Wednesday, February 17, 2016

JIBU KWA WASABATO KUHUSU KUTUNZA SIKU YA SABATO KATIKA UFALME MPYA WA MUNGU - ISAYA 66 AYA YA 22 NA 23

Ndugu msomaji,

Leo nitajibu hii hoja kuitunza siku ya Sabato katika Ufalme Mpya wa Mungu. Hebu tusome kwanza aya wanazo zitumia kusaidia hoja ya Sabato katika Ufalme Mpya wa Mungu.
ISAYA 66: 22-24
22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. 
23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana. 
24 Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.

Wasabato-SDA wamekuwa wakitumia aya ya 22 na 23 ya Isaya Sura ya 66 kuwa Sabato ni ya milele. NUKUU “22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. 23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.” 

Hoja hapa inakuja kwasababu katika hizi aya pamezungumzia pia Mbingu Mpya na Dunia Mpya, ambazo zimetajwa vile vile na Yohana katika kitabu cha Ufunuo, kwamba tutakuwa tunatunza Sabato. Lakini ikumbukwe kuwa katika aya hizi hizi pamesemwa vile vile kuhusu “MWEZI MPYA” Sasa kifikra lazima tujiulize swali hili: Je, kwanini hatutunzi siku ya MWEZI MPYA? Je, tutakuwa tunatunza MWEZI MPYA katika Dunia Mpya na Mbingu Mpya?
Swali la Kwanza nimeliweka na limekuja kwababu ya wazo yakinifu la Mwezi Mpya kuwepo pamoja na Sabato katika aya ya 23.
Sababu ya Wasabato kutumia hizi aya “22-23” ni kulinda dai au hoja yao ya kuitunza Sabato sasa na baadae. Hili ni kosa, kwasababu Isaya 66: 22-23 haizungumzii kuitunza Sabato sasa, LASIVYO, inatubidi kuitunza na siku ya MWEZI MPYA, sasa. Je, Wasabato wanaitunza siku ya MWEZI MPYA?

Swali la pili ni la kushangaza kidogo, na kuna mambo kadhaa ya muhimu lazima tuyawekee umaanani. KWANZA: Neno ambalo ni tafsir ya “mwezi mpya” katika Kihebrania ni “CHODESH” likimaanisha MWEZI. Hili neno halikuwa na maana ya watu washerekee MWEZI MPYA. Kwa mara ya kwanza lilitumika katika Kitabu cha Mwanzo 7 aya ya 11. , likiwa na tafsir ya “Mwezi”, zamani zaidi kabla ya chodesh kuwa sikukuu ya Wayahudi katika taifa la Israel.
Zaidi ya hapo, neno “mbingu mpya” na dunia mpya” linatupa mwanga kuwa mpango wa Mungu ni kurejesha kila kitu kama ambavyo alitaka kiwe kabla ya dhambi kuingia duniani kama ilivyo semwa kwenye Sura mbili za kitabu cha Mwanzo.  Mfalme mwenye hekima anatuambia kuwa Mhubiri 3:  14 Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye. 

Na katika Sura ya kwanza ya Mhubiri 1: 4 inasema: 4 Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima. 
Iwapo unaamini kuwa Dunia itakuwa milele au la, hapa jambo la muhimu ni hili” Mungu atarejesha kila kitu na kuwa sawa kama pale mwanzo kabla ya dhambi kuingia duniani”
Matendo ya Mitume 3: 20-21 inasema: 20 apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani; 
21 ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu. 
Kwa maneno mengine, kila kitu kitarudishwa na kuwa thabiti kama pale mwanzo. Ushahidi zaidi ni yale maono ya Yohana ya Mbingu Mpya na Dunia Mpya. UFUNUO 22. Utagundua hata Mti wa Uzima ambao wakati Fulani ulikuwa katika Bustani ya Edeni (Mwanzo 2:9), umetajwa hapo.

Ufunuo 22:2  katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. 
Hapo mwanzo tumekutana na mambo mengi, moja wapo ikiwa ni Siku ya Saba Sabato (Mwanzo 2:1-3). Ndio maana hatushangai kuwa, Nabii alisema kuhusu Sabato bado ipo hata baada ya dhambi kuingia, kwa marejesho ya kila kitu ikajumlisha na mwanzo wa Siku ya Saba. Hata hivyo, tunasoma kuhusu jinsi dunia ya kwanza katika Mwanzo 1 na 2, na hatusomi kitu chechote kile kuhusu shereza za MWEZI MPYA. Haikutajwa hiyo sherehe kabisa, je, hii ni kwanini? Jibu lako utalipata katika Ufunuo 22: 2

Ufunuo 22: 2 inasema: katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. 
Kumbuka kuwa neno la MWEZI MPYA linamaanisha “mwezi” na tunapo linganisha maneno ya Isaya na ya Yohana, tunajifunza kuwa maneno ya mwezi mpya kwa mwezi imaanisha ni mkusanyiko wa Watakatifu, mara moja kwa mwezi, kwasabu ya kula mti wa uzima.  Hivyo, jibu kwa swali letu kama Mwezi Mpya utakuwepo katika dunia mpya, jawabu ni NDIO.  Ingawa sababu ya kukutana katika mwezi mpya ni kula mti wa uzima. Hivyo, sababu ya kusherekea Sabato itabadilika na sio kusherekea kila wiki kama ilivyo semwa katika Kutoka 20:11,  Hapa tutasherekea kuumbwa kwa dunia mpya, ndio maana Isaya alisema kuhusu MBINGU MPYA  na DUNIA MPYA –AMBAYO NITAIFANYA Isaya 66:22.
Isaya aliona mwezi mpya katika maono yake kama marejesho ya kila kitu katika ukamilifu wake, hususan Yerusalemu, na tunajua kuwa kutakuwa na Yerusalemu mpya. Kuona kwake kwa mwezi mpya au mwezi, ni sambamba na Yohana alipo ona kurejeshwa kwa mji (Ufunuo 22:20) hii ndio maona ambayo Isaya aliyaona katika aya ya 22-23 ya Sabato ya uumbaji, pamoja na kukutana kwa watakatifu wote, mara moja kwa mwezi, kufurahi na Bwana na kula Mti wa Uzima.
 HOJA:
Sasa tuendelee na aya ya 24 ya Isaya 66 inasema 24 Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.
Hii aya inaweza kujibu zaidi hoja ya SDA, KATIKA AYA YA 15 ya Isaya 16, INATUAMBIA KUWA Bwana Mungu “Maana Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto. Na katika aya ya 16 anasema Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi. 
Wakristo wengi wanaamini kuwa hizi aya zinazungumzia kuja kwa Bwana kwa mara ya pili, au kuja kwa Bwana na watakatifu wakati wa Milenium.
Je, kwanini hatutunzi siku ya MWEZI MPYA?
Je, tutakuwa tunatunza MWEZI MPYA katika Dunia Mpya na Mbingu Mpya?
Je, Adam na Hawa walisherekea Sabato?

Hivyo basi, leo tumejifuza kidogo kuhusu Isaya 66 aya ya 22 na 23 na kijibu hoja ya Wasabato kuhusu umilele wa kuitunza Sabato.
Mungu awabariki sana.
Max Shimba

For Max Shimba Ministries Org.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW