Tuesday, June 21, 2016

UTHIBITISHO: ADAM NA HAWA WALITUMIA LUGHA YA KIEBRANIA NA SIO KIARABU


Ndugu msomaji,
Katika somo letu hili, tutajifunza na kujibu swali kuhusu; ni lugha ipi Adam na Hawa walitumia wakati wakiwa katika Bustani ya Edeni?
Tunaweza kuthibitisha kuwa Adam na Hawa walitumia Kiebrania kwasababu ya majina mawili ambayo Adam alimpa Hawa ambayo yanaweza kuwa yakinifu pekee katika lugha ya Kiebrania. Adam alimuita Hawa jina la “ISHA” ikiwa na maana ya MWANAMKE kwasabau ya kuwa alitoka kwa “ISH” ikiwa na maana ya MWANAUME , zaidi ya hapo, Adam alimuita mkewe “CHAVA” [HAWA] ikiwa na maana ya mama wa watu wote “CHAI” [UHAI].
Zaidi ya hapo, jina la ADAM linatokana na neno la Kiebrania “ADAMAH” likimaanisha “udongo”, hili jina linathibitisha kuwa Mungu alimuumba Adam kutoka kwenye udongo, kama ambavyo Biblia inasema katika Kitabu cha Mwanzo Mlango 2 na aya ya 7. Hivyo basi, tokea wakati wa Adam na Hawa mpaka wakati wa Mnara wa Babeli, watu wote walitumia lugha ya Kiebrania. Bereshet 2:23, 3:20, Midrash Bereshet Rabbah 38
Wasomi wa Kiyahudi na wa Kikristo wanaendelea kuthibitsiha kuwa Lugha ya Kiebrania ndio ilikuwa lugha ya kwanza, na majadiliano makali yalifanywa zamani na watafiti kama Dante Alighierl (1265-3121), Guillaume Postel (1510-1581) Claude Duret (1570-1611), Etienne Guichard (wakati huo huo wa ATHANASIUS Kircher (1602-1680) na Franciscus Mercurius van Helmont (1614-1698) wana sema kuwa, lugha ya Kiebrania ndio ilitumika na Adam na Hawa. Kwa mfano Mtaalam Guichard alisema kuwa neno la Kilatini “divider” likimaanisha tenganisha au kutenganisha limetokana na neno la Kiebrania la “batar” likimaanisha kukata katika sehemu mbili, hili neno lilifanana na la “tarab” ambalo lilikuja neno la Kilatini la “tribus” likimaanisha “kabila “tribe”
Hebu tuangalie ushahid mchache kutoka Biblia:
Matendo ya Mitume 26:14 Tukaanguka nchi sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya KIEBRANIA, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi? Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo.
Yohana 19: 17 Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa KIEBRANIA, Golgotha.
Matendo ya Mitume 22: 2 Waliposikia kwamba anasema nao kwa lugha ya Kiebrania wakazidi kunyamaza; akasema,
Kutoka 2:6 Akakifungua, akamwona mtoto, na tazama, mtoto yule analia. Basi akamhurumia, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania.
Katika kitabu cha Kutoka hapo juu, tunajifunza kuwa MUSA ANAITWA MTOTO WA KIEBRANIA “Eevriym in Hebrew” na katika kipindi chote watoto wa Kiisraeli waliitwa kama WAEBRANIA ambao ni watoto au wajukuu wa Ibrahim na Musa. Soma Mwanzo 10:24. Zaidi ya hapo, katika kitabu cha Mwanzo 14:13 tunasoma kuwa Ibrahim anaitwa Muebrania (Eevriy in Hebrew).
Huu ni ushahid tosha kuwa Lugha ya Mungu kwa Adam na Hawa ilikuwa ni Kiebrania na sio Kiarabu au lugha nyengine.
Je, Kwanini Mungu alitumia Kiebrani alipo zungumza na Adm na Hawa?
Kwanini Adam na Hawa walitumia Kiebrania walipo kuwa katika Bustani ya Edeni?
Hapa pana hitaji ufunuo wa hali ya kuu kufahamu kwanini Mungu alitumia lugha ya Kiebrania ambayo ni tofauti kabisa na Allah anaye tumia Kiarabu tu.
Kumbe sababu za Allah kutumia Kiarabu ni kupinga Mungu wa Biblia ambaye alitumia Kiebrani na kuwapinga Waisraeli ambao waliitwa wana wa KIEBRANIA.
References:
1. Merrill F. Unger, "Tower of Babel," Unger's Bible Dictionary, 1977 ed.: 115. (BCE - Before the Common Era, equivalent to BC)
2. J.I. Packer, Merril C. Tenney, William White, Jr., Nelson's Illustrated Encyclopedia of Bible Facts (Nashville: Thomas Nelson, 1995) 337.
3. Madelene S. Miller and J. Lane Miller, "Sumer," Harper's Bible Dictionary, 1973 ed.: 710.
4. Unger, "Scythian," 987.
5. Unger, "Egypt," 288.
6. William Smith, "Hebrew Language," Smith's Bible Dictionary, 1948 ed.: 238.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 12, 2016

Sunday, June 19, 2016

YESU ANAKIRI KWA MDOMO WAKE KUWA YEYE NI MUNGU

Ndugu zanguni, leo YESU anawajibu Waislam kwa mara nyingine tena kuwa yeye ni Mungu, "YESU NI MUNGU".
Hii aya hapa chini katika kitabu cha Ufunuo ni ya Yesu mwenyewee akiongea na Yohana. Yesu anakiri kuwa yeye ni Mungu. Hebu tuisome kwanza:
Ufunuo 21: 6 Yesu Akaniambia, “Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Yeye aonaye kiu nitampa kunywa kutoka katika chemchemi ya maji ya uzima bila gharama yo yote. 7 Yeye atakayeshinda atayarithi haya yote, NAMI NITAKUWA MUNGU WAKE, naye atakuwa mwanangu.
Mara nyingi kumekuwa na mtanashi kutoka Waislam kuwa eti Yesu hakuwai sema yeye ni Mungu. Mara zote wamekuwa wakidai kuwa, tuwaletee aya ambayo Yesu anasema yeye ni Mungu. Ingawa, Biblia imewajibu kuwa Yesu ni Mungu kutoka sehemu mbalimbali, lakini wamekuwa wabishi na kung'ang'ania waletewe aya, ili wabatizwe na kuwa Wakristo. Kwasababu Biblia imekamilika na haina shaka ndani yake. Leo Biblia inawajibu tena kuwa Yesu ni Mungu.
Aya ya 7 inasema kuwa, NUKUU: [Yeye atakayeshinda atayarithi haya yote, NAMI NITAKUWA MUNGU WAKE, naye atakuwa mwanangu.]
Yesu amekiri kuwa mtu yeyote yule atakaye urithi ufalme wake, basi ifahamike kuwa.
Moja: Yesu atakuwa Mungu wake
Pili: Wewe utakuwa Mwana wake.
Huu ni ushaidi mwingine kuwa Yesu ni Mungu. Waislam, ningependa mfahamu kuwa, Yesu ni Mungu kama ilivyo andikwa kwenye Ufunuo Sura 21 na aya ya 7.
Je, Upo tayari kumfuata Yesu ambaye ni Mungu? Kumbukeni kuwa, Yesu ndie Njia pekee ya kwenda Mbinguni. Dini haita wapeleka popote pale, lakini Yesu Kristo aliye hai ambaye sasa tunasoma kukiri kwake kuwa yeye ni Mungu, ndie njia pekee ya Uzima wa Milele.
Mpokee Yesu leo ili upate uzima wa milele.
Katika Huduma yake,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
Kwa Max Shimba Ministries Org 2014

MAOMBI YA KUSAMBARATISHA UCHAWI NA NGUVU ZA GIZA

Baba katika Jina la Yesu.
Laana zote nilizo tupiwa na wabaya wangu zimeshindwa kwa jina la Yesu na nazivunja na kuzisambaratisha kwa Damu ya Yesu. Mshindwe wote mnao tuma laana kwangu katika Jina la La Yesu.
Nawavunja na kuwaharibu na kuwakatakata Wachawi wote kwa damu ya Yesu.
Nasambaratisha kila neno la uovu lililosemwa juu yangu na famila yangu katika jina la Yesu.
Naharibu na kuisambaratisha madhabahu yenu mliyo fanyia kafara kwa damu ya Yesu.
Navunjavunja na kubomoa kila uovu na uchawi mnaonifanyia katika jina la Yesu.
Nairudisha misukule yote na majini yote yawarudie nyie na kuwalipa dhambi zote mnazo fanya katika jina la Yesu.
Naharibu kila uchawi, kila urogi, kila ndumba kila aina ya uovu ambao mnaufanya ili uniumize mimi na familia yangu katika jina la Yesu.
Nawateketeza kupitia damu ya Yesu Wachawi wote walio tumiwa kunitumia uchawi katika jina la Yesu.
Nawateketeza na kuwaharibu majini yote yaliyo tumwa kuja kufanya kazi hiyo waliyo tumwa na Wachawi katika jina la Yesu.
Nawateketeza na kuwauwa Makuhani wote ambao walienda kunishitaki kwa Wachawi ili waniharibie maisha, nawateketeza kupitia damu ya Yesu. Nawachoma kwa Moto wa Roho Mtakatifu katika Jina la Yesu.

SHEHE OMARI ASEMA QURUANI IMEJAA UCHAWI NA USHIRIKINA

SIRI YA WATOTO WA DAWA YAWEKWA HADHARANI NA SHEIKH OMARI
**********************************************************************************************
Sheikh Omari akifundisha hapo jana kanisa la Ufufuo na Uzima Kawe jijini Dar es salaam.
Shehe Omari akielezea jinsi alivyokuwa akitengeza watoto dawa na Dalili zake.
Kwasababu ya mila nyingi za kiafrika, watu wengi sana wamejikuta wakikimbilia kwa waganga pale wanapogundua kukosa mtoto. Wakati ninasomea falaki nilijifunza namna 11 jinsi ya kumpatia mwanamke mtoto hata kama hana uwezo wa kuzaa. Wakati nikiwa mkuu wa chuo cha kichawi pale temeke, tulikuwa tukifundisha watu kwa habari ya mimba za kijini.
Kwa wakati mteja alipokuwa ananijia kwaajili ya kuaguliwa, jinni ambalo lilikuwa ndani yangu lilikuwa linapanda ndani yangu na kwenda na kumwendea mteja alafu husoma taarifa ya mteja. Baada ya muda hutoka kwa mteja na kurudi kuja kuniambia mimi tatizo la mgonjwa huyo. Baada ya hapo nilikuwa namtajia mteja tatizo lake na kumfanya aniamini kuwa nitatatua tatizo lake hapo kila nitachomwambia lazima atafanya.
Baada yakuupata (win) moyo wa mteja, nilikuwa namwagiza vitu mbalimbali vya kufanya na kuniletea kwaajili ya uaguzi. Baada ya siku kadhaa lazima mteja huyo (ambao wengi wao walikuwa wanawake) atarudi kwaajili ya uaguzi. Katika namna hii ya kwanza ya kutengeneza mtoto wa dawa; tulikuwa tunaingiza jini ndani mwanamke na jinni yule alikuwa na uwezo wa kwenda kuiba mtoto katika nyumba ya mtu wa karibu na kumwingiza katika tumbo la mwanamke yule. Matokeo ya aina hii ya mtoto wa dawa ni uwezekano wa wazazi wakitanzania kujikuta wamezaa mzungu au mtoto mwenye sura ya jirani yake.
Madhara ya aina hii, husababisha ile mimba ambayo imeibiwa kwa mtu wajirani kupotea. Na ndio maana unaweza kumwona mtu alikuwa mjauzito lakini baada ya muda mimba ile ikapotea. Na ikitokea yule jini ameshindwa kumpatia mtoto kutoka katika maeneo yale, huamua kujitengenezea nyama kutoka katika mwili wa mwanamke. Matokeo ya aina hii mwanamke anasumbuliwa sana na mimba; unaweza kuta ni muda mfupi tu wa ujauzito lakini mwanamke huyo anakuwa ameshasumbuliwa sana na magonjwa mbalimbali.

KWANINI ALLAH AMBAE SIO YEHOVA ALIOGOPA KUYAAMRISHA MAJINI YAISIKILIZE TAURAT, ZABUR NA INJILI?

ALLAH ANASEMA KUWA MAJINI MACHAFU YALITUMWA KWA MUHAMMAD ILI KUSIKILIZA QURAN
ALLAH HUYO HUYO ALISEMA KUWA KILA WATU WALIPEWA KITABU CHAO. HAPO TEYARI KUNA SHAKA KWENYE QURAN YA MUHAMMAD AMBAYO SASA INAKABIDHIWA MAJINI MACHAFU.
Allah kasema katika Suratil Ahqaaf aya ya 29 mpaka 32, “
]وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِنْ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنْصِتُوا فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَى قَوْمِهِمْ مُنْذِرِينَ * قَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنْزِلَ مِنْ بَعْدِ مُوسَى مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَى طَرِيقٍ مُسْتَقِيمٍ * يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِي اللَّهِ وَآمِنُوا بِهِ يَغْفِرْ لَكُمْ مِنْ ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُمْ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ * وَمَنْ لا يُجِبْ دَاعِي اللَّهِ فَلَيْسَ بِمُعْجِزٍ فِي الأرْضِ وَلَيْسَ لَهُ مِنْ دُونِهِ أَولِيَاءُ أُوْلَئِكَ فِي ضَلالٍ مُبِينٍ[
Maana yake, “Na (wakumbushe) wakati tulipowaleta kundi la Majini kuja kwako kusikiliza Qurani. Basi walipoihudhuria walisema (kuambiana): “Nyamazeni! (Msikilize maneno ya Mwenyezi Mungu)” Na ilipokwisha somwa walirudi kwa jamaa zao kwenda kuwaonya. Wakasema “Enyi watu wetu! Sisi tumesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya (Nabii) Musa, kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake na kinachoongoza kwenye haki na kwenye njia iliyonyooka. Enyi kaumu yetu! Muitikieni Mlingani, (Muitaji) wa Mwenyezi Mungu na muaminini, atakusameheni (Mwenyezi Mungu) dhambi zenu na atakukingeni na adhabu iumizayo. Na wasiomuitikia Muitaji wa Mwenyezi Mungu, basi hao hawatamshinda (asiwapate) hapa katika ardhi, wala hawatakuwa na walinzi mbele Yake. Hao wamo katika upotofu ulio dhahiri.”
Na kisa kingine ni cha Majini waliosikia Qurani kutoka kwa Mtume S.A.W wakati alipokuwa akiwasalisha Masahaba wake Sala ya Alfajiri. Na hii ilikuwa bila ya yeye kuwa na habari mpaka Mwenyezi Mungu S.W.T. alipomjulisha. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Jin aya ya 1 na ya 2, “
]قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِنْ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا * يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَنْ نُشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا[
Maana yake, “Sema: “Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la Majini lilisikiliza (Qurani) likasema: “Hakika sisi tumesikia Qurani ya ajabu. Inaongoza katika uwongofu; kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote tena na Mola wetu.”
Makala haya yametolewa katika kitabu changu kiitwacho, "Hakika ya Majini."
MASWALI KUHUSU MAJINI:

ROHO, NAFSI NA MWILI

Ndugu msomaji,
Je, mwanadamu ni nani?
Kwa kifupi ninaweza kusema kuwa Mwanadamu ni Roho, ina Nafsi na inakaa ndani ya Mwili.
Ukisoma 1 Wathesalonike 5:23 Inatusaidia Kuona maeneo yote matatu ya mwanadam/mtu;
"Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi NAFSI ZENU na ROHO ZENU na MIILI YENU Mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo"
Hapa unaona Nafsi, Roho na Mwili vimetajwa kwenye hiyo aya.
ROHO NI NINI?
Roho ambayo inahusisha mambo ya Mungu.
Ni ile sehemu ya mtu yenye ufahamu wa Mungu, ambayo hufanywa hai na hutiwa nguvu na Roho wa Mungu wakati wa Wokovu. Kabla ya mtu Kuokoka, sehemu hii, haifanyi kazi kwa utimilifu kabisa kwa sababu ya dhambi. Dhambi huifanya kuondolewa nguvu ya kutenda kazi sawa sawa, kwa Amani na Roho ya Mungu. Lakini kupitia Ubatizo wa Roho Mtakatifu, mwanadamu hupokea nguvu ya kiroho, inayomwezesha kuishi maisha ya Kristo.
Roho inahusika na:-
i) Maombi na Ibada na Mungu,
ii) Ushirika na Mungu,
iii) Mapokezi ya karama za Roho,
iv) Vita vya kiroho,
v) Kuunda Mawazo na Ndoto,
vi) Dhamira, Kupambanua,
vii) Udadisi, Kuuliza,
viii) Ufahamu, Kutafsiri,
ix) Shuhuda kwa Wanadamu
NAFSI NI NINI?
Nafsi inahusika na mambo ya mtu.
Ni ile sehemu ambayo ina ufahamu wamtu mwenyewe au kiini cha ubinafsi wa mtu. Kazi yake ni:-
i) Kufikiri – Kutafakari, kuona
ii) Hisia – Kujisikia kuwa na tamaa na Upendo
iii) Utashi – Nia, Kuamua
MWILI NI NINI?

Saturday, June 18, 2016

Urithi wa Uislamu kutoka kwenye dini za kipagani za Uarabuni - sehemu ya 1





Allah alitokea wapi?

Uislamu unajinadi kwamba Allah ndiye Mungu yuleyule aliyejishughulisha ya Wayahudi tokea nyakati za Ibrahimu katika Agano la Kale. Je, jambo hilo ni kweli?

Uislamu ulianza na Muhammad kwenye miaka 600 baada Kristo. Je, kabla yake imani za Waarabu zilikuwaje? Je, yako mambo yoyote kutoka kwenye imani hizo ambayo yaliingia kwenye Uislamu? Kwa maneno mengine, je, Uislamu hauna upagani ndani yake?

Fuatana nami kwenye makala haya marefu yanayochambua chimbuko la Uislamu ili tuweze kuona iwapo upo uhusiano wowote kati ya Uislamu na upagani uliokuwa ukitawala miongoni mwa jamii za Waarabu kabla ya kutokea kwa Muhammad?


Asili Ya Allah

Jamii za wanadamu KOTE duniani zimekuwa na kawaida ya kujiuliza ni wapi ulimwengu huu umetokea, nini maana ya maisha na wapi watu huenda baada ya kufa. Matokeo yake, kila jamii ilifikia kuamini kuwa kuna aliye na nguvu (au walio na nguvu) kuliko wanadamu wote ambao ndio wanapaswa kuabudiwa na kuombwa msaada pale matatizo yanapotokea.

Hawa wenye nguvu wakajulikana kwa majina mbalimbali kwenye jamii tofauti. Vilevile, kila jamii ilianzisha utaratibu maalum wa kuwasiliana na hawa wenye nguvu, yaani miungu.

Lakini jambo moja ni dhahiri, kwamba UKIACHA JAMII YA WAYAHUDI PEKE YAO, jamii zote za wanadamu zilizobakia duniani – iwe ni Afrika, Ulaya, Asia, n.k. - zimeanzia kwenye ibada za kipagani.  Jamii hizi ziliabudu miungu mbalimbali. Na miungu hii iliwakilishwa na vitu kama vile milima, miti mikubwa, jua, mwezi, majoka makubwa, sanamu, wafalme, n.k. Kwa mfano, Warumi walikuwa na miungu kama vile artemi, jupiter, minerva, atlas, n.k. Tazama hapa. Wagiriki walikuwa na miungu kama vile chronos, dionysus, eros, ares, appolo, hermes, poseidon, n.k. Tazama hapa. Wahindi wana miungu kama vile durga, ganesha, garusha, brahma, n.k. Tazama hapa. Imani hizi za kipagani ziliweza hata kukua sana na kuenea maeneo mengi. Kwa mfano, imani ya ubudha ni imani ya kipagani lakini iliweza kuenea sehemu kubwa sana ya Asia – India, Japan, Sri Lanka, Uchina, n.k.

Kwa hiyo, jamii za Kiarabu, kama ilivyo kwa wanadamu wengine, vilevile hazikuwa tofauti. Jamii hizi nazo zilikuwa zina ibada zao za kipagani.

Waarabu walikuwa wakiabudu kile ambacho kinajulikana leo kama “star family”, au “familia ya nyota.” Tazama hapa. Inaitwa ‘familia ya nyota’ kwa sababu walichukulia miungu yao kwa tabia za kibinadamu. Mwezi ulichukuliwa kuwa ni mungu mwanamume na jua kama mke wa mwezi. Kisha hawa walizaa watoto. Kwa mfano, waliaminika kuwa walikuwa na mabinti watatu waliojulikana kwa majina ya al-lat, al-uzza na manat.

Ndiyo maana hata quran ikasema: Have you considered Al-Lat and Al- Uzzah, and another, the third (goddess) Manat? (Sura 53:19-20).

Yaani: Mmemwona Al-Lat na Al – Uzza, na mwingine, wa tatu (mungu mke) Manat?

Na hata Muhammad alikuwa akiabudu miungu hii kabla ya kuanzisha Uislamu. Tunasoma kutoka Hisham al-Kalbi, Kitab al-Asnam (Book of Idols), uk.17 kwamba:


'We have been told that the Apostle of Allah once mentioned al-Uzza saying, "I have offered a white sheep to al-'Uzza, while I was a follower of the religion of my people."

Yaani:
Tulishaambiwa kwamba Mtume wa Allah aliwahi kumtaja al-Uzza akisema, “Nilitoa kondoo mweupe kwa al-Uzza, wakati nilipokuwa nikifuata dini ya watu wangu.” Watu wake ni Waquresh.

Jina Allah linatokana na al-llahAl ni kama neno la Kiingereza, yaani article ‘a’; na ilah ni mungu. Kwa hiyo, al-ilah maana yake ‘a god’ au tu mungu kwa Kiswahili – maana Kiswahili hakina neno linalofanana na ‘a’.

Kwa sababu lugha huenda ikibadilika, ndipo jina hili likafupishwa na akuwa ‘allah’. Ni kama unavyoona kwenye Kiswahili utasikia mtu akisema ‘mambo ndo ivo bwana.’ Kumbe ‘ndo ivo’ ni kifupi cha ‘ndiyo hivyo’. Huenda miaka hamsini au mia ijayo watu hawatajua kuwa kumbe asili ya ‘ndo ivo’ ni maneno ‘ndiyo hivyo.’

Sasa, allah alikuwa ni nani? Allah alikuwa ni mungu mwezi, ambaye tumesema mke wake alikuwa ni jua na watoto (mabinti zao) walikuwa ni al-lat, al-uzza na manat. Hawa ndio walikuwa wakichukuliwa kuwa ni miungu wakuu miongoni mwa mamia ya miungu iliyokuwa ikiabudiwa na Waarabu kabla ya Uislamu – kipindi ambacho Waislamu hukiita ‘Jahiliyah’.

YESU NDIYE ATAKAYE HUKUMU WATU WOTE, WAFU NA WALIO HAI

Ndugu msomaji,
Kama ulikuwa haujui nani atahukumu walimwengu wote pamoja na imani na dini zote, basi fahamu kuwa Hakimu Mkuu ni Yesu Kristo.
Tuanze kwa kuthibitisha haya kwa kutumia aya za Biblia:
ZABURI 58:11 inasema kuwa: ‘Hakika yuko Mungu anayetawala katika dunia“. (UFUNUO 18;8 ) “Kwasababu hiyo, mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti na huzuni na njaanaye atateketeza kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu“. Tena ndiye atakaye ihukumu Dunia yote “Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana (YESU) hukumu yote“.
Neno la Mungu linatufundisha kuwa, atakaye toa hukumu ni Mwana ikimaanisha ni Yesu. Hivyo basi ni vyema umfuate Mwana ambaye atatoa hukumu na kuachana na miungu kama Allah wa Waislam.
Kumbe Muhammad na Waislam wote watahukumiwa na Yesu.
MATHAYO 25:31-32 inasema: “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu (YESU) katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake. Na mataifa yote yatakusanyika mbele zake, naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi”.
Yesu atayatoa Magugu "Waislam" na kuyatupa kwenye ziwa la moto. Ni vyema uanze kufuata mafundisho ya Yesu na kuachana na Allah aka Muhammad. Biblia inatuhakikishia kuwa Yesu ndie Hakimu Mkuu na sio Allah.
MATENDO 10:42 inasema: “Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudiaya kuwa huyu ndiye (Yesu) aliyeamriwa na Mungu awe mhukumu wa wahai na wafu” ( WARUMI 2:16 ) “Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu“.
Unaona sasa? Yesu ndie Hakimu Mkuu na sio Allah wa Waislamu. Muhammad na Waislamu wote watapiga goti mbele ya Yesu na kukiri kuwa Hakika Yesu ni Mungu.
2 TIMOTHEO 4:1 inasema “Nakuagiza mmbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakaye wahukumu waliohai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake’.
Kristo ndie atakaye hukumu waliohai na wafu kama Muhammad wa Waislam.
Ndugu nakushauri uchukue hatua na kumkubali Yesu hii leo. Yesu bado anakupenda na anataka kukuokoa kutoka dhambi.
Wasiliana nasi kama haufahamu nini cha kufanya ili uokoke.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

UTHIBITISHO WA KIMAANDIKO KUHUSU MWILI WA ALLAH

Ndugu zanguni,
Natanguliza kwa kusema huu ni Msiba Mkubwa sana kwa ndugu zetu kwa kupitia Adam wanao pinga kuwa Allah hana mfano.
Leo nitawawekea mifano kadhaa kama ushahid kuwa Allah ni kiumbe.
Haya, ungana nami moja kwa moja na tujifunze kuhusu huyu Allah kiumbe.
ALLAH ANA-VAA NGUO KAMA VIUMBE
الكبرياء ردائي والعظمة إزاري
Allah ansema katika Hadithi hii Qudsi "Ukuu ndi vazi langu la juu na utukufu ndio vazi langu la chini".
Sasa kama Allah anavaa nguo inamana kuwa Allah ana mwili kama viumbe?
Msiba huu ni mkubwa sana ndugu wasomaji.
Katika Hadithi nyengine Qudsi, Allah anasema: "….Na mja wangu hajikurubishi kwangu kwa kitu nikipendacho zaidi kuliko yale niliomfaradhishia juu yake. Na mja huwa anaendelea kujikurubisha kwangu kwa nawafil (ibada zisizo za lazima) mpaka nampenda: "فإذا أحببته كنت سمعه الذي يسمع به، وبصره الذي يبصر به ويده التي يبطش بها ورجله) (التي يمشي بها" Basi nikimpenda nakuwa (Mimi ndio) sikio lake analosikia kwalo, na jicho lake analoonea na mkono wake anaoshikia na mguu wake anaoendea."
Hapo Allah kesha kiri kuwa yeye ana masikio, mikono na macho.
ALLAH ANAKAA KWENYE KITI KAMA VIUMBE
Katika Sura 69:17 Surat al-Haaqqah tunasoma maneno haya:
“Na malaika watakuwa kandoni mwake na malaika wa namna nane watachukua kiti cha enzi cha Mola wako juu ya…”
Tena katika Sura 85:15 Syrat Buruj inamtaja Mungu wa Waislamu aitwaye Allah kuwa yeye ndiye mmiliki wa kiti cha enzi.
Swali ambalo napenda kuwauliza Waislamu wote Allah kumiliki kiti cha enzi. Je, kiti hicho anakifanyia nini? Huenda watu wakanishangaa. Nasema hivyo nikiwa na maana ya je, Allah naye anakaa katika kiti kama wakaavyo wanadamu? Je, ana miguu kama mwanadamu kama anakaa kama mwanadamu katika kiti cha enzi, basi haikosi hana tofauti na mwanadamu.
Angalia katika Sura ya 69: 44-45 Surat Al-haqqah twasoma.
“Na kama (mtume) angelizuia juu yetu baadhi ya maneno tu bila shaka tungalimshika kwa mkono wa kuume”.
Aya hii inaonesha kuwa Allah ana mkono wa kuume. Na kama Allah ana mkono wa kuume atakosaje mkono wa kushoto? Na kama Allah anasema atakosaje mdomo? Basi ondoeni dhana ya kwamba Allah hana mfano.
Ndugu wasomaji, teyari mmesha uelewa kuwa Allah ni kiumbe kama binadamu.
Mungu awabariki sana.
Katika Huduma yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

YESU KRISTO ATAMHUKUMU MUHAMMAD NA WAISLAM WOTE SIKU YA KIYAMA

HAKIKA YESU NI MUNGU
Ndugu msomaji:
Jambo hili si mzaha wala uzushi bali ni kweli; Yesu Kristo anakuja kuhukumu ulimwengu wote pamoja na Muhammad na Waislam wote. Yesu Kristo ametutamkia kwa kiywa Chake kwa kusema kwamba;
“Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote; ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba.” (Yohana 5:22,23)
Hukumu ya mwisho ambayo itakuja baada ya ufufuko. Mungu Baba, kupitia Yesu Kristo, atamhukumu kila mtu ili kuamua utukufu wa milele atakaoupokea. Hukumu hii itategemea utiifu wa kila mtu kwa amri za Mungu, ikiwa ni pamoja na kukubali kwake kwa dhabihu ya upatanisho Yesu Kristo ya kutulipia dhambi.
Baba amekabidhi hukumu yote kwa Mwana "Yesu Kristo": Yohana. 5:22.
Hapa tunajifunza kuwa atakaye toa hukumu ya nani kupokea taji la uzima wa Milele na nani kutumbukizwa Jehannam ni Yesu na sio Allah wa Waislam.
Sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo: Warumi. 14:10.
Sisi sote inamaanisha PAMOJA NA MUHAMMAD NABII WA ALLAH.
Wafu walihukumiwa kutokana na mambo yale yaliyokuwa yameandikwa: Ufunuo. 20:12.
Katika hukumu siku ya kiyama hatutegemei kumwona YEHOVA akija kuhukumu ulimwengu, bali, Yesu Kristo ndiye ajaye kuhukumu ulimwengu. Hii itakuwa hivyo ili WATU WOTE WAMHESHIMU Yesu sawa sawa na jinsi ambavyo wanamheshimu YEHOVA. Hapo ndipo viumbe vyote watathibitisha kuwa Yesu ni Mungu. Biblia Takatifu inasema kwamba:
“...kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA...” (Wafilipi 2:10,11)
Kama unataka kuokoka sasa hivi; Tafuta mahali palipo na utulivu, na usome kwa kutamka kwa kinywa chako sala ifuatayo: (ukiweza unaweza kupiga magoti unapoomba sala hii)
“Ee Mungu wangu ulie Mtakatifu. Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu yote. Ninatubu kwa dhati ya kweli kutoka rohoni mwangu. Naomba damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi yangu na mwili wangu. Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho Wako – Uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Nakuomba unifanye niwe vile utakavyo mimi niwe. Ahsante kwa kunisamehe na kwa kuniokoa. Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina."
Ikiwa umesoma sala hii kwa kukusudia kabisa na kwa imani, basi wewe umeokoka na dhambi zako zote zimesamehewa kabisa.
Damu ya Yesu iko juu yako sasa.
Mungu awabariki sana,
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

The Angelic Guardianship in Psalm 91:11: A Scholarly and Inspirational Exploration

The Angelic Guardianship in Psalm 91:11: A Scholarly and Inspirational Exploration By Dr. Maxwell Shimba Shimba Theological Institute A...

TRENDING NOW