Thursday, July 30, 2015

VIOJA VYA UISLAM KUHUSU KIFO NA KUFUFUKA WAKATI WA KIYAMA

1. Eti Binadamu asili yake ni MBEGU YA "Ajabu Dhanab"
2. Eti Siku ya Kiyama Allah atanyeshea Mvua Ajab Dhanad na itafufuka tena.

Ndugu Msomaji, ebu jiunge nami leo na jifunze kuhusu Sayansi dhaif ya Allah na Muhammad.


MTU ANAPOKUFA, ZILE ASILI TATU KILA MOJA INARUDI MAHALA PAKE PA ASILI
Kwa kifo, udongo ambao kwao ndio mwili ulijengeka, unarudi mahala pake pa asili napo ni ardhini.
Mwenyezi Mungu anasema:
"Kwa hakika tunajua kiasi cha kila kinachopunguzwa na ardhi katika miili yao (wakati wanapooza huko makaburini) Na kwetu kiko kitabu kinachohifadhi (kila kitu)".
Qaf -4

AJABU DHANAB- ETI BINADAMU NDIO KATOKEA HAPO
Kinachobaki katika mwili wa mwanadamu ni kitu kidogo kinachoitwa "Ajabu dhanab" (kilichoingia pamoja na mbegu). Hii ni sehemu ambayo ndani yake mtu aliumbiwa, na kitu hiki asili yake kilikuwa katika uti wa mgongo wa Baba yetu Adamu(AS), kwa vile kitu hiki ni kidogo sana (Hakiwezi kuonekana ila kwa kutumia microscope zenye nguvu sana), ndiyo maana uti wa mgongo wa Baba yetu Adamu(AS) uliweza kuzibeba asili hizi zote za wanawe.
Na sehemu hii iitwayo "Ajabu dhanab" haiozi wala haivurugiki.
Mtume(SAW) amesema:-
<<Mwili wote wa mwanaadamu unaoza isipokuwa "Ajabu dhanab", kutokana nayo ameumbwa na kutokana nayo atakusanywa tena >>.
Bukhari – Muslim – An Nasai, Malik katika Muwata a na Abu Daud.

Ama Roho itarudi mahali anapopataka Mwenyezi Mungu (katika Barzakh) mpaka Siku ya Kiama.

SIKU YA KUFUFULIWA ZILE SEHEMU TATU ZINAKUSANYIKA TENA
Unapofika wakati wa kufufuliwa, Mwenyezi Mungu atateremsha mvua na kuifanya ile mbegu isiyooza "AJABU DHANAB”, imee tena.

Mtume (SAW) amesema:-
<<Kisha inateremshwa mvua na watamea kama imeavyo mboga, na hapana katika mwili wa mwanadamu kisicholiwa na ardhi isipokuwa fupa moja nalo ni "Ajabu dhanab" ndani yake humo watakusanywa viumbe Siku ya Kiama>>.
(Bukhari, Muslim, Imam Malik, Abu Daud na AnNasaiy)

Yaliyofanana na haya yanatokea duniani kila siku. Panapotokea ukame, tunaona miti ikianguka na kufa (na kutoweka). Hauonekani mti wowote wala mmea. Lakini Mwenyezi Mungu amejaalia ndani ya ardhi au ndani ya mawe kuwemo mbegu, na mbegu hizo hazionekani kwa macho, isipokuwa mvua inaponyesha ndipo hupasuka na kuchipua miti na mimea mbali mbali.

Mwenyezi Mungu anasema:-
"Hukitoa kilicho hai katika kilichokufa na hukitoa kilicho kufa katika kilicho hai na huihuisha ardhi baada ya kufa kwake na hivyo ndivyo mtakavyofufuliwa".
(Al - Rum - 19).
Mtu mmoja alimuuliza Mtume (SAW):-
"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, namna gani MwenyeziMungu atawarudisha tena viumbe, na nini dalili yake?” 

 Mtume (SAW) akamjibu;
"Uliwahi kupita bondeni kijijini kwenu wakati wa ukame (miti yote ikiwa imekufa), kisha ukapita tena wakati miti (imeota tena na) imejaa na ardhi ikageuka (na kuwa) rangi ya kijani?
Akasema:- "Naam".
Mtume(SAW) akamjibu:
"Basi hiyo ndiyo dalili ya Mwenyezi Mungu katika kuumba kwake na hivyo ndivyo atakavyowafufuwa wafu".
(Imam Ahmad )

(Siku ya Kiama), Pale Ajab dhanab itakapochipua na kutoka ndani ya ardhi na mwili ukarudi tena, ndipo zitakapokuja roho na kuingia kila moja katika mwili wake.
Ndio sababu Mwenyezi Mungu akasema:
"Na nafsi zitakapounganishwa (na viwiliwili vyake)."
(At - Takwiyr - 7)
Na hivi ndivyo watakavyorudi viumbe mara ya pili kama walivyoanzishwa hapo mwanzo.

Mwenyezi Mungu anasema:-
"Kama tulivyoanza umbo la awali tutalirudisha tena, ni ahadi ilio juu yetu, bila shaka sisi ni wenye kufanya (tusemavyo).”
(Al - Anbiyaa -104).

Ndugu msomaji, hivi ni kweli Allah wa hii dini ya Kiislam aliumba? Mbona hii imani imejaa shaka na utata kila kona?

Leo Allah kesha jisahau na kusema kuwa eti wewe umetoka katika Ajabu Dhanab na sio tena vumbi.

UHAKIKA WA UFUFUO WA WAFU KWA WAKRISTO


Ufufuo wa wafu, ni moja kati ya masomo ya msingi sana katika Ukristo na ni mafundisho ya kwanza ambayo kila Mkristo inampasa kuyafahamu ( WAEBRANIA 6:1-2 ). Kiyama ya wafu au Ufufuo wa wafu, umetabiriwa mapema katika Neno la Mungu ( LUKA 14:13-14; YOHANA 5:28-29; WAFILIPI 3:10-11; 1 WATHESALONIKE 4:16 ). Yesu Kristo ndiye kielelezo cha wafu na uhakika wa ufufuo wa wafu kwa watu wote ( 1WAKORINTHO 15:21, 20-23). Yesu Kristo alitabiri mapema juu ya kufufuka kwake kabla hata hajafa (MATHAYO 16:21; 17:22-23; 20:17-19; MARKO 8:31-32; 10:32-34; LUKA 9:20-22; 18:31-34). 

Yesu Kristo huyuhuyu alitabiri juu ya kufufuka kwake na ikawa hivyo, ndiye pia aliyetabiri juu ya ufufuo wa watu wote ( YOHANA 5:25-29 ). Ni muhimu kufahamu kwamba walikuwepo watu wenye mashaka, ambao hawakuamini kwamba Yesu angefufuka kama alivyosema ( LUKA 18:31-34 );lakini kutokuamini kwao hakukuzuia kufufuka kwa Yesu. Vivyo hivyo leo, pamoja na kuwapo watu wasioamini kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, kutokuaminii kwao hakutaweza kuzuia jambo hilo kutokea ( WARUMI 3:3-4 ). Uongo wa askari Walinzi wa kaburi la Yesu, waliutawanya baada ya kupokea rushwa na kufundishwa kusema uongo, kwa kuabiwa “ semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala “, ni uongo ulio dhahiri ( MATHAYO 28:11-15 ). Ikiwa walinzi walikuwa wamelala usingizi, waliwaona namna gani watu waliokuja kuuiba mwili wa Yesu na kufahamu kwa hakika ni wanafunzi wake? Na kama waliwaona kwa nini waliwaacha wakauiba mwili huo na wasiwazuie kufanya hivyo? Ni uongo ulio wazi. Ni jambo lililo dhahiri kwamba Yesu alifufuka! Kwa jinsi hiyohiyo, ufufuo wa wafu wote ni jambo lililo dhahiri kabisa kutokea.

Max Shimba Ministries Org.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW