimu kwa sababu inaonyesha kuwa aya ilibatilishwa, bali baada ya kubatilishwa ilipotea kabisa. Hivyo ama:
a) Kurani kwenye mbao zenye maandishi [mbinguni] ilikuwa na toleo la awali, na toleo lililofuata lilitofautiana na mbao hizo. Kurani ya leo inatofautiana na mbao zenye maandishi za mbinguni.
b) Kurani kwenye mbao zenye maandishi za mbinguni zina toleo la baadaye, na toleo la awali linatofautiana nalo. Kwa hiyo maneno ya kwanza yalitolewa kama kiwakilishi cha mbao zenye maandishi za mbinguni wakati ukweli ni kwamba ilikuwa ni uongo.
Kipi ni kipi? Mbao za maandishi [mbinguni] kwenye Sura 85:20-22 hazidhaniwi kutengenezwa kwa puti ya kipumbavu.

Pingamizi la 6 la Waislam: Tabari anawezakuwa hakukusanya habari kiuhakiki.
Itikio: Ingawa hatuna ushahidi wa mada haya, waandishi wengine watatu wa maisha [ya Muhammad] pia waliandika jambo hili. Wawili kati yao waliandika kabla ya Tabari, kwa hiyo hata kama Tabari alionekana kutokuwa mhakiki, jambo hilo haliwezi kuathiri kitu chochote kwa kiasi kukubwa kwani bado tuna watu wengine watatu. Muislam anaweza kupenda kuona kuwa waandishi wote wa maisha ya Muhammad wanaonekana kuwa na dosari sana, lakini vyanzo mbalimbali vinaonyesha usahihi wao.
Pamoja na hayo, Tabari hakupokea vitu vyote bila kuvihakiki. Kwa mfano, kwenye juzuu ya 1, uk.532 anasimulia tamaduni nyingi za kiislam za Adam na Hawa alizojifunza kutoka kwa watu wenye Torati. Anazinukuu nyingi zake lakini anasema kuwa ana mashaka na uhakika wa hizi Hadithi. (Kutoka kwenye kitabu cha Barbara Freye Stowasser kiitwacho Woman in the Qur’an, Tradition, and Their Interpretation uk.28).

Pingamizi la 7 la Waislam wa Madhehebu ya Suni: Hadithi zenye uhakika hazilisemi jambo hili moja kwa moja.
Itikio: Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 19 sura ya 42 na.173, uk.100; juzuu ya 3 kitabu cha 19 sura ya 43 na.176, uk.101; juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 286-287 na.385-386, uk.364-365; Abu Dawud juzuu ya 1 kitabu cha 2 sura ya 481 na.1401, uk.369 zinaeleza hali waliokuwa nayo watu wa Maka walipokuwa wanasujudu waliposikia Sura 53. Ni vigumu kueleza tofauti kitu kilichokuwepo kuhusiana na sura hii kilichowafanya wapagani wasujudu kwa ajili ya sura hii, ikiwa hawakusujudu kwa ajili ya kitu kingine. Kurani yenyewe pia inasema kuhusu "kunong’oneza" kwa Shetani.

Pingamizi la 8 la Waislam wa madhehebu ya Suni: Shaykh al-Albani, kwenye vitabu vyake vinavyohusu mtiririko wa waenezaji wa tamaduni, alisema ushahidi wa aya za Shetani una mlolongo mbaya wa ueneaji (isnad).
Itikio: http://answering-islam.org/Responses/ Saifullah/sverses.htm inasema, "Kuhusu al-Albani, nimefahamishwa kuwa siku hizi al-Albani ameelezwa vibaya sana kwa kutokuwa sahihi kuhusu isnads, hata anaandika kwenye kitabu kimoja kuwa mtu fulani ni mkweli lakini kwenye kingine anasema kwamba jambo hilo si sahihi! Kitabu kiitwacho Al-Albani Unveiled kilichoandikwa na Sayf ad-Din Ahmed Ibn Muhammad Amirul Islam kinatoa mifano mingi sana. Upande wa nyuma unasema: Kitabu hiki ni uchunguzi mchanganifu wa mmoja wa mashehe muhimu zaidi wa Hadithi(Muhammad Nasiruddeen al-Albani) wa harakati ya kisasa ya kiislam inayojulikana kama ‘Salafiya’. Mtunzi ameeleza wazi kabisa kupingana kwa Al-Albani kwa kutumia msaada wa kazi iliyoandikwa kwanza kwa Kiarabu (Tanaqadat al-Albani al-Wadihat), na mwanazuoni wa wa Hadithi wa Kijordani anayejulikana sana - Shakh Hasan ibn Ali al-Saqqaf."

Pingamizi la 9 la Waislam: Watu wasio Waislam wanampinga Muhammad na uislam.
Itikio: Tukio hili halikuundwa na watu wasiokuwa Waislam, bali liliandikwa na Waislam wenyewe. Waislam hawa wasahilina walikuwa na vyanzo vya zamani zaidi kuliko Waislam wa sasa. Kulifumbia macho jambo linalokosoa mtazamo wako kwa sababu tu linakosoa maoni yako, hakuendani na kuufuata ukweli. Kwa kuwa Wakristo wanadai kufundisha ukweli, tunao wajibu wa kumtaja nabii wa uongo. Hatufanyi hivi kwa sababu ya chuki au matakwa binafsi, bali kwa sababu ya upendo na haja ya kuwaona Waislam wanaepukana na mafundisho ya uongo, na kumgeukia Yesu wa kweli na kuwa nasi mbinguni pamoja na Mungu wa kweli.

Unakwenda wapi kutoka hapa?

Waislam wenyewe hawajakubaliana endapo maneno ya Shetani yalikuwemo kwenye Kurani mwanzoni.

Chaguo la 1: Itakuwa vipi endapo Muhammad aliongea kama nabii kuhusu maombezi ya mabinti wa Allah? Jambo hili litamfanya Muhammad kuwa nabii wa uongo kwa kipindi fulani.

Chaguo la 2: Itakuwa vipi endapo Muhammad hakuwahi kusema aya za Shetani? Waandishi wote wanne wa maisha ya Muhammad watakuwa wamekubaliana kukosea kuwa Muhammad alikuwa nabii wa uongo. Baadhi ya watu watachagua, kwa hiari yao wenyewe, kufuata kitu hata kama wanaamini kuwa kiongozi wao aliongea mambo ya Shetani. Hata kama jambo hili ni kweli, utafanya nini na aya za Kurani zinazohusu minong’ono ya Shetani ambayo Muhammad aliipata?

Kwa vyovyote vile, uislam unafundisha kuwa Allah anaruhusu maneno yake yabadilishwe kiasi kikubwa sana, na Allah anaruhusu wafuasi wake wazuri wajifunze njia za uongo kama njia ya ukweli. Hii ni kwa sababu Kurani kwenye Sura 43:44-45, inaonyesha kuwa manabii wote waliotangulia walikuwa na ujumbe mmoja. Sura 41:43 inasema kwamba hakuna kitu kilichotumwa kwa Muhammad ambacho hakikuwahi kutumwa kwa manabii waliomtangulia pia. Kwa hiyo kwa Waislam, ama
a) Allah aliruhusu ujumbe wake uliopotoshwa hapo awali,
b) Au, Kurani ndio ujumbe uliopotoka.
Kwa vyovyote vile, uislam unasema, Allah hawezi kutumainiwa kulitunza neno lake dhidi ya mabadiliko makubwa ya mafundisho.

Mwamini Mungu

Mungu Mwenye nguvu anao uwezo wa kuutunza ujumbe wake. Watu wanatakiwa kumwamini Mungu zaidi.

Mwamini Mungu kuwa amelitunza neno lake. Sura 5:46-48 inasema kwamba Yesu aliithibitisha Torati (kwa wakati wake), Mungu alituma Maandiko kwa Wayahudi na Wakristo, na hata wakati wa uhai wa Muhammad wangeweza kuupima ukweli kwa kuyatumia [Maandiko]. Sura 3:48 na 5:110-111 zinamwonyesha Yesu kuwa alikuwa na Torati na Injili. Wanafunzi wa Yesu pia walikuwa wamevuviwa. Kwenye Biblia, Isaya 59:21; 40:8; Zab. 119:89 zinaonyesha kuwa neno la Mungu hudumu milele. Neno lake halikuwa na kosa lolote hapo awali, na limetunzwa bila makosa (bila makosa makubwa) hadi leo hii. (Isa. 55:11; 1 Petro 1:23-25; Zaburi 119:89, 91, 144, 160).

Tumaini kuwa Mungu anataka uufuate ukweli na uje kwake. Mungu hataki mtu yoyote aangamie (Ezekiel 18:23, 32; 2 Petro 3:9). Watu wote wanatakiwa kuiamini Injili ya Yesu Kristo kwenye 2 Wathesalonike 1:8.

Usimtumaini mwanadamu ambaye maisha yake yana ukomo. Usiwatumaini watu wengine ambao wanakugeuzia mbali na Mungu. "Usiwe mwenye hekima machoni pako (Mithali 3:7). Badala yake, "Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako" (Mithali 3:5-6). Je unaamini kuwa Mungu anaweza kunyoosha njia zako kama ukimkiri?

Mtumaini Yesu; Yeye ametoka kwa Mungu na ujumbe wa Mungu umetunzwa. Yesu si mwizi wala mnyang’anyi (Yohana 10:8-10). Amini kuwa Yesu alitoa uhai wake kama fidia ya ukombozi (Mathayo 20:28), ili iwe sadaka ya dhambi (Warumi 8:3), kwa njia ya damu yake aliyoimwaga msalabani (Waeb. 10:19).


Mwamini Bwana Yesu nawe utaokolewa (Matendo 16:31). "… ‘Kila amwaminiye hatatahayarika’" (Warumi 10:11). Kwa hiyo mtumaini Mungu, na amini kuwa anaongoza kwa uaminifu. Hakuacha neno lake lipotoshwe, kwa hiyo Biblia inaaminika. Mpe Yesu maisha yako, na atakupa amani na furaha.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW