Monday, August 3, 2015

ALLAH ANA-VAA NGUO KAMA VIUMBE

1. Kumbe Allah ana mwili kama viumbe!
2. Kumbe Allah anavaa nguo kama viumbe!
3. Kumbe Allah anao mfano, maana anavaa nguo kama viumbe!
Ndugu znguni,
Huu ni Msiba mwingine kwa Allah. Huyu Allah aliyesema kuwa hana mfano wala hawezi kufananishwa, leo hii kaja na mpya na kujisahau na kukiri kuwa, anavaa nguo kama viumbe.
Haya, twende moja kwa moja na tusome ushahid kutoka vitabu vya Waislam.
الكبرياء ردائي والعظمة إزاري
Allah ansema katika Hadithi hii Qudsi "Ukuu ndi vazi langu la juu na utukufu ndio vazi langu la chini".
Sasa kama Allah anavaa nguo inamana kuwa Allah ana mwili kama viumbe?
Msiba huu ni mkubwa sana ndugu wasomaji.
Katika Hadithi nyengine Qudsi, Allah anasema: "….Na mja wangu hajikurubishi kwangu kwa kitu nikipendacho zaidi kuliko yale niliomfaradhishia juu yake. Na mja huwa anaendelea kujikurubisha kwangu kwa nawafil (ibada zisizo za lazima) mpaka nampenda: "فإذا أحببته كنت سمعه الذي يسمع به، وبصره الذي يبصر به ويده التي يبطش بها ورجله) (التي يمشي بها" Basi nikimpenda nakuwa (Mimi ndio) sikio lake analosikia kwalo, na jicho lake analoonea na mkono wake anaoshikia na mguu wake anaoendea."
Hapo Allah kesha kiri kuwa yeye ana masikio, mikono na macho.
Ndugu wasomaji, teyari mmesha uelewa kuwa Allah ni kiumbe kama binadamu kwasabau ana vaa nguo.
Mungu awabariki sana.
Katika Huduma yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

ALLAH ANA MIKONO KAMA VIUMBE

Ndugu msomaji,
Tunaendelea na mada kuhusu Allah ambaye ni kiumbe kama sisi. Leo ninawaletea ushahidi kuwa, Allah ana MIKONO kama binadamu. Haya ungana nami na tuanze kusoma ushahid kutoka vitabu vya Kiislam.
وَمَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ {67}
“Na hawakumheshimu Mwenyezi Mungu heshima ipasayo, na siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kulia, …” (Az-Zumar; 39: 67)
“Mikono” Ya Mwenyezi Mungu Kama Ilivyosimuliwa Na Madhehebu Ya Makhalifa.
Wanazuoni wa madhehebu hiyo hapo juu wamesimulia ndani ya vitabu vyao kutoka kwa Abu Huraira ambaye amesimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama ifuatavyo:
“Adamu na Musa walikuwa na mazungumzo yafuatayo: Musa alisema: ‘Ewe Adamu! Mwenyezi Mungu alikuumba kwa mikono Yake Mwenyewe… Lakini uliwateremsha wanadamu kutoka kwenye bustani kwa sababu ya dhambi yako.’
Adamu akajibu: ‘Ewe Musa, Mwenyezi Mungu kwa hakika amekutukuza wewe, na akaandika Taurati kwa ajili yako kwa mikono Yake Mwenyewe.’”
Katika hadithi nyingine iliyosimuliwa kutoka kwa Abu Huraira, tunakuta:
“Mwenyezi Mungu huwa anashuka mpaka kwenye mbingu ya kwanza, na ananyoosha mikono Yake miwili na anasema…”
Halafu anaendelea kunukuu Ayah zifuatazo kwa ithibati ya madai yake:
وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنْفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ {64}
“Na Wayahudi walisema: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba. Mikono yao ndio iliyofumba, na wamelaaniwa kwa sababuya yale waliyoyasema. Lakini mikono ya Mwenyezi Mungu iwazi, hutoa apen- davyo …” (Al-Maida; 5: 64)
فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ {83}
“Basi ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo ufalme wa kila kitu, na kwake mtarejea.” (Yaasin; 36: 83)
قُلِ اللَّهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَنْ تَشَاءُ وَتَنْزِعُ الْمُلْكَ مِمَّنْ تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَنْ تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَنْ تَشَاءُ ۖ بِيَدِكَ الْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ {26}
“Sema: Ewe Mola Mwenye kumiliki ufalme, humpa ufalme umtakaye, na humnyang’anya ufalme umtakaye. Na humtukuza yule umtakaye na kumdhalilisha umtakaye. Kheri yote imo mikononi mwako. Hakika wewe ni Mweza juu ya kila kitu.” (Aali Imraan; 3: 26)
Muhammad bin Muslim alimuuliza Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) kuhusu Ayah ifuatayo:2
قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَنْ تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ ۖ {75}
“Akasema: Ewe Iblis, ni nini kimekuzuia kumtii yule niliyemuumba kwa mikono yangu?... (Swaad; 38: 75)
Swali ningependa kuwauliza Waislam, hivi kwanini mnasema kuwa Allah hana mfano wakati teyari Allah anajidhihirisha kuwa ana MIKONO? Je, Mikono so mfano wa binadamu? Kwanini mnamzulia Allh uongo kuwa hana Mikono?

Mikono

Tunaamini kuwa Allaah Anayo mikono miwili mitukufu.
Anasema:
بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاء
"Bali mikono yake (miwili - yadaahu) iwazi. Hutoa Apendavyo."
Al-Maaidah – 64
Na Akasema:
وَمَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالأرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّماوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَى عَمَّا يُشْرِكُونَ
"Na wala hawakumhishimu Allaah kama Anavyostahiki kadiri Yake. Na Siku ya Qiyaamah ardhi yote itakuwa mkononi Mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono Wake wa kuume. Subhaanahu wa Ta’ala Ametakasika na Ametukuka na hayo wanayomshirikisha nayo."
Az-Zumar – 67
(Siku ya Ridhwaan Waislamu walipofungamana na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) chini ya mti kwa kumpa mkono wote kwa pamoja, mmoja baada ya mwengine, na Allaah Akateremsha kauli Yake:
إِنَّ الَّذِينَ يُبَايِعُونَكَ إِنَّمَا يُبَايِعُونَ اللَّهَ يَدُ اللَّهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ
"Bila Shaka wale wanaofungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Allaah. Mkono wa Allaah uko juu ya mikono yao."
Al-Fat-h – 10
Ieleweke kuwa Allaah Anaposema Anayo mikono au macho, ina maana kuwa mikono Yake ni sawa na mikono yetu, au macho Yake ni sawa na macho yetu - AstaghfiruLlaah. Meza inayo miguu na viti vina miguu, lakini miguu ya viti na ya meza ni tofauti na miguu ya mwanaadamu aloitengeneza meza ile, kwani sifa ya mtengenezaji lazima iwe tofauti na sifa ya kilichotengenezwa, ama sivyo mtengenezaji na kilichotengenezwa watakuwa kitu kimoja. Na Allaah Ndiye mwenye kupigiwa mifano bora, sifa Zake Subhaanahu wa Ta’ala haziwezi kufananishwa na sifa zetu. Lakini wakati huo huo lazima tukikubali kila Alichojinasibisha nacho Subhaanahu wa Ta’ala.)

Macho

Na tunaamini kuwa Allaah Anayo macho mawili kikweli, na hii inatokana na kauli Yake Subhaanahu wa Ta’ala Aliposema kumwambia Nuuh (‘Alayhis-Salaam):
وَاصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا
"Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu."
Huud – 37
Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
"Pazia yake ni nuru, na lau kama Ataiondoa basi nuru ya Wajihi Wake ingeunguza kila kilichokifikia."
Na alipokuwa akihadithia juu ya Ad-Dajjaal alisema:
"Dajjaal ana chongo na Mola wenu Hana chongo."
Na tunaamini kuwa macho yetu hayamfikii kumuona Allaah.
Allaah Anasema: 
لاَّ تُدْرِكُهُ الأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الأَبْصَارَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ
"Macho hayamfikilii, bali Yeye anayafikilia macho. Naye ni Mjuzi, Mwenye khabari."
Al-An’aam – 103
Ndugu wasomaji, teyari mmesha elewa kuwa Allah ni kiumbe kama binadamu kwasabau ana Mikono.
Mungu awabariki sana.
Katika Huduma yake,
Max Shimba
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

ALLAH ANAKIRI KUWA YEYE ANA USO KAMA VIUMBE

Ndugu zanguni,
Natangulia kwa kusema huu ni Msiba Mkubwa sana kwa ndugu zetu kwa kupitia Adam wanao pinga kuwa Allah hana mfano.
Leo nitawawekea mifano kadhaa kama ushahid kuwa Allah ni kiumbe.
Haya, ungana nami moja kwa moja na tujifunze kuhusu huyu Allah kiumbe.
1) Allah anasema: "Popote mutapogeukia kuna USO wa Mwenyezi Mungu". Sura 2, Aya 115.
Kwenye hiyo aya hapo juu, Allah amesha wajibu wanao bisha kuwa Allah hana USO. Je, kuwa na USO si sifa ya binadamu?
2) Allah anasema: "كل شيء هالك إلا وجهه" (Kila kitu kitaangamia isipokuwa USO wake (Allah)." Sura 28 Aya 88.
Ndugu zanguni, Allah anaendelea kukiri kuwa yeye ana USO kama viumbe.
Endelea kusoma:

ALLAH ANAKIRI KUWA USO WAKE UNA MACHO"Wakati mmoja MACHO ya Allah yalikuwa yanauma, na Malaika walikwenda kumuona, na kwamba Allah alitokwa na Machozi, kwa ajili ya Mafuriko ya Nabii Nuhu mpaka macho yake yakawa mekundu. (Al Milal Wannihal J. 1 uk. 141)
Nafahamu Waislam watakana kuwa hiyo hadith ni dhaif na haipo kwenye Quran. Hebu tuendelee kusoma ushahid mwingine kuwa Allah anamacho mawili na kaandikwa Kafir kati ya macho yake.
Hadithi ya Anas (r.a) amesema, Mtume (s.a.w) amesema, "Hakuna Mtume aliyetumwa, isipokuwa amewahadharisha watu wake na mwenye Jicho moja mrongo. Eleweni kuwa yeye ana jicho moja na hakika Bwana wenu hana Jicho moja kati ya Macho yake pameandikwa neno 'KAFIRI." (Bukhari, Hadithi Na. 245, Juzuu ya 9).

ALLAH ANAKIRI KUWA ANAMASIKIO NA MACHOSurat An Nisaai 58. Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika haya anayo kuwaidhini Mwenyezi Mungu ni mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye KUSIKIA, Mwenye KUONA. ***
Waislam nafahamu huu kwenu ni Mwiba katika nyoyo zenu.

Ndugu wasomaji, teyari mmesha uelewa kuwa Allah ni kiumbe kama binadamu na ana USO wenye MACHO NA MASIKIO.

Mungu awabariki sana.
Katika Huduma yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

ALLAH SIO MUNGU (SEHEMU YA KWANZA)

Kwanza Qruani inajua kabisa kwamba mungu wake si mungu aliyeumba Mbingu na Nchi! Kwasababu hii ndiyo maana hakuna aya hata moja ndani ya Qruani ambayo mungu wa Qruan anasema kwamba “Mimi ndiye niliyeziumba Mbingu na Nchi” bali utakutana na aya ikisema “Mwenyezi Mungu aliziumba mbingu na nchi”

SASA, kama Allah ni Mungu, kwanini anasema kuwa Mwenyezi Mungu kaumba mbingu na Nchi na HASEMA Mimi nimeumba Mbingu na Nchi?

Pia ujulikane kwamba kila kitu hutambulika kwa majina yake. Hata wanadamu hutambulika kwa majina ndipo mtu utapata kuelewa kwamba anayekusudiwa ni fulani. Mungu wa Biblia anaitwa Niko ambaye Niko, Yehova, Bwana wa Majeshi, Alfa na Omega. Lakini mungu wa Qruani jina lake ni Allah, sasa hoja inakuja hapa, KAMA mungu wa waislam na Mungu wa Wakristo ni mmoja:

1. Ni andiko gani katika Biblia linalosema kwamba Mungu jina lake ni Allah?
2. Pia ni aya gani ndani ya Qruani inayokubali kwamba Mungu jina lake ni Yehova?
Lakini katika kufanya utafiti nimegundua kwamba Allah si Mungu wa kweli bali ni Shetani kwamujibu wa Qruani Surat Muhamad aya ya 15. Inasema hivi “Mfano wa pepo aliyowaandalia waja wake mwenyezi Mungu iko hivi, ndani yake kuna mito ya maziwa na mito ya ulevi wenye ladha kwa wanywaji. Humo watapata kuburudishwa kwa matunda ya kila namna na samahani kutoka kwa mola wao.” Lakini ukisoma Qruani hiyo hiyo Sura ya 5 aya ya 90, inasema hivi: “Enyi mlioamini bila shaka ulevi na kamari na kuombwa yeyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni uchafu na ni kazi ya shetani.”

Sasa rafiki yangu kwa mujbu wa aya hizi hebu fikiria sasa aya ya kwanza imesema Allah katika pepo yake kuna mito ya ulevi, lakini Qruani hiyo hiyo imesema ulevi ni kazi ya shetani, kama aya zenyewe ndizo hizi hoja yangu inakuja hapa: Yeye Allah kama siye Shetani amepata wapi ulevi hali yakuwa ulevi ni wa shetani? lakini Biblia imesemaje kuhusu ulevi: Walevi na wachawi na wazinzi hawataurithi ufalme wa mbinguni. Mungu anasema katika isaya Ole wao waamkao asubuhi na kufuata ulevi. mpendwa kuwa macho hizi ni nyakati mbaya za Mpinga Kristo.

Leo tumejifunza tena kuwa, Allah sio Mungu bali ni Mpinga Mungu.

Hakika Allah aabudiwe na Waislam sio Mungu.
Katika Hudma yake
Max Shimba Ministries
@July 2015.

NI NANI ALIYECHOMA KURAN? NI NANI ANAYEENDELEZA UCHOMAJI WA KURAN?

**********************************************************
Sasa inefahamika kuwa aliyekuwa wa kwanza kuchoma kitabu cha “haki, kikamilifu na kisichokuwa na dosari” kiitwaacho “KURAN TAKATIFU” ni yule yule aliyeandika kuran.
Caliph Uthman aliandika Quran na kuchoma aya ambazo hakupendezwa nazo! 
(Sahih Bukhari 6:61:510)
CALIPH UTHMAN ALIANDIKA QURAN NA KUCHOMA AYA AMBAZO HAKUPENDEZWA NAZO!-(Sahih Bukhari 6:61:510)
Caliph Uthman hakuchoma tu aya za kuran bali aya zingine alizifuta kwa maksudi. (Bukhari 6:61:527).
HAPA MASWALI NYETI YANAIBUKA;
**************************
Je, ni aya gani hizo alizozichoma?
Je, aliakuwa anaandika kuran kwa manufaa ya nani?
Je, aliandika kuran kwa mamlaka ya nani?
Je, mwenye mamlaka hayo hakumwongoza aandike kurani mufti bila dosari kama wanavyodai waumini wa kiislamu kuwa kuran haina dosari?
SWALI:-KWANINI BASI WAISLAMU WALALAMIKE KUWA KURAN YAO INACHOMWA?
JIBU:-WAO NDIO WALIOANZISHA UCHOMAJI NA HADI SASA HAO NDIO WANAOENDELEZA UCHOMAJI WA KURAN.

JE, MBINGU YA YEHOVA NI SAWA NA PEPO YA ALLAH?

MBINGU YA YEHOVA:
Luka 20:34-36
Yesu akawaambia wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa, lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule. Na kule kufufuka katika wafu hawaoi wala hawaolewi. wala hawawezi kufa tena. Kwa sababu huwa sawa sawa na malaika, nao ni wana wa Mungu kwa vile walivyo wana wa ufufuo.

Maandiko haya yanatuthimbitishia Wakristo kuwa tutakapofufuliwa na kuingia mbinguni, hakuna mambo ya kuolewa wala kuoa, maana tutakuwa na miili ya kiroho (1 Korintho 15:43-54) Aidha maandiko yanatufundisha kuwa ufalme wa Mungu siyo kula wala kunywa bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. (Tazama Warumi 14:17). Mungu wetu anafundisha wazi wazi kuwa kule mbinguni katika ufalme hakuna njaa, wala kiu wala jua kutupiga (Ufunuo 7:16-17.)

PEPO AU MBINGU YA ALLAH ITAKUWA HIVI:
i). Maghorofa
Qurani 39:20 Suratul Zumar (makundi/vikosi)
Lakini waliomcha mola wao watapata ghorofa zilizojengwa juu ya ghorofa chini (mbele) yake hupita mito. Ndiyo ahadi ya Mwenyenzi Mungu, Mwenyenzi Mungu havunji ahadi yake.
ii) mito ya maji, maziwa, ulevi, asali na matunda
Qurani 47:15 Suratul Muhammad
Mfano wa pepo waliyoahidiwa watawa (wacha Mungu itakuwa hivi). Imo mito ya maji yasiyovunda, na mito ya ulevi wenye ladha kwa wanywao na mito ya asali iliyosafishwa. Tena humo watapata matunda ya kila namna, na samahani kutoka kwa mola wao. Basi hao watakuwa sawa na wale wataokaa motoni na kunyweshwa maji yachemkayo yatakayokata chango zao?.
Je Matunda hayo ni sawa na ya wapi?
Qurani 2:25 Suratul Al- Baqarah (ngombe jike)
Na wabashirie walioamini na kufanya vitendo vizuri, kwamba watapata mabustani yapitayo mito mbele yake. Kila mara watakapopewa matunda humo kuwa ni chakula watasema “haya ndiyo yale tuliyopewa zamani (ulimwenguni) kwani wataletewa (matunda hayo) hali yatakuwa yamefanana (na yale waliyokuwa wakiyajuwa ulimwenguni wataletewa kwa sura hiyo lakini utamu mwingine kabisa) na humo watapata wake waliotakasika (na kila mabaya na machafu) na watakaa milele humo.
iii). Watapata wanawake aina hizi na nyama za ndege
Qurani 56:15-23 Suratul Al Waaqiah (Tukio) nanukuu aya ya 21-23 tu
Na nyama za ndege kama watakavyotamani (wenyewe). Na wanawake wenye macho mazuri na makubwa (ya vikombe). (wanapendeza na safi) kana kwamba ni lulu zilizofichwa (katika machaza yake, ndio kwanza zinapasuliwa)
Qurani 37:48-49 Suratul As-Saaffat (Wapangao mistari)
Na pamoja nao watakuwa wanawake wenye macho mazuri makubwa. (Safi) wanawake hao kama mayai (ya mbuni) yaliyohifadhiwa.
Qurani 37:44-46 Suratul As-Saaffat (Wapangao mistari)
Wako juu ya vitanda (viti vya enzi vya fahari), wamekabiliana (wanazungumza). Wanazungushiwa gilasi zenye (vinywaji) safi.Vyeupe yenye ladha kwa hao wavinywao.
Kupitia aya hizi tumeona kuwa Allah Sub-haana Wataala Mungu anayeabudiwa na Waislamu ametoa ahadi ya kuwaingiza Waislamu peponi (mbingu) na kuwa watapata mito ya maji, mito ya maziwa na ulevi na pia mito ya asali vilevile watapata matunda, nyama ya ndege na pia wataozeshwa na Allah mungu wao wanawake wenye macho makubwa kama mayai ya mbuni. na wengine makubwa kama vikombe.
Jambo la kushangaza zaidi ni pale tunaposoma kitabu cha Hadithi, maana imani ya Dini ya Uislamu imejengwa pia katika vitabu vya hadithi. Soma
Qurani 42:10 Suratul Ash-Shuura (mashauriano)
Mkihitalifiana katika jambo lolote (rejeeni kitabu cha Mwenyenzi Mungu na Hadithi za mtume kwani)…
Tunaposoma kitabu cha Hadithi ya mtume kiitwacho Sunnan Ibn-1- Majah vol 5 ukurasa wa 546 Hadithi No: 4337 kuna maelezo haya

Im simuliwa na Abu' Umama ya kuwa mjumbe wa Allah (baraka na amani ya Allah iwe juu yake) alisema Allah hatamruhusu yeyote kuingia peponi ila kwa idhini ya Allah, Mwenye nguvu na utukufu naye atamwozesha mwanamume wake sabini na mbili. Wawili watakuwa mabikira (mahurul-ain) yaani wanawake wa peponi wenye macho makubwa, na sabini watakao warithi ambao watu (mabwana zao) wametupwa katika moto wa jahanamu kila mmoja wao (hao wanawake) wana uke wa kupendeza. Na mwanamume, Nguvu ya uume wake katika kujamiana hautapinda (kusinyaa) bali utadumu sana
Kwa kiingereza Hadithi hii inasomeka hivi:-

Abu-Umama (Allah be pleased with him) reported that Allah's messenger (peace and blessings of Allah be upon him)said Allah will not admit anyone in the paradise but Allah the mighty and Glorous, will marry him with seventy two wives two will from virgins (haurine) with big eyes and seventy will be his inheritance from the people of the Hell- Fire (1).Everyone of them will have apleasant vagina and he (the man) have sexual organ that does not bend down (during sexual intercouse)

Hivi ndivyo Allah Mungu wa Waislamu alivyoahidi. Hili ni jambo ambalo kwa Mkristo linamshangaza sana kwani jambo hili linalofundishwa na Allah halipo kabisa kwa Mungu wetu Yehova hapa ulimwenguni ndiko kwenye ulevi,matunda,nyama za ndege, kuoana, maghorofa, magari, mito, bahari na vinginevyo.
Tafakari, je huyo Allah ni nani?

JE, MJI ALIO UCHAGUA ALLAH NI SAWA NA WA YEHOVA?

MJI WA ALLAH:
Qurani 27:91 An-Naml (sisimizi/mchwa/wadudu chungu)
Bila shaka nimeamrishwa nimuabudu mola wa mji huu (wa Makka) ambaye ameutukuza na ni vyake tu (Mwenyezi Mungu) vitu vyote…
Qurani 3:96 Suratul Aal-Imran (watu wa Imram)
Kwa yakini nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ibada) ni ile iliyo Makka yenye baraka na uwongozi kwa ajili ya walimwengu wote.
Qurani 106:3-4 Suratul Quraysh (Makureshi-kabila)
Basi nawamuabudu Bwana wa nyumba hii (Al-ka'ba) Ambaye anawalisha (wakati Waarabu wenzi wao wamo) katika njaa na anawapa amani wakati wenzi wao wamo katika khofu.
Hivyo tunaona kuwa Allah ndiye bwana wa Al-ka'ba kadiri ya aya hii na Al-ka'ba iko katika Makka. Kupitia aya hizi tunaona Allah mungu anayeabudiwa na Waislamu amechagua mji wa Makka kuwa ndio mji wake mtakatifu na tena Muhammad (s.a.w) aliamrishwa amuabudu mola wa mji huo wa Makka ambaye ndiye Allah.

MJI WA YEHOVA:Je, Mungu wetu aitwae Yehova alichagua mji gani? Endelea ……..
Mji aliouchagua Mungu wetu Yehova ni huu…
2 Nyakati 6:4-6
Akasema, BWANA, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenena kwa kinywa chake na baba yangu Daudi, akalitimiza kwa mikono yake, akasema, Tangu siku ile nilipowatoa watu wangu katika nchi ya Misri, sikuchagua mji wowote wa kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe humo; wala sikumchagua mtu yeyote awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, lakini nimeuchagua Yerusalemu, jina langu liwe humo, na Daudi nimemchagua awe juu ya watu wangu Israeli.
Maandiko hayaelezi mji mwingine wowote aliouchagua Mungu wetu hapa duniani bali ni mji wa Yerusalemu tu. (tazama 2 Nyakati 12:13,Ezra 6:12; 7:15,27; Zaburi 26:8; Zakaria 2:12)

Kupitia aya hizi tunaona Mungu wetu Yehova, mji wake aliouchagua niYerusalemu. Neno Yerusalemu ni la lugha ya Kiebrania na maana yake ni "chimbuko la amani". Hata Waisraeli walipokuwa mbali na mji wa Yerusalemu bado walipiga magoti na kuelekeza nyuso zao Yerusalemu. (Tazama Danieli 6:10). Mji aliouchagua Yehova ni Yerusalemu, na mji aliouchagua Allah ni Makka. Na hii ndio tofauti ya mji wa Allah na Yehova.

Leo tumejifunza tena kuwa Allah wa Quran sio Mungu wa Biblia. Allah sio Mungu bali ni kiumbe bandia.
Max Shimba Ministries Org.

MUNGU HANA DINI

Mungu Mtakatifu hana ushirika na dhambi. Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi. Mwanadamu hujaribu kumfikia Mungu kwa nija nyingi: DINI, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi zote hazitoshi. Mwanadamu bado ni mwenye dhambi.

Dini ni jaribio la mwanadamu kuwa na uhusiano na Mungu. Imani ya kikristo ni uhusiano na Mungu kwa sababu yale ametufanyia kupitia kwa kusulubiwa kwa Yesu Kristo.
Kuna njia moja tu ya kushirikiana na Mungu . .

YESU KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI
Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yetu.

ALIKUFA ILI ATULETE KWA MUNGU
Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu.1 Petro 3:18

YESU YU HAI
Kristo alikufa kwa ojili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alitufuka siku ya tatu, kama yanenavyojil maandiko.1 Wakorintho 15:3,4

YESU NDIYE NJIA YA PEKEE
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.Yohana 14:6
Mwanadamu peke yake hawezi kushirikiana na Mungu. Mungu alimtuma Yesu afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na tena awe daraja kati yetu na Mungu ili atulete kwa Mungu.
Sasa kanuni ya nne itakuambia jinsi uwezavyo kumjua maishani mwako . . .
INAKUPASA KUMPOKEA YESU AWE MWOKOZI NA MTAWALA WAKO. Ndipo utajua upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yako.

UNAMPOKEA KRISTO KWA IMANI
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.Yohana 1:12
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.Waefeso 2:8,9
INAKUPASA KUMKARIBISHA YESU, MAISHANI MWAKO
Tazama, nasimama milangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake . . .
Kumpokea Yesu Kristo ni:
Kujua wewe ni mwenye dhambi na kugeuka nafsi yako kwa Mungu na kutubu.
Kumtegemea Mungu kwa kukusamehe kabisa.
Kumkaribisha Yesu Kristo atawale maisha yako kwa imani, ili uwe kama anavyopenda.
swa3

Je, ni picha gani aliye mfano wa maisha yako?
Je, ni picha gani ambaye ungependa awe mfano wa maisha yako?
Yafuatayo ni maelezo ya jinsi uwezavyo kumpokea Kristo ndani ya maisha yako?

UNAWEZA KUMPOKEA KRISTO SASA
Mungu anaufahamu moyo wako. Yafuatayo katika sala hii yanaweza kukusaidia kumpokea Kristo ukiomba kwa moyo wa kweli.
Bwana Yesu Kristo, ninakuhitaji, mimi ni mwenye dhambi. Nimekubali kwamba nimejitawala maisha yangu mwenyewe, na kutengana nawe. Asante kwa kifo chako msalabani kwa ajili ya dhambi zangu na kwa kunisamehe zote. Sasa nageuka na kutubu. Bwana, nakuomba uingie ndani ya maisha yangu na kunitawala kabisa. Badili maisha yangu yawe kama upendavyo wewe. Amin.
Je, sala hii ni sawa na haja ya moyo wako?
Kama sala hii ni sawa na haja ya moyo wako, basi omba sasa na umkaribishe Kristo aingie maishani mwako.

YESU YUMO MAISHANI MWAKO
Sasa, je, umemkaribisha Yesu maishani mwako? Unajuaje?
Kwa hiyo yuko wapi sasa? Kumbuka Ufunuo 3:20.
Yesu alisema ataingia katika maisha yako. Je, si kweli?
Je, unajuaje kuwa Mungu amesikia ombi lako? Mungu ameahidi kwanba lo lote tuombalo na kuamini litatendeka.

ALIYE NA YESU, ANAO UZIMA WA MILELE
Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele na uzima huu umo katika Mwana. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa Mungu. 1 Yohana 5:11-13
Umshukuru Mungu kila siku kwamba Yesu anaishi katika maisha yako.
Uwe na hakika kwamba hatakuacha kabisa. (Mathayo 28:20). Amekupa uzima wa milele.

USIYATEGEMEE MAWAZO YA MOYO WAKO.
Unaweza kujisikia leo unalfuraha kisha kesho ukawa na huzuni. Kwa vyovyote utakavyojisikia Yesu Kristo habadiliki maishani mwako. Waebrania 13:8.
swa4
Ukweli wa Mungu ndio wenye uwezo wa kutuongoza.
Tunaunganishwa na uwezo wa ukweli kwa imani.
Tunapotii ukweli, hali ya kujisikia ya moyo (maoni) huongozwa vyema.
Tunamtegea Mungu na ukweli wake wala sio hali ya kujisikia ya moyo.
Tukifanya dhambi tunatubu na yeye anatusamehe.
Basi, usitegemee mawazo yako, bali utegemee ukweli wa Neno la Mungu kwa imani.

KWA KUWA SASA UMEMPOKEA YESU
Tangu ulipompokea Kristo mabadiliko mengi yametokea.
Yesu ameingia katika maisha yako. (Ufunuo 3:20)
Umesamehewa dhambi zako. (Wakolosai 1:14)
Umefanyika kuwa mwana wa Mungu. (Yohana 1:12)
Utazidi kujua makusudi ya Mungu kwa maisha yako. (2 Wakorintho 5:14,15,17)
Je, unafikiri kuna jambo lililo bora kuliko kumpokea Yesu katika maisha yako?
Basi, labda ungependa kumshukuru Mungu sasa kwa vile alivyokurehemu.
Tunathibitisha imani yetu tunapomshukuru Mungu kwa maombi.
Tuombe tukiwa huru.
Na sasa je?

JINSI YA KUKUA KIROHO
Kama mtoto mchanga unahitaji kukua
Utaendelea vizuri katika maisha ya kiroho ukiyafuata mashauri yafuatayo kila siku:
Zungumza na Mungu kwa maombi (Yohana 15:7)
Soma Neno la Mungu (Matendo 17:11)
Uwe mwaminifu kwa Mungu (Yohana 14:21)
Mshuhudie Kristo kwa matendo yako na maneno yako (Mathayo 4:19 na Yohana 15:8)
Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1 Petro 5:7)
Umruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-18 na Matendo 1:8)

NI MUHIMU KWA WAKRISTO KUSHIRIKIANA
Biblia inatuambia kukusanyika pamoja (Waebrania 10:25)
Ebu, tutumie mfano wa moto. Kuni nyingi zikirundikwa pamoja zinawaka vizuri sana, lakini ukiuondoa ukuni mmoja na kuuweka peke yake utapoa. Vile vile wewe haifai kuishi maisha ya kikristo peke yako.
Ukishirikiana na watu wengine ambao wamempokea Yesu kuwa Mwokozi wao utazidi kuwa na moto wa imani.
Uhudhurie kanisa ambapo watu wanaiamini Biblia kuwa ni kweli na Yesu anatukuzwa.
Max Shimba Ministries Org

MWANAMKE WA KIISLAM HANA HAKI MBELE YA MUMEWE

Leo nitawapa hadith kadhaa kuhusu Wanawake wa Kiislam na jinsi wanavyo onewa na Mtume Muhammad.

NGONO NI LAZIMA HATA KAMA MWANAMKE ANAUMWAKutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mume atakapomwita mkewe kwenye kitanda chake [kwa tendo la ndoa] na yule mke akakataa kumuitika, Malaika humlaani mpaka kupambazuke”[Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Nikaah, mlango wa atakapolala mwanamke hali ya kuwa amekihama kitanda cha mumewe. Hadiyth namba 4821 na namba 4822; Muslim, kitabu cha Nikaah, mlango uharamu wa mwanamke kujizuilia [kujitenga] na kitanda cha mumewe, Hadiyth namba 2602 na Hadiyth namba 2603 na 2604.]

MWANAMKE KABLA YA KUFUNGA LAZIMA APEWE RUHUSA NA MUMEWE. HUU NI MSIBAImepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Asifunge mwanamke [Swawm ya Sunnah] na huku mumewe yuko pamoja nae isipokuwa kwa idhini yake huyo mume na wala asimruhusu mtu katika nyumba ikiwa mumewe yuko isipokuwa kwa idhini yake huyo mume” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Nikaah, mlango wa Swamw ya Sunnah ya mwanamke kwa idhini ya mumewe, Hadiyth namba 4820; na katika Kitabu cha Tafsiri Qur aan, Suuratul Qul A’uwdhu birabbil Falaq, Hadiyth namba 4823; na Muslim, katika Kitabu cha Zakaah, mlango wa atachotoa mtumishi katika mali ya tajiri wake, Hadiyth namba 1710].

MWANAMKE WA KIISLAM HARUHUSIWI KUSAIDIA NDUGU ZAKEImepokelewa kutoka kwa Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Asitoe mwanamke kitu chochote kutoka katika nyumba ya mumewe isipokuwa kwa idhini ya mumewe.” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Nikaah, mlango wa Swawm ya Sunnah ya mwanamke kwa idhini ya mumewe, Hadiyth namba 4823; na Muslim, katika Kitabu cha Zakaah, mlango wa atachotoa mtumishi katika mali ya tajiri wake, Hadiyth namba 1710].

MWANAMKE WA KIISLAM KAZI YAKE NI KUMFURAISHA MUMEWE NA NGONO TU.Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu ‘anhu) amesema kwamba aliulizwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wanawake gani bora? Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Ambae humfurahisha [humpendezesha]anapomtazama, na humtii anapomwamrisha, mke humhifadhi katika nafsi yake na mali ya mumewe” [Imepokelewa na Ahmad, katika Musnad ya Kumi waliobashiriwa Jannah, Musnad waliobakia katika Mukthiriyna katika Swahaabah (Radhiya Allahu ‘anhum), Musnad Abi Hurayrah (Radhiya Allahu ‘anhu), Hadiyth namba 7245 na 9377 na 9445].

MWANAMKE WA KIISLAM HARUHUSIWI KUOMBA TALAKAKatazo La Kudai Talaka Bila Ya Sababu Inayokubalika
Ndoa ni katika mambo Aliyoyaamrishwa Allaah na kuyahimizaMjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ndoa ni mafungamano ya kishari’ah baina ya mwanamme na mwanamke yenye mipaka, nidhamu, vidhibiti na kanuni maalumu; na inaathiri mengi; ima kujenga na kusimamisha familia ya Kiislamu yenye kuongozwa na kuongoka kwa uongofu wa Qur-aan na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kuwa miongoni mwa tofali la kuijenga jamiirabbaaniy [yenye kumuabudu Allaah pekee Mola wa viumbe vyote na yenye kufundisha Kitabu, kukisoma na kukifuata]; na ima kuvunja na kubomoa familia kwa kuivuruga vuruga na kuisambaratisha na kusababisha athari mbaya kwa jamii na watoto kwa kuachana kwa mume na mke.

Na katika yaliyokatazwa ambayo yameenea na kuzagaa kwa wenye kupenda dunia na kuiweka kando Aakhirah ni kwa mwanamke kumtaka au kumghilibu mumewe; iwe kwa kumhadaa au vinginevyo kwa kumshurutisha amuache mkewe ili apate kuolewa yeye au abakie yeye pekee yake [kama ni mke mwenza] hili limekatazwa kama ilivyothibiti katika Hadiythi kuwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwanamke asitake (katika Riwayah: Si halali kwa mwanamke kudai kuachwa ukhti wake [mwanamke mwenzake] ili aichukue nafasi yake na kuolewa yeye; kwani hatopata isipokuwa yale aliyoandikiwa.” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha tafsiyr ya Qur-aan, Surat Qul A’uwdhu Birabbil Falaq, Hadiyth namba 6141 na 4782; na Muslim, katika Kitabu cha ndoa, mlango wa Uharamu wa kuwakusanya mwanamke na Shangazi yake, Hadiyth namba 2527; na Abu Daawuud, katika Kitabu cha atw-Twalaaq, mlango katika mwanamke anamtaka mumewe talaka ya mke wake, Hadiyth namba1865].
Max Shimba Ministries Org

YESU ANAOKOA**JESUS SAVES

Sala ya Toba
Inawezekana kabisa ya kuwa wewe unayesoma ujumbe huu hujaokoka - yaani hujampokea Yesu Kristo ndani ya moyo wako kama Bwana na Mwokozi wako. Lakini sasa umeona umuhimu wa kumpokea Yesu Kristo katika maisha yako.
Naamini Roho Mtakatifu ameweka fursa hii mikononi mwako kwa mpango maalum wa Mungu ili ufike mahali pa kutubu na kuokoka. Inawezekana kabisa, pia ya kuwa hujawahi kuambiwa juu ya umuhimu wa wewe kuokoka. Lakini napenda kukuambia ya kuwa ni mpango wa Mungu uokoke. Soma Wakolosai 1:13,14 na Yohana 1:12-14 na 1 Timotheo 2:3-6 na Warumi 1:16,17 na Yohana 3:7. Ni vigumu kuona baraka za Damu ya Yesu bila ya kuokoka.
Kwa hiyo kama unataka kuokoka - tafuta mahali palipo na utulivu, na usome kwa sauti sala ifuatayo: (ukiweza unaweza kupiga magoti unapoomba sala hii)
“Ee Mungu wangu ulie Mtakatifu. Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu. Ninatubu kweli. Naomba damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi yangu na mwili wangu.
Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho wako – uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Ahsante kwa kunisamehe na kwa kuniokoa. Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina.
Ikiwa umesoma sala hii kwa kukusudia kabisa na kwa imani, basi wewe umeokoka na dhambi zako zimesamehewa na kusahauliwa na Mungu sawasawa na alivyoandika katika neno lake. Damu ya Yesu iko juu yako sasa.
Baada ya kuokoka
Unapoanza maisha haya mapya katika Yesu Kristo nakushauri mambo yafuatayo:
1.Zungumza na Mungu kwa maombi kila siku (Yohana 15:7)
2. Soma Neno la Mungu (Biblia) kila siku (Matendo ya Mitume 17:11)
3.Mruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-25; Warumi 8:14-17)
4.Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1Petro 5:7; Zekaria 4:6)
5.Usiache kukusanyika na kushirikiana na wengine waliompokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao kama wewe ili uimarike zaidi (Waebrania 10:25)
Ukipenda unaweza kuniandikia kwa anwani hii hapa chini juu ya uamuzi uliofikia leo wa kuokoka, ili tumshukuru Mungu pamoja, na tuzidi kukuombea; na pia, tukutumie maandiko mengine ya kukusaidia:

TRENDING NOW