Friday, February 19, 2016

BIBLIA INAKATAZA USHOGA

Je, Biblia inasema nini juu ya Ushoga?
Je, Ushoga ni dhambi?

Ndugu msomaji,

Leo, watu wengi kupitia viongozi fulani wa dini hawashutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja. Hata hivyo, Biblia iko wazi kuhusu jambo hilo. Inatuambia Mungu aliumba mwanamume na mwanamke na kwamba alikusudia ngono ifanywe kati ya mume na mke tu. (Mwanzo 1:27, 28; 2:24) Hivyo, haishangazi kwamba Biblia inashutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja.—Waroma 1:26, 27.

Waislam mara nyingi wamekuwa wakisema na kuwashutumu Wakristo, eti, Ukristo unaruhusu ushoga, huku ikifahamika kuwa, hakuna aya hata moja inayo ruhusu huu uchafu.

Walawi 18:22-23 "Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko".

Neno la Mungu kama lisemavyo kwenye Biblia linasisitiza kila mara kwamba ushoga na usagaji ni dhambi (Mwanzo 19:1-13; Mambo ya Walawi 18: 22; Warumi 1:26-27; Wakorintho wa kwanza 6:9). Warumi 1:26-27 inatufundisha ya kwamba ushoga ni njia mojawapo ya kumkana na kutomtii Mungu. Mtu anapodumu katika dhambi na kutokuamini biblia inatuambia ya kwamba “Mungu huwaachilia” kutenda maovu zaidi ili wapate kujua ubatili wa maisha bila Uwepo wa Mungu. Wakorintho wa kwanza 6:9 inasema kuwa mashoga hawataurithi ufalme wa Mungu.

Wanadamu wanajinenea kuwa wenye hekima na kupumbazika. Mtume Paulo ameeleza vizuri katika Waroma1:21-27.

Mungu amewaacha wafuate akili zao. Kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao ,Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.Waroma1:28

Watu wengine wanasema kwamba ushoga upo kwenye chembe za urithi. Wengine wanasema kwamba mtu hujifunza zoea hilo. Si kusudi la makala hii kujadili ikiwa zoea hilo ni la kurithiwa au ni la kujifunza. Kwa wazi, kusema kwamba ushoga unasababishwa na jambo fulani hususa haingekuwa kweli. Inaonekana kwamba kama ilivyo kwa mazoea mengine, ni vigumu kufahamu chanzo cha zoea hilo.


Hata chanzo kiwe nini, jambo muhimu ni kutambua kwamba Biblia inashutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja.


Mungu hakuumba mwanadamu mwenye tamaa ya ushoga. Biblia inatuambia mtu huwa shoga kwa sababu ya dhambi. (Warumi 1:24-27), na pia kwa sababu ya uamuzi wake mwenyewe. Mtu anaweza kuzaliwa na msukumo juu ya ushoga kama vile watu pia huzaliwa na msukumo juu ya fujo na dhambi nyinginezo. Hili halihalalishi dhambi yoyote inayofanywa na wanadamu. Je, mtu akizaliwa na msukumo wa hasira mbaya, ni halali aendeleze hasira zake mbaya? La, hasha. Hata kwa ushoga pia si halali.
Hata hivyo Biblia haiitaji dhambi ya ushoga kuwa ndiyo kubwa zaidi. Kila dhambi ni chukizo kwa Mungu. Ushoga ni mojawapo ya mambo yaliyoorodheshwa katika wakorintho wa kwanza 6:9-10 yatakayozuia mtu asiingie katika ufalme wa Mungu. Kulingana na Biblia msamaha wa Mungu juu ya shoga upo sawa na wa mzinzi, muabudu sanamu, muuaji, mwizi na kadhalika. Mungu tena aahidi uwezo juu ya kushinda dhambi, pamoja na ushoga, kwa wale wote watakao mwaminiYesu kristo kwa wokovu wao (wakorintho wa kwanza 6:11; wakorintho wa pili 5:17).


JE, UNAWEZA KUISHINDA TAMAA HII YA USHOGA?
Unaweza kuepukaje kujihusisha na ngono ya watu wa jinsia moja?

▪ Kwanza Mtupie Mungu mahangaiko yako yote kupitia sala, ukiwa na uhakika kwamba ‘anakujali wewe.’ (1 Petro 5:7; Zaburi 55:22) Mungu anaweza kukuimarisha kwa kukupa amani “yenye ubora unaozidi fikira zote.” Amani hiyo ‘itaulinda moyo wako na nguvu zako za akili’ na kukupa “nguvu zinazopita zile za kawaida” ili usitende kulingana na tamaa zisizofaa. (Wafilipi 4:7; 2 Wakorintho 4:7) Sarah, ambaye alihofia kwamba anavutiwa na watu wa jinsia zote mbili, anasema: “Kila wakati ninapopatwa na hisia hizo, mimi husali; na Yehova hunitegemeza. Nisingeweza kukabiliana na tatizo hilo bila msaada wake. Sala ndiyo msaada wangu mkubwa!”—Zaburi 94:18, 19; Waefeso 3:20.

▪ Pili Jaza akili yako mambo ya kiroho yenye kujenga. (Wafilipi 4:8) Soma Biblia kila siku. Usidharau uwezo wake wa kuongoza akili na moyo wako daima. (Waebrania 4:12) Kijana mmoja anayeitwa Jason anasema: “Biblia—kutia ndani maandiko kama vile 1 Wakorintho 6:9, 10; na Waefeso 5:3—imenisaidia sana. Mimi husoma maandiko haya kila wakati tamaa mbaya zinaponijia.”

▪ Tatu Epuka ponografia, yaani picha au habari za kingono na propaganda za ngono kati ya watu wa jinsia moja ambazo zinaweza kuchochea mawazo yasiyofaa.* (Zaburi 119:37; Wakolosai 3:5, 6) Sinema na vipindi fulani vya televisheni pia huendeleza wazo la kwamba ngono kati ya watu wa jinsia moja ni mtindo mwingine tu wa maisha. “Maoni yaliyopotoka ya ulimwengu yaliathiri sana akili yangu, na kufanya nichanganyikiwe kuhusu hisia za kuvutiwa na watu wa jinsia yangu,” anasema Anna. “Sasa mimi huepuka kabisa kitu chochote au mtu yeyote ambaye anaunga mkono ngono kati ya watu wa jinsia moja.”—Methali 13:20.

▪ Nne Zungumza na mtu unayemwamini kuhusu hisia zako. (Methali 23:26; 31:26; 2 Timotheo 1:1, 2; 3:10)

MAMBO YA KUFIKIRIA
▪ Kwa nini Mungu hushutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja?
▪ Utafanya nini ikiwa unakabiliana na hisia za kuvutiwa kingono na mtu wa jinsia yako?
▪ Unaweza kuongea na nani ikiwa unahangaishwa na hisia za kufanya ngono na mtu wa jinsia yako?

Walawi 18:22-23 "Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko".

Ushoga ni dhambi na umekatazwa kwenye Biblia.

Mungu awabariki sana.

Max Shimba

For Max Shimba Ministries Org.

MAHAKAMA YA KADHI HAIPO KWENYE QURAN

Ndugu wasomaji.
Leo ningependa kusema kuwa, dai la Waislam wa Tanzania la Mahakama ya Kadhi halina msingi wala usaidizi wa Quran.
Kwa wanao ifahamu Quran, watakubaliana na mimi kuwa HAKUNA AYA HATA MOJA ambayo Allah alisema na au Waamrisha Waislam waende kwenye Mahakama ya Kadhi. Narudia tena hakuna aya.
SASA NDUGU WAISLAM:
1. Who appoints Chief Kadhi and Kadhis?
--Nani na au mnamteuaje Kadhi Mkuu na Kadhi? Leteni aya.
2. What are the qualification for appointment to the office of a Kadhi (including a Chief Kadhi)?
-- Je, mnatumia qualification/elimu zipi kuchagua/kufanya utezi wa Ofisi ya Kadhi na Kadhi mkuu/ Leteni aya.
3. Since the Kadhis are not trained lawyers who understand the Evidence Act and the Civil Procedure Act, how and/or what will they use to administer their Courts?
-- Inafahamika kuwa Kadhi sio Mawakili walio somea ambao wanaelewa ushahid wa keshi ambazo si za jinai na jinai, SASA hawa Kadhi watatumia nini katika kusimamia Mahakama ya Kadhi?
4. Muslims are mainly of two sects in Tanzania - the Sunni and Shia. Majority of the Muslims in Tanzania are Sunni Muslims but there is a significant population of Shia Muslims too and consideration ought to be given to the appointment of Kadhis of the Shia Sect to cater the interest of the Shia Muslims. Will they have two different Courts? For Sunni and Shia?
--- Waislam wapo katika makundi mawili makubwa, Sunni na Shia. Wengi wa Waislam wa Tanzania ni Sunni, ingawa kuna Shia wengi vile vile. JE, Hii Mahakama ya Kadhi itatumia Kadhi wa dhehebu lipi katia ya hayo mawili? Je, watakuwa na Mahakama mbili tofauti za Sunni na Shia?
5. How will Muslim Women be protected since: Muslim law regards women as less than men in matters of both marriage and divorce, as well as devolution of property: Holy Quran Surah 2:228-232, and Surah 65:1-7 (only a man may divorce his wife even if he is required to provide for her); a man may beat his wife, even if lightly, the evidence of two women, is equal to evidence of one man (Surah 2:282). The application of such beliefs of faith are contrary to the Constitution.
---Kivipi Wanawake wa Kiislamu watatetewa kwenye hizi mahakama? Inafahamika kuwa Sheria za Kiislam zinakiri kuwa Mwanamke ni nusu ya Mwanaume, au yupo chini sana ya Mwanaume. Je, katika kesi ya kutoa talaka na mirathi, hii mahakama itawezaje kumtetea Mwanamke ambaye yupo nusu ya Mwaume? Sura 2: 228-232 na Sura 65:1-7 ( zinasema mwenye haki ya kutoa talaka ni Mwaume tu) Mume anahaki ya kumpiga mkewe, Ushahidi wa wanawake wawili ni sawa na ushahid wa mwanaume mmoja, (Sura 2:282). Huu utamaduni wa Kiislam, ni kinyume na sheria za nchi.
Je, Mwanamke atatetewa vipi kwenye hizi Mahakama?
Islamic "Kadhi" courtsis illegal and discriminatory.
Kwanini mnamsaidia Allah kwa kuanzisha Mahakama ya Kadhi?
Waislam, nileteeni aya ambayo Allah anasema kuwa muende kwenye Mahakama ya Kadhi.
Mkiniletea aya kutoka Quran inayo waamrisha kwenda kwenye Mahakama za Kadhi, leo hii nitasilimu na kuwa Muislam.
Haya nasubiri ajibu ya aya na sio matusi.
Max Shimba
For Max Shimba Ministries Org.

MAHAKAMA YA KADHI NI HATUA YA AWALI KATIKA KUIFANYA TANZANIA KUWA TAIFA LA KIISLAM

na Max Shimba Ministries
Mahakama ya Kadhi ni nini?
Mahakama ya kadhi ni chombo cha kiislam kwa ajili ya kufanya mashauri ya ndoa , mirathi na mambo ya kidini kwa kutumia Sharia.
Sharia ni nini?
Sharia ni mkusanyiko wa sheria za dini ya kiislam ambazo zinatokana na kitabu cha quran na tamaduni za kiislam kwa kufuata mafundisho na hadithi za Mtume Muhammad.
Mambo ya kidini yanayo hukumiwa na mahakama ya kadhi ni yapi?
Ni mambo yote yanayokwenda kinyume na tamaduni za kiislamu. Mfano Kula hadharani wakati wa mwezi, wa ramadhani, kuchinja kwa mtu ambaye siyo muislamu, kufanya biashara ya vileo, biashara ya nyumba za kulala wageni, biashara ya nguruwe, mavazi yasiyoendana na tamaduni za kiislam kwa maana hiyo ili uwe salama kwa swala la mavazi sharti uvae hijabu kwa wanawake, kanzu na kibaragashia kwa wanaume, msuri na visuruari vizivyogusa viatu.
Kwa nini waislam wanataka Mahakama ya kadhi iingizwe kwenye katiba ya nchi?
Waislam wanataka mahakama ya kadhi iingizwe kwenye katiba ya nchi ili itambulike kisheria na iwe na nguvu kama mahakama za kawaida za makosa ya jinai na hiyo iwe na mamlaka ya kuhukumu watu wote waislam, wakristu na hata wapagani limradi tu hawaishi kwa kufuata tamaduni za kiislam. Mfano mtu atakaye kutwa anakula hadharani wakati wa mwezi wa ramadhani sharia itachukuwa mkondo wake na hukumu iliyotawala kwenye sharia kwa mtu anayeishi kinyume na tamaduni za kiislam ni kuuwawa kwa kuchinywa na jukumu hilo liko kwa Makadhi.
Hivyo basi mahakama ya kadhi ikiingizwa kwenye katiba itakuwa na nguvu za kuhukumu mambo ya siasa, kijamii na makosa ya jinai kwa ujumla kwa raia wote na si kwa waislam peke.
Muundo wa mahakama ya kadhi
Mahakama ya kazi inafuata muundo wa mahakama za kawaida hivyo zinaanzia ngazi ya chini kabisa kwenye wilaya na hadi ngazi ya kitaifa na mahakimu wa mahakama za kadhi ni makadhi amboa wote ni waislam
Kazi za Makadhi
1.Kusikiliza mashauri na kuhukumu kwa kufuata sharia
2.Kuhakikisha anatokomeza ukristu katika eneo lake na uislam unatawala
3.Kuhakikisha hakuna kanisa linajengwa katika eneo lake na wala kanisa linapo bomoka halitaruhusiwa kukarabatiwa wala kujengwa tena. Kujenga kanisa ni kinyume na tamaduni za kiislam ndiyo maana utaona wameanza kuchoma makanisa huko Zanzibar na sehemu zingine za Afrika kama Nigeria.
Madhara ya Mahakama ya Kadhi
1.Kuvunjika kwa umoja wa kitaifa uliopo kati ya waislam, wakristu na wapagani
2.Ugomvi wa kimasrahi kati ya wakristu, wapagani na waislam. Endapo Mahakama ya kadhi itaingizwa kwenye katiba ya nchi ni wazi itagharamikiwa na serikali na hivyo viongozi wa dini ya kiislam ambao ndiyo watakuwa makadhi watatumia fedha za walipa kodi wa Tanzania ambao ni waislam, wakristu na wapangani kujinufaisha wenyewe kwa kujitengenezea ajira. Vipi kuhusu viongozi wa dini za wakristu Maaskofu, Mapadri, Wachungaji na Viongozi wa dini za Jadi nao watakuwa wanalipwa na Serikali?
3.Kutoweka kwa wakristu kutokana na utawala wa sharia, sababu hukumu iliyo tawala kwenye sharia ni kifo hivyo wakristu
watauwawa kwa kuwa hawatakubali kuishi tamaduni za kiislam
4.Kuporomoka kwa uchumi wa nchi na kuongezeka kwa tatizo la ajira kwa mfano mashule ya wakristu au taasisi za kikristu zitachomwa kama ambavyo unaona yanatokea nchini Nigeria.
Viwanda vyote vya vileo vitafungwa, makumbi ya starehe yote yatafungwa. Ukiangalia uchumi wa Tanzania unategemea sana viwanda vya bia, Sigara nk. Sector hiyo ndiyo imeajiri watu wengi sana, anzia kwenye viwanda vyenyewe njoo kwenye mabaa, grosary na makumbi ya starehe
MAHAKAMA YA KADHI NI HARAM=TANZANIA
Max Shimba
For Max Shimba Ministries

JE, WAKRISTO WANASTAHILI KUITUNZA SIKU YA SABATO? (SEHEMU YA KWANZA)

Ndugu msomaji,
Leo tutajikumbusha kwa mara nyingine tena kama tunatakiwa kuitunza Sabato.
Sabato ilipeanwa kwa Waisraeli, si kanisa. Sabato bado ingali siku ya Jumamosi si Jumapili na haijawai badilishwa. Bali sabato ni sehemu ya sheria ya Agano La Kale na Wakristo wako huru kutoka kwa mkono wa sheria (Wagalatia 4:1-26; Warumi 6:14). Wakristo hawitakiwi kuitunza sabato hata kama iko siku ya Jumamosi au Jumapili. Siku ya kwanza ya juma, siku ya Bwana (Ufunuo 1:10) za sherekea kiumbe kipya Kristo aliyefufuka akiwa kiongozi wetu. Hatujaamrishwa kiufuata sheria ya Musa ya sabato ya kustarehe, bali tuko huru kumfuata Kristo aliyefufuka. Mtume Paulo alisema kwamba kila mkristo amue mweneyewe kama ataifuata sabato, “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku; mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe” (Warumi 14:5). Twastahili kumwabudu Mungu kila siku, si Jumamosi pekee or Jumapili pekee.
Lengo la Mungu kupeana sabato kwa Waisraeli haikuwa kukumbuka uumbaji, bali waukumbuke utumwa wa Wamisri na kule kuokolewa na Bwana. Kumbuka yanayohitajika kwa kuitunza sabato: mtu aliyewekwa chini ya hiyo sheria hangeweza kutoka kwa boma yake (Kutoka 16:29), hangewakisha moto (Kutoka 35:3), angeruhusu mtu yeyote kufanya kazi (Kumbukumbu La Torati 5:14). Mtu mwenye angivunja shreria ya sabato angeuwawa (Kutoka 31:15; Hesabu 15:32-35).
Uchunganusi wa ukurasa wa Agano Jipya watuonyesha mambo mane muimu: 1) Popote Kristo alionekena baada ya kufufuka kwake na siku zimetajwa, kila wakati ni siku ya kwanza ya Juma (Mathayo 28:1,9, 10; Mariko 16:9; Luka 24:1,13,15; Yohana 20:19, 26). 2) Wakati pekee sabato imetajwa kutoka kwa kitabu cha Matendo ya Mitume hadi ufunuo ni kwa sababu ya lengo la uinjilisti kwa Wayahudi kwenye Masinagogi (Matendo Ya Mitume 13-18). Paulo aliandika, “Nilikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi” (1 Wakorintho 9:20). Paulo hakuenda kaitka Masinagogi kuwa na ushirika na kuwajenga waumini, bali alienda ili awathibitishie injili na kuwaokoa walikuwa wamepotea. 3) Mara moja Paulo anasema, “tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa” (Matendo Ya Mitume 18:6), sabato tena haitajwi kamwe. Na 4) Badala ya kupendekeza kuwa waitunze siku ya sabato, sehemu nyingine ya Agano Jipya iliyobaki yasema kinyume ( ikijumulisha sehemu ya tatu ilioachwa nche hapo juu, inapatika katika Wakolosai 2:16).
Kwa kuingalia hoja ya nne kwa makini, tutafumbua kwamba, hakuna jukumu lolote la kuitunza sabato kwa waumini wa Agano Jipya. Pia tutaonyesha kuwa dhana ya Jumapili “Sabato ya Wakristo” si ya kibibilia. Vile imejadiliwa hapo juu, hakuna wakati sabato imetajwa baada ya Paulo kuanza kuangazia Mataifa, “Basi mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” (Wakolosai 2:16-17). Sabato ya Kiyahudi ilifutiliwa msalabani hamali ambapo Kristo “Akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki” (Wakolosai 2:14).
Wazo hili limerudiwa zaidi ya mara moja katika Agano Jipya: “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku; mwinginie aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishaye siku huiadhimisha kwa Bwana” (Warumi 14:5-6a). “Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? Mnashika siku, na miezi, na nyaktati, na miaka” (Wagalatia 4:9-10).
Ni siku gani ya sabato, Jumamosi au Jumapili? Wakristo wastahili kuitunza hii siku?
Twastahili kumwabudu Mungu kila siku, si Jumamosi pekee or Jumapili pekee.
Mungu awabariki sana,

JE, WAKRISTO WANASTAHILI KUITUNZA SIKU YA SABATO? (SEHEMU YA PILI)


Ndugu msomaji,

Kwa kuwa Kristo alitimiza Sheria, je, Wakristo wana wajibu au daraka la kushika Sabato ya kila juma?

Akiongozwa na Roho wa Mungu, mtume Paulo anajibu hivi: “Kwa hiyo mtu yeyote asiwahukumu ninyi katika kula na kunywa au kuhusu sherehe au kuhusu kushika mwezi mpya au sabato; kwa maana mambo hayo ni kivuli cha mambo yanayokuja, bali uhalisi ni wa Kristo.”—Wakolosai 2:16, 17.


Maneno hayo yaliyoongozwa na Roho wa Mungu yanaonyesha kwamba matakwa ambayo Mungu aliwapa watumishi wake yalibadilika sana. Kwa nini yalibadilika? Kwa sababu Wakristo wako chini ya sheria mpya, “sheria ya Kristo.” (Wagalatia 6:2) Agano la zamani la Sheria ambalo Mungu aliwapa Waisraeli kupitia Musa lilifikia mwisho wake wakati kifo cha Yesu kilipotimiza agano hilo. (Waroma 10:4; Waefeso 2:15)


Je, amri ya kushika Sabato ilifikia mwisho pia?
Ndiyo. Baada ya kusema kwamba “tumefunguliwa kutoka katika Sheria,” Paulo alitaja amri moja kati ya zile Amri Kumi. (Waroma 7:6, 7) Kwa hiyo, zile Amri Kumi, kutia ndani sheria ya Sabato, ni sehemu ya ile Sheria ambayo ilifikia mwisho. Kwa hiyo, waabudu wa Mungu, hawako chini ya takwa la kushika Sabato ya kila juma.


Mfano unaofuata unaweza kutusaidia kuelewa badiliko kutoka katika ibada ya Waisraeli kuingia katika ibada ya Kikristo: Nchi inaweza kubadili katiba yake. Baada ya katiba mpya kukubaliwa kisheria, watu hawatakiwi tena kufuata katiba ya zamani. Hata ingawa huenda sheria fulani katika katiba hiyo mpya zikafanana na sheria fulani za katiba ya zamani, sheria nyingine zinaweza kuwa tofauti. Kwa hiyo, mtu angehitaji kujifunza katiba mpya kwa uangalifu ili aone sheria ambazo zinatumika sasa. Kwa kuongezea, raia mshikamanifu angependa kujua katiba hiyo mpya ilianza kutumika wakati gani.


Vivyo hivyo, Mungu aliwapa Waisraeli sheria zaidi ya 600, pamoja na zile amri 10 za msingi. Sheria hizo zilitia ndani sheria kuhusu maadili, dhabihu, mambo ya kiafya, na kushika Sabato. Hata hivyo, Yesu alisema kwamba wafuasi wake watiwa-mafuta wangekuwa “taifa” jipya. (Mathayo 21:43) Kuanzia mwaka wa 33 W.K. na kuendelea, taifa hilo limekuwa na “katiba” mpya ambayo inategemea sheria mbili za msingi, yaani, kumpenda Mungu na kumpenda jirani. (Mathayo 22:36-40) Ingawa “sheria ya Kristo” inatia ndani maagizo mengi ambayo yanalingana na sheria ambazo Waisraeli walipewa, hata hivyo, Sheria fulani ni tofauti kabisa na sheria nyingine hazihitajiwi tena. Sheria ya kushika Sabato ya kila juma ni moja kati ya sheria ambazo hazitumiki tena.


Je, Mungu Amebadili Viwango Vyake?

Je, badiliko hilo la kuacha Sheria ya Musa na kufuata sheria ya Kristo linamaanisha kwamba Mungu amebadili viwango vyake?
Hapana. Yehova amebadili sheria ambazo watu wake wanapaswa kutii kama vile tu mzazi anavyobadili sheria anazowawekea watoto wake ikitegemea umri na hali zao. Mtume Paulo anaeleza hivi jambo hilo: “Kabla ya ile imani kufika, tulikuwa tukilindwa chini ya sheria, tukiwekwa pamoja kifungoni, tukiitazamia imani iliyokusudiwa kufunuliwa. Kwa sababu hiyo Sheria imekuwa mtunzaji wetu kutuongoza kwa Kristo, ili tutangazwe kuwa waadilifu kutokana na imani. Lakini sasa kwa kuwa imani imefika, sisi hatuko tena chini ya mtunzaji.”—Wagalatia 3:23-25.


Hoja hizo za Paulo zinaihusu vipi Sabato?
Fikiria mfano huu: Mwanafunzi anaweza kuagizwa ajifunze somo fulani shuleni, kama vile useremala, siku fulani ya juma. Hata hivyo, anapoanza kufanya kazi, huenda akahitaji kutumia ustadi aliojifunza, kila siku ya juma badala ya kuutumia siku moja tu. Vivyo hivyo, Waisraeli walipokuwa chini ya Sheria walitakiwa watenge siku moja kila juma ya kupumzika na kuabudu. Hata hivyo, Wakristo wanatakiwa wamwabudu Mungu kila siku badala ya siku moja tu kwa juma.


Basi je, ni kosa kutenga siku moja kila juma ili kupumzika na kuabudu?
Hapana. Neno la Mungu linamruhusu kila mtu ajiamulie jambo hilo, linasema hivi: “Mtu mmoja anaamua kwamba siku moja ni takatifu kuliko nyingine. Mtu mwingine anaamua kwamba siku zote ni sawa. Ni lazima kila mtu afanye uamuzi wake mwenyewe.” (Waroma 14:5, tafsiri ya God’s Word) Ingawa huenda watu fulani wakaamua kuona siku moja kuwa takatifu kuliko siku nyingine, Biblia inaonyesha waziwazi kwamba Mungu hatarajii Wakristo washike Sabato ya kila juma.


“Sheria imekuwa mtunzaji wetu kutuongoza kwa Kristo, ili tutangazwe kuwa waadilifu kutokana na imani. Lakini sasa kwa kuwa imani imefika, sisi hatuko tena chini ya mtunzaji.”—WAGALATIA 3:24, 25

Ndugu msomaji, leo tumejikumbusha tena kuwa hatupo chini ya Sheria bali tuna haki ya kuzitunza siku zote za Juma na kumwabudu Mungu kila siku, na sio siku moja to ya Jumamosi.

Mungu awabariki sana,

Max Shimba



For Max Shimba Ministries

Wednesday, February 17, 2016

ASILIA MBILI YA YESU KRISTO “MUNGU NA BINADAMU”

Tokea Dunia ianze, hapajawai toke Mtu yeyote alieishi kama Yesu Kristo. Yesu ni mtu wa maana sana ambaye ni Mwokozi, Mungu katika Mwili “Emanueli” (Isaya 9:6). Yesu sio Nusu Mungu na Nusu Binadamu kama watu na au imani nyingi zinavyo sema. Yesu yeye ni Mungu na ni Binadamu kwa wakati mmoja. Kwa maneno mengine, Yesu alikuwa na asilia Mbili tofauti ambazo ni Mungu na Binadamu kwa wakati mmoja.

Biblia inasema kuwa, Yesu ni “Neno” ambaye ni Mungu na alikuwa kwa Mungu na akafanywa kuwa Mwili na kuishi nasi, soma Yohana 1:1 na 14. Hii inamaanisha kuwa, mtu huyu mmoja ambaye ni Yesu alikuwa ana asilia mbili za Mungu na Binadamu.

Hii asilia ya Mungu haikubadirika pale ambapo “NENO” lilipo kuwa Mwili (Yohana 1:1, 14). Badala yake, Neno liliunga ubinadamu (Wakolosai 2:9). Hivyo basi, Umungu wa Yesu Kristo haukuharibika na au badirika. Zaidi ya hapo, Yesu hakuwa mtu tu ambaye alikuwa na Mungu ndani yake au Mtu aliye fanya kazi ya Mungu pekee, la hasha, Yesu ni Mungu katika Mwili na ni sehemu ya Pili katika Utatu Mtakatifu. Biblia inatuambia katika Waebrania 1 aya ya 3kuwa: Mwana ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi Yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno Lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko mbinguni. Hivyo basi, asilia hizi mbili za Yesu Kristo haziwezi kuchanganywa (Eutychianism), vile vile haziwezi kuwa pamoja na kuwa Mungu-Mtu (Monophysitism). Hizi asili mbili ni tofauti na zinajitemea na wakati huohuo ni moja katika Yesu (person of Jesus). Huu muungano unaitwa Hypostatic Union.

Jedwari lifuatalo litakusaidia uone hizi asilia mbili za Yesu Kristo:
MUNGU
BINADAMU
Yesu anaabudiwa (Matayo. 2:2, 11; 14:33)
Yesu anamwabudu Mungu Baba (Yohana 17)
Yesu anaitwa Mungu (Yohana  20:28; Waebrania 1:8)
Yesu anaitwa Mtu/Binadamu (Marko 15:39; Yohana 19:5)
Yesu aliitwa Mwana wa Mungu (Marko 1:1)
Yesu aliitwa Mwana wa Adam (Yohana 9:35-37)
Anaombwa/prayed(Matendo ya Mitume7:59)
Anamwomba Mungu Baba (Yohona 17)
Yesu hana dhambi/sinless (1 Petro. 2:22; Waebrania 4:15)
Yesu alijaribiwa (Matayo. 4:1)
Yesu anafahamu kila kitu (Yohana 21:17)
Yesu alikuwa na Hekima (Luka 2:52)
Yesu anatoa uzima wa milele (Yohana 10:28)
Yesu Alikufa (Rom. 5:8)
Adhama zote za Mungu zipo ndani ya Yesu (Wakolosai 2:9)
Alikuwa na Mwili na Mifupa (Luka 24:39)

USHAHIDI ZAIDI WA ASILIA MBILI YA YESU

Mafundisho ya muungano wa Hypostatic ni ya “communication idiomatum” (Ni maneno ya Kilatini “Communication of properties”). Haya ni mafundisho ya adhama mbili za Yesu Kristo za Mungu na Binadamu zote zipo ndani ya Yesu Mtu “person of Jesus”. Hii inamaanisha kuwa, binadamu Yesu alikuwa na haki ya kusema kuwa “Alikuwa na utukufu na Baba Mungu kabla ya dunia kuumbwa soma Yohana 17:5), vile ile kudai kuwa  alitoka Mbinguni (Yohana 3:13), na kudai kuwa alikuwa kila mahalai “omnipresence (Matayo 28:20). Haya madai yote ya Yesu ni adhama za Mungu na kuwa yeye Yesu alikuwanayo.
Moja ya Makosa makubwa sana yanayo fanywa na wasio Wakristo ni kushindwa kwao kuelewa kuwa Yesu alikuwa na ASILIA MBILI. Kwa mfano, Mashahidi wa Yehova wao wanamwangali Yesu kama Binadamu na kupuuza adhama zake za Umungu. Mara zote wao hutumia zile aya ambazo zinakiri Ubinadamu wa Yesu na kuzipambanisha na aya ambazo zinasema kuwa Yesu ni Mungu. Kwa upande mwingine, Masayantisti wa Kikristo wao hufanya kinyume chake. Wao wana angalia zaidi upande wa Yesu ni Mungu na kusahau kuwa, Yesu alikuwa Binadamu vile vile.

Ili kumwelewa Yesu vyema, basi kila mafundisho ambayo yanamuhusisha Yesu, hayana budi kuzumgumzia Yesu kama Mungu na Yesu kama Binadamu. Hizo asilia Mbili ni zake. Kumbe ndio maana Yesu katika Luka 2:52 inasema: Naye Yesu akakua katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu. Na wakati huo huo alikuwa kila kitu “omniscient” Soma Yohana 21:17. Yesu ni Neno la Mungu aliye kuwa Mwili/Binadamu (Yohana 1:1, 14).
Zaidi ya hapo, Biblia inamhusu Yesu (Yohana 5:39. Mitume wote walimtabiri Yesu (Matendo ya Mitume 10:43). Mungu Baba anatoa ushahidi kuhusu Yesu, Soma Yohana 5:37; 8:18. Roho Mtakatifu naye anato Ushahidi kuhusu Yesu, Soma Yohana 15:26. Kazi zake Yesu nazo zinashuhudia kuhusu Yesu Soma Yohana 5:36; 10:25. Makundi ya watu nayo yanashuhudia kuhusu Yesu, Soma Yohana 12:17. NA YESU anajishuhudia mwenyewe Soma Yohana 14:6 ; 18:6.
Kuna aya nyingine nyingi ambazo zinamshuhudia Yesu kuwa ni Mungu nazo ni
Yohana 10:30-33; 20:28; Wakolosai. 2:9; Wafilipi. 2:5-8; Waebrania 1:6-8; na 2 Petro. 1:1.
1 Timoteo 2:5 inasema , " Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani, mwanadamu Kristo Yesu, 6. aliyejitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wanadamu wote, jambo hili lilishuhudiwa kwa wakati wake "   Hivi sasa, kuna Mtu Mbinguni ambaye yupo katika kiti cha Enzi. Yeye ni Mpatanishi wetu kwa Mungu Baba (1 Yohana 2:1). Ni Mwokozi wetu (Tito 2:13). Ni Bwana wetu (Warumi 10:9-10) Huyo Mtu anaitwa YESU.
Hakika Yesu Ni Mungu.
Kwa Maswali zaidi wasiliana nasi katika maxshimbaministries@gmail.com
Imeletwa kwenu na Max Shimba
Kwa Max Shimba Ministries Org.

@2015, April.  

JIBU KWA WASABATO KUHUSU KUTUNZA SIKU YA SABATO KATIKA UFALME MPYA WA MUNGU - ISAYA 66 AYA YA 22 NA 23

Ndugu msomaji,

Leo nitajibu hii hoja kuitunza siku ya Sabato katika Ufalme Mpya wa Mungu. Hebu tusome kwanza aya wanazo zitumia kusaidia hoja ya Sabato katika Ufalme Mpya wa Mungu.
ISAYA 66: 22-24
22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. 
23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana. 
24 Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.

Wasabato-SDA wamekuwa wakitumia aya ya 22 na 23 ya Isaya Sura ya 66 kuwa Sabato ni ya milele. NUKUU “22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. 23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.” 

Hoja hapa inakuja kwasababu katika hizi aya pamezungumzia pia Mbingu Mpya na Dunia Mpya, ambazo zimetajwa vile vile na Yohana katika kitabu cha Ufunuo, kwamba tutakuwa tunatunza Sabato. Lakini ikumbukwe kuwa katika aya hizi hizi pamesemwa vile vile kuhusu “MWEZI MPYA” Sasa kifikra lazima tujiulize swali hili: Je, kwanini hatutunzi siku ya MWEZI MPYA? Je, tutakuwa tunatunza MWEZI MPYA katika Dunia Mpya na Mbingu Mpya?
Swali la Kwanza nimeliweka na limekuja kwababu ya wazo yakinifu la Mwezi Mpya kuwepo pamoja na Sabato katika aya ya 23.
Sababu ya Wasabato kutumia hizi aya “22-23” ni kulinda dai au hoja yao ya kuitunza Sabato sasa na baadae. Hili ni kosa, kwasababu Isaya 66: 22-23 haizungumzii kuitunza Sabato sasa, LASIVYO, inatubidi kuitunza na siku ya MWEZI MPYA, sasa. Je, Wasabato wanaitunza siku ya MWEZI MPYA?

Swali la pili ni la kushangaza kidogo, na kuna mambo kadhaa ya muhimu lazima tuyawekee umaanani. KWANZA: Neno ambalo ni tafsir ya “mwezi mpya” katika Kihebrania ni “CHODESH” likimaanisha MWEZI. Hili neno halikuwa na maana ya watu washerekee MWEZI MPYA. Kwa mara ya kwanza lilitumika katika Kitabu cha Mwanzo 7 aya ya 11. , likiwa na tafsir ya “Mwezi”, zamani zaidi kabla ya chodesh kuwa sikukuu ya Wayahudi katika taifa la Israel.
Zaidi ya hapo, neno “mbingu mpya” na dunia mpya” linatupa mwanga kuwa mpango wa Mungu ni kurejesha kila kitu kama ambavyo alitaka kiwe kabla ya dhambi kuingia duniani kama ilivyo semwa kwenye Sura mbili za kitabu cha Mwanzo.  Mfalme mwenye hekima anatuambia kuwa Mhubiri 3:  14 Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye. 

Na katika Sura ya kwanza ya Mhubiri 1: 4 inasema: 4 Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima. 
Iwapo unaamini kuwa Dunia itakuwa milele au la, hapa jambo la muhimu ni hili” Mungu atarejesha kila kitu na kuwa sawa kama pale mwanzo kabla ya dhambi kuingia duniani”
Matendo ya Mitume 3: 20-21 inasema: 20 apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani; 
21 ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu. 
Kwa maneno mengine, kila kitu kitarudishwa na kuwa thabiti kama pale mwanzo. Ushahidi zaidi ni yale maono ya Yohana ya Mbingu Mpya na Dunia Mpya. UFUNUO 22. Utagundua hata Mti wa Uzima ambao wakati Fulani ulikuwa katika Bustani ya Edeni (Mwanzo 2:9), umetajwa hapo.

Ufunuo 22:2  katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. 
Hapo mwanzo tumekutana na mambo mengi, moja wapo ikiwa ni Siku ya Saba Sabato (Mwanzo 2:1-3). Ndio maana hatushangai kuwa, Nabii alisema kuhusu Sabato bado ipo hata baada ya dhambi kuingia, kwa marejesho ya kila kitu ikajumlisha na mwanzo wa Siku ya Saba. Hata hivyo, tunasoma kuhusu jinsi dunia ya kwanza katika Mwanzo 1 na 2, na hatusomi kitu chechote kile kuhusu shereza za MWEZI MPYA. Haikutajwa hiyo sherehe kabisa, je, hii ni kwanini? Jibu lako utalipata katika Ufunuo 22: 2

Ufunuo 22: 2 inasema: katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. 
Kumbuka kuwa neno la MWEZI MPYA linamaanisha “mwezi” na tunapo linganisha maneno ya Isaya na ya Yohana, tunajifunza kuwa maneno ya mwezi mpya kwa mwezi imaanisha ni mkusanyiko wa Watakatifu, mara moja kwa mwezi, kwasabu ya kula mti wa uzima.  Hivyo, jibu kwa swali letu kama Mwezi Mpya utakuwepo katika dunia mpya, jawabu ni NDIO.  Ingawa sababu ya kukutana katika mwezi mpya ni kula mti wa uzima. Hivyo, sababu ya kusherekea Sabato itabadilika na sio kusherekea kila wiki kama ilivyo semwa katika Kutoka 20:11,  Hapa tutasherekea kuumbwa kwa dunia mpya, ndio maana Isaya alisema kuhusu MBINGU MPYA  na DUNIA MPYA –AMBAYO NITAIFANYA Isaya 66:22.
Isaya aliona mwezi mpya katika maono yake kama marejesho ya kila kitu katika ukamilifu wake, hususan Yerusalemu, na tunajua kuwa kutakuwa na Yerusalemu mpya. Kuona kwake kwa mwezi mpya au mwezi, ni sambamba na Yohana alipo ona kurejeshwa kwa mji (Ufunuo 22:20) hii ndio maona ambayo Isaya aliyaona katika aya ya 22-23 ya Sabato ya uumbaji, pamoja na kukutana kwa watakatifu wote, mara moja kwa mwezi, kufurahi na Bwana na kula Mti wa Uzima.
 HOJA:
Sasa tuendelee na aya ya 24 ya Isaya 66 inasema 24 Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.
Hii aya inaweza kujibu zaidi hoja ya SDA, KATIKA AYA YA 15 ya Isaya 16, INATUAMBIA KUWA Bwana Mungu “Maana Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto. Na katika aya ya 16 anasema Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi. 
Wakristo wengi wanaamini kuwa hizi aya zinazungumzia kuja kwa Bwana kwa mara ya pili, au kuja kwa Bwana na watakatifu wakati wa Milenium.
Je, kwanini hatutunzi siku ya MWEZI MPYA?
Je, tutakuwa tunatunza MWEZI MPYA katika Dunia Mpya na Mbingu Mpya?
Je, Adam na Hawa walisherekea Sabato?

Hivyo basi, leo tumejifuza kidogo kuhusu Isaya 66 aya ya 22 na 23 na kijibu hoja ya Wasabato kuhusu umilele wa kuitunza Sabato.
Mungu awabariki sana.
Max Shimba

For Max Shimba Ministries Org.

Contradictions in the Quran: A Theological and Textual Examination

Contradictions in the Quran: A Theological and Textual Examination By Dr. Maxwell Shimba, Shimba Theological Institute Introduction Muslims ...

TRENDING NOW