Eti Mungu wa Biblia ni Kahaba Kulingana na Isaya 23:17-18
Kama kawaida yao, Waislamu wanaendelea kudanganywa na walimu wao na kujipa matumaini kuwa wako kwenye njia ya uzima kutokana na kile wanachoamini kuwa Biblia si Neno la Mungu bali Quran ndiyo Neno la Mungu.
Kwa sababu wanaonekana ni watu wasiokuwa na utayari wa kuchunguza kile wanachoambiwa, basi wanaamini kila uongo na udanganyifu wanaopewa na kuubeba kama ulivyo na kuutangaza kwa ujasiri kabisa kana kwamba ndiyo kweli halisi!
Mojawapo ya uongo mkubwa na wa wazi unahusu aya zilizoko kwenye kitabu cha Isaya. Aya hizo zinasema hizi:
Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, Bwana ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia. Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa Bwana, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za Bwana, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari. (Isaya 23:17-18).

Waislamu hulishikilia andiko hili kwa nguvu na kwa kejeli nyingi wakisema, “Mnaona ninyi Wakristo’ Mungu wenu ni kahaba. Mungu gani wa kufuata huyu. Njoni kwa Allah.”
Kwa Wakristo wasio makini, maandiko ya aina hii yanawapotosha kabisa na kuwafanya waone Ukristo kuwa ni dini ya uongo kiasi cha wao kuamua kungia kwenye Uislamu – kumbe wasijue kuwa wanatoka uzimani na kutumbukia mautini. Uongo wa namna hii ni mwingi mno miongoni mwa Waislamu na unaenezwa kupitia intaneti, mihadhara, mabishano ya ana kwa ana, vitabu na kadhalika. Kuna mamia ya aya za Biblia ambazo wamezipotosha na ndizo watakazozitumia kukuondoa Yerusalemu Mpya. Je, wewe ni mmoja wa waliodanganywa na kunaswa?