SHALOM TENA,
Kwa mara nyingine twamshukuru Yehova Mungu kwa kutupa neema hii tena ili tuweze kukufikishia ujumbe huu wa Biblia na kweli zake.
Kwa muda wa miaka mingi sana pia duniani pote imekuwa ni kawaida kuwasikia waislamu wakifundisha watu wao na kuwadanganya bila ya wao kujuwa ao wengine wakiwa wanakijuwa wanachokifanya kuwa ISA bin Maryam’ Kama Qurani inavyofundisha ndiye “YESU KRISTO”.
Mafundisho haya hivi sasa yanaendeshwa kwa kulinganisha aya za Biblia na Qurani. Ma sheihk, ma Imam na wahubiri wengi wa dini ya kiislamu wanaendesha mihadhara kwa uwingi duniani. Wahadhiri hao pia hutumia mbinu zingine mbali-mbali kama majarida na kurekodi kanda za audio na video, ambazo zimesababisha baadhi ya wakristo nusu au wakristo wajinga waamini kuwa Isa Bin Maryamu ndiye Yesu Kristo. Swali la msingi kwa wakristo wote;Je, ni kweli Isa bin Maryam ndiye Yesu Kristo?
Nakusihi kwa jina lake Bwana wetu Yesu Kristo kufuatilia somo hili kwa umakini wote kama tulivyokuahidi katika lile somo ambalo lilitangulia wiki jana.
SEHEMU KUU ZA SOMO HILI
1. Madai yanayotumika na waislamu kusema Isa ndiye Yesu
2. Je, mama wa Isa ndiye wa Yesu?
3. Maana ya jina Isa
4. Maana ya jina Yesu
5. Je, kuzaliwa kwa Yesu ni sawa na Isa?
6. Je, Isa bin Mariamu ni mwana wa Mungu?
7. Je, mamlaka ya Isa na Yesu ni sawa?
8. Ikiwa Yesu ndiye Isa je, Isa.
9. Ujue umuhimu wa kumwamini Bwana Yesu
1. Kisingizio N0.1
Waislamu husema Isa ndiye Yesu
Qr.3 au surat I’mran 45
(Kumbukeni) waliposem malaika. ‘Ewe Maryamu Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za (kumzaa moto bila mume bali hali kwa kutamka) Neno tu litokalo kwake (la kumwambia zaa ukazaa pasina kuingiliwa) jina lake ni Masihi Isa mwana Maryamu, mwenye hishima kaitka dunia na ahera na miongoni mwa waliopelekwa mbele na Mwenyezi Mungu.
(Kumbukeni) waliposem malaika. ‘Ewe Maryamu Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za (kumzaa moto bila mume bali hali kwa kutamka) Neno tu litokalo kwake (la kumwambia zaa ukazaa pasina kuingiliwa) jina lake ni Masihi Isa mwana Maryamu, mwenye hishima kaitka dunia na ahera na miongoni mwa waliopelekwa mbele na Mwenyezi Mungu.
Marko 6:3-4, Huyo si Yule seremala, mwana wa Mariamu na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. Yesu akawaambia ‘Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake na nyumbani mwake.
Hapa Waislamu wanasema kana vile Qurani inavyofundisha jina la mama wa Isa ni Mariamu kadhalika Biblia inafundisha jina la mamake Yesu ni Mariamu. Hivyo wanasema kuwa Yesu ndiye Isa.
Soma pia Mathayo 1: 18-21 na Yohana 2:1.
2. Kisingizio N0.2
Isa ni Mtume wa Allah kwa Waisraeli
Qr. 4 au surat An-Nisaai 171
Enyi watu wa kitabu misipindukie mipaka katika dini yenu, wala msiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila yaliyo kweli. Masihi Isa bin Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu…
Hapa tunaona kuwa Qurani imemtaja Isa kuwa ni ntume, je, mtume kwa akina nani? Endelea kusoma aya hizi katika Qurani:
Qr. 61 au surat Ass’af 6
Na Isa bin Maryamu aliposema: enyi wana wa Israili! Mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu. Nisadikishaye yaliyo kuwa kabla yangu kaitka Taurati. Na kutoa habari njema ya mtume atakeayewajia nyuma yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad…
Soma pia katika Qr. 3 au surat Al I’mran 49:
Ayah ii inathibitisha kuwa Isa ni mtume kwa Waisraeli. Je, Yesu ni mtume kwa akina nani? Waislamu wanaoendesha mihadhra pia husoma aya hizi za Biblia.
Waebrania 3:1, Kwa hiyo ndugu watakatifu wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtakafarini sana mtume na kuhani mkuu wa maungamo yetu Yesu.
Mathayo 15:24, Akajibu, akasema, ‘Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
Kwa hivyo kama Qurani inavyofundisha kuwa Isa mwana wa Maryamu ni mtume kwa Waisreali ndivyo Biblia inafundisha kuwa Yesu ni mtume kwa waisraeli hivyo basi Isa ndiye Yesu. Hapa ndipo wahadhiri wa dini ya Uislamu wanavyoifundisha na kuwashika mateka na jamii za wakristo-nusu. Je, madai haya ni sahihi? Biblia itatusaidia kujibu huko mbele.
3. Kisingizio N0.3
Isa bin Maryamu alifanya miujiza
Qr. 5 au surat Al Maida 110
Na pale Mwenyezi Mungu atakaposema, Ewe Isa mwana wa Maryamu kumbuka neema yangu juu yako na juu ya mama yako. Nilipokutia nguvu kwa Roho takatifu (Jibrili), ukazumgumza na watu katika utoto (wako) na katika utuuzima (wako). Na nilipokufundisha kuandika na hikima na Torati na Injili na ulipotengeneza kwa undongo sura za ndege kwa idhini yangu, na ulipo waponesha vipofu na wenye ukoma kwa idhini yangu, na ulipowafufua (baadhi ya) wafu (makaburi mwao) kwa idhini yangu, na nilipokuzuilia wana wa Israeli (wasikudhuru) ulipowafikia kwa joha zilizo wazi; wale walio kufuru miongoni mwao wakasema: Haya si chochote ila ni uchawi dhahiri
Waislamu wanasem huu ni ushahidi wakutosha kwani Allah anasema Isa alifanya miujuza mingi hii.
Isa aliponyesha vipovu ndiye Yesu aliponyesha vipovu Mk 10:46-52, aliyewafufua wafu makaburi ndiye Yesu aliyewafufua pia huu upande, Mk 5:21-43 na aliyewaponyesha wenye ukoma ndiye…Yesu aliponya Ukima Luka17:1
Walimu wa kiislamu hao wanasema kama vile Qurani invyosimulia kuwa Isa amefanya miujiza mingi, ndiyo Biblia inavyofundisha hivyo Yesu ndiye Isa, isitoshe wanasema hivi pia:
Isa ibin Maryamu ni Nabii, Quran suratul 4:171, kadhalika Biblia inafundisha kuwa Yesu ni Nabii, Yohana 6:14, Yohan 7:40, Luka 13:33; 24:19, Marko 6:4, na Mathayo 13:57.
Kulingana na watafiti wa Biblia imeelezwa kuwa imerikodiwa kwamba Yesu ni Nabii mara 12. Vile vile wahadhiri wa Kiislamu wanafundisha ya kwamba Isa ni Neno la Kiarabu, katika kiingreza Jesus na kwa Kiswahili ni Yesu. Kupitia ushawishi huu wamara kwa mara baadhi ya Wakristo wameshawishika kuamini kuwa Isa ndiye Yesu. Lakini, lazima tuzichunguze hizi hoja moja kwa moja ili tujue ukweli.
Kulingana na watafiti wa Biblia imeelezwa kuwa imerikodiwa kwamba Yesu ni Nabii mara 12. Vile vile wahadhiri wa Kiislamu wanafundisha ya kwamba Isa ni Neno la Kiarabu, katika kiingreza Jesus na kwa Kiswahili ni Yesu. Kupitia ushawishi huu wamara kwa mara baadhi ya Wakristo wameshawishika kuamini kuwa Isa ndiye Yesu. Lakini, lazima tuzichunguze hizi hoja moja kwa moja ili tujue ukweli.
4. TUFANYE UCHUNGUZI PAMOJA
1. Je, Mama wa Isa ndiye yule wa Yesu Kristo?







