Thursday, July 30, 2015

JE, ISA BIN MARYAM NDIYE YESU KRISTO?



 Utangulizi

SHALOM TENA,

Kwa mara nyingine twamshukuru Yehova Mungu kwa kutupa neema hii tena ili tuweze kukufikishia ujumbe huu wa Biblia na kweli zake.

Kwa muda wa miaka mingi sana pia duniani pote imekuwa ni kawaida kuwasikia waislamu wakifundisha watu wao na kuwadanganya bila ya wao kujuwa ao wengine wakiwa wanakijuwa wanachokifanya kuwa ISA bin Maryam’ Kama Qurani inavyofundisha ndiye “YESU KRISTO”.

Mafundisho haya hivi sasa yanaendeshwa kwa kulinganisha aya za Biblia na Qurani. Ma sheihk, ma Imam na wahubiri wengi wa dini ya kiislamu wanaendesha mihadhara kwa uwingi duniani. Wahadhiri hao pia hutumia mbinu zingine mbali-mbali kama majarida na kurekodi kanda za audio na video, ambazo zimesababisha baadhi ya wakristo nusu au wakristo wajinga waamini kuwa Isa Bin Maryamu ndiye Yesu Kristo. Swali la msingi kwa wakristo wote;Je, ni kweli Isa bin Maryam ndiye Yesu Kristo?

Nakusihi kwa jina lake Bwana wetu Yesu Kristo kufuatilia somo hili kwa umakini wote kama tulivyokuahidi katika lile somo ambalo lilitangulia wiki jana.

SEHEMU KUU ZA SOMO HILI

1. Madai yanayotumika na waislamu kusema Isa ndiye Yesu

2. Je, mama wa Isa ndiye wa Yesu?
3. Maana ya jina Isa
4. Maana ya jina Yesu
5. Je, kuzaliwa kwa Yesu ni sawa na Isa?
6. Je, Isa bin Mariamu ni mwana wa Mungu?
7. Je, mamlaka ya Isa na Yesu ni sawa?
8. Ikiwa Yesu ndiye Isa je, Isa.
9. Ujue umuhimu wa kumwamini Bwana Yesu

1.  Kisingizio N0.1
Waislamu husema Isa ndiye Yesu
Qr.3 au surat I’mran 45
(Kumbukeni) waliposem malaika. ‘Ewe Maryamu Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za (kumzaa moto bila mume bali hali kwa kutamka) Neno tu litokalo kwake (la kumwambia zaa ukazaa pasina kuingiliwa) jina lake ni Masihi Isa mwana Maryamu, mwenye hishima kaitka dunia na ahera na miongoni mwa waliopelekwa mbele na Mwenyezi Mungu.
Marko 6:3-4, Huyo si Yule seremala, mwana wa Mariamu na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. Yesu akawaambia ‘Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake na nyumbani mwake.
Hapa Waislamu wanasema kana vile Qurani inavyofundisha jina la mama wa Isa ni Mariamu kadhalika Biblia inafundisha jina la mamake Yesu ni Mariamu. Hivyo wanasema kuwa Yesu ndiye Isa.
Soma pia Mathayo 1: 18-21 na Yohana 2:1.
2. Kisingizio N0.2
Isa ni Mtume wa Allah kwa Waisraeli
Qr. 4 au surat An-Nisaai 171
Enyi watu wa kitabu misipindukie mipaka katika dini yenu, wala msiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila yaliyo kweli. Masihi Isa bin Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu…
Hapa tunaona kuwa Qurani imemtaja Isa kuwa ni ntume, je, mtume kwa akina nani? Endelea kusoma aya hizi katika Qurani:
Qr.  61 au surat Ass’af 6
Na Isa bin Maryamu aliposema: enyi wana wa Israili! Mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu. Nisadikishaye yaliyo kuwa kabla yangu kaitka Taurati. Na kutoa habari njema ya mtume atakeayewajia nyuma yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad…
Soma pia katika Qr. 3 au surat Al I’mran 49:
Ayah ii inathibitisha kuwa Isa ni mtume kwa Waisraeli. Je, Yesu ni mtume kwa akina nani? Waislamu wanaoendesha mihadhra pia husoma aya hizi za Biblia.
Waebrania 3:1Kwa hiyo ndugu watakatifu wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtakafarini sana mtume na kuhani mkuu wa maungamo yetu Yesu.
Mathayo 15:24Akajibu, akasema, ‘Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
Kwa hivyo kama Qurani inavyofundisha kuwa Isa mwana wa Maryamu ni mtume kwa Waisreali ndivyo Biblia inafundisha kuwa Yesu ni mtume kwa waisraeli hivyo basi Isa ndiye Yesu. Hapa ndipo wahadhiri wa dini ya Uislamu wanavyoifundisha na kuwashika mateka na jamii za wakristo-nusu. Je, madai haya ni sahihi? Biblia itatusaidia kujibu huko mbele.
3. Kisingizio N0.3
Isa bin Maryamu alifanya miujiza
Qr. 5 au surat Al Maida 110
Na pale Mwenyezi Mungu atakaposema, Ewe Isa mwana wa Maryamu kumbuka neema yangu juu yako na juu ya mama yako. Nilipokutia nguvu kwa Roho takatifu (Jibrili), ukazumgumza na watu katika utoto (wako) na katika utuuzima (wako). Na nilipokufundisha kuandika na hikima na Torati na Injili na ulipotengeneza kwa undongo sura za ndege kwa idhini yangu, na ulipo waponesha vipofu na wenye ukoma kwa idhini yangu, na ulipowafufua (baadhi ya) wafu (makaburi mwao) kwa idhini yangu, na nilipokuzuilia wana wa Israeli (wasikudhuru) ulipowafikia kwa joha zilizo wazi; wale walio kufuru miongoni mwao wakasema: Haya si chochote ila ni uchawi dhahiri
Waislamu wanasem huu ni ushahidi wakutosha kwani Allah anasema Isa alifanya miujuza mingi hii.
Isa aliponyesha vipovu ndiye Yesu aliponyesha vipovu Mk 10:46-52, aliyewafufua wafu makaburi ndiye Yesu aliyewafufua pia huu upande, Mk 5:21-43 na aliyewaponyesha wenye ukoma ndiye…Yesu aliponya Ukima  Luka17:1
Walimu wa kiislamu hao wanasema kama vile Qurani invyosimulia kuwa Isa amefanya miujiza mingi, ndiyo Biblia inavyofundisha hivyo Yesu ndiye Isa, isitoshe wanasema hivi pia:
Isa ibin Maryamu ni Nabii, Quran suratul 4:171, kadhalika Biblia inafundisha kuwa Yesu ni Nabii, Yohana 6:14Yohan 7:40Luka 13:3324:19Marko 6:4, na Mathayo 13:57.
Kulingana na watafiti wa Biblia imeelezwa kuwa imerikodiwa kwamba Yesu ni Nabii mara 12. Vile vile wahadhiri wa Kiislamu wanafundisha ya kwamba Isa ni Neno la Kiarabu, katika kiingreza Jesus na kwa Kiswahili ni Yesu. Kupitia ushawishi huu wamara kwa mara baadhi ya Wakristo wameshawishika kuamini kuwa Isa ndiye Yesu. Lakini, lazima tuzichunguze hizi hoja moja kwa moja ili tujue ukweli.

          4. TUFANYE UCHUNGUZI PAMOJA
 
1. Je, Mama wa Isa ndiye yule wa Yesu Kristo?
Hapo awali tumeona kuwa mama wa Isa anaitwa Maryamu,
Qr.3:45 na pia mama wa Yesu anaitwa Mariamu Mathayo 1:18-21Marko 6: 3-4 lakini kufanana kwa majina hakuwezi kamwe kumaanisha kuwa ni mtu mmoja, kwani walio na jina hilo ni wengi.
Biblia inatufundisha hivi.
Yohana 19:25, Na penye Msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama,Mamaye, na umbu la mamaye Mariamu wa Klopa na Mariamu Magdalena.
Hapa tunaona Mariamu watatu. Ili kutambua tofauti baina ya Mariamu mama wa Isa na mama wa Yesu, lazima tulinganishe ujumbe wa Qurani na Biblia. Qurani inasimulia kuhusu baba na kaka wa Mariamu mama wa Isa hivi.
Qr. 66:12,
Na Maryamu mtoto wa Imrani aliyejihifadhi nafsi yake na tukampuliza humo roho yetu, (inayotokana na sisi) na akayasadikisha maneno ya mola wake, na vitabu vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyeke.
Qr. 19:28,
Ewe dada yake Haruni. Baba yako hakuwa mtu mbaya. Wala mama yako hakuwa hasharati.
Hapa tunaona kuwa Maryamu mama wa Isa, baba yake ni Imrani na kaka yake aliitwa Haruni.
Tusomapo Biblia inatueleza kuwa Amrani aliwazaa hawa:
Hesabu 26:59,
Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amram Haruni, na Musa, na Miriamu umbu lao.
Pia soma 1Nyakati 6:1-3 na Kutoka 6:20.
Huyo Amrani aliishi miaka mingi kabla ya Yesu, tena ametokana na kizazi cha Lawi mtoto wa watu wa mzee Yakobo.
Mwanzo 29:34Kutoka2:1-10
Ukweli huu hapa,
Ikiwa Mariamu wa Qurani na waislamu baba yake ni Imrani basi atakuwa ameishi miaka 1 500 kabla mama yake Yesu hajazaliwa!
Je, Mariamu mama wa Yesu ametokana na kizazi gani?
Tunaposoma Biblia tunaona kwamba Yesu anaitwa mwana wa Daudi,Mathayo1:1Marko 10:47 na Luka 1:27,32, ndiyo maana pia Yesu anaitwa Simba wa Yuda Ufunuo 5:5. Hivyo basi ukoo aliyetoka Yusufu na Mariamu wa Yesu ni mmoja.
3. Maana ya ISA ni nini?
Ni jambo la kawaida sana jina au majina kuwa na maan. Mfano majina haya y kiarabu yana maana hizi: Muhammad, linamaanisha mwenye kushukuriwa, Abdalla ni Mtumwa wa Allah; Abu-Bakar maana yake ni Baba wa bikira; Abu Huraira ni baba wa Mapaka. Aidha majina ya Kiebrania nayo pie yana maana. Malaki ni mtumishi au Mjumbe wa Yehova, Isaya ni Wokovu wa Yehova; Ezekiel inamaanisha Mungu hutia nguvu, Daniel – Mungu ni hakimu wangu.
Jina Isa maana yake ni hii
Katika Qurani yenye jumla ya juzuu 30; Surah 114; aya 6236; maneno yenye kutamkia 76,440; herufi 322,373; jina Isa linatamkwa lisa au Aysi limetajwa mara 25. Isa pia ameitwa masihi mara 93. Lakini tunaposoma Qurani iliofarsiriwa na Imam Baidawi vol 1ukurasa 160 ameeleza kuwa Isa jina la Kiarabu maana yake ni Wekundu unaozidiana na weupe.
4. Maana ya jina Yesu
JINA Yesu lintokana na lugha ya Kiebrania ‘Yehoshua’ katika lugha ya Kigiriki wanasema ‘lesous’ inatamka ‘Yesous’ yaani Yesu. Katika lugha ya Kiarabu wanasema ‘Yasu’, kwa kiingereza ni “Jesus” maana yake ‘Bwana anaokoa au Bwana ni Mwokozi’ Isaya 43:6, 10-11. Katika Biblia ambayo in jumla ya Sura 1189; aya 31,102; vitabu 66 – Agano la kale vitabu 39 na agano Jipya vitabu 27; neon Mwokozi kiiengereza wanasema ‘Saviour’ limetajwa mara 55. Ikumbukwe kwamba katika agano jiypa jina Yesu au Yehoshua (kwa kiebrania) limetajwa mara 1275 katika aya zipatazo 1226. Zingatia pia kuwa agano jipya lina jumla ya aya 7930 na sura 260 hivyo hapa tunaona jina Yesu maana yake ni Mwokozi na jina Isa ni wekundu uliozidiana na weupe. Kwa kuwa maana ya haya majina tofauti bila shaka Isa sio Bwana Yesu.
Lakini waislamu wanadai yeye ni mtu tu wa kawaida na mtume wa Allah kama Qur’ani,
Surat Al-Maidah 5:75 “ Masih bin Maryam si chochote ila ni mtume tu……”
5. Je, kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni sawa na Isa?
a) Taarfa za Malaika kabla ya kuzaliwa kwao, kadiri ya Qurani na Biblia.
Jibrili alivyomtokea Mama wa Isa Gabrieli alivyomtokea mama wa Yesu
Qurani yasema: Alienda kwa Mariamu aliyekuwa msikitini, Qr.19 au surat Maryam 16-17
Mimba ya Isa ilikuwa ya siku moja peke yake
Qr. 19 Surat Maryam 21-22
“(Malaika) akasema: “ Nikama hivyo (unavyosema; lakini) Mola wako amesema ‘Haya ni sahali Kwangu, na ili Tumfanye muujiza kwa wanaasamu na rehema itokayo Kwetu (ndiyo Tumefanya hivi);’ Na hili ni jambo lililokwisha kuhukumiwa.” Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali
Biblia inasema: Alienda kwa Mariamu aliyekuwa nyumbani kwake, Luka 1:26-28
Qurani yasema:
Mariamu mama wa Isa haijulikani aliishi kijiji kipi wala mji gani wala hata nchi haijulikani. Isitoshe Qurani inasema kuwa Jibril ndiye aliyemletea mtume Muhammad asiwapelekee Mayahudi (hana kosa) Qr. 2 au Surat Al- Baqara 97
Biblia inasema:
Mariamu mama yake Yesu alitokewa na malaika Gabriel akiwa katika kijiji cha Nazareti mji wa Galilaya nchi ya Israeli Luka 1:26Mariamu mama wa Yesu ni Myahudi.
Qurani yasema:
Jibrili hakutoa salamu kwa Mariamu mama wa Isa ila alijizihirisha kwake kama binadamu aliye kamili, Quran 19 au Surat Maryam 17
Biblia inasema: Malaika Gabrieli alimsalimia Mariamu Mama wa Yesu. Luka 1:28
Qurani yasema: Jibril alimwambia Mariamu, mimi ni mjumbe wa mola wako ili nikupe mwana mtakatifu, Qr19-19
Biblia inasema: Malaika Gabrieli alimwambia mama wa Yesu kuwa utachukua mimba. Luka1: 31
Qurani yasema: Jibrili alisema kwa Mariamu kuwa ili tumfanye mtoto ishara kwa wanadamu, Qr. 19: 21.
Isitoshe Jibrili hakutaja jina la mwana kwa Mariamu!!!! Bali alisema ili nikupe mwana mtakatifu.
Biblia inasema: Malaika Gabrieli alisema kwa Mariamu mama ya Yesu kuwa mtoto jina lake utamwita Yesu. Luka 1:312:21Gabrieli hakusema kuwa atampa mwana Mariamu. Bali alisema, Roho mtakatifu atakujilia juu yako, yaani mtoto atazaliwa kwa uwezo wa Mungu.
b) Tofauti ya kuzaliwa Isa na Yesu ni hii
- Isa alizaliwa katika shina la mtemde, Qr, 19:23
- Yesu kazaliwa katika hori la kulishia ng’ombe. Luka 2:7
- Kuzaliwa kwa Isa haijulikani mimba ya mama yake ilichukua muda gani maana malaika Jibrili alisema nikupe mwana mtakatifu mara akachukua mimba na kuzaa. 19: 22-23
-  Isa alipozaliwa sauti ya faraja ilitoka chini ya ardhi.
Suratul Maryam 19:23-24
Kisha uchungu ukampeleka katika shina la mtende, (akawa anazaa na huku) anasema: “ Laiti ningekufa kabla ya haya, na ningekuwa niliyesahaulika kabisa.” Mara ikamfikia sauti kutoka chini yake (inamwambia): usihuzunike. Hakika Mola wako amejaalia (ameweka) kijito cha maji chini yako;
Mafundisho ya Kiislamu yanaeleza kuwa huko chini ya ardhi kuna mnyama. Na huyo mnyama anazijua aya za Qur’an.
Lakini alipozaliwa Yesu Kristo sauti za malaika zilitoka juu
Luka 2:13-16
“Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. Ikawa malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika alilotujulisha Bwana. Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini”
- Lakini Mariamu mama wa Yesu siku zake za kuzaa zilitimia. Luka 2:6-7
- Qurani haionyeshi kama Isa alitabiriwa na manabii kuwa atazaliwa
- Lakini Biblia inatuthibitishia kuwa manabii walitabiri kuzaliwa kwa Yesu,  Isaya 7:14; 9:6 utabili huu ulitolewa na Nabii Isaya miaka 750 kabla ya Yesu kuja kuzaliwa na hatimaye ulitimia. Mathayo 1:18-2

- Isa haijulikani alizaliwa katika kijiji gani wala mji, wala nchi aliyozaliwa Qurani haikueleza. Biblia inatujulisha kuwa Yesu alizaliwa Bethelehemu ya Uyahudi katika Mji wa Daudi umbali wa maili 5 toka kusini mwa Yerusalemu nchi ya Israeli Luka 2:8-16. Kuzaliwa kwake mahali hapo pia ni kutimiza unabii uliotolewa na nabii Mika miaka 750-686 kabla ya kristo kuja wakati wa wafalme hawa wakitawala  na ilitabiriwa katika miaka yakutawala kwa hawa wafalme, Jotham, Ahaz na Hezekia wafalme wa Yuda. Yesu mwenyewe alizaliwa kama mwaka wa 4 wakati wa Mfalme Herode. Isa aliongea na watu akiwa mototo mchanga, na kusema kuwa yeye ni mja wa Mungu amepewa kitabu na amefanywa Nabii. Qr. 19:30-33
- Yesu hakuongea na mtu akiwa mototo mchanga. Alianza kuwauliza maswali na kutoa majibu akiwa na wazee Hekaluni akiwa na miaka 12. Luka 2: 42-49
Hivyo tunaona kwamba tuna tofauti nyingi tu kati ya Bwana Yesu na Isa. Swali kwako mfuatiliaji.
Hapa ambapo tumefikia tukiyachambua maandiko ya vitabu hivi viwili tofauti, Je, Isa bin Maryam ndiye Bwana Yesu Mwokozi?
Tafakari.
c) Je, bado tu Isa bin Mariamu ni mwana wa Mungu?
Kama kuna jambo ambalo Allah Mungu anayeabudiwa na waislamu analitataa sana kupitia Qurani basi jambo hilo si linguine bali ni uwana wa Mungu. Allah ansema hivi.
Qr, 6:101,
Yeye ndiye mwumba wa mbingu na ardhi, inamkinikaje awe na mwana, hali hana mke? Naye ndiye aliye umba kila kitu (sio baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu.
Quran 9:30,
Na mayahudi wanasema ‘uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu’ na ‘wakristo wanasema Masihi ni mwana wa Mwenyezi Mungu’ haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasina kuyapima).Wanayaiga maneno ya wale walilkufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa?
Hili ni agizo la kutisha kwamba Wakristo na Wayahudi tuangamizwe kwa kuwa tunaamini Mungu ana Mwana, au wana, lakini Wakristo tunaoamini hivyo kwa sababu Mungu wetu:
- Yehova alifundisha kuhusu Bwana Yesu hivi:
Kutoka 4:22…Israeli ni mwanangu mimi……
Mathayo 17:5……Huyu ni mwanangu mpendwa wangu….
- Malaika wa Mungu alisem hivi.
Luka 1:30-31, 35,
Malaika akamwambia usiogope Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama utachukua mimba na kuzaa motto mwanamume; na jina lake utmwita Yesu. Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kuvuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu Mwana wa Mungu.
 
             WAKRISTO WA KWELI, YESU KRISTO WETU SIYE YULE ISA WA WAISLAM
 
1) Unabii huu umetimia kwa Yesu Kristo.Tunasoma hayo
Katika Waebrania 7:14
“Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lolote juu yake katika mambo ya ukuhani”
Lakini tusomapo habari za Isa, yeye mama yake anatoka ukoo wa Imrani. Ambaye ni baba yao Haruni, Miriamu na Musa.
Tunayasoma hayo katika Surat Al-Maryam 19:28 “Ewe dada yake Haruni.Baba yako hakuwa mtu mbaya. Wala mama yako hakuwa hasharati”.
Ufafanuzi huu unaofafanua surah hii ya Maryam 19:28 uliyomo ndani ya Qur’an, tafsiri ya King Fahd uk. 405, unasomeka hivi kwa Qurani aliyoitafsiri kwa lugha ya kiingereza:
“This Harun (Aaron) is not the brother of Musa (Moses), but he was another pious man at the time of Maryam (Mary)”
Mimi MWAMBA nikijaribu kutafsiri kwa lugha ya Kiswahili naamini itasimama hivi:
“Huyu Harun siyo ndugu yake Musa, bali alikuwa ni mtu mwingine tu mcha Mungu, aliyeishi wakati wa kipindi cha Maryam”
Kulingana na Biblia, Haruni ni mtoto wa mzee Amran na mama yao anaitwa Yekobedi na kwao wamezaliwa watoto watatu Haruni, Miriam na mdogo wao Musa. Tunasoma haya katika kitabu cha Hesabu 26:59.
b) Tofauti nyingine ni kuumbwa kwao:
  ISA BIN MARYAM KAUMBWA
Qr. 3 au surat Imran 59
 “Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam; alimwumba kwa udongo kisha akamwambia: “Kuwa”; basi akawa”
YESU, YEYE HAKUUMBWA BALI NI NENO LA MUNGU
Yoh 1:1,14,
“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu……..Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu…….”
Mika 5:2
“Bali wewe, Bethlehem Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israel; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele”
Yoh: 8:58  “Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahim asijakuwako, mimi niko”.
Zaidi ya hayo Biblia inatujulisha kuwa yeye ndiye Muumbaji mwenyewe
Yoh 1:3 “Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika”
Kol 1:16-17
“Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake”
c) Baada ya kuishi na kufa kwa Isa bin Maryam wa waislamu, inadaiwa na uislam kama hajawahi kumtokea kimaono yeyote yule!
 1. Baada ya panda mbinguni Yesu Kristo aliwatokea wengi na hasa Sauli kabla awe Paulo.
Matendo 9:4
“Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Saul, Saul, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe”
d) Isa bin Maryam wao alitabiri kwamba baada yake atakuja nabii Muhammad
 Qr. 61 au Surat As-Saff 6
“Na (wakumbushe) aliposema (Nabii) Isa bin Maryamu (kuwaambia mayahudi) enyi wana wa Israili! Mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu. Nisadikishaye yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati. Na kutoa habari njema ya mtume atakayewajia nyuma yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad (Muhammad). Na maana ya majina mawili yote haya ni moja. Maana yake Mwenye kushukuriwa kwa maneno yake mazuri na vitendo vyake vizuri na kila chake kwani vyake vyote ni vizuri).Lakini alipowajia kwa hoja zilizowazi walisema: “Huu ni udanganyifu uliyo dhahiri”.
e) Yesu Kristo aliahidi msaidizi akamtuma Roho Mtakatifu siku ya pentekoste
Yoh: 14:26
“Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia”
Katka Kiyunani anaitwa “Paracletos” yaani msaidizi au mfariji
Yoh 15:26
“Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia”
Yoh 16:7
“Lakini mimi ninawaambia iliyo kweli; yawafaa nyinyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu nitampeleka kwenu”.
2. JINA LA ISA HALINA NGUVU WALA UWEZO WA KUOKOA BALI NI RANGI MBILI
Katika hadithi Al-Lu’lu’war-Marjani, Juzuu namba 1, Hadithi namba 104 ukurasa 64 “Hadithi ya Ibn Abbas kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema:
“Nilimuona Musa katika usiku wa Al-Isra, niliopelekwa, naye ni mtu mrefu, mwenye nywele za hudhurungi zimejikunjakunja kama mtu wa Shanua. Na nilimuona Isa, naye ni mtu wa wastani wa umbo, unaelekea kwenye wekundu na weupe, ana nywele zilizonyooka……”
Lakini YESU KRISTO: JINA LAKE NI WOKOVU.
 Mdo 4:9-10, 12
 “kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa, jueni nyinyi nyote na watu wote wa Israel ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye nyinyi mlimsulubisha, na Mungu alimfufua katika wafu kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu…Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo”
Baadhi ya aya ndani ya Qur’an zinaeleza kuwa Isa aliwaponya wenye upofu. Ni akina nani hao tutajiwe angalau mmoja? Yesu alimponya vipofu na mmoja wao ni Batromayo.
Aya zingine zinasema Isa a.s alifufua wafu. Ni akina nani hao?  Yesu Kristo alimfufua Lazaro.
Jina tulilopewa ni jina moja tu lenye wokovu la Yesu Kristo. Jina la Isa bin Maryam lisilokuwa hata mbegu moja ya wokovu limehusishwa na jina la Yesu Kristo wetu namna gani?
Mdo 16:31 “Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka wewe pamoja na nyumba yako.”
Naamini wengi wenu hapo wawe ni waislam au siyo tumeshakubaliana na maandiko toka pande zote mbili kwamba ISA BIN MARYAM WAO SI MWANA WA MUNGU kama tulivyopata ushahidi katika Suratul Al An-Am 6:101 “Yeye ndiye Mwumba wa mbingu na ardhi. Inawezekanaje awe na mwana, hali hana mke. Naye ndiye aliye umba kila kitu (sio baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu”.
Qurani Suratul At-Tawba (Kutubu), 9:30 “Na Mayahudi wanasema “Uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu” na “Wakristo wanasema “Masihi ni Mwana wa Mwenyezi Mungu” Haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasi na kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa!
Fundisho la Uwana wa Mungu kama Biblia inavyofundisha, halimo katika mafundisho na itikadi ya dini ya Kiislamu kwa hiyo Isa wao siyo mwana wa Mungu.
 
YESU KRISTO: YEYE NI MWANA WA MUNGU.
 Luka 1:30-31,35
“Malaika akamwambia usiogope Mariamu,kwa maana umepata neema kwa Mungu.Tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Malaika akajibu akamwambia,Roho Mtakatifu atakujilia juu yako,na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu Mwana wa Mungu.
Hivyo Isa siyo Mwana Mungu lakini Yesu ni mwana wa Mungu. Kwa hivyo Yesu siyo Isa.
 
 3) ISSA A.S: YEYE SIYO MUNGU ALIYEFANYIKA MWILI.
Suratul Al- Maidah (meza) 5:72-73
Bila ya shaka wamekufuru wale waliosema, “Mwenyezi Mungu ni Masih (issa) bin Maryam”.(Na hali ya kuwa)Masihi alisema “Enyi wana wa Israel! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wenu. Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahali pake (patakuwa) ni Motoni. Na madhalimu hawatakuwa na wasaidizi (wa kuwasaidia siku ya Kiama) “Kwa hakika wamekufuru wale waliosema mwenyenzi Mungu ni mmoja katika (wale waungu) watatu (yeye ndiye watatu wao ) hali hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja ( tu peke yake) na kama hawataacha hayo wasemayo kwa yakini itawakamata wale wanaoendelea na ukafiri miongoni mwao adhabu iumizayo”.
YESU YEYE NI NENO LA MUNGU LILILOFANYIKA MWILI
Yoh 1 : 1, 14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu……..Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu…….”
4) ISA BIN MARYAM HAJAWAHI KUSULUBIWA WALA KUUWAWA
Qurani Suratul An-Nisaa (Wanawake) 4:157-158
“Na kwa (ajili ya) kusema kwao sisi tumemuua masihi Isa mwana wa Maryamu, mtume wa Mungu. Hali hawakumuua wala hawakumsulubisha bali walibabaishiwa (mtu mwingine wakamdhani nabii Isa.) Na kwa hakika wale waliohitilafiana katika (hakika) hiyo (ya kumuua nabii Isa) wamo katika shaka nalo (jambo hilo kusema kauwawa]. Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo) hili (la kuwa kweli wamemuua nabii isa) isipokuwa wanafuata dhana tu.Na kwa yakini hawakumuua. Bali mwenyenzi Mungu alimnyanyua kwake. Na mwenyenzi Mungu ni mwenye nguvu na mwenye hikima.
 
 YESU KRISTO YEYE ALISULUBIWA JUU YA  MTI
Yohana 19:1831,33
“Wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja,  huku na mmoja huku, na Yesu katikati.Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato (maana sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe, wakaondolewe. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu”.
 
5)  ISSA BIN MARYAM HANA SIFA NA RUHUSA YA KUABUDIWA NA BINADAMU YEYOTE.
Suratul Al-Maidah, 5:116
“Na (kumbukeni) Mwenyezi Mungu atakaposema: “Ewe Isa bin Maryam! Je, wewe uliwaambia watu: ‘Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu?” Aseme (Nabii Isa): “Wewe umetakasika na kuwa na mshirika, hainijuzii mimi kusema ambayo si haki yangu (kuyasema, kwa kuwa ni ya uongo), kama ningalisema bila shaka ungalijua ; unayajua yaliyomo nafsini mwangu, lakini mimi siyajui yaliyomo nafsini mwako; hakika Wewe ndiye ujuaye mambo ya ghaibu.
 
 BALI YESU KRISTO ANASTAHILI KUABUDIWA NA WANADAMU NA MALAIKA
Math 2: 2
 “Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? kwa maana tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumsujudia.”
Yoh 9: 35
“ Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu? Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini? Yesu akamwambia Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. Akasema, naamini, Bwana, akamsujudia.”
Filipi 2:10-11
“ili kwa Jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”
Ebr 1:6
“Hata tena amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu Malaika wote wa Mungu.

6) ISA BIN MARYAM HASTAHILI KUWA MWOMBEZI WA WATU KWA MUNGU
Sahih Al-Bukhari, vol.6, Hadithi no 3, The Noble Qur’an, English Translation ukurasa 8
“Nenda kwa Musa, mtumishi wa Allah ambaye Allah alizungumza naye uso kwa uso na alimpa Torati. Hivyo watakwenda kwake naye atasema ‘ Mimi sistahili kwa jukumu hilo la uombezi, na atataja mauaji aliyoyafanya kwa mtu ambaye si muuaji, na hivyo atajisikia aibu mbele ya Mola wake, naye atasema nendeni kwa Isa, mtumishi wa Allah, Mjumbe wake neno lake na roho iliyotoka kwake. Isa atasema sistahili mimi kubeba jukumu la uombezi”
 
 YESU KRISTO NI MWOMBEZI WA WANADAMU KWA MUNGU
1 Tim 2:5
“Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;”
Waebrania 7:24-25
“Bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu Hai siku zote ili awaombee.
 
 7) ISA BIN MARYAM NI NABII MWINGINE TU ASIYE TOFAUTI NA WENGINE
Suratul Baqarah, (ng’ombe) 2:136
“Semeni nyinyi (Waislamu waambiwe Mayahudi na Manasara; waambieni): “Tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa, na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahimu na Ismail na Is-haqa na Yaaqubu na kizazi (chake Yaaqubu); na waliyopewa Musa na Isa na pia yale waliyopewa Manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao; hatutofautishi baina ya yoyote katika hao. (Wote tunawaamini); na sisi tumenyenyekea Kwake.”
 
 YESU YEYE YUKO JUU KULIKO VITU VYOTE
Efeso 1:20-23
“Aliyotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na malaika, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; akavitia vitu vyote chini ya miguu yake akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya Kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”
8) ISA BIN MARYAM ATAKAPORUDI, ATAOA NA KUZAA WATOTO
Mishkat Al- Masabih, vol 2 uk.1159 na Sahih Muslim, vol. 1 uk 92 wanadai kwamba Isa atakaporudi ataishi miaka arobaini (40), muda ambao atakuwa ameoa na kuzaa watoto, na atafanya ibada ya hija.
 
 BALI YESU KRISTO ATAKAPORUDI ATAKUJA KULINYAKUA KANISA, YAANI BIBI ARUSI
Efeso 5:25-26, 32-33 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa…..
Uf 19:7
“Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana Kondoo imekuja na mkewe amejiweka tayari.akajitoa kwa ajili yake, ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;…..Siri hiyo ni kubwa ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mmewe.”
 
 9) ISA ATAKUFA BAADA YA KUISHI MIAKA AROBAINI
Mishkat Al- Masabih, vol 2 uk. 1159, Sunan Abu Dawud, Hadithi namba 4310,Sahih Muslim, vol.1, uk.92, zadai kwamba “Isa atakaporudi ataondosha dini zote zisiwepo isipokuwa Uislamu. Atamharibu Masih Dajjal, na ataishi duniani miaka arobaini (40) na kisha atakufa. Na baada ya kufa atazikwa pembeni mwa kaburi la Muhammad.”
 
 BALI YESU KRISTO BAADA YA KUFUFUKA YU HAI SIKU ZOTE HAFI TENA
Rum 6:9 “ tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena.”
Ebr 7:24-25
“Bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu Hai siku zote ili awaombee.”
Ufunuo 1:17-18
“ Nami nilipomwona nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, mimi ni wa kwanza na wa mwisho, aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hai hata milele na milele nami ninazo funguo za mauti na za kuzimu.”
 
  10) ISA BIN MARYAM HANA UFAHAMU WA MAMBO MBALIMBALI
Katika Al-Lu’lu’ war- Marjan, kitabu cha 3 Hadithi namba 1528 ukurasa wa 883“Hadithi ya Abu Huraira kutoka kwa Mtume amesema “Issa bin Mariam alimwona mtu anaiba akamuuliza umeiba? akasema hapana Naapa kwa Allah ambaye hakuna mola isipokuwa yeye. Isa akasema nimemuamini Allah na nimeliogopea jicho langu”.
LAKINI YESU ANAYAJUA YOTE
Yohana 1:47-48
“Basi Yesu akamwona Nathanael anakuja kwake, akanena habari zake “Tazama Mwizraeli kweli kweli hamna hila ndani yake. Nathaeli akamwambia umepataje kunitambua? Yesu akajibu akamwambia, Kabla Filipo hajakuita ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona”

Yoh 2:24-25
“Lakini Yesu hakujiaminisha kwao, Kwa kuwa yeye aliwajua wote; na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe aliyajua yaliyomo ndani ya mwanadamu”
 
 11) ISA BIN MARYAM ATAKAPORUDI ATAKUJA KUVUNJA MISALABA NA KUUA NGURUWE
Mkweli Mwaminifu, Juzuu 3-4, uk.20, Hadithi namba 753
“Haisimami saa ya (kiyama) mpaka akuteremkieni nabii Isa  mwana wa Maryamu atahukumu (kwa sheria ya Kiislamu) (na) muadilifu, basi atavunja misalaba (ya Wakristo Makanisani) na ataua nguruwe, na Ataondosha fedheha au (aibu), na mali itazidi kuwa nyingi sana mpaka hataikubali (ataikataa) mtu (kwa kuogopa kiyama)”
Soma pia katika Sahihi Bukhar, vol. 3, Hadithi na 425, na Al-Lu’lu’war-Marjan, juzuu ya 1, Hadithi na 95 uk.51. The Noble Qur’an uk.757

LAKINI YESU KRISTO ATAKAPORUDI ATAWATUMA MALAIKA ZAKE KUWAKUSANYA WATAKATIFU
Mathayo 24:30-31
“Ndipo itakapoonekana ishara ya mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi, naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.”
 
 ONYO LA YESU KRISTO KWAKO.
Math 24:24
Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini hata walio wateule.” (Angalia pia Marko 13:22)
 Yoh 8:24
Kwa hiyo naliwambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; Kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye mtakufa katika dhambi zenu.”
Naamini ndugu muislam au yeyote yule asiyekuwa katika upotevu na upotofu huo kwamba umesaidika, na kama nimekuumiza kwa njia yoyote ile nakuomba radhi maana siyo mimi bali maandiko toka pande zote mbili.
Muislamu baada yakuijuwa kweli nakusihi kwa upendo wake Kristo ukimbie kwa ajili yakuiponya nafsi yako ndani ya Kristo.
Basi tunakushukuru kwa kuweza kusoma haya mafundisho na tahadhari za Maandiko Matakatifu.
Ni ndugu zako katika Kristo Yesu
Fred Nguli MWAMBA & Matthew Daniel Makenzi

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW