MUHAMMAD AWAAGIZA WAISLAM WOTE KUVAA VIATU WAKATI WANASWALI MSIKITINI
KUMBE KUVUA VIATU NI UTAMADUNI WA WAYAHUDI.
Ndugu msomaji,
Leo ningependa tujikumbushe na kujifunza kuhusu kusali na viatu katika nyumba za ibada. Hususan Msikitini.
Waislam mara nyingi wamekuwa wakiwashutumu Wakristo na kuwakejeli kuwa, eti wanasali na viatu Kanisani.
Je, Mtume wa Allah aitwaye Muhammad alivaa viatu alipo kuwa anaswali Msikitini?
Je, Mtume wa Allah aitwaye Muhammad alivaa viatu alipo kuwa anaswali Msikitini?
Hebu tuangalie ushahidi huu hapa:
Ukisoma kitabu cha Al-u-lu wal-marjan Uk. 179
14. Mlango:
Ruhusa ya kusali na Viatu.
325. Hadithi ya Anas Bin Malik (R.a) kutoka kwa Said Bin Yazid Al-Azid (r.a) amesema, Nilimuuliza Anas Bin Malik (r.a) “Hivi Mtume (s.a.w) alisali huku amevaa viatu vyake?” Akanijibu, “Ndiyo” (Bukhari, Hadithi N. 383, Juzuu ya 1)

Hapo tunamuona Muhammad akisali na Viatu, na mlango hapo umesema, Ruhusa ya kusali na Viatu, maana yake waislamu hapo wameruhusiwa kusali na Viatu, pia haikuishia hapo, Muhammad akasema tena kuwaambia Waislamu.
Ukisoma kitabu kinachoitwa “TAFSIRI YA BULUGH AL-MARAM MIN JAM’I ADILLATIL AHKAM
Ukurasa wa 101 Hadithi Na. 171
Abu Said (r.a) amesimulia: Mtume (S.a.w) amesema: “Ye yote miongoni mwenu atakapoenda msikitini kusali, basi atizame, akiona uchafu au najisi katika viatu vyake aondoe kisha aswali navyo”. Abu Dawud Ibnu Khuzaimah ameipa daraja ya Sahih.

*Murad wa kutwaharisha viatu:
Iwapo mtu amekanyaga najisi kwa kiatu, atakitwaharisha kwa kusugua chini mchangani*

Hapo kwa mtu mwenye akili zake timilifu, hawezi kukomaa na kuanza kuwalaumu Wakristo, eti kwa nini wana Sali na viatu? Wakati Muhammad mwenyewe, alisali huku amevaa viatu, na pia akawaambia waislamu wanapoenda kusali, basi watazame viatu vyao kama kuna najisi, basi wavisugue chini mchangani, labda waislamu watuambie wao kusali na viatu, ni Uviviu wa kusugua viatu mchangani? Au mazingira yao wanayoishi hayana mchanga?