Friday, February 10, 2017

MJUE MSAIDIZI ALIYETABIRIWA NA YESU

Image may contain: cloud and text


Na Mtumishi: Zacharia Maseke
Kabla YESU hajaondoka duniani, aliahidi kutuletea 'MSAIDIZI', Rejea YOHANA 16:7-8 👉 "Lakini mimi nawaambia iliyo kweli, yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo MSAIDIZI hatakuja kwenu, bali mimi nikienda zangu nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja huyo, atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu."👈
Sasa makafiri waislamu wanasema kuwa hapo YESU, Alitabiri ujio wa mtume Muhammad, wanadai kuwa mtume Muhammad ndiye MSAIDIZI ambaye BWANA YESU Aliahidi kumleta!
JE, NI KWELI MTUME MUHAMMAD NDIYE MSAIDIZI ALIYETABIRIWA NA YESU?
Fuatana nami katika somo hili, ili tuweze kumbaini huyo MSAIDIZI ni nani?👇👇👇
Basi, bila kupoteza wakati, awali ya yote napenda turejee maneno ya BWANA YESU, Akizungumza kuhusu huyo MSAIDIZI, Anasema 👉"Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa MSAIDIZI mwingine, 👍ILI AKAE NANYI HATA MILELE, ndiye ROHO wa kweli, ambaye ulimwengu HAUWEZI KUMPOKEA, Kwa kuwa HAUMWONI WALA HAUMTAMBUI, bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, Naye atakuwa NDANI yenu."👈
YOHANA 14:15-17
Hapo tunapata sifa za huyo MSAIDIZI, ambazo ni kama ifuatavyo:👇
1:MSAIDIZI ATAKAA NA SISI MILELE,
Hiyo ndio sifa ya kwanza ya MSAIDIZI, lazima akae na sisi milele. Je, mtume Muhammad yuko wapi sasa? Kama Muhammad ndiye huyo MSAIDIZI mbona amekufa ametuacha, kwa nini hakukaa na sisi MILELE? Hapo utagundua kuwa Muhammad sio MSAIDIZI, maana MSAIDIZI wetu hafi, YESU alisema 👉"Nami nitamwomba Baba, naye atawapa MSAIDIZI mwingine, ILI AKAE NANYI HATA MILELE".👈 YOHANA 14:16. Sasa mtume Muhammad alishakufa kitambo sana. 😥😳😢 Hivyo Muhammad hana sifa ya kuwa MSAIDIZI.

2: MSAIDIZI NI ROHO,
Wala Sio kiumbe cha kawaida kama mwanadamu. YESU alisema 👉"ndiye ROHO wa kweli, ambaye ulimwengu HAUWEZI KUMPOKEA, Kwa kuwa HAUMWONI..."👈 YOHANA 14:17. Rejea pia YOHANA 15:26 👉"Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo ROHO wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia"👈 Soma pia YOHANA 16:13,👉"Lakini yeye atakapokuja, huyo ROHO wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake"👈 Je, mtume Muhammad ni ROHO? Muhammad sio Roho, ila alikuwa mtu. Hivyo Muhammad hana sifa ya kuitwa MSAIDIZI.
3: MSAIDIZI HAONEKANI WALA HATAMBULIKI NA ULIMWENGU:
Hiyo ndio sifa nyingine ya MSAIDIZI. Haonekani kwa sababu ni Roho. Rejea YOHANA 14:17 👉"ndiye ROHO wa kweli, ambaye ulimwengu HAUWEZI KUMPOKEA, Kwa kuwa HAUMWONI WALA HAUMTAMBUI, bali ninyi mnamtambua..."👈 Sasa Je, Mtume Muhammad alikuwa HAONEKANI? Au Je ulimwengu haukumtambua Muhammad? Ukweli ni kuwa Muhammad alikuwa ANAONEKANA, maana alikuwa MWANADAMU na alitambulika na Ulimwengu. Kama Muhammad hakuwa anaonekana, Waislam thibitisheni leo, ili tujue ukweli. YESU pia aliwaambia wanafunzi, 👉"bali ninyi mnamtambua..." Kumbe MSAIDIZI wanafunzi walikuwa wanamtambua, sasa ukisema MSAIDIZI ni Muhammad, je wanafunzi wa YESU walikuwa wanamtambua mtume Muhammad? Walimuona wapi? Maana mpaka wanakufa, Muhammad hakuwepo. Hivyo Muhammad tena hana sifa ya kuitwa MSAIDIZI.
4:MSAIDIZI ANAKAA NDANI YETU:
Hii ndio sifa nyingine ya huyo MSAIDIZI, kwamba sharti akae ndani ya mioyo ya watu. Rejea YOHANA 14:17 👉"...bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, Naye atakuwa NDANI yenu"👈 Sasa ili mtume Muhammad awe MSAIDIZI, lazima uwepo ushahidi kuwa, Muhammad alikuwa anakaa ndani ya watu. Kitu ambacho hakipo kabisa! Maana mtume Muhammad hakuwahi kukaa ndani ya mioyo ya wanafunzi wa YESU. Kwanza atakaaje ndani yetu wakati alishakufa? Je marehemu aweza kukaa ndani ya mioyo ya wafuasi wa YESU? Hapa tena mtume Muhammad S.a.w amepoteza sifa ya kuitwa MSAIDIZI.
5:MSAIDIZI ALITUMWA NA MUNGU KWA JINA LA YESU:
Rejea YOHANA 14:26 👉"Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia."👈Sasa Ili Muhammad awe MSAIDIZI, lazima uwepo ushahidi kuwa alitumwa kwa jina la YESU, cha ajabu ni kuwa hakuna muislam anaeweza kukubali kwamba, mtume Muhammad alitumwa na Allah kwa jina la YESU. Hii inamfanya mtume Muhammad apoteze sifa ya kuitwa MSAIDIZI.
6:PIA MSAIDIZI ALITUMWA NA YESU KUTOKA KWA BABA:
YESU aliwaahidi wanafunzi kuwa atawatumia MSAIDIZI, rejea YOHANA 15:26, 👉"Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo ROHO wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia"👈soma pia LUKA 24:49 👉""Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu, LAKINI KAENI HUMU MJINI, hata mvikwe uwezo utokao juu."👈, Hakuna sehemu ambayo Muhammad amedai kuwa alitumwa na YESU, hata Waislam wenyewe hawakubali kwamba Muhammad alitumwa na YESU, wanaamini alitumwa na Allah. Kwa hiyo Muhammad siyo MSAIDIZI, maana HAKUTUMWA NA YESU. 😨😨😨😨
7: MSAIDIZI LAZIMA AMSHUHUDIE YESU:
Rejea YOHANA 15:26, 👉"Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo ROHO wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia"👈 Cha ajabu ni kuwa mtume Muhammad, anayedaiwa kuwa MSAIDIZI, hakuwahi kumshuhudia YESU, Ila alimshuhudia Mungu mwingine tu aitwaye Allah! Kwa sababu hiyo tena, Muhammad hawezi kamwe akawa MSAIDIZI, maana hakumshuhudia YESU.😊😊😊
8 :MSAIDIZI SHARTI AMTUKUZE YESU NA ATWAE MAFUNDISHO YA YESU AWAPE WATU:
Rejea YOHANA 16:13-14 👉 "Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari"👈 Ili mtume Muhammad awe MSAIDIZI, alitakiwa amtukuze YESU na atwae katika yaliyo ya YESU awapashe watu habari. Je Muhammad alifanya hivyo? HAPANA! Badala yake Mtume Muhammad alimtukuza Mungu mwingine anayeitwa Allah, Muhammad hakuwahubiri watu Mafundisho ya YESU, bali alihubiri mafundisho ya Allah, hivyo Muhammad hana sifa ya kuitwa MSAIDIZI.

9 :MSAIDIZI LAZIMA AWAFUNDISHE NA KUWAKUMBUSHA WANAFUNZI YOTE ALIYOSEMA YESU:
MSAIDIZI alitakiwa kufanya hivyo kuanzia kwa wanafunzi wa YESU, rejea YOHANA 14:26 👉 "Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia"👈 Sasa mtume Muhammad yeye alikuja kuzaliwa baadaye sana, wakati ambapo wanafunzi wa YESU walishakufa zamani sana, hakuwahi hata kukaa nao awafundishe na kuwakumbusha kile alichosema YESU. Na hata katika mafundisho yake, Muhammad hakuwahi kufundisha wala kukumbushia kile alichosema YESU, badala yake alikuja kupingana na YESU, mfano YESU alisema yeye ni MWANA WA MUNGU, Muhammad akaja kupinga, akasema Mungu hana Mwana. Hivyo basi Muhammad hana sifa ya kuwa MSAIDIZI
10: MSAIDIZI ILITAKIWA AJE ENZI ZA UHAI WA WANAFUNZI WA YESU, TENA WAKIWA BADO HAWAJATAWANYIKA YERUSALEMU:
YESU baada ya kufufuka katika wafu, aliwaambia WANAFUNZI wake, wasitoke YERUSALEMU, rejea MATENDO 1:4 👉"Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu"👈, Rejea pia LUKA 24:49, YESU anawaambia wanafunzi, 👉"Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu, LAKINI KAENI HUMU MJINI, hata mvikwe uwezo utokao juu."👈, Tukio la kuja kwa MSAIDIZI lilitokea YERUSALEMU, siku ya PENTEKOSTE, Ndipo MSAIDIZI alipowashukia wanafunzi, soma MATENDO YA MITUME 2:1-5 👉"
1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.
2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.
3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
5 Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu."👈 Hivyo ndivyo ahadi ya kuja kwa MSAIDIZI ilivyotimia. Sasa mtume Muhammad hawezi kuwa MSAIDIZI, kwa sababu kwanza, Muhammad hakuwepo enzi za uhai wa wanafunzi wa YESU, alikuwa HAJAZALIWA BADO, Na kwa mujibu wa maelezo ya YESU MSAIDIZI lazima angekuja wakati bado mitume wako hai. Pili, ujio wa MSAIDIZI ulitokea YERUSALEMU, siku ya PENTEKOSTE. Lakini Muhammad hajatokea YERUSALEMU, na aliyeshuka siku ya PENTEKOSTE hakuwa Muhammad, isitoshe, wakati huo Muhammad hata mimba yake tu haikuwa imetungwa😃😃😃😂😂😂😂! Kama mtume Muhammad ndie MSAIDIZI basi alitakiwa awashukie mitume siku ya PENTEKOSTE kule YERUSALEMU.
HIVYO BASI MTUME MUHAMMAD SIO MSAIDIZI TULIYEAHIDIWA NA YESU, KWA SABABU MUHAMMAD HANA SIFA ZA KUWA MSAIDIZI.
JE, MSAIDIZI NI NANI SASA?
Ukisoma BIBLIA, utamuona MSAIDIZI ametajwa waziwazi kabisaaa!
YESU alisema, 👉"Lakini huyo MSAIDIZI, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia."👈 YOHANA 14:26
Kumbe MSAIDIZI ni ROHO MTAKATIFU, Hiyo ni kwa mujibu wa maelezo ya YESU mwenyewe 👆, na ukirejea sifa za MSAIDIZI, zote ROHO MTAKATIFU anazo,
Mfano:
👉ROHO MTAKATIFU, ANAKAA NA SISI MILELE. YOHANA 14:16
👉ROHO MTAKATIFU, NI ROHO, SIO MTU. YOHANA 16:13
👉ROHO MTAKATIFU, HAONEKANI WALA HATAMBULIKI NA ULIMWENGU. YOHANA 14:17
👉ROHO MTAKATIFU, ANAKAA NDANI YETU. YOHANA 14:17
👉ROHO MTAKATIFU NDIYE ALITUMWA NA MUNGU KWA JINA LA YESU. YOHANA 14:26
👉ROHO MTAKATIFU VILEVILE, NDIYE ALILETWA NA YESU KUTOKA KWA BABA. YOHANA 15:26
👉ROHO MTAKATIFU ANAMSHUHUDIA YESU. YOHANA 15:26
👉ROHO MTAKATIFU, ANAMTUKUZA YESU, PIA ANATWAA MAFUNDISHO YAKE NA KUTUPATIA. YOHANA 16:13-14
👉ROHO MTAKATIFU, ANATUFUNDISHA NA KUTUKUMBUSHA YOTE ALIYOSEMA YESU. YOHANA 14:26
👉ROHO MTAKATIFU, NDIYE ALIWASHUKIA MITUME KULE YERUSALEMU, SIKU YA PENTEKOSTE. MATENDO YA MITUME
2:1-4 👉"Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.
2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.
3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka."👈
HUYO NDIYE MSAIDIZI AMBAYE YESU ALIAHIDI, YAANI ROHO MTAKATIFU.
Ongezea na WAEFESO 1:13 👉"Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu."👈
Waislam wasikudanganye, mtume Muhammad sio MSAIDIZI, Muhammad hana sifa za kuwa MSAIDIZI, na hakuna sehemu inayomtaja mtume Muhammad kwenye biblia. (Labda katika yale makundi ya manabii wa uongo).
Somo hili limeandaliwa na kuletwa kwako na mimi mtumwa wa YESU KRISTO, Zacharia Maseke, lengo sio kukashifu wala kukejeli dini ya mtu, bali tunajifunza ili tuweze kubaini ukweli sahihi.
Unaruhusiwa kukopi na kusambaza ujumbe huu, ila usibadili yaliyomo. BWANA AKUBARIKI Kwa kutumia muda wako kusoma mada hii.
Amina.
Shalom
Mtumishi: Zacharia Maseke

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW