Sunday, January 29, 2017

YESU ANAKUPENDA (SEHEMU YA KWANZA)

Image may contain: text
Swali la muhimu linazuka: Je, Mungu anampenda kila mmoja wetu?
Baadhi ya watu wanakubali kwamba Mungu anawapenda wanadamu kwa ujumla kama andiko la Yohana 3:16 linavyosema. Lakini wanahisi hivi: ‘Mungu hawezi kamwe kunipenda mimi.’
Shetani Ibilisi anataka sana tuamini kwamba Yesu hatupendi wala hatuthamini. Kwa upande mwingine, Yesu anatuhakikishia kuwa anamthamini kila mmoja wa watumishi wake waaminifu hata kama tunafikiri hatupendwi au hatuthaminiwi.
Kwa mfano, fikiria maneno ya Yesu kwenye Mathayo 10:29-31. Yesu alitoa mfano huu ili kuonyesha kwamba wanafunzi wake wana thamani: “Je, shore wawili hawauzwi kwa sarafu ya thamani ndogo? Na bado hakuna hata mmoja wao atakayeanguka kwenye ardhi bila Baba yenu kujua. Lakini nywele zenyewe za kichwa chenu zimehesabiwa zote. Kwa hiyo msiwe na hofu: nyinyi ni bora zaidi kuliko shore wengi.” Hebu fikiria jinsi wasikilizaji wa Yesu katika karne ya kwanza walivyoyaelewa maneno hayo.
Katika siku za Yesu, Shore alikuwa ndege wa bei rahisi sana aliyenunuliwa ili kuliwa. Mtu aliyelipa sarafu moja ya thamani ndogo sana, alipewa Shore wawili. Lakini kulingana na andiko la Luka 12:6, 7, baadaye Yesu alisema kwamba mtu aliyelipa sarafu mbili, alipewa shore watano badala ya shore wanne. Shore mmoja aliongezwa kana kwamba hakuwa na thamani yoyote. Huenda ndege hao hawakuwa na thamani machoni pa wanadamu, lakini Muumba aliwaonaje? Yesu alisema: “Hakuna hata mmoja wao [hata yule aliyeongezwa] hupata kusahaulika mbele ya Mungu.” Sasa huenda tumeanza kuelewa alilomaanisha Yesu. Ikiwa Mungu anamthamini sana shore mmoja, namna gani mwanadamu! Kama Yesu alivyosema, Mungu Baba anatujua vizuri sana. Kwani, hata nywele za kichwa chetu zimehesabiwa zote!
Kwa nini tunaweza kuwa na hakika kwamba Yesu hakutia chumvi aliposema kwamba nywele za kichwa chetu zimehesabiwa?
Huenda wengine wakafikiri kwamba Yesu alitia chumvi. Hata hivyo, hebu fikiria ufufuo. Ni lazima Mungu Baba awe anatujua vizuri sana ili aweze kutuumba upya! Anatuthamini sana hivi kwamba anakumbuka kila jambo, hata chembe zetu za urithi, kumbukumbu, na ujuzi wetu wote. Kichwa cha mtu huwa na nywele 100,000 hivi, kwa hiyo kuhesabu nywele za vichwa vyetu ni jambo rahisi sana ikilinganishwa na kukumbuka mambo hayo yote. Bila shaka, maneno hayo ya Yesu yanatuhakikishia kabisa kwamba Mungu Baba anamjali kila mmoja wetu.
Kisa cha Mfalme Yehoshafati kinaonyeshaje kwamba Mungu hutafuta mema ndani yetu ingawa sisi si wakamilifu?
Biblia hufunua jambo lingine linalotuhakikishia kwamba Mungu anatupenda. Yeye hutafuta na huthamini mema yaliyo ndani yetu. Kwa mfano, fikiria Mfalme Yehoshafati aliyekuwa mwema. Mfalme huyo alipotenda jambo la kipumbavu, nabii wa Mungu alimwambia hivi: “Kwa ajili ya hayo ghadhabu i juu yako itokayo kwa BWANA.” Ulikuwa ujumbe wenye kuogofya kama nini! Lakini ujumbe wa Mungu haukukomea hapo. Uliendelea kusema hivi: “Walakini yameonekana mema ndani yako.” (2 Mambo ya Nyakati 19:1-3) Kwa hiyo, hasira adilifu ya Mungu haikumzuia asione “mema” yaliyokuwa ndani ya Yehoshafati. Inatia moyo sana kujua kwamba Mungu wetu hutafuta mema ndani yetu hata ingawa sisi si wakamilifu.
Kumbuka kuwa Yesu anakupenda.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Max Shimba Ministries @ 2015

YESU AKUBALI KUITWA MUNGU

No automatic alt text available.
Ndugu msomaji,
Kwenye somo letu la leo ninakuletea uthibitisho Saba (7) wa Yesu kuitwa Mungu.
Bila ya kupoteza muda tuanze kusoma aya za Biblia.
1. THOMASO ANAMWITA YESU MUNGU
Tomaso mwanafunzi wa Yesu alisema kuhusu Yesu, “Bwana na Mungu wangu” (Yohana 20:28). 28 Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! 29 Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.
Baada ya Thomaso kumwita Yesu "Bwana na Mungu wangu", tunasoma kuwa Yesu anakubali na kumwabia, wewe Thomaso unameniona ndio unasadiki. Sasa Thomaso anasadiki nini? Kumbe Thomaso sasa anasadiki aliyo sema kuwa Yesu ni Bwana na Mungu.
2. YESU ANAITWA MUNGU MKUU NA WAFUASI WAKE
Tito 2:13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
KUMBE HATA WANAFUNZI NA WAFUASI WA YESU WALIMWITA YESU MUNGU tena MKUU. Tumesoma katika Tito Mlango wa 2 na aya ya 13 kuwa, Kristo Yesu ni Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Sasa wapi Yesu alikataa kuitwa Mungu Mkuu?
3. PETRO ANAKIRI KUWA YEYE NI MTUMWA WA YESU AMBAYE NI MUNGU WETU NA MWOKOZI WETU
2 Petro 1:1 Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, kwa wale waliopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika hali ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo.
Petro anajitambulisha kuwa yeye ni mtumwa wa Yesu Kristo ambaye ni Mungu wetu na Mwokozi wetu.
Kumbuka Petro aliishi WAKATI WA YESU NA ALIKUWA MMOJA WA WANAFUNZI WAKE. Kama Petro aliye kuwa na Yesu anamwita Yesu Mungu, je, wewe ni nani kupinga ukweli huu?
4. MUNGU BABA ANAMWITA MWANA - YESU "MUNGU"

THOMASO ANASADIKI UUNGU WA YESU

No automatic alt text available.
Tomaso mwanafunzi wa Yesu alisema kuhusu Yesu, “Bwana na Mungu wangu” (Yohana 20:28). 28 Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! 29 Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.
Baada ya Thomaso kumwita Yesu "Bwana na Mungu wangu", tunasoma kuwa Yesu anakubali na kumwabia, wewe Thomaso unameniona ndio unasadiki. Sasa Thomaso anasadiki nini? Kumbe Thomaso sasa anasadiki aliyo sema kuwa Yesu ni Bwana na Mungu.
Shalom.
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

YESU ANAITWA MUNGU MKUU NA WAFUASI WAKE

Image may contain: text


Tito 2:13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
KUMBE HATA WANAFUNZI NA WAFUASI WA YESU WALIMWITA YESU MUNGU tena MKUU.
Tumesoma katika Tito Mlango wa 2 na aya ya 13 kuwa, Kristo Yesu ni Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Sasa wapi Yesu alikataa kuitwa Mungu Mkuu?
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

YESU NI NJIA YA KWELI NA UZIMA

Image may contain: 1 person, text
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Yohana 14 :6
Kuna mambo mawili ya msingi kwenye huu mstari
1)Kutambua njia ya kweli
2)Kufahamu uzima unaopatikana katika hiyo njia.
Kama kuna njia ya kweli ni wazi kabisa ziko njia za uongo, na kama kuna uzima katika njia ya kweli ni wazi kwamba iko mauti kwenye njia ya uongo!
Kila njia ambayo imebeba mauti kwenye maisha yako ikafungwe kwa jina la Yesu, tunaifunga hiyo njia na kuiteketeza kwa jina la Yesu, Mungu akukumbuke siku ya leo, njia zote za mauti zikuachie.
Sema Amen kama unayo imani ndani ya Kristo Yesu

FURAHA KATIKA ROHO MTAKATIFU

Image may contain: text
Mara kadhaa nimesikia watu wakisema, “Nikienda kanisani najisikia raha kweli; lakini nikitoka, hali ya uzito wa moyo inanirudia tena.”
Ndugu, Biblia inasema: Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. (Rum. 14:17).
Hebu tujiulize swali hapa. Sehemu nyingine tunaposoma, Bwana anasema kwamba:
Ulimwenguni mnayo dhiki, lakini jipeni moyo. Mimi nimeushinda ulimwengu. (Yohana 16:33)
Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. (Mathayo. 10:22);
Jaribu halikuwapata ninyi isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu. (1Wakorintho10:13)
Hata mtume Paulo aliye mtume mkuu namna ile wa Bwana hakuweza kuyaepuka majaribu licha ya kuwa mwaminifu sana kwenye huduma aliyokabidhiwa. Lakini licha ya mateso mengi aliyopitia, ni yeye huyohuyo ndiye anayeongelea juu ya kuwa na furaha katika Roho Mtakatifu!
Paulo alipitia mambo magumu sana ambayo si wengi wanaweza kustahimili. Anasema: ...katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi. Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja. Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini; katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang‟anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo; katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi. (2Wakorintho 11:23-27). Hebu piga picha ya maisha hayo!!
Na hii hali ya kupita kwenye majaribu ndiyo hali halisi ya maisha ya kila mwanadamu! Majaribu si lazima yafanane kwa kila mtu lakini suala la msingi ni kwamba, hakuna mtu ambaye hayamkuti.
Inakuwaje basi Mungu anataka tuwe na furaha huku wakati huohuo anasema kuwa tutapita katika majaribu? Unapataje furaha huku unaumwa; huku huna mtoto; huku umefukuzwa kazi au umefukuzwa nyumbani kwenu?

JE, UNAISHI MAISHA YA AINA MBILI?

Image may contain: sky and outdoor
UTANGULIZI
Mwandishi mmoja alimwuliza Bwana Yesu: Katika amri zote ni ipi iliyo kuu? (Mk. 12:28).
Bwana alimjibu: Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. (Mk. 12:29-30). Hicho ndicho kipimo cha utimilifu wa utii.
Tunapoamua kumfuata Yesu, hata hivyo, hatukamiliki kwa siku moja. Maisha ya wokovu ni safari; ni mchakato wa kukua kuanzia uchanga, utu uzima, hadi utimilifu wa Kristo. (1 Pt. 2:2; Ebr. 5:12-14).
Mabadiliko ya ukuaji wetu kiroho hayafanyiki kwa juhudi zetu wenyewe – ni Roho Mtakatifu ndiye anayetubadilisha. Wajibu wetu ni kumpa nafasi ili aweze kufanya hivyo. Hiyo ni kusema kwamba, kazi ya Roho Mtakatifu ndani yetu inategemea mwenendo wetu na kiwango kile cha utayari tulio nao wa kutii neno lake; na pia bidii na shauku yetu ya kumtafuta Bwana. Yeye anasema: Nawapenda wale wanipendao na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. (Mith. 8:17).
KABLA YA KUOKOLEWA
Kabla ya kuokolewa tunakuwa ni watu wa duniani. Mawazo, maneno, na matendo yetu yanakuwa ni ya kidunia; maana dunia ina kawaida zake ambazo ni tofauti kabisa na zile za kimbingu.
Maandiko yanasema: Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu. (1 Kor. 6:9-11).
Vilevile imeandikwa: Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo ... (Gal. 5:19-21).
Huko ndiko ambako tunakuwa kabla ya kuamua kumpokea Yesu mioyoni mwetu na kumwachia utawala wa maisha yetu. Wakati tungali kule, maandiko yanasema: Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nao tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine. (Efe. 2:1-3).
BAADA YA KUOKOLEWA

Thursday, January 26, 2017

THOMASO ANASADIKI KUWA YESU NI MUNGU




Tomaso mwanafunzi wa Yesu alisema kuhusu Yesu, “Bwana na Mungu wangu” (Yohana 20:28). 28 Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! 29 Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.
Baada ya Thomaso kumwita Yesu "Bwana na Mungu wangu", tunasoma kuwa Yesu anakubali na kumwabia, wewe Thomaso unameniona ndio unasadiki. Sasa Thomaso anasadiki nini? Kumbe Thomaso sasa anasadiki aliyo sema kuwa Yesu ni Bwana na Mungu.

Saturday, January 21, 2017

Animal cruelty! Two TROGLODYTES MUHAMMADANS post photos of them cutting off a dog's ears ...and people are trying to bring them to justice

Some folks in Turkey are mobilizing into action after they saw shocking photos of animal cruelty perpetuated by two Turkish men. The men posted vicious online video and photos of them cutting off a dog’s ears. Internet vigilantes tracked down the men and are now working with law enforcement in Turkey to bring them to justice.

Photos: Man spotted butchering a zebra near Nairobi Highway


Photos of a man butchering a zebra in broad daylight next to Nairobi highway has shocked many. 
Mombasa County Government Watch posted the photos on Facebook yesterday and wrote:
Unconcerned man butchers a zebra in broad daylight on the busy Nairobi-Nakuru Highway. It seems illegal game meat which is unfit for human consumption is finding its way to the butcheries. A man in Naivasha was seen stashing zebra meat in paper bag.

Ancient Jewish Wedding Ceremony: “No man knows the day or hour, only the Father”

  The Ancient Jewish Marriage Rite: A Detailed Exposition of Betrothal, Preparation, and Consummation Dr. Maxwell Shimba Shimba Theological ...

TRENDING NOW