Wednesday, April 12, 2017

KUMBE MUHAMMAD NI MCHUNGAJI WA WAISLAM

Image may contain: one or more people and hat
1. Muhammad ni Mchungaji "Quran 2:104 Tafsiri ya Sheikh Abdulla Saleh Farsy"
2. Wachungaji ni Mbwa "Isaya 56: 10"
Ndugu msomaji wangu,
Bila ya kupoteza muda tuanze kusoma Sura Al Baqara 2:104” nayo inasema: Enyi mlio amini! Msiseme: "Raa'ina", na semeni: "Ndhurna". Na sikieni! (amri) Na makafiri watapata adhabu inayoumiza,http://www.quranitukufu.net/002.html
Najua wengi wenu hamfahamu nini tafsiri ya hii aya, basi SASA TUSOME ufafanuzi wa aya hiyo katika Tafsiri ya Sheikh Abdulla Saleh Farsy, ufafanuzi nao unasema.
Quran 2:104 Waislamu walikuwa wakati mwingine wakimwambia Mtume “Raa inaa” (Yaani kuwa ukituchunga kama MCHUNGAJI mzuri anavyochunga wanyama wake, kwani sisi Waislamu ni wajinga, hatujui la madhara wala la maslaha)….
HAYA WAISLAM, TUMESHA SOMA AYA HAPO JUU KUWA MUHAMMAD NI MCHUNGAJI WA WAISLAM.
Lakini nilipo kuwa kwenye mhadhara na Waislam, niliambiwa kuwa mimi Mkristu nafuata Mbwa. Eti, Wachungaji wote ni Mbwa na wakanipa uthibitisho kutoka Isaya 56 aya ya 10 na 11.
Isaya 56: 10 Walinzi wake ni vipofu, wote pia HAWANA MAARIFA; wote ni MBWA walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi. 11 Naam, mbwa hao WANA CHOYO sana, HAWASHIBI kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote
Tumemuona MCHUNGAJI Muhammad katika Suratul Al Baqara aya 104 nawe Muislam unasema kuwa kila Mchungaji ni Mbwa kutokana na Isaya 56 aya 10 na 11, Sasa unakubali kuwa Muhammad ni Mbwa?
NGOJA NIWAKUMBUSHE WAISLAM
Nyie si mnasema kuwa kila mchungaji ni Mbwa, Tafsiri ya Sheikh Abdulla Saleh Farsy ya Suratul Al Baqara aya 104 inasema kuwa Muhammad ni MCHUNGAJI kama tulivyo soma hapo juu. Je, sasa utaendelea kukiri kuwa WACHUNGAJI wote ni Mbwa? Je, sasa unakiri kuwa Muhamamd ni Mchungaji na ni Mbwa kama unavyo waita Wachungaji?
Zaidi ya hapo, katika Isaya hiyo hiyo, imeweka sifa za Mchungaji ambaye ni Mbwa. Ngoja niziweke kwa wale ambao hawakuziona walipo soma hiyo ISAYA 56:10-11
SIFA ZA MCHUNGAJI MBWA HIZI HAPA:
1. Hawana Maarifa (Hawafahamu neno)
2. Wana Choyo sana.
3. Hawashibi
Hizi SIFA zinamwangukia Muhammad mmoja kwa moja, maana maandiko yaapo yanaoa thibitisha hayo.
JE, MUHAMMAD ANAZO HIZI SIFA ZA MCHUNGAJI MBWA?
Muhammad ni Mchungaji, sasa tumtazame kama sifa hizo tatu, kama anazo au hana, Tusome Quran 7:157
SIFA YA KWANZA YA MCHYNGAJI MBWA: "Hawana maarifa"
157. Ambao kwamba wanamfuata Mtume, Nabii, asiyejua kusoma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa
Kwa mujibu andiko hili Muhammad, hana maarifa ya kusoma na kuandika, hiyo ni sifa moja ya Mchungaji Mbwa, kwa kuwa Sifa ya Mchungaji mbwa, ni kutokuwa na maarifa na kutolifahamu neno, na Muhammad ni Mchungaji, ambae hajui kusoma neno wala kuliandika, neno, huyo atakuwa nani?
SIFA YA PILI YA MCHUNGAJI MBWA "Wana choyo sana"
Sifa ya pili, mchoyo, Ikasomwa Quran 33:55
53. Enyi mlio amini! Msiingie nyumba za Nabii ila mpewe ruhusa kwenda kula, sio kungojea kiwive. Lakini mtakapo itwa basi ingieni, na mkisha kula tawanyikeni, wala msiweke mazungumzo. Hakika hayo yanamuudhi Nabii naye anakustahini, lakini Mwenyezi Mungu hastahi kwa jambo la haki. Na mnapo wauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia. Hivyo ndio usafi zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao. Wala haikufalieni kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala kuwaoa wake zake baada yake kabisa. Hakika jambo hilo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu
Hapa Muhammad ameonyesha uchoyo wa hali ya juu, kwa kuwataka Waislamu wenye njaa wasiende kwake, kupiga stori, ili chakula kiive, bali mpaka watakapopewa ruhusa, ina maana kama asipokuitwa nawe una njaa, basi huna ruhusa ya kula, na jambo la kukaa kusubiri Chakula kiive, ni jambo ambalo, linamkwaza Muhammad, kwa sifa hii ya Uchoyo, atakuwa nani?
SIFA YA TATU YA MCHUNGAJI MBWA "Hawashibi"
Kitabu cha Historia ya Mtume Muhammad kilichoandikwa na Mohammed RIDAY wa Mombasa Kenya, Uk wa 176, Paragraph ya 5 Kinasema,
“Mtume Muhammad alikuwa hali chakula, mpaka ashikwe na Njaa, na akila hashibi…..”
Kwa kuwa sifa ya ya tatu ya Mchungaji mbwa, ni kutokushiba, na Muhammad tumeambiwa alikuwa akila hashibi, kwa mujibu wa andiko hilo atakuwa nani?
Waislam msikilizeni Mchungaji huyu hapa. Yohana 10:11 Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
Ndugu msomaji, nategemea sasa unafahamu kuwa Muhammad ni Chungaji ingawa hii ni siri kubwa sana kwa Waislam. SASA MUISLAM ANAPO SEMA WACHUNGAJI NI MBWA, BASI MPE HII MADA NA ASOME MWENYE KUWA HATA MUHAMMAD ALIKUWA MCHUNGAJI NA HIVYO BASI SIFA YA UMBWA NI YAKE.
Mimi nawaonea huruma sana Waislam wanao mfuata Mchungaji Muhammad.
Leo namaliza kwa kusema kuwa Muhammad ni Mchungaji na amefanikiwa kunyakua sifa ya Isaya 56 aya 10-11 kuwa Wachungaji ni Mbwa.
Ni mimi Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

DALILI ZA MWANAMKE ALIYEOLEWA NA JINI

Image may contain: 1 person, text and closeup
1. Hapendi kabisa kuwa karibu na wanaume, kwa kuwa tayari ana mume wa kiroho
2. Akichumbiwa lazima aharibu uchumba mwenyewe , lazima atabadilisha mawazo na kusema simtaki mwaume huyo tena, yule jini ndiye anamletea mawazo ya kukataa mwenyewe. Huyu ni JINI TWAYR {qarnail}.
3. Kama akikaribia kuolewa lazima atakataa lakini baadaye umri ukienda anajisikia vibaya
4. Kama aking’anga’ana na kuolewa hawezi kuifurahia ndoa yake kabisa ataona ndoa kama ni mateso, vile vile hawezi kumpenda mume wake kabisa , mumewe akiwa mbali anamumiss akija anajisikia kumchukia kabisa, kumchukia mwenza wako pindi anapo kuwa karibu na wewe. Huyu ni JINI SUBIANI.
5. Kama ameolewa hawezi kupata mtoto kwa maana Yule mume anaona wivu kuona mkwewe anazaa na mume mwingine, Hata kama akifanya biashara hawezi kufanikiwa kabisa kwa maana jini yule anammiliki.
6. Kua na hasira sana bila hata sababu za msingi
7. Kuwa na hali ya kutojali au kuthaminni wengine umimi na kujiona wa thamani peke yako kuliko wengine.
8. Kuchukiwa na ndugu jamaa na marafiki anakufanya ufanye mambo yakuchukiza wengine
9. Kujiona mtu mwenye mikosi nuksi na balaa tupu
10. Kuvurugika kwa mipango/ mambo yako/ hasa ya maendeleo na kila unachopanga hushindikana hata kama ukisaidiwa na mwisho hujiona hufai
11. Kuumwa kichwa pindi wakat unasoma Biblia au masomo ya kawaida
12. Kutokujisikia kuomba au kusinzia pindi unapotaka kuanza maombi, huishiwa nguvu kabisa, Na kuishia kuhangaika kama mtu asiyejua lakufanya
Kwa hiyo inawezekana jini anapoanza kumfuata mtu na kufanya mapenzi naye, mtoto anaweza kuzaliwa. Nje ni mtu lakini kwa ndani siyo mtu ni shetani. Kuna mtu yuko hapa ni zao la ndoa za rohoni ndiyo maana unajiona ni wa ajabu ajabu, kuna wengine usiku unaota amezaa watoto siyo kwamba umeota ni kweli umezaa watoto wa kijini, na wale wanaporudi ujijini wanakurudi na kukuletea wewe matatizo.
Mwanamke aliyeolewa na jini huwa anawekewa alama zifuatazo ili aendelea kumilikiwa na huyo jini
1. Na kila mwanamke anayeolewa anakuwa na cheti cha ndoa, huwezi kukiona rohoni lazima kinakuwepo kama hati ya kumilikiwa.
2. Alama nyingine ni alama ya ndoa ambayo ni pete ya kiroho, mtu anaweza kuokota pete au kuota anafunga ndoa na kuvalishwa pete
3. Alama kama chapa au chata , mtu anaweza kuwekewa alama kama chata /chapa rohoni na hiyo alama inampa mamlaka jini kummiliki mtu.
Matendo 16:13
Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.
Mungu huwa anaweka maelekezo ndani ya moyo wa mtu, sasa moyo wa mtu unaweza kuibiwa na kupewa moyo wenye maelekezo tofauti, maana yake umewekewa alama moyoni ya kushindwa, ndiyo maana ukisema huyo hawezi kuwa kiongozi maana yake ni maelekezo hasi, kwa jina la Yesu leo nakataa moyo wa kushindwa , kuanzia leo nitakuwa mbunge , nitasafiri nje ya nchi, nitaolewa na kuwa na ndoa njema,
Usikate tamaa, Yesu anaweza kukufungua sasa hivi kutoka kwenye hii ndoa ya majini.
Kwa jina la Yesu leo nafanya vita na kila mtu wa uzao wa kishetani namung’oa kwa jina la Yesu. Nakataa kwa jina la Yesu kama kuna mtu yeyote aliyezaliwa rohoni kutoka tumboni kwangu leo namteketeza kwa jina la Yesu.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

WANEFILI WALIKUWA NANI NA WALITOKA WAPI?

Image may contain: 3 people, people standing and text
Kwa mujibu wa Hebraic, kitabu cha Henoko na thibitisho nyinginezo za maandiko yasiyo ya kibiblia, walikuwa kizazi kikubwa cha mashujaa "Majitu makubwa" maarufu ambao walifanya vitendo vya uovu mkubwa. Kawaida ukubwa na nguvu zao zilitokana na mchanganyiko wa “chembe cha za damu” ya mapepo na zile za binadamu. Yote ambayo Biblia moja kwa moja inasema kuhusu wao ni kwamba walikuwa "mashujaa wa zamani, watu wenye sifa" (Mwanzo 6:4). Wanefili walikuwa si wageni, walikuwa halisi, viumbe wa kimwili zinazozalishwa kutoka muungano wa wana wa Mungu na binti wa watu (Mwanzo 6:1-5).
NUKUU:
MWANZO 6:
(A.) 1 Ikawa WANADAMU walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 2 WANA WA MUNGU waliwaona hao BINTI ZA WANADAMU ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. 3 BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni mnyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
(B.) 4a Nao WANEFILI walikuwako duniani siku zile;
(C.) 4b tena, baada ya hayo, WANA WA MUNGU walipoingia kwa binti za binadamu, wakazaa nao wana; hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.
(D.) 5 BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. 6 BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. 7 BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. 8 Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.
(E.) 9 Hivi ndivyo VIZAZI VYA NUHU. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu. 10 Nuhu akazaa wana watatu wa kiume, Shemu, na Hamu, na Yafethi.
(F. ) 11 DUNIA IKAHARIBIKA MBELE ZA MUNGU, dunia ikajaa dhuluma. 12 Mungu akaiona dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani.
BINADAMU KAMA KABILA LA MAJITU/WANEFILI (Wamoabu waliyaita majitu hayo WAEMI-yaani magaidi; Waamoni waliyaita WAZUMZIMI), WAREFAI, WAANAKI yalikuwa wenyeji wa Hebron ulioitwa Kirjatharba, Mfano Goliati (mrefai), Ishbibonebu, Sipai, na mfalme Ogu.
MPANGO WA IBILISI KUKICHAFUA KIZAZI CHA WANADAMU KIMWILI KUPITIA VINASABA
Kwa nini mapepo wafanye jambo kama hilo?
Mapepo ni maovu, viumbe-ivilvyo geuzwa kwa hivyo hakuna kitu wanachokitenda kinafaa kutushangaza. Kama motisha ya kipekee, uvumi bora zaidi ni kwamba mapepo walikuwa wanajaribu kuchafua damu ya binadamu ili kuzuia ujio wa Masihi, Yesu Kristo. Mungu aliahidi kwamba Masihi atakuja kutoka uzao wa Hawa (Mwanzo 3:15) ambaye ataponda kichwa cha joka hilo, Shetani. Hivyo, mapepo walikuwa uwezekano wa kujaribu kuzuia hili na kuchafua ukoo wa binadamu, na kuifanya vigumu kwa ajili ya Masihi asiye na dhambi siku moja kuzaliwa. Tena, hili si jibu hasa la kibiblia, lakini ni uwezakano na si katika utata na kitu chochote Biblia inafundisha.
NUKUU:
Mwanzo 3:15 '' nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.''
WANEFILI-majitu yenye urefu wa kati ya futi 9 hadi futi 35.
Yalikuwa ni majitu kabla ya gharika ya Nuhu kwa namna mbili; kwanza ni yale makatili, yenye kuua na kula nyama za watu, yaliishi katika miji yao bila kuchangamana na watu. Hayakuwa wanadamu, bali ni uzao uliotengenezwa(zalishwa) na wajumbe wa shetani(makaika walioanguka) Pili yalikuwa ni majitu ambayo yaliishi kwa kuchangamana, kuwatawala, na kuwafanyia watu kila yalichotaka-hata.
Ni nini kilichotokea kwa Wanefili?
Wanefili walikuwa moja ya sababu za msingi kwa ajili ya mafuriko kubwa katika wakati wa Nuhu. Pindi tu baada ya Wanefili wametajwa, neno la Mungu linatuambia hivi: "Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba niewafanya" (Mwanzo 6:5-7). Hivyo, Mungu aliendelea na mafuriko kwa dunia nzima, na kuua kila mtu na kila kitu (ikiwa ni pamoja na Wanefili) zaidi ya Nuhu na familia yake na wanyama waliokuwemo ndani ya safina (Mwanzo 6:11-22).
Je, kulikuwa na Wanefili baada ya mafuriko?
Mwanzo 6:4 inatuambia, "Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa." Inaonekana kwamba mapepo walirudia tendo la dhambi wakati mwingine baada ya mafuriko. Hata hivyo, ilifanyika kwa kiasi kidogo kuliko ilivyokuwa kabla ya mafuriko. Wakati wana wa Israeli walipeleleza nchi ya Kanaani wao walimpasa Musa taarifa: "Kisha huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona"(Hesabu 13:33). Basi, kifungu hiki hakisemi hasa kwamba Wanefili walikuwapo, ila wapelelezi waliwaza kuwa waliona Wanefili. Kuna uwezekano zaidi kuwa wapelelezi walishuhudia watu wakubwa sana katika Kanaani na kimakosa wakaamini kuwa wao ni Wanefili. Au, inawezekana kwamba baada ya mafuriko mapepo tena walijumbiana na wanawake binadamu, na kuzalisha zaidi Wanefili. Kwa hali yoyote ile, hawa "majitu" waliharibiwa na wana wa Israeli wakati wa uvamizi wao kwa Kanaani (Yoshua 11:21-22) na baadaye katika historia yao (Kumbukumbu 3:11; 1 Samweli 17).
Ni nini inazuia mapepo kutoka kuzalisha Wanefili Zaidi hii leo? Inaonekana kwamba Mungu alikomesha mapepo kuchumbiana na binadamu kwa kuweka mapepo yote waliofanya kitendo kama hicho katika lindi kuu. Yuda mstari wa 6 inatuambia, "Na, malaika walioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu." Ni wazi, si mapepo yamewekwa katika "gerezani" hii leo, hivyo lazima kuna kundi la mapepo wamekuwa wakifanya dhambi chungu zaidi ile ya awali ya kuanguka. Takribani, mapepo ambayo yalichumbina na wanawake binadamu ni wale ambao "wamefungwa minyororo ya milele." Hii itazuia mapepo yoyote zaidi kujaribu kitendo kama hicho.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA YESU MUNGU

Image may contain: 1 person, text
Ndugu, tukimuamini Mungu kwa mioyo yetu yote hakika yote yanawezekana.
Baba mmoja ambaye mwanawe alikuwa akisumbuliwa na pepo la kifafa alimleta mwanawe kwa wanafunzi wa Yesu nao hawakuweza kumpa suluhisho. Ndipo alipomfuata Yesu na kumwambia ukiweza naomba umponye mwanangu. Yesu alishangaa! Akauliza ukiweza? Akamwambia “ Yote yawezekana kwake aaminiye”
“Lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia. Yesu akamwambia, ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.” (Marko.9:22-23)
Hakuna jambo lililo gumu la kumshinda Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo.
Zekaria 8:6, Bwana wa majeshi alimwambia Musa; “ ingawa hili ni neon lililo gumu mbele za macho ya mabaki ya watu hawa, je, liwe neno gumu mbele za macho yangu?. Hata kama jambo ni gumu na linaonekaka kama halitawezekana mbele za macho yetu sisi wanadamu, Mungu wa Ibrahim Isaack na Yakobo, yaani Mungu wa Israel, anaweza yote. hakuna jambo lililo gumu la kumshinda Mungu wetu.
Mwanzo 18:14, Bwana alimwambia Sara mke wa Ibrahimu kuwa, Jambo gani lililo gumu linalomshinda Bwana? Mungu wetu anaweza yote. Mungu wetu ana nguvu, ni mkuu ni unique, na anaweza mambo yote. hafananishwi na chochote, hashindani na chochote wala yoyote, ni mkuu mno, nguvu zake hazichunguziki, mawazo yake hayachunguziki, na njia zake hazichunguziki.
Hesabu 11:23, Bwana Mungu wetu alimwambia Musa, Je, mkono wa Bwana umepungua urefu wake? Sasa utaona kwamba neno langu litatimizwa kwako au la. (soma mpaka isaya 59:1, kuwa mkono wa bwana si mfupi hata usiweze kuokoa….sikio lake si zito lisiweze kusikia, ila maovu yetu ndo kikwazo…., pamoja na yote hayo, hapa, Mungu alitaka kumwonyesha Musa kuwa hakuna jambo lililo gumu kwake.
Ayubu 42:2, Neno la Bwana kwa kinywa cha Ayubu linasema”najua ya kwamba waweza kufanya mambo yote, na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuiliwa. Hakuna mtu wala kitu chochote kinachoweza kumzuia Mungu kufanya atakacho. Mungu akisema ndiyo hakuna mtu wa kusema hapana, na akisema hapana hakuna wa kusema ndiyo.
Luka 1:37, Malaika alimwambia mariam kuwa, hakuna Neno lisilowezekana kwa Mungu. Kwa Mungu wa ibrahim isaka na Yakobo, Mungu wa kweli aliyeumba mbingu na nchi na vyote vijazavyo, anaweza yote.
Yeremia 32:17, Neno la Bwan alinasema “Aa! Bwana Mungu tazama wewe umeziumba mbingu na nchi kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa, hapana neno gumu usiloliweza.
Efeso 3 :20, Neno la Mungu linasema, Basi, atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu. Mungu anao uwezo wa kufanya mambo makubwa na ya ajabu kuliko yale tuliyowahi kuyaona,kuyaomba au kuyawaza. Mungu aweza kufanya mambo makubwa sana na ya ajabu.
Mathayo 19 :26, Yesu akawakazi macho akawaambia kwa wanadamu hilo haliwezekani, bali kwa Mungu yote yanawezekana. Yesu mwenyewe ndiye alitoa ahadi na ufafanuzi huu hapa kuwa, kwa Mungu yote yanawezekana.
Hivyo, hakuna sababu ya kuwa na hofu tumwombapo Mungu, tunajua kuwa Mungu ano uwezo wa kufanya mambo yote hata yale ambayo sisi tunayaona kama magumu sana.

Marko 10 :27, Yesu akawakazi macho akasema, « kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo, maana yote yanawezekana kwa Mungu ». hakuna jambo liwalo lote lile ambalo Mungu linamshinda.

Shalom

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo. 

Tuesday, April 11, 2017

VAENI SILAHA ZOTE ZA MUNGU

Image may contain: text
Je, umesha vaa silaha zote za Mungu?
Waefeso 6:10-12 yasema, “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Ujumbe huu wafunza baadhi ya kweli muimu: tutaweza kuwa na uwezo kwa nguvu za Mungu, ni silaha ya Mungu ambayo yatulinda, na vita ni kupinga na nguvu za giza za ulimwengu huu.
Mfano wa nguvu sana juu ya ngunvu za Bwana ni ule wa malaika Mikaeli katika Yuda 9. Mikaeli ambaye ni mwenye nguvu zaidi ya malaika wote wa Mungu, hakumkemea Shetani kwa nguvu zake, bali alisema, “Mungu anakukemea!” Ufunuo 12:7-8 yanakiri kwamba katika nyakati za mwisho Mikaeli atamshinda Shetani. Bado, wakati inafikia mapigano yake na Shetani, Mikaeli alimkemea Shetani katika jina la Mungu na mamlaka yake, si kwa nguvu zake. Ni kupitia kwa uhusiano wetu na Yesu Kristo kuwa Wakristo wako na mamlaka yoyote juu ya Shetani na mapepo yake. Ni kupitia kwa jina lake kuwa kemeo letu liko na nguvu.
Waefeso 6:13-18 yatupa elezo la silaha za kiroho Mungu anapeana. Tunastahili kusimama dhabiti na kufunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kufuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani, kuchukua ngao ya wokovu na kwa kuomba katika roho.
Kwa ufupi, njia za ufanisi wa vita vya kiroho ni zipi?
Shalom
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

Monday, April 10, 2017

UNAWAFAHAMU MALAIKA WAKUU SABA WA MUNGU "ARCHANGELS OF GOD? (SEHEMU YA SABA)


Kiumbe wa roho anayeitwa Mikaeli hatajwi mara nyingi katika Biblia. Hata hivyo, kila mara anatajwa akitenda jambo fulani. Katika kitabu cha Danieli, Mikaeli anapigana na malaika waovu; katika barua ya Yuda, anabishana na Shetani; na katika Ufunuo, anapigana na Ibilisi na malaika wake waovu. Anapoutetea utawala wa Mungu na kupigana na adui za Mungu, Mikaeli anatenda kupatana na maana ya jina lake—“Ni Nani Aliye Kama Mungu?” Lakini Mikaeli ni nani?

Malaika Mikaeli (kwa Kiebrania מִיכָאֵל, Micha'el au Mîkhā'ēl, maana yake Nani kama Mungu; kwa Kigiriki Μιχαήλ, Mikhaḗl; kwa Kiarabu ميخائيل, Mīkhā'īl) anaheshimiwa kama malaika mkuu katika imani ya dini za Uyahudi na Ukristo.

Mikaeli ni malaika mkuu, neno “malaika mkuu” la kigiriki ni ἀρχάγγελος (archaggelos) linalomaanisha “mtawala wa malaika” au “mkuu wa malaika”; kwa uhalisia “mkuu wa wajumbe”.
Katika Biblia ya Kiebrania anatajwa mara tatu katika Kitabu cha Danieli.

Katika Agano Jipya la Biblia ya Kikristo anatajwa katika Waraka wa Yuda na katika Kitabu cha Ufunuo.

Je Malaika wa Bwana anaweza kuwa ndiye malaika mkuu Mikaeli?

Zekaria 3:1-2 inasema, “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye. Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni?”

Hapa tunamwona malaika wa Bwana akimwambia shetani kwamba”Bwana na akukemee”, Ukisoma fungu la 3 utaona Yoshua alikuwa amevaa “mavazi machafu” hii inawakilisha dhambi. Halafu shetani akaja kwa Yoshua akidai kuwa yuko upande wake, na malaika wa Bwana hivyo hivyo, alikuja kumuondolea Yoshua uovu wake, hivyo akamwambia shetani kwamba Bwana na akukemee. Je ni wapi tena tunaona jambo kama hili hili?

Yuda 1:9 inasema, “Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.”

Hapa tunaona kama hilo hilo lilitoke wakati wa Musa, na malaika aliyefanya hivyo ni Mikaeli malaika mkuu; kwa hakika “malaika wa Bwana” ndiye “Mikaeli”.

Danieli 12:1,2 inasema, “Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako;…na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.”

Zingatia Danieli 12:1 inamwita Mikaeli kama “Jemedari Mkuu”, na katika Ufunuo 12:7 “Mikaeli na Malaika zake anapigana na shetani na malaika zake”. Shetani ni mkuu wa malaika zake na malaika zake humwabudu yeye na kutii amri zake; na malaika zake ni jeshi lake, vivyo hivyo Mikaeli ni mkuu wa malaika zake, na malaika zake ni jeshi lake, nao hutii amri zake (Ebrania 1:6-7

Yohana 5:28,29 “Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.”

Ufunuo 12:7 Na vita vikatokea ghafula mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka mkubwa, naye joka mkubwa na malaika zake wakapigana.

Sehemu zote tumeona Mikaeli ni malaika mkuu wa vita. Ukiona mambo hujayapata kama inavyotakiwa maana yake yupo azuiaye mahali amejificha hivyo fanya vita vya kiroho na utafanikiwa kwajina la Yesu.

Yupo saizi ya ibilisi ambaye anaitwa Malaika Mikaeli. Shetani alikuwa malaika lakini alimwasi Mungu na Mikaeli ndiye aliyemshughulikia.

Ukiona mambo kwenye maisha yako yameshindikana usifikiri Mungu hajakusikia maombi yako na amekuacha, kuna kizuizi cha mkuu wa anga mahali ambaye amekuzuia na huyo lazima ashughulikiwe na yale majibu yako yaje kwako kwa jina la Yesu.

Yupo malaika Mikaeli mkuu wa majeshi ya malaika ambaye tunamtumia ili tupigane na huyu mkuu wa anga na wakala zake waliozuia baraka zetu kwa jina la Yesu. Mashetani wote waliojificha kwenye ulimwengu wa rohoni lazima tuwafuate na kuwateketeza kwa jina la Yesu.

Malaika Mikaeli ni kiumbe wa Rohoni na wale waliokuzuia nao ni viumbe wa Rohoni na hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu wetu. Mikaeli anajua mbinu za vita na leo tunaungana na majeshi ya malaika Mikaeli ili kupigana na mkuu wa anga la uajemi na mapepo yake.

USIKOSE SEHEMU YA NANE. MALAIKA URIEL NA KAZI ZAKE.......


Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

JE! KUANGALIA PICHA ZA NGONO NI DHAMBI? (SEHEMU YA PILI)

Image may contain: 1 person, sitting and text
Kuangalia picha za ngono "NI DHAMBI" kwa herufi kubwa. Katika Sheria ya Musa ilikuwa mtu anahesabika kuwa ametenda dhambi pale ambapo atakutwa akifanya kitendo hicho au kukiwa na mashahidi wawili au watatu atatakiwa kuhukumiwa sawasawa na Sheria husika.
Kwenye dhambi ya uzinzi mtu alitakiwa apigwe mawe hadi afe sivyo kwa Sheria ya Kristo yenyewe inazungumzia juu ya kitendo cha "kutamani" tu unahesabika kuwa umefanyika DHAMBI (Mathayo 6:27-29, Waebrania 10:28). Tamaa mbaya ni dhambi kama dhambi nyinginezo. Kwa kawaida tamaa huja na ile tamaa huchukua mimba na baadaye huzaa dhambi (Yakobo 1:13-16). Kitendo cha kuangalia picha za ngono hupofusha "FIKRA" nzuri za mtu alizonazo. Mawazo machafu uanza kutawala katika ubongo wako hadi "USHUSHE" huo mzigo ulioko kwenye viungo vyako vya uzazi. Ahaaa ni hatari aiseeee.
Wewe unayengalia picha za ngono Kama ndiyo starehe yako unaiharibi nafsi yako "unakuwa zezeta wa akili" Biblia inasema "taa ya Mwili jicho na jicho lako likiwa safi mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini jicho lako likiwa bovu mwili wako wote utakuwa na giza.."(Mathayo 6:22-23). Kwa wale wanandoa ni "MWIKO" kutumia picha za ngono ili kunogesha kufanya Tendo la Ndoa.
Wewe mume unaye hapo "chombo" unakiona "live" na kimethibitishwa na Mungu mwenyewe sasa hiyo mipicha ya nini? Kila kiungo Mungu alikiweka kwa ajili ya kusudi maalum kama ni mdomo kwa ajili ya kuongea na kupitisha chakula na si kunyonya sehemu za Siri za mwenzi wako. Mungu ameweka sehemu ya "haja kubwa" kwa ajili ya kutolea uchafu uliotengenezwa na tumbo na si kiungo kingine kiende kukoroga "zege" hilo huo ni uchafu(Ufunuo 22:10-15).
Warumi 1:26:27
“Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.”
USIKOSE SEHEMU YA TATU "JINSI YA KUSHINDA DHAMBI YA KUANGALIA PICHA ZA NGONO"
Shalom

KITABU CHA MWANZO (SEHEMU YA TATU)

Image may contain: cloud, text and nature
S: Kwenye Mwanzo 1:10, ilikuwaje Mungu aumbe dunia wakati dunia ilikuwa tayari imeishaumbwa kwenye Mwanzo 1:1?
J: Neno la Kiebrania (eres) ni hilo hilo linalotumika sehemu zote. Kama ilivyo kwenye kiingereza, eres inaweza kumaanisha ulimwengu chini ya anga, na inaweza kumaanisha ardhi au nchi kavu. Kwa hiyo Mungu aliiumba sayari kwenye Mwanzo 1:1, na nchi kavu kwenye Mwanzo 1:12. Tazama Encyclopedia of Bible Difficulties uk.65-66.
S: Kwenye Mwanzo 1 na 2, kwa nini inaonekana kana kwamba kuna matukio mawili ya uumbaji?
J: Mwanzo 1 ni uumbaji wa mbingu na nchi, na Mwanzo 2 ni uumbaji wa wanadamu kwenye bustani ya Edeni.
S: Kwenye Mwanzo 1 na sehemu nyingine, kwa nini Mungu anaitwa Elohim, wakati sehemu nyingine tena kama Mwanzo 2 Mungu anaitwa Yahweh?
J: Mungu ana idadi kubwa ya majina kwenye Biblia. Inaonekana kuwa jina Yahweh linaangalia zaidi uhusiano binafsi wa Mungu na sisi tofauti na Elohim, ambalo linaangalia zaidi haki na ukuu wake.
Lilikuwa jambo la kawaida katika jamii za zamani kuwa na majina zaidi ya moja kwa mungu huyohuyo. Hii hapa ni mifano:
Osiris - Wennefer, Khent-amentius, Neb-abdu
Bel - Enlil, Nunamnir
Sin - Nanna
El - Latpan
Baal - Larpan
Elohim is the general name for God and is used in the context of God as creator. It emphasizes that God is distant and powerful. It is used to describe God as the awesome and majestic creator. In our English Bibles, Elohim is translated as God.
Yahweh (the LORD) is God's personal name and is used in the context of God having a relationship with His people. When God goes about creating humanity, it is Yahweh who does this act. When the Lord is personally involved with His people, Yahweh is the proper way to designate Him. In our English Bibles Yahweh is translated as the LORD with all capital letters.
S: Kwenye Mwanzo 1, je Mungu aliweza kuumba dunia kwa siku sita halisi zenye masaa 24 kila moja?
J: Bila kujali kama wanadhani dunia iliumbwa miaka mingi iliyopita au michache, Wakristo wote wanapaswa kujibu swali hili "ndiyo."
Badala ya siku sita, Mwenye enzi angeweza kuiumba kwa muda wa sekunde sita kama angependa kufanya hivyo. Suala hapa si jinsi gani Mungu alipaswa kuumba bali ni jinsi gani Maandiko na ulimwengu vinaonyesha alichagua kuumba.
Kama nyongeza, Maandiko hayasemi siku ina urefu gani kwa Mungu kwenye Mwanzo 1. Kumbukumbu 7:1 inaonyesha kuwa "siku" inaweza kuwa ni kipindi cha muda kinachozidi masaa 24, kama ilivyoeleweka kuwa "siku" za Musa. Zaburi 90:4; 2 Peter 3:8 zinaonyesha kuwa siku za Mungu zinaweza kuwa ndefu sana.
S: Kwenye Mwanzo 1, je kufanana kwa maelezo haya ya uumbaji na yale ya Wababeli kunathibitisha kuwa yote haya yametoka kwenye chanzo kimoja kilichotungwa na watu?
J: Maelezo ya Wababeli yanafanana kwenye ufafanuzi wa kinaganaga lakini karibu ni kinyume kabisa kuhusiana na chanzo. Tofauti na Marduk aliyekuwa anashindana na vurugu za joka kubwa Tiamat, Mungu anaamuru nini kitokee. Kama kuna kitu cha kweli kwenye jamii zisizokuwa za kibiblia jambo hili halipaswi kutushangaza. Isitoshe mtindo wa Mwanzo 1 unaelekea kuwa ni utofauti uliokusudiwa dhidi ya nadharia za kipagani.
USIKOSE SEHEMU YA NNE: Kwenye Mwanzo 1:26 na 3:22, kwa nini neno "tumfanye" linatumiwa kwa Mungu Mmoja wa Kweli?
Shalom,

JE, MUNGU ALIMUUMBA SHETANI?

Image may contain: text

Mungu aliwaumba viumbe wote wakiwa Wakamilifu, lakini walikuwa na uhuru wa kuchagua Kumtii Mungu au Kutomtii Mungu. Tunajua ya kwamba wengine kati yao walitenda dhambi, na Biblia inawataja kama “Malaika walioanguka” (Mwanzo 6:2,4; Yuda. 1:6)
LUSIFA ALIKUWA NANI?
Lusifa alikuwa amejaa hekima na alikuwa Mkamilifu katika uzuri wote, lakini aliingia katika majivuno na kuwa asiyefaa kitu na kugeuka kuendelea katika njia ya dhambi, (Ezekieli 28:12-15). Alifikiri angeweza kujiinua juu ya Kiti cha Enzi cha Mungu (Isaya 14:12-14). Maasi yake yalishindwa na kutupwa chini, duniani katika nchi (Luka 10:18; pia katika Ufunuo 12:7,9).
MWANZO WA JINA LA SHETANI:
Lusifa alishawishi theluthi ya malaika kumfuata katika maasi yake. Ambao alifukuzwa nao na jina lake likabadilika na kuitwa shetani, yule joka mkubwa (Ibilisi) na malaika waliofuatana naye wanajulikana kama pepo wachafu (demons). Wote wanajulikana kama “Jeshi lililoanguka”
Biblia inamfafanua Shetani kuwa kiumbe halisi ambaye yuko katika makao ya roho. (Ayubu 1:6) Inatueleza kuhusu sifa zake za ukatili kutia ndani matendo yake ya uovu. (Ayubu 1:13-19; 2:7, 8; 2 Timotheo 2:26) Pia inasimulia mazungumzo kati ya Shetani na Mungu na pia kati yake na Yesu.—Ayubu 1:7-12; Mathayo 4:1-11.
MAANA YA JINA LA SHETANI:
Jina hilo ni la kumfafanua, na linamaanisha “Mpinzani; Adui; Mshtaki.” Alikuja kuitwa Shetani kwa sababu alichagua kumpinga Mungu.
Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata itakapokuja ile hukumu (1 Petro 3:18-20; 2 Petro 2:4-5; Yuda 1:6). Mapepo wengine wachafu, huzunguka zunguka katika dunia hii wakitafuta watu ili wawameze (Ayubu 1:6-12; Lk 8:30-32).
JE, UMEJIULIZA HIVI?
 Shetani alitoka wapi?—Ayubu 38:4-7; Yohana 8:44.
 Shetani huathiri ulimwengu kadiri gani?—Yohana 12:31; 1 Yohana 5:19; Ufunuo 12:9.
 Tunaweza kufanya nini ili kujilinda kutokana na mbinu za uovu za Shetani?—1 Petro 5:8-10.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

JE! KUANGALIA PICHA ZA NGONO NI DHAMBI? (SEHEMU YA TATU)

Image may contain: one or more people, people sitting, shoes, indoor and text
JINSI YA KUSHINDA DHAMBI YA KUANGALIA PICHA ZA NGONO
PICHA ZA NGONO zinavutia sana kuziangalia ila zina maangamizo makubwa sana katika maisha yako. Lazima ufikie mahali kukata shauri ndani ya Moyo wako kuambatana na Mungu. Kusudi kubwa la shetani kuachilia mambo yake ya NGONO kwenye mitandao ili apate wafuasi wengi zaidi. Hakuna kitu unachoweza kukifanya katika simu za Android wengine wasikitambue. Kila unalolipitia na kuliangalia kwa Siri siku ya siku litaletwa hukumuni na Mungu mwenyewe (Warumi 2:16, Mhubiri 12:14)
USHAURI WAKIVITENDO:
I) Yatie Nuru macho yako - Zaburi 13:3, 19:8 - Yaruhusu macho yako yaingiziwe nuru na Yesu. Chukua muda wa kutosha kuingiza PICHA zinazomhusu Mungu zaidi. Angalia wahubiri mbalimbali.
II) Tazama mambo ya Adili(mema) - Zaburi 17:2-3 - Kuna nguvu kubwa sana tunapokuwa tunaangalia mambo mema. Vipindi vizuri vya neno la Mungu. PICHA zinazojenga siyo zinazoharibu fikra zetu.
III) Kumuomba Mungu afumbue macho yako - Zaburi 119:18, 146:8- Maombi ni muhimu ili kufanya macho yako kuona kusudi la Mungu na Kutambua uwepo wa shetani katika PICHA ZA NGONO.
IV) Weka maneno ya Mungu Mbele za macho yako - Mithali 4:20-21
Wakati wote soma neno la Mungu kupitia kifaa chochote cha ki-electronic ili uweze kumjua Mungu zaidi.
V) Macho yako yatazame Mbele - Mithali 4:25-27
Kutazama Mbele maana yake uwe na maono. Maono ni PICHA au TASWIRA ya Mbele ya maisha yako. Yeremia aliulizwa unaona nini naye akasema "anaona ufito wa mlozi" anaona kitu kizuri (Yeremia 1:11-12).
VI) Pendezwa na njia za Mungu - Mithali 23:26
Kuanzia sasa anza kupendezwa na njia za Mungu katika maisha yako. Acha kuzifuata njia zako katika kuufurahisha mwili wako wa PICHA zisizofaa.
VII) Tafuta watumishi wa Mungu ili wakufundishe - Isaya 48:17, 30:20-21
Kuna mambo ambayo yanatupa shida katika maisha yetu ni vizuri kuwaona waalimu ili watusaidie jinsi ya kutoka katika mtego huo.
VIII) Omba rehema na neema ya Yesu - Waebrania 4:16
Tunahitaji neema ya Mungu ili kushinda Hali hiyo ya kupenda KUANGALIA PICHA ZA NGONO na pia kufunguliwa kutoka katika vifungo hivyo vya pepo wa tamaa na mahaba.
Mungu atakubariki ukipeleka ujumbe huu kwa wengine.
TUMEFIKIA MWISHO WA SOMO LETU KUHUSU DHAMBI YA PICHA ZA NGONO.
Barikiwa sana.
Shalom,

The Angelic Guardianship in Psalm 91:11: A Scholarly and Inspirational Exploration

The Angelic Guardianship in Psalm 91:11: A Scholarly and Inspirational Exploration By Dr. Maxwell Shimba Shimba Theological Institute A...

TRENDING NOW