Friday, February 12, 2016

UTHIBITISHO 10 KUWA YESU NI MUNGU

“Wahubiri wa injili” wa Kiislamu huwa wanapinga kuwa Yesu ni Mungu na unapowakatalia wanakwambia, “Lete andiko.”
Maandiko yapo mengi sana ndani ya Biblia juu ya ukweli kwamba Yesu ni Mungu. Ni mengi mno!
Ukishawapa andiko, wanabadilika na kusema, “Nataka maneno aliyoongea Yesu mwenyewe.” Kwa madai haya hata kwenye Qurana hawawezi thibitisha kuwa Allah Allah ni mungu, zaidi ya hapo, hata Utume wa Muhammad unakuwa kwenye njia panda, maana hakuna aya kwenye Quran Muhammad anasema mimi Muhammad ni mtume wa Mungu.
Hiki ni kigezo POTOFU na si cha kibiblia hata kidogo. Ukweli ni kwamba, Biblia YOTE ni Neno la Mungu. Haijalishi amezungumza Musa, Isaya, Yohana, Petro au Yesu mwenyewe. Imeandikwa:
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. (2Petro 1:21).
Hivyo, kudai kwao eti, “Nataka maneno aliyosema Yesu mwenyewe,” ni kigezo batili na kisicho na mantiki hata kidogo.
1. YESU ALIKUWEPO KABLA YA KUZALIWAUfuatao ni ushahidi wa kibiblia kwamba YESU KRISTO ni Mungu.
Yohana 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye IBRAHIMU ASIJAKUWAKO, MIMI NIKO.
NIKO ni jina la Mungu peke yake. Tunakutana na jina hilo pale Musa alipoongea na Mungu na kutumwa kuwakomboa wana wa Israeli kutoka Misri. Imeandikwa:
Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n'nani? Niwaambie nini? Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO (Kutoka 3:13-14).
Mwanadamu yuko kwa sababu Mungu alisababisha awepo. Gari liko kwa sababu injinia au mbunifu alisababisha liwepo. Nyumba ipo kwa sababu fundi alisababisha iwepo. Lakini Mungu YEYE YUKO TU!! Hayupo kwa kusababishwa na yeyote! Ndiyo maana akasema MIMI NIKO AMBAYE NIKO! Yesu ni NIKO. Kwa hiyo, Yeye ni Mungu.
2. YESU NA BABA NI WAMOJAYohana 10:30
Mimi na Baba tu umoja.
Waislamu wana msemo wao kwamba eti, Yesu na Mungu ni wamoja katika malengo, si katika asili yao. Basi huwa nawauliza swali kuhusu aya ifuatayo ya Isaya, nao wanazimika na kukosa jibu:
Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu MTOTO amezaliwa, Tumepewa MTOTO MWANAMUME; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE, Mfalme wa amani.
Aya hii iko wazi kabisa. anayetajwa ni Yesu kwamba Yeye ni Mungu mwenye nguvu.
Yohana 14:9
Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? ALIYENIONA MIMI AMEMWONA BABA; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
Maneno haya Yesu aliyasema baada ya kuulizwa swali lililo wazi kabisa, ambalo lilikuwa na lengo la kumjua MUNGU BABA! Imeandikwa: Filipo akamwambia, Bwana, UTUONYESHE BABA, yatutosha. Ndipo Yesu akajibu waziwazi: ALIYENIONA MIMI AMEMWONA BABA. Maana yake ni kuwa, “Mimi ndio Baba mwenyewe.”
3. YESU NI MWANZO NA MWISHOUfunuo 1:17 na Ufunuo 22:13
Mimi ni wa kwanza na wa mwisho
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
Ni Mungu TU ndiye mwenye uwezo wa kuwa wa kwanza na wa mwisho; Yesu ni Alfa na Omega. Kwa hiyo Yeye ni Mungu.
4. YESU NI NENOYohana 1:1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye NENO ALIKUWA MUNGU.
Andiko hili Waislamu hawalipendi kabisa. ni kwa sababu liko wazi mno. Yesu ni Neno; na Neno ni Mungu; hivyo, Yesu ni Mungu!
5. THOMASO AKIRI KUWA YESU NI MUNGU, NA YESU HAKUKATAA KUITWA MUNGUYohana 20:28
Tomaso akajibu, akamwambia, BWANA WANGU NA MUNGU WANGU!
Tomaso aliposema hivi, Bwana Yesu hakukanusha na kusema, “Mimi sio Mungu.” Badala yake: Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki. (Yoh 20:29).
Kama Thomaso alikuwa muongo, kwanini Yesu hakukataa kuitwa Mungu. Imani zote zinakiri kuwa Yesu hakufanya dhambi na hakuwa na dhambi.
6. DAMU YA YESU INAMAMLAKAMatendo 20:28
Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake MUNGU, ALILOLINUNUA KWA DAMU YAKE MWENYEWE.
Ni Mungu gani mwenye damu huyu? Jibu liko wazi. Huyu ni Yesu Kristo. Huyu ndiye aliyetoa uhai wake na kumwaga damu yake msalabani; na hapo ndipo alipoanzisha Kanisa.
7. KATIKA YESU, KILA KITU KILIUMBWAWakolosai 1:16
Kwa kuwa KATIKA YEYE VITU VYOTE VILIUMBWA, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
Katika Yeye Yesu vitu vyote viliumbwa. Ina maana kuwa vitu vyote vilitokana na Yesu; maana Yesu ni Neno la Mungu. Na tunajua kuwa Muumba wa vitu vyote ni Mungu; hivyo, Yesu ni Muumba – Yeye ni Mungu!!
8. KATIKA YESU, UNAKAA UTIMILIFU WA MUNGUWakolosai 2:9
Maana KATIKA YEYE UNAKAA UTIMILIFU WOTE WA MUNGU, kwa jinsi ya kimwili.
Sisi sote ni watu wasio wakamilifu. Tunaanguka tena na tena kwenye dhambi. Kwa hiyo, hakuna mwanadamu wa kawaida ambaye anaweza kujigamba kwamba yeye ametimia kama alivyo Mungu. Lakini katika Yesu “utimilifu WOTE wa Mungu unakaa.” Kwa nini? Kwa sababu Yeye ndiye Mungu huyohuyo.
9. YESU NI MUNGU PAMOJA NASI "EMMANUEL"1Timotheo 3:16
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. MUNGU ALIDHIHIRISHWA KATIKA MWILI, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Ni Mungu gani aliyedhihirishwa katika mwili? Jibu liko wazi. Ni Yesu Kristo peke yake.
10. YESU NI MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETUTito 2:13
….tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU
Yesu Kristo ni Mungu Mkuu!!
Shida KUU ya Waislamu ni hii: Wanampima Mungu kwa vigezo vya kibinadamu. Mungu anasema: Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza? (Yer 32:27)
Jibu liko wazo. HAKUNA!
Lakini utakuta Waislamu wanauliza maswali ya ajabu sana. Eti, kama Yesu ni Mungu, wakati amekufa, nani alikuwa anaangalia dunia?
Hili ni swali linalofaa kuulizwa juu ya kiumbe. Kama tungesema kuwa mwanadamu fulani alikuwa amekufa, ndipo kuna mantiki kuuliza kwamba, wakati amekufa nani alikuwa anatunza familia yake? Maana hili ni swali linalohusu tabia za kibinadamu kwa kuwa mwanadamu hawezi kuwa mahali kuwili au zaidi kwa pamoja. MUNGU SI MWANADAMU! ANAWEZA YOTE – NA HASA MUNGU WA IBRAHIMU, ISAKA NA YAKOBO!
YESU NI MUNGU MILELE NA MILELE!!
HALELUYA!!
Tafakari
Hoji mambo
Chukua hatua!

Thursday, February 11, 2016

ALLAH KUPITIA MUHAMMAD AMEHARIMISHA KUVAA PETE YENYE DHAHABU


Ndugu msomaji,
Kuharamishwa uvaaji wa dhahabu kwa wanaume kumethibiti katika hadithi nyingi sahihi zilizopokelewa kutika kwa Mtume wa Allah –Rehema na Amani zimshukie.
Amepokea (riwaya) Imamu Bukhaariy, Muislam na Ahmad kwamba Mtume wa Allah “Amekataza (kuvaa) pete ya dhahabu”.
Imepokelewa kutoka kawa Ibn Abbaas-Allah awawiye radhi-kwamba Mtume wa Allah aliiona pete ya dhahabu kidoleni mwa mtu, akamvua na kuitupa (huku) akisema
“ Mmoja wenu analikusudia kaa la moto na kulivaa mkononi?” Mtu yule akaambiwa baada ya kwenda zake mtume “ Itwae pete yako unufaike nayo. Akawajibu Wallah hapana, kamwe sitaichukua ikiwa aliyeitupa ni Mtume wa Allah –Rehema na Amani zimshukie.” Muislam
Na katika jumla ya riwaya zilizopokelewa kwamba Mtume wa Allah –Rehema na Amani zimshukie amesema : “ Ye yote mwenye kumuamini Allah na siku ya mwisho basi asivae hariri wala dhahabu.” Al-musnad {Musnadul–Imam Ahmad}
Huu ni msiba kwa Waislam. Maana siku hizi hawa Waislam wanavaa nguo za harirti pamoja na pete ya dhabu. Ona picha ya Usma Bin Laden na yeye amevaa pete ya dhabu. Astgahfurillah.

Max Shimba Ministries Org

UHUSIANO NA KUFANANA KATI YA WASABATO NA MASHAHIDI WA YEHOVA

Wasabato "SDA" na Mashahidi wa Yehova wote wawili walianzia katika muamko ulio kuwa katika miaka ya 1800 ambao msingi wake ulikuwa ni unabii wa Miller. Mafundisho yao yalianzia kutoka kwenye huu utabiri wa Miller na unafanana katika mambo mengi.
Huu muamko ulianza kupitia utabiri wa kifalme katika mwaka wa 1844, na ulikuwa na waamini wachache sana, ambao wengi wao walitoka katika Makanisa ya Kiroho baada ya kufukuzwa huko kwa sababu ya kufuata utabiri wa Miller.
Baada ya kufukuzwa, walianza kufikiri jinsi ya kuazisha kanisa au mkusanyiko, ingawa hawakuwa na "Mfumo wa hilo kanisa", lakini walipata muamko mkubwa zaidia baada ya kupa ujumbe mwengine uliandikwa na Ellen G. White. Barua hii ya Ellen G. White ndio iliyo anzisha kanisa la Wasabato, na Mwaka 1860 ndio jina la "Seventh Day Adventist" lilichaguliwa na kuwa na kanisa la kwanza.
Mafundisho mengi ya MSINGI ya Wasabato ni yaleyale ambayo yanafundishwa na Mashahidi wa Yehova. Tofauti kubwa ni ile ya Wasabato kuamini kuwa Jumamosi ndio siku pekee ya kuabudu, wakati Mashahidi wa Yehova wao hawashikirii hiyo siku kuwa ni ya muhimu sana.
Wote hao wawili Wasabato na Mashahdi wa Yehova wanakata kushiri Vita ikiwa nchi ipo kwenye matatizo, ingawa wanakubali kufanya kazi za kijeshi ambazo sio za kivita, kama ambavyo Mashahdi wa Yehova walivyo goma kwenda kwenye Vita Kuu ya kwanza ya dunia.
KIFO: Wanaamini kuwa mtu "mwili, roho na nafsi" akifa basi hubakia kwenye kaburi.
Mwanzo 2: 1 Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.
2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. 3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
Ingawa, hakuna aya hata moja kwenye Biblia inayo sema Mungu alimwambia Adama aitunze siku ya Saba" SABATO" kila wiki. Lakini Wasabato wanashikiria kuwa hiyo ndio siku halali ya kusali.
1. Je, Adam alikuwa anafanya na au tenda dhambi kwa kutoa itunza Sabato?
2. Je, baba wa Imani, Ibrahimu, alikuwa anatenda dhambi kwa kuto itunza Sabato, ingawa hakuambiwa afanye hivyo?
3. Je, wana wa Israel walipo kuwa Misri, walikuwa watenda dhambi, maana sheria ya kutunza Sabato ilikuwa bado hawana?
YESU NI MALAIKA MIKAELI
Wote, Wasabato na Mashahidi wa Yehova wanaamini kuwa Yesu Kristo ndie Malaika Mkuu Mikaeli. Ingawa hakuna aya hata moja inayo sema hivyo.
ROHO MTAKATIFU
Wote, SDA-WASABATO na Mashahidi wa Yehova hawaamini kuwa Roho Mtakatifu ni Mungu. Mashahidi wa Yehova wanaami kuwa Roho Mtakatifu ni kama NISHATI FULANI,
Ellen G. White yeye anasema kuwa Roho Mtakatifu ni nguvu fulani ya Mungu, lakini amekataa kusema kuwa Roho Mtakatifu ni "Person" -mtu./Mungu kamili kama alivyo Baba yetu aliye Mbinguni na ana adhama/attributes zote za Mungu
KIFO NI KULALA KWA NAFSI
Wote, Wasabato na Mashahidi wa Yehova wanaamini kuwa kifo ni kulala kwa nafsi kaburini na hubakia kaburini mpaka siku ya kiyama.
JEHANNAM
SDA-Wasbato wanaamini kuwa kuna Jehannam lakini wenda dhambi hawata kaa huko milele bali kwa muda tu, huku Mashahidi wa Yehowa wanaamini kuwa Jehannam itawaangamiza watu mara moja, na hawato kuwepo tena.
Mahusiano yao mengini ni kuwa, Mwanzilishi wa Mashahidi wa Yehova Charles Taze Russell, aliingiza mafundisho ya Wasabato kuhusu siku ya mwisho. Wakati Russell alipo kuwa na miaka 23 alifundishwa mafundisho ya Nelson H. Barbour ambaye ni Msabato na kwamba Yesu atarudi bila ya kuonekana mwaka 1874, ingawa Msabato William Miller alidai hapo nyuma kuwa Yesu atarudi kwa mara ya pili mwaka wa 1843.
Wote wawili Russell na Barbour wanaamini kuwa Yesu alirudi bila ya kuoneka mwaka wa 1874 na kwamba katika "Spring" ya mwaka 1878 kutatokea kunyakuliwa kwa Kanisa. Kunyakuliwa kwa Kanisa kulipo shindikana kutokea, Barbour alikuja na utabiri mwengine "new light" na mafundisho mengine mengi kusaidia ujumbe wake, lakini Russell alikataa kuyakubali.
Russell ndio akajitoa kutoa Kanisa la SDA-WASABATO ambalo ndio lilianzishwa na Ellen G. White. Ilipo fika mwaka wa 1874 Russell alianzisha kikundi kinacho itwa Wanafunzi wa Biblia. Na Julai ya 1879 Russell alichapisha jarida la Watch Tower and Herald of Christ's Presence. Mwaka 1882 Russell alikana UTATU wa Mungu, na ilipo fika 1916 Russell alifariki.
Leo tumejifunza kuhusu kushabihana na kufanana kwa hawa wawili, Mashahidi wa Yehova na SDA- Wasabato. Wote hawa walianzia katika vuguvugu la mwaka wa
Mungu awabariki sana,
Max Shimba
For Max Shimba Ministries Org.

Wednesday, February 10, 2016

WASABATO WANASEMA KUWA YESU KRISTO NDIE MALAIKA MIKAELI


Kanisa na Imani au dini ya Wasabato inafundisha kuwa Yesu Kristo na Malaika Mkuu Mikaeli ni mtu mmoja. Hata hivyo, watu wengine kimakosa wanafikiria kuwa SDA wanafundisha kuwa, Yesu ni Malaika aliye umbwa, na kwahiyo hakuwa mtakatifu "divine" . Lakini, hivyo sio Wasabato wanavyo amini. Badala yake, wanasema katika Agano la Kale kuwa, udhihirisho wa Malaika Mkuu Mikaeli ulikuwa ni utambulisho wa Yesu Kristo kabla hajaja duniani na kwamba Malaika Mkuu Mikaeli hakuumbwa. KATIKA MADAI HAYA, wamekosea katika kulinganisha kwao, lakini katika kukubali kuwa hana na hakuumbwa, wanakubali kuwa Yesu ni Mungu.

Hebu tosome Biblia kwanza:
Yohana 8: 58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.

Hapa kuna matatizo makubwa kwa Wasabato, kwasababu neno la Kigiriki ego eimi linamaanisha " MIMI NIKO". Hili neno liliwafanya Wayahudi wachukie sana , pale Yesu alipo sema yeye ni NIKO "I AM" kiasi cha kutaka kumuua kwasababu alikua anatumia aya ya KUTOKA 3:14 pale Mungu alipo sema kuwa Jina lake ni NIKO" 14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; ["akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma kwenu"]. Angalia vile vile katika Yohana 10: 30-33 kwa uhakikisho wa haya maneno.

Wasabato wanakubali kuwa Yesu ni Mungu, lakini kigeugeu chao kinawafanya wawe sawa na Mashahidi wa Jehovah na kupingana na aya za Biblia Takatifu na kualzimisha kuwa eti, Malaika Mkuu Mikaeli ni Yesu.


DAI LA KWANZA LA WASABATO KUWA YESU NI MALAIKA MIKAELI
1 Wasesalonike 4: 16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

Wasabato wanafurai sana hii aya, kwa kuweka ufafanuzi wa kithiolojia. Wasabato wanafundisha kuwa Yesu Kristo ni Malaika Mkuu Mikaeli, na hivyo kubadilisha maana halisi ya hii aya ili kusaidia theolojia ya imani yao kuwa Yesu ni Malaika Mkuu Mikaeli. Madai ya Wasabato ni makosa maana wanaizuia Biblia kuzungunza katika context/mazingira yake.

HOJA::::
Katika aya hapo ju, ipo wazi kuwa: Moja, Bwana atashuka, Pili, tunasoma kuhusu sauti ya Malaika Mkuu. Tatu, Tunajifunza kuwa kumbe Bwana wetu Yesu sio Malaika Mkuu, maana hiyo aya imewatenganisha hao wawili.


DAI LA PILI LA WASABATO KUWA YESU NI MALAIKA MIKAELI
Yuda 1: 9 Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.

Huu ni mfano mwingine wa thiolojia ya Wasabato inayo linda dai lao la Yesu ni Malaika Mikaeli. Ukizungumza kwa kutumia Biblia, YESU SIO MALAIKA MIKAELI. Hao ni wawili tofauti kabisa, na kuwaunganisha na kusema kuwa Yesu ni Mikaeli ni MAKOSA ambayo Wasabato wanafanya kwa kutengeneza hii aya ili isaidia thiolojia yao.

HOJA:::::
KATIKA AYA HAPO JUU, tunajifunza kuwa Malika Mkuu anasema kuwa NUKUU "Bwana akukemee" Sasa inafahamika kuwa Yesu ni Bwana. kivipi basi Mikaeli aseme Bwana akukemee kama yeye ndie huyo huyo Bwana Yesu? Kwanini hakusema NAKUKEMEA......



DAI LA TATU LA WASABATO KUWA YESU NI MALAIKA MIKAELI
Ufunuo 12:7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

Ona tena hapa, jinsi Wasabato wanavyo itumia thiolojia kusaidia dai lao la Yesu ni Malaika Mikaeli. Hii haya haisemi hivyo wala saidia thiolojia ya Wasabato kuwa Yesu ni Mikaeli.

HOJA::::
Hiyo aya hapo juu inazungumzia Malaika Mikaeli akipigana na Joka, na ahakuna sehemu yeyote ile inamzungumzia Yesu.



BIBLIA INAKUJIBU KAMA IFUATAVYO
Waebrania 1: 5 Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?

Mungu Baba katika Waebrania 1: 5 anauliza, wapi kasema katika Biblia kwa Malaika yeyote yule kuwa wewe ni Mwanangu? Mungu anapinga dai la WASABATO KUWA Malaika Mkuu Mikaeli ni Yesu. Mungu anasema kuwa hajawai muita Mailaka yeyote yule kuwa yeye ni Mwanae.

MUNGU ANAENDELEA KUSEMA katika Waebrania 1 aya 13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?

Hatusome sehemu yeyote ile kuwa Malaika Mkuu Mikaeli aliambiwa akae mkono wa Kuume wa Mungu Baba. Hivyo basi, dai la Wasabato kuwa Yesu ni Malaika Mikaleli limeshindwa kwa mara nyingine hapa.

MUNGU ANAWAAMURU MALAIKA WOTE WAMSUJUDU YESU
Waebrania 1: 6 Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu malaika wote wa Mungu.

Je, katika hiyo aya ya 6, ni nani huyo anaye sujudiwa? Hakika Biblia ipo wazi na inapinga thiolojia ya Wasabato kuwa Yesu ni Malaika Mkuu Mikaeli.

Max Shimba

For Max Shimba Ministries Org

JE, NI HAKI KWA MKRISTO KUSALI (KUOMBA) JUMAPILI?

(SEHEMU YA PILI)

Ndugu msomaji:

Katika ujumbe wa leo, nitawaletea ushahidi mbali mbali unao sema na au mruhumsu Mkristo kusali Jumapili kama ulivyo wekwa na shahidiwa katika Agano Jipya.

Ushahidi wa kubadilika kwa siku ya kusali unaweza kuuona mapema sana katika Agano Jipya. Agano Jipya lina ushahid mwingi sana ambao unasema kuwa SIKU YA SABATO haina nguvu tena na au si Sheria tena kusali Siku ya Saba ya Wiki.


SIKU ZOTE NI ZA BWANA MUNGU
Warumi 14: 5-6 inasema: 5 Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.
6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.

Ni vyema kuisoma Sura nzima ya Warumi 14, ingawa kuna ushahid mkubwa kuanzia aya ya 1 mpaka ya 12. Hata hivyo, maelekezo hapa ni kwa mtu binafsi kuamua katika akili yake ni siku ipi aitunze na au aitumie kusali na kumwabudu Bwana Mungu. Kwasabau hiyo, basi chaguo ni la Mtu na sio Mungu.


SABATO IMESEMWA NI KIVULI. YESU NDIE SABATO
Wakolosai 2: 16-17 inasema: 16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.

Angalia kwa makini hapa jinsi siku zilivyo orodheshwa. Sikukuu huwa ni ya Kimwaka, Mwandamo wa Mwezi ni ya Kimwezi, Sabato ni ya Kiwiki. Hakuna mwenye ruhusa ya kuhukumu katika hili. Sabato imesemwa ni KIVULI. Ukweli kamili ni Yesu. Yesu ndie Sabato yetu.


WALIKUTANA SIKU YA KWANZA YA JUMA
Matendo ya Mitume 20 aya 7 Inasema: 7 Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.

Siku ya Kwanza ya Juma ni Jumapili, na hii ni siku ambayo watu walikusanyika na Kumwabudu Bwana Mungu. Hivyo basi, hii aya inaweza kuonyesha kuwa Kanisa lilikutana/kusanyika siku ya Jumapili.

Katika mkusanyiko huu, kuna mambo Mawili Muhimu sana yalifanyika:
1. Walimeka Mkate -Kula Meza ya Bwana. [Communion]
2. Walisoma Neno.

Zaidi ya hapo, Luka hakutumia njia ya Kiyahudi katika kuhesabu siku, yaani kutua kwa jua mpaka kutua kwa jua. Luka alitumia njia ya Kirumi ambayo siku inaanza Saa Sita ya Usiku. [midnight to midnight.] Huu ni ushahidi tosha kuwa Luka hakutumia na au hesabu siku kwa kutumia Njia ya Kiyahudi ya kuhesabu Sabato.


PAULO ANALIAMBIA KANISA LIKUTANE SIKU YA KWANZA YA JUMA
1 Wakorintho 16: 1-2 inasema: 1 Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo.
2 Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;

Ona hapa Mtume Paulo analiambia Kanisa likutane siku ya kwanza ya Juma ambayo ni Jumapili na aliwataka waweke akiba katika siku hiyo ya kwanza ya Juma.

Hivyo basi, siku ambayo Kanisa liliambiwa likutane ni Jumapili. Je, hii ni siku ya kisheria ya Mkristo kukutana? Jibu ni lako na uchaguzi ni wako.


YOHANA ALIKUWA KATIKA ROHO SIKU YA BWANA
Ufunuo 1 :10-11 inasema: 10 Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
11 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.

Katika Kamusi ya Biblia kuhsu "SIKU YA BWANA" katika Ufunuo 1:10. hii ni tukui la kwanza katika maandishi ya Kikristo kuwa watu wakuna siku ya kwanza τῇ κυριακῇ ἡμέρᾳ, "ta kuriaka hamera." Hii ni uthibitisho kuwa, ilikuwa ni desturi ya Wakristo kukutana katika siku hio. Vile vile, ushahid huu uliweza kuoneka katika Karne ya Pili, Soma (Ignatius, Epistle to the Magnesians, 1. 67).


Katika Makanisa mengi sana ya leo" SIKU YA BWANA" inafahamika kuwa ni Jumapili kama ilivyo kuwa tokea Karne ya Pili

Nategemea huu ushahid unatosha kukuambia kuwa Biblia hamlazimishi mtu kusali siku ya Jumamosi. Kma unashida ya aya angalau moja basi Warumi 14 aya ya 1-12 imetupa haki ya kuchagua siku ya kumwabudu Bwana Mungu ambayo inaweza kuwa Jumatau, Jumanne, Tuma Tano, Alahamisi, Ijumaa, Jumamosi au JUMAPILI. Zote hizo ni siku za Bwana.

Na hakuna mwenye haki ya kukuhukumu unapo amua kusali Jumatatu au siku yoyote ile. Soma Warumi 6 aya 14. KUMBUKA TUPO HURU KATIKA KRISTO.

Hivyo basi, leo nimewapa ushahid kadhaa kuhusu siku halali ya kuwambudu Bwana Mungu. SIKU ZOTE NI ZA BWANA.

Mungu awabariki sana,

Max Shimba

For Max Shimba Ministries Org

MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED

Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

Tuesday, February 9, 2016

UTAFITI: BIBLIA NDIO KITABU BORA NA KINACHO SOMWA SANA KULIKO VYOTE DUNIANI


Mtafiti James Chapman ameweka kumi bora ya vitabu vinavyo somwa sana duniani. Kwa taarifa yako, Biblia ndio kitabu kinacho ongoza kusomwa kuliko vitabu vyote hapa duniani. Quran HAIPO hata kwenye 20 bora.

Zaidi ya hapo, Biblia ndio kitabu kilicho chapishwa sana katika kipindi cha miaka 50 iliyo pita.

Biblia inaongoza kwa kuwa na nakala zaidi ya Bilioni 4 zilizo chapishwa katika kipindi cha miaka 50.

Ikifuatiwa na kitabu cha "Works of Mao Tse-tung" chenye nakala Milioni 820. Kitabu cha Harry Potter nakala millioni 400, The lord of the Rings trilogy nakala milioni 103 na kitabu cha Paulo Coelho's the Alchemist chenye nakala millioni 65.

Sunday, February 7, 2016

JE, MUHAMMAD AU JIBRIL NI ROHO YA KWELI/ROHO MTAKATIFU?

Leo nitawajibu Waislam wote duniani kwa kutumia Biblia Takatifu kuwa Muhammad hakuwa Roho ya Kweli kama alivyo ahidiwa na Yesu Kristo ambaye ni Bwana na Mwokozi wetu.

Mara nyingi Waislam wanauliza, "Roho ya Kweli ni nani ambaye Yesu alimuhadi katika Yohana 16 aya ya 12 mpaka 14.
Nimekuwa nikiwauliza Waislam, hivi wao wanafikiri huyu Roho wa Kweli ni nani? Na wakanijibu kuwa huyo Roho wa Kweli ni Malaika Jibril.

Yohana 16:13 inasema: Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

Zaidi ya hapo, Waislam wengi wanadai kuwa, Yesu alikuwa anamtabiri Muhammad, na wakati huo huo, wengine wanasema kuwa alikuwa anatabiriwa Jibril. KINYUME CHAKE, kama ilivyo shahidiwa katika Yohana 16 aya 13, Yesu alikuwa anamzungumzia Roho Mtakatifu. Tunafahamu hili kwasababu Yesu anamzungunzia Roho ambaye atawaongoza Wanafunzi wake kuanzia wakati huo na sio miaka mamia baadae.

Ukiisoma Biblia kwa makini kuanzia Yohana 16 aya ya 5 mpaka 15 utagundua hapo hapo kuwa Waislam wote pamoja na Allah wao ni waongo.

Lakini, kuna njia nyingi tunaweza kuzitumia kufahamu kama Waislam wako sahihi katika ufafanuzi wao kwa kuangalia na au soma kila wakati Yesu alipo sema "ROHO" katika Injili hiyo hiyo ya Yohana na tuone kama kweli alikuwa anamtabiri Muhammad wa Waislam katika aya mojawapo.

UTHIBITISHO WA KWANZA:
Yohana 1 aya ya 32 inasema: Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake "YESU".

Wote tunafahamu kuwa Muhammad hakuwa Mtakatifu na vile vile hakuwa anapaa kama ndege na alikuja miaka 600 baada ya Kristo, hivyo basi, ni dhahiri kuwa Roho Mtakatifu sio Muhammad ambaye alikuja miaka 600 baadae. Yohana hakuwai mwona Muhammad.

UTHIBITISHO WA PILI:
Yohana 1:33, [ Yohana Mbatizaji anaendelea kusema] "Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu."

Yohana anaweka kiuwazi zaidi aya hiyo hapo juu kuwa Yesu ndie atakaye kuwa anabatiza kwa Roho Mtakatifu.

Kwa kifupi Yesu atamtuma ROHO ambaye ni Mwenye Nguvu ya Mungu na ni Mungu.

Je, Muhammad ni huyo Roho? HAPANA KABISA, kwasababu Yesu aliwabatiza Wanafunzi wake na zaidi ya hapo, wafuasi wake walibatizwa kwa Roho Mtakatifu katika siku ya Pentekoste. Mda mchache baada ya Yesu kupaa kwenda kwa Baba yake Mbinguni, hivyo basi, na narudia tena, hii ilifanyika Miaka mia sita 600 kabla ya Muhammad kuzaliwa. Wanafunzi wa Yesu hawakubatizwa kwa kupitia Muhammad wala Waislam hawabatizi au batizwa.

UTHIBITISHO WA TATU:
Yohana 3 aya ya 5 inasema: Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

Nauhakika hakuna Muislam duniani pote anayeweza kusema kuwa Muhammad anazaa, maana katika ya hapo juu Yesu anasema Mtu lazima azaliwe kwa Roho, JE, MUHAMMAD ALIZAA/ANAZAA?

UTHIBITISHO WA NNE:
Yohona 3 aya ya 6 inasema: Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

Hapa Muhammad anatupwa nje mara moja kwasababu ya haya maneno ambayo Yesu ameyasema, kwasababu #1 Muhammad alikuwa binadamu, mbaya zaidi hivi sasa amekufa -marehemu. na #2 KwasaMbabu tena, Roho inazaa kwa kutumia Nguvu ya Mungu, ambaye ni Roho Mtakatifu. Huku kuzaliwa kwa Roho kulianza miaka 600 kabla ya Muhammad kuzaliwa.

UTHIBITISHO WA TANO:
Yohana 3 aya ya 8 inasema: Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.

HAKUNA HATA MMOJA WETU ALIYE ZALIWA KUPITIA MUHAMMAD. Hivyo basi Muhammad anashindwa tena kuwa Roho ya Kweli.

UTHIBITISHO WA SITA:
Yohana 3 aya ya 34 inasema: Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.

Je, Muhamamd alikuwa hana kipimo? Hapo tena Muhammad kashindwa maana alikuwa amepimiwa maneno tu na Allah wake. Muhammad alikiri kuwa yeye hajui Mungu atamfanya nini baada ya kifo, pale alipo ulizwa na watu, je, nini kitatokea baada ya kifo. Muhammad hakuwa "omniscient".


UTHIBITISHO WA SABA:
Yohana 4 aya ya 24 inasema: Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Mungu sio Muhammad, asante Mungu, kwa kuweka huu ukweli kuwa Roho Mtakatifu ni Mungu. Kumbe hata Jibril sio Roho Mtakatifu.

UTHIBITISHO WA NANE:
Yohana 6 aya ya 63 inasema: Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.

Muhammad hawezi kutoa uzima wa milele, ni kitu ambacho Mungu peke yake anaweza kukupa. Ndio maana tunajua kuwa Yesu ni Mungu, kwasababu, Yesu anatoa uzima wa Milele kwa wale wote wamwaminio.

UTHIBITISHO WA TISA:
Yohana 7 aya ya 39 inasema: Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.

Je, Muhammad atapewa kwa kila mtu ambaye anamwamini Yesu? HAPANA KABISA, Quran inasema kuwa Ukimwanini Mwamad/Allah basi umemwamini Allah. Hivyo Muhammad hawezi kuwa Roho ya Kweli, maana tunao Mwamini Yesu tumepewa Roho Mtakatifu na sio Muhammad ambaye amesha kufa.

UTHIBITISHO WA KUMI:
Yohana 14 aya ya 16,17, na 18 inasema: 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.

Hizi aya zinapendwa sana na Waislam na wanapenda kuzitumia kama ushahidi wao. Je, Muhammad aliishi na Mitume wa Yesu katika karne/Century ya kwanza? HAPANA KABISA TENA KABISA. Muhammad hakuwepo wakati wa karne/Century ya kwanza pale Wafuasi wa Yesu walipo pewa huyo Roho Mtakatifu. Yesu alisema kwa Wanafunzi wake kuwa hata waacha YATIMA, Je, iweje Muhammad aliye kuja miaka 600 baadae awe na Wanafunzi wa Yesu katika karne/Century ya Kwanza?

UTHIBITISHO WA KUMI NA MOJA:
Yohana 14 aya ya 26. Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Hii aya Waislam hawaipendi kabisaa, kwasababu Yesu anasema KIUWAZI KABISA KUWA, ni nani huyu WAKILI wetu, NI WATATU KATIKA MUUNGANO MTAKATIFU. Huyu Roho Mtakatifu ana adhama zote za Baba na Mwana, HIVYO BASI, Muhammad tena ameshindwa vibaya sana hapa. Muhammad alikuwa Mtenda dhambi, huku Yesu hakuwai tenda dhambi hata moja.

UTHIBITISHO WA KUMI NA MBILI:
Yohana 15 aya ya 26 inasema: Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.

Kwa mara nyingine tena, hii ndio raha ya kufundisha katika context yake. Tumesoma katika aya hapo juu kuwa Yesu alisema nani ni Msaidizi wetu, na kwa undani zaidi, HAPA KWENYE HII AYA YA 26 Yesu anasema kuwa huyo Msaidizi ni Roho Mtakatifu.
Je, Muhammad aliishi wakati wa Mitume wa Yesu na kuwa msaidizi wao, HAPANA KABISA, inafahamika kuwa Muhammad alikuja miaka 600 baadae.

UTHIBITISHO WA KUMI NA TATU:
Yohana 16 aya ya 13 inasema: Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

Muhammad tena ameshindwa hapa, maana hakunena na wala hakuwai sikia kutoka kwa Mungu, Yehova, bali kwa Jibril ambaye anadai kuwa alitumwa na Allah. Zaidi ya hapo, Muhammad hakutoa utabiri wa mambo yatakayo kuja. MUHAMMAD AMESHINDWA TENA KWA MARA YA KUMI NA TATU.

UTHIBITISHO WA KUMI NA NNE:
Yohana 16 aya ya 15 inasema: Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.

Yesu anasema kuwa yote ya Baba ni yangu, je, binadamu wa kawaida anaweza kudai kuwa kila kitu cha Mungu Baba ni chake? Hakika Yesu ni Mungu. ZAIDI YA HAPO, Yesu anasema kuwa huyo Roho Mtakatifu atatufundisha kuhusu YEYE/Yesu, wakati inafahamika kuwa Muhammad hakuwai fundisha kuhusu Yesu na wala Muhammad hakuwai sema kuwa Yesu ana Baba. Kumbe basi Roho Mtakatifu hawezi kuwa Jibril au Muislam bali ni Mungu mwenye adhama zote za Baba na Mwana.

UTHIBITISHO WA KUMI NA TANO:
YESU ANAWAPA ROHO MTAKATIFU WANAFUNZI WAKE
Yohana 20 aya ya 21 na 22 inasema: 21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. 22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.

AYA HAPO JUU IPO WAZI kabisa kuwa YESU ALIWAPA ROHO MTAKATIFU WANAFUNZI WAKE NA HAKUWAPA MUHAMMAD AMBAYE alikuwa bado HAJAZALIWA.

Hivyo basi, leo nimetoa USHAHIDI ZAIDI YA KUMI NA TAKO KUTOKA INJILI YOAHANA kuwa Muhammad hakuwa Roho ya Kweli, zaidi ya hapo, Jibril hakuwa Roho ya kweli.

LEO NIMEJIBU KUHUSU ROHO WA KWELI AMBAYE YESU ALIKUWA ANAMSEMA kwa kutumia Aya hizo hizo ambazo Yesu alizitumia kumzungumzia huyo Roho wa Kweli.

Katika huduma yake,

Max Shimba,

Max Shimba Ministries 2013
December 26, 2013
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

Contradictions in the Quran: A Theological and Textual Examination

Contradictions in the Quran: A Theological and Textual Examination By Dr. Maxwell Shimba, Shimba Theological Institute Introduction Muslims ...

TRENDING NOW