Ndugu wasomaji,
Leo nitaielezea aya ya Yohana 17: 3 ambayo Waislam wamekuwa wakiitumia mara nyingi sana kudai kuwa eti, Yesu amekana kuwa yeye ni Mungu.
Waislam kwa kupitia mihadhara ya kidini na kwa kutumia vijarida mbali mbali wanatishia Umma wa Wakristo kuwa, Yesu ameukana Uungu. Je, hayo madai ya Waislam ni kweli? Je, hiyo aya ina la zaidi la kujifunza?
Ili uielewe Biblia vizuri, nilazima usome aya kadhaa ili upate kuelewa nini hasa Mungu anasema kupitia Neno lake. Hivyo basi, nimeweka aya ya 4 na ya 5 ili kufafanua nini hasa Yesu alikuwa anasema katika Yohana 17.
Ngoja niziweke aya zote hapa:
Yohana 17: 3 Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue Wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma.4 Nimekutukuza Wewe duniani kwa kuitimizaile kazi uliyonipa niifanye. 5 Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na Wewe kabla ulimwengu haujakuwako.
Yesu katika aya ya 5 [Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na Wewe kabla ulimwengu haujakuwako]
==> YESU anasema kuwa
1. Yeye aliishi kabla ya Ulimwengu kuwepo! Hapo panaanza kukupa mwanga halisi, wa nini Yesu alikuwa anasema na Yesu ni nani. Imani zote zinakiri kuwa aliye kuwepo kabla ya vitu vyote ni Mungu. Lakini katika aya ya 5, Yesu nae anadai kuwepo kabla ya uumbaji.
2. Yesu anaendelea kusema katika aya hiyo hiyo kuwa, yeye alikuwa na adhama ya Mungu -"UTUKUFU". Yesu anamwambia Mungu Baba kuwa, AMTUKUZE YESU KWA UTUKUFU ALIOKUWA NAO KABLA YA ULIMWENGU HAUJAKUWAKO.
Sasa, kama Yesu, sio Mungu na alikuwa Binadamu wa kawaida, aliwezaje kuishi kabla ya ulimwengu kuwepo? Zaidi ya hapo, kwanini Yesu anamwambia BABA YAKE AMTUKUZE? Yesu anatumia mamlaka gani hayo kudai Utukufu ambao sio wake bali ni wa Mungu pekee?