Wednesday, August 10, 2016

MAPEPO NI NINI? [SEHEMU YA TANO]


Somo:MAPEPO
Mada Ndogo: Njia 8 za kuyashinda mapepo.
Bwana Yesu asifiwe sana,
Ndugu mpendwa, katika sehemu Nne zilizotangulia, tumejifunza maana,asili/ chanzo cha mapepo na dalili kuu za mtu alievamiwa na mapepo. Natumai umebarikiwa sana. Haleluya! Ndugu mpendwa, napenda kukukaribisha katika mwendelezo wa mafundisho yetu juu ya mapepo,ambapo kwasasa tutaangalia kwa kina mbinu/njia za kumshinda pepo.
Ndugu yangu mpendwa, kanisa la leo, liko katika mapambano makubwa sana. Upinzani mkubwa unatoka kwa ibilisi alie shetani, mwenye sifa kuu ya uharibifu.
Hatahivyo, Mungu ameliweka kanisa kwa wakati huu wa mashambulizi kwaajili ya kuukomboa ulimwengu. Amelifanya kanisa kama asikari wa mwamvuli ambaye hushushwa katikati ya eneo ambalo bado liko mikononi mwa adui, ila ikikusudiwa kupambana na hata kushinda. Kwa mantiki hiyo, si hoja tena juu ya kushinda kwa kanisa, bali daima linashinda na litaendelea kushinda.
Katika mwendelezo wa somo letu, leo tutaziangalia njia/uwezo wa kuyashinda mapepo.
Kwanza; Yesu alitoa mamlaka kwa kanisa juu ya mapepo (Marko 16:17). Uweza huu wa ajabu, Mungu ameutoa kwa watu wote wanaomwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wao (Yohana 17:20-23). Ujue, watu wengine wanateseka kwa kuwa hawajui, yule aliye ndani yao. Biblia inasema, aliyeko ndani ya aliyeokoka ni mkubwa mno, maana yake ni kuwa, anayashinda mapepo. Usikubali kuteswa na mapepo, kemea kwa jina la Yesu, lililo jina kuu kupita majina Yote, nawe utakuwa huru.
Pili; Mapepo huamriwa kwa jina la Yesu tu (Marko 16:17). Jina maagano na ahadi ni jina la Yesu tu. Usitumie jina lingine lolote lililo nje ya jina la Yesu. Ni jina la Yesu pekee huweza kuponya,kuokoa na kuhuisha, hata mapepo yanajua hivyo. Kutumia majina mengine ni sawa na kukosea anwani wakati wa kutuma barua, ni kweli barua itaenda ila usitegemee kupokea majibu uliyotarajia kwa kuwa barua haitaenda kwa mlengwa.
Tatu; Yafukuize kwa kutumia mamlaka uliyonayo kama ilivyoelezwa katika hoja ya kwanza. Usiyabembeleze. Tumia amri. Watu wengine hutumia majadiliano, huyafanyia sherehe, huyafukizia uvumba,udi na hata kuyachezea muziki wa asili. Ndugu yangu, waswahili wanasema” ukifanya urafiki na mkia wa fisi,utakufirisi” usikubali kukaa meza moja na mapepo, shetani habembelezwi, yatimue kwa mamlaka ya Jina la Yesu (Mathayo 12:28,Luka 11:20).

Nne; Usiyaruhusu kujieleza. Mpiganaji mzuri, hamuulizi adui ametoka wapi, yeye hushambulia hata kikosi kizimahukimaliza, kwa kuwa ni jasili na anajiamani, hababaishwi. Usikubalia kuhojiana na pepo, pepo ni waongo, watakudanganya kwa kutoa habari za uongo ili kulibomoa kanisa (mwili wa kristo) ili kuwatenganisha. Wataibua uadui kati yenu. We yaaamuru yaondoke, hata Yesu mwenyewe aliyaamuru tu yakaondoka (Luka 4:41,Marko 1:34).
Tano; Kwa kufunga na kuomba (Marko 9:29). Ndugu yangu mpendwa, kila mara, adui hushinwa kwa sala na kusoma neno. Jaama mamlaka ya mbinguni ili kumshinda ibilisi. Mtu asiye na maombi ni sawa na bunduki isiyo na risasi, na mtu asiyeomba anafanana na mlinzi anaetegea kazi yake, hutoa mwanya kwa mwizi kuvamia na kupora. Usikubali kuwa mlango wa ulegevu, daima jitahidi kuwekeza neno kwa wingi ili ujipatie maarifa zaidi.
Sita; Kuwa na Imani thabiti (Mathayo 17:19-20). Maombi pasipo imani, ni sawa na dhihaka. Ni bora ya majaribio, kuliko kudhihaki. Daima, kuwa jasili na umwamini Mungu na neno lake, ndipo litatimia kwako. Mtu asiyeamini, maombi yake hupeperushwa na mawimbi,hivyo hata majibu ya maombi yake hupeperushwa tu,kwakuwa hayana nguvu yoyote ndani yake.
Saba; Kwa Kumwamini Mungu (Marko 6:5&6), ukimwamini utamtegemea kwa kila jambo(Marko 9:23&24). Ukiwa na imani kwake, utakuwa na ujasili. Mwamini Mungu,ili athibitishe ujasili wako.
Nane; Kwa Muujiza. Mungu, ni Mungu wa maajabu, hufanya mambo yaliyojuu ya fahamu za mwanadamu. Hufanya mambo ya kushangaza, kuweza kufanya miujiza mikubwa mno,amabayo hata uwezo wa wasomi,hufikia kikomo. (Matendo 19:11&12), tunaonao nguo za Paulo zikifanya maajabu, ni muujiza wa nguo kutoa pepo. Ni kwa kuwa kuna upako unaokuwa sambamba na wamchao Bwana. Tegemea Miujiza kama uko kwenye uwepo muda wote. Kumbuka, imani wakati mwingine haionekani (Matendo 16:16-19), hivyo miujiza huithibitisha imani.
Swali la kujiuliza ni je, kila mtu anaweza kumtoa pepo?Jibu ni Hapana, si kila atakaye tumia jina la Yesu anaweza kutoa pepo, tena anaweza hata kujikuta yuko kwenye wakati mgumu zaidi kwa kuwa jina la Yesu lina uwezo wa ajabu, hivyo mtu anapaswa kulitumia kama silaha huku akihakikisha amejilinda vizuri mahali alipo (Matendo 16:13-16), mtu asiyejulikana katika ufalme wa Mungu, anapoliita jina la Yesu, huwa kama mtoto anaemlilia mama asiye wake, hata akimuonea huruma vipi, hawezi kuwa mama yake kabisa. Hii ni kwasababu, hawana utambulisho kwa Yesu, japo wanatumia jina lake(Luka 7:22&23).
Ifahamike kuwa, mtu ambaye hajamwamini Yesu,pengine ni mpagani kabisa, akiombewa, pepo hutii amri ya mwombaji na kuondoka, lakini kwa kuwa anayeombewa hajaamini, yule pepo huweza kurudi na kufanya makao tena ndani yake. Ni sawa na mpiganaji vitani anaevamia, na kupamabana na kuondoka bila kuacha walinzi. Adui, anakuwa na uwezo wa kurudi tena na kujimilikisha na hata akaweka ulinzi wake ulio imara zaidi kuliko ule wa awali (Mathayo 12:44&45).
Ndugu mpendwa, naimani unaendelea kubarikiwa kwa mafundisho yetu. Huu ndiyo utakuwa mwisho wa mada yetu. Usikose mada zijazo. Mungu akubariki.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW