Somo: MAPEPO
Mada ndogo: “Mtu anawezaje kupata mapepo?”
Lengo kuu: kuzijua mbinu zamapepo na kujilinda nazo
Lengo mahsusi: kudumu katika maombi ya vita kuzipinga roho za kipepo.
Kama tulivyokwisha kuona kuwa pepo ni roho wachafu wasio na mwili wala umbo wenye uwezo wa kuingia ndani ya kiumbe hai na kuchukua umbo na sura ya kiumbe huyo,pamoja na namna mwanadamu anavyoweza kujikuta katika uhusiano na pepo kupitia ibada za sanamu, sadaka, kuyafuga n.k. hapa tutaendelea kujifunza juu ya habari hizi ambazo kila mtu ni vema akizijua.
Wakati mwingine, mtu huweza kujikuta katika hali ya kuvamiwa bila yeye kujua. Ndugu yangu mpendwa, kuvamiwa na pepo si mpaka uugue au ujisikie kuwa dhaifu, pepo huweza kuharibu vitu vyako pole pole, mtu aliyevamiwa na pepo, anaweza kumvuruga awe na hasira tu, asifanikiwe katika shughuli zake tofauti kama vile biashara, masomo, kazi ya ajira, ufugaji,kilimo n.k.
Mtu aliyefungwa kwa namna hii, huambiwa kuwa nyota yake imechukuliwa, na hapa ndipo waganga wa kienyeji na waaguzi husema kuwa umetupiwa mikosi au mizimu imekasirika na kupaswa kutaaswa kwa kuogeshwa dawa, kuchanjwa au kunyweshwa; hatua hii ni hatari sana, kwa humfanya mwanadamu aingie mikataba mingine na mapepo, na hii huwa ni njia ya moja kwa moja, baada ya kipindi fulani, ile hali ya zamani hujirudia na kulazimika kwenda kwa mganga tena ili kukupatia dawa kali zaidi, bila kujiujua unakuwa unafanya mikataba migumu zaidi na kuzidi kuangamia; utakuta mtu anapewa miiko mikubwa mikubwa ambayo haitekelezeki na mwisho wake mtu huyu anakuwa mtumwa na miiko ya kipepo na anapoivunja basi humwangamiza kabisa.
Mpendwa, dawa iko kwa Yesu, jisalimishe leo uwe huru. Yeye pekee ndiye anayeweza kukuweka huru, ndiye anayeweza kuisafisha nyota yako, ndiye anayeweza kukuinua, njoo kwake leo, usikubali kudanganywa,Yesu ndiye yote ndani ya yote. Haleluya.
Zifuatazo ni njia kuu tano za mtu kupatwa na mapepo;-
Zifuatazo ni njia kuu tano za mtu kupatwa na mapepo;-




