Wednesday, August 10, 2016

MAPEPO NI NINI [SEHEMU YA NNE]


Somo: MAPEPO
Mada Ndogo: Dalili 10 za mtu mwenye mapepo.
Lengo kuu: kuyajua mapepo na kazi zake.
Lengo Mahsusi: Kila mtu kuweza kumpinga pepo na kazi zake zote kwa Jina la Yesu.
Bwana Yesu asifiwe sana,
Ndugu mpendwa, katika sehemu tatu zilizotangulia, tumejifunza maana, asili/ chanzo cha ,mapepo. Natumai umebarikiwa sana.
Haleluya! Ndugu mpendwa, napenda kukukarisha katika mwendelezo wa mafundisho yetu juu ya mapepo, ambapo kwasasa tutaangalia kwa kina tabia/dalili za mtu aliyevamiwa na mapepo.
Ni muhimu sana kujua hili. Tabibu mzuri, ni yule anaetibu ugonjwa anaoufahamu, hivyo ni muhimu sana, kujifunza habari hizi,ili kuweza kukabiliana na kila hali kwa usahihi wake.
Pamoja na dalili nyingine ambazo sitazitaja; kwapamoja tuzichunguze hizi zifuatazo:-
(a) Kuwa na nguvu nyingi. Kwa hali isiyo ya kawaida, mgonjwa aliyedhoofu na pengine kulala kwa muda mrefu akiwa hajiwezi, huweza kuwa na nguvu nyingi sana na za ajabu. (Luka 8:28, Marko 5:3&4, Luka 8:29, Matendo 9:15&16). Mtu huyu, huweza kuwa mkali sana, mgomvi na wakati mwingine huweza kuwa na uvutano kama umeme/shoti. Hujiamini sana na hukasirika zaidi anapowaona wanamaombi.
(b) Kujaa ujasili na kujiamini kupita kiasi. Mtu aliyevamiwa na pepo wachafu, hujiamini na kujiona shujaa; tukio hili hulenga kumchosha mwili, kuwaumiza wanaomuuguza na yeye mwenyewe. Anaweza kujiangusha bila sababu,kujiuma meno, kutafuna baadhi ya sehemu zake za mwili,kujipiga,kujiuma meno,kujikatakata n.k. (Mathayo 17:15, Marko 5:5). Pia,mapepom hutumia njia hii ili watu wamwogope washindwe namna ya kumsaidia mtu wa namna hii kwa kuhofia usalama wao, na kubaki kumwonea huruma tu.
(c) Huonesha maumivu hata anapojiumiza mwenyewe ila haachi kujiumiza. Hili hutokana na kuwa yeye hajitawali,bali hutawaliwa na kuongozwa na pepo wabaya. Huumizwa sana ndani kwa ndani,ila hulazimika kuendelea kufanya kile kitu kinachomuumiza. Mfano, kujikatakata,kujiangusha, kurukaruka n.k. (Marko9:20-22).

(d) Kutokwa povu mdomoni na kuzilai. Mtu aliye na mapepo, anakawaida ya kupoteza fahamu. Aghalabu, hutokwa povu mdomoni anapokuwa hajitambui (Marko9:20). Tukio hili,huwa ni lakumfanyia mazoezi mtu huyu katika maandalizi ya kumuua. Humhamisha kimazingara na kuanza kumchezea, wakati wingine mtu huweza kufa mara moja. Kifo cha namna hii,huwa si kifo halisi,bali huwa amahamishwa kimazingara/uchawi.
(e) Kunena/kuongea kupitia kinywa cha mgonjwa. Mapepo huweza kujitokeza na kunena hadharani,huku yakitoa amri au maelekezo juu ya mahitaji yao. Mengine hudai yanataka damu,yametumwa damu na baadhi ya mambo. (Mathayo 8:29-31,Marko5:5). Kitendo hiki cha kuilaghai,hupelekea uchonganishi,uhasama miongoni mwa jamii na hata maamuzi mabaya. Ndugu mpendwa,usimsikilize pepo,siku zote yeye ni mharibifu tu,hawezi kusema ukweli, na usifuate maelekezo yake,daima msikilize MUNGU.
(f) Wanaweza kutumika kama walimu makanisani kwa mafunuo, ndoto au maono. Hizi roho zinaweza kuleta mafunuo yanayolenga kuwaaminisha maumini kuwa ni mafunuo ya ki Mungu,ili kutaka kuwateka waumini na kuyaamini. Unapaswa kuwa makini sana katika hili. Kumbuka hata Sauli, alitoa unabii kipindi anateswa na roho wabaya. (1Timotheo4:1-5). Jiepushe kuyasikilza maneno yanayonenwa na mtu aliyepagawa na mapepo.
NB: mapepo yanaweza kuongea habari juu ya Yesu, ila tu, hayawezi kuongea habari sahihi juu yake. (Matendo 16:16&17, Marko1:24). Usikubali kuyasikiliza wala usiyahoji, yanadanganya tu, kumbuka , hata Yesu aliyakemea yaondoke tu,hata yalipotaka kuongea jambo lolote,yeye aliyaamuru yaondoke (Marko1:34)
(g) Humwamuru mtu kujitenga. Humtenga mtu na watu wengine. Humpeleka maeneo yasiyoyakawaida. Mfano misituni, vichakani ,mtoni, kwenye maziwa na bahari,makaburini nk (Luka8:27). Lengo ni kutaka huyu huyu mtu aendelee kuogopwa, lakini pia kumtenga na maeneo ambayo ibada na MUNGU wa kweli hutajwa.
Kumkimbuzia maeneo yaligubikwa na ibada za kipepo ili kuweka mikataba zaidi na kuendelea kumfunga.
(h) Kufanya mambo ya ajabu na aibu. Humwondolea utu wake na sitaha. Huishiwa ustaarabu, ndiyo maana anaweza kutembea uchi, kujiasaidia hadharani,kula vyakula vichafu, kufanya mambo yasiyofaa kwa furaha na kwa uhuru wote. Hii ni kwasababu, anakuwa ametengwa na jamii (Luka 8:27) hivyo huwa si sehemu ya mila na utamaduni wa jamii hiyo.
(i) Kuteswa kwa magonjwa ya mwili. Pepo akishamaliza kuingia, mtu huweza kumtesa kwa magonjwa ya kawaida kabisa ili kupumbaza wanaomuuguza mtu,wasijue chanzo cha tatizo.pia hutafutia kisababu cha kumuua.
Mfano wa baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na mapepo ni:-
Ububu (Marko 9:17)
Uziwi na ububu (Marko 9:25)
Upofu na Ububu (Mathayo 12:22)
Kupooza/ uwete (Matendo 8:7)
Kifafa (Marko 1:26,9:20, Luka 9:36) n.k. hufunga masikio kwa uziwi na kinywa kwa ububu ili kutomfanya mtu aweze kujieleza au kukili imani ya wokovu,hii ni kinga kwa mapepo ili kuendelea kumuweka chini ya himaya yao.
(j) Kuabudu miungu/ sanamu.(Walawi17:7,Torati 32:17,Ufunuo 9:20). Wakati mwingine,mtu alifungwa na mapepo, huweza kufundishwa ibada za sanamu na kuanza kuzifanya. Wengine husema, anamizimu ya kiganga (Walawi 20”27), na kujenga uhusiano na mizimu (1Samweli 15:23) kitendo kinachoplekea kuwa mchawi (Isaya 47:9-13,Matendo 19:18&19).
Ndugu yangu mpendwa, habari hizi ni nzito sana,na unapaswa kuzijua ili kujiepushwa nazo wewe na uzao wako na kizazi chako chote.
Swali la kujiuliza ni je, kufukuza pepo ndiyo uponyaji, au kuna uponyaji bila ya kufukuza pepo?
Kama tulivyoona, mapepo husababisha magonjwa, hivyo ili mgonjwa apone sharti pepo atoke.afukuzwe. kuna watu wanajidai eti wanatuliza mapepo, hakuna jambo kama hilo, kikubwa ni kumkemea pepo kwa Jina la Yesu, aondoke akae Roho Mtakatifu.
Mungu aendelee kukubariki na kukufunulia zaidi.
Endelea kujifunza pamoja nasi katika sehemu ya Tano, ili kujua hatua 8 katika kuyafukuza mapepo.
Somo:MAPEPO NI NINI? ENDELEA [SEHEMU YA TANO]

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW