Friday, July 14, 2017

MASHOGA WA KIISLAM WAFUNGA NDOA

Image may contain: one or more people and closeup


Image may contain: 2 people, people smiling

Image may contain: 2 people

Jahed Choudhury, 24, alifunga ndoa ya Kishoga na mkewe Rogan mwenye miaka 19 huko Uingereza.
Choudhury aliye taka kujiua kwa sababu ya "bullying", alimpata mkewe Rogan wakati akiwa analia huko Darlaston, Uingereza.
Ndoa yao ilibarikiwa na Imamu na Shehe wa huko huko Uingereza.
Kwa habari kamili ingia hapa

ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAPONYWA

Image may contain: one or more people and text


Nabii Yoeli alitabiri kuwa, “Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana. (Yoeli 2:32)
Mtume Paulo alitilia mkazo unabii huu aliposema,
“Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka” (Warumi 10:12-13).
Kila anayeliitia Jina la Bwana Yesu kwa imani anaponywa na, anaokoka kwa kuwa ndani ya jina hili la Yesu Kristo mna uponyaji na wokovu kwa kila amwaminiye Yesu Kristo.
Lakini mtume Paulo anauliza swali muhimu, ambalo ni muhimu kulitafakari, anasema, “Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?” (Warumi 10:14)
Hili jambo ni kweli. Huwezi kumwita mtu usiyemwamini. Hii ina maana ya kuwa ikiwa tunataka watu waliitie jina la Yesu Kristo ili waokoke na kuponywa madhaifu yao, inatubidi tufundishe na kuhubiri juu ya Yesu na jina lake.
Ndiyo maana Bwana Yesu Kristo alimwambia anania ya kuwa Paulo “ni chombo kiteule kwangu, ALICHUKUE JINA LANGU mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.” (Matendo ya mitume 9:15).
Biblia inasema pia kuwa, “Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, AKAWAHUBIRI KRISTO. Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia Kwa sauti kuu; Na watu wengi waliopooza, Na viwete, wakaponywa. Ikawa furaha kubwa katika mji ule” (Matendo 8:5-8)
Smith Wigglesworth aliyekuwa mhibiri wa inili nchini uiengereza miaka ya 1930 aliwahi kushuhudia katika mahubiri yake kuwa siku moja aliitwa kwenda kumuombea mgomjwa mmoja wa kifafaaliyekuwa amezidiwa hata kushindwa kuamka. Anasema watu wa eneno lile hata ndugu zake yule mgonjwa walikuwa wamekata tama. Waliona ndugu yao atakufa kwa ugonjwa huo, kwa hiyo ilimchukua muda Bwana Smith Wigglesworthkupata walio tayari kushirikiana naye katika kumwombea mgojwa yule.
Mwishowe alifanikiwa kuwapata na anasema walikizunguka kitanda cha yule mgonjwa na wakaanza kuliitia Jina La Yesu kwa pamoja wakisema “Yesu, Yesu, Yesu…” kwa kulirudia rudia jina hili. Baada ya kulitia jina la Yesu kwa muda hivi, anasema nguvu za Mungu zilishuka kitandani mwa yule mgonjwa, zikamtingisha mgonjwa na kitanda chake.
Yule mgonjwa akapona saa ile ile, akavaa nguo na kutoka nje. Kijiji kizima kilitaharuki na kushangaa kilipomuona mtu yule amepona. Smith Wigglesworth alipoona watu wamekusanyika hivyo wakishangaa, alichukua Biblia yake akahubiri, na watu wengi waliokoka na kutubu siku ile.
Ni muhimu ufahamu kuwa muujiza unaofanyika kwa Jina la Yesu Kristo unawavuta watu kwa Yesu Kristo, wamwamini na kumfuata. Ndiyo maana imeandikwa juu ya Yesu Kristo kuwa;
“Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizozifanya” (Yohana 2:23)
siku moja nilikuwa katika sehemu Fulani nikifundisha juu ya Jina La Yesu Kristo. Mwisho wa somo nilisema wanaotaka kujazwa na Roho Mtakatifu na wanene kwa lugha mpya pamoja na wagonjwa waje mbele. Watu wengi walikuja mbele.
Niliwaambia kuwa hatutaomba neno lolote zaidi ya kuliitia jina la Yesu kwa pamoja na kwa kulirudia rudia. Kwa pamoja tukaanza kuliitia jina la Yesu tukisema kwa sauti, “Yesu, Yesu, Yesu….”
Muda haukupia mwingi tukiwa bado tunaliitia Jina hili nikasikia toka upande wangu wa kushoto sauti ya mengi yakiporomoka. Nilijua hii ni ishara ya uwepo wa Roho Mtakatifukwani mahali tulipokuwa hakukuwa na mto wowote karibu, wala mvua ilikuw hainyeshi. Baadaye nilipowaeleza watu juu ya sauti hiyo ya maji mengi, kuna wengine waliosema kuwa pia waliisikia.
Tulipoendelea kuliitia Jina la Yesu Kristo, wagonjwa walipona, waliokuwa na mapepo walifunguliwa, na wengine walijazwa Roho mtakatifu na kuanza kuzungumza kwa lugha mpya! Ishara na miujiza mingi ilifanyika kwa Jina la Yesu Kristo!
Kumbuka Yesu Kristo alisema, “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya” (Marko 16:17-18).
Shalom,
Max Shimba mtuma wa Yesu Kristo.

UTHIBITISHO WA MISTARI ILIYO FUTWA KWENYE QURAN

Image may contain: one or more people
Ndugu msomaji,
Kama Quran imekamilika kama jinsi Waislam wanavyo dai, kwanini Muhammad alifuta mistari kwenye kitabu cha Allah?
Kama Quran ni maneno ya Allah, je, nani alimpa mamlaka Muhammad kufuta aya za Allah?
Je, hii Quran imekamilka au haijtakamiliak, maana sasa tunafahamu kuwa kuna aya zilifutwa na Muhammad bila ya ruhusa ya Allah.
Huu ni Msiba. Soma ushahid hapa chini.
"Baada ya hapo, Mungu alitufunulia mstari uliokuwa miongoni mwa ile iliyofutwa baadaye." Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 (Kitabu cha Safari za Kijeshi) sura ya 27 na.416 uk.288.
"Anas bin Malik alisimulia: ... Walifunuliwa wale waliouawa Bi’r-Ma’una, mstari wa Kurani tuliozoea kuukariri, lakini badaye ulifutwa. Mstari wenyewe ulikuwa: ‘Wafahamishe watu wetu kuwa tumekutana na Bwana wetu. Amefurahishwa nasi na ametufurahisha.’" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 (Kitabu cha Jihad) sura ya 19 na.69 uk.53. Tazama pia Historia ya al-Tabari juzuu ya 7 uk.156.
Kumbukumbu nyingine za mistari iliyofutwa ni Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 (Kitabu cha Jihad) sura ya 8 na.57 uk.45, Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 (Kitabu cha Jihad) sura ya 184 na.299 uk.191, na Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 (Kitabu cha Safari za Kijeshi) sura ya 27 na.421 uk.293 zote zinarudia kitu hicho hicho kuhusu mstari huo huo.
Wakati fulani Muhammad aliafikiana na kusema kuwa kuhusiana na mabinti wa Allah kwenye Sura 53:19 "sala ya ya kuombea ilipaswa kutumainiwa." Muhammad alisema tunapaswa kutegemea msaada wa sanamu hizi tatu.
Wafuasi wa Muhammad walishangazwa kuwa amesema hivi. Baadaye, Muhammad alibadilisha msimamo wake na kusema kuwa Shetani alimdanganya. Mistari hii ilibatilishwa au kutolewa. Wanazuoni wa Kiislam wanaiita mistari hii "aya za Shetani." Inafurahisha kusoma maelezo ya Waislam kuhusu namna ambayo nabii wa kweli angeweza kusema hivi.
MASWALI:
1. Kwanini Allah aliruhusu Shetani kumdanganya Nabii wake?
2. Kama Muhammad aliweza kudanganywa na Shetani, je, tutaiamini vipi Quran ambayo imejaa shaka?
3. Je, kuna aya ngapi ambazo ni za Shetani kwenye Quruan, ikiwa sasa tunafahamu kuwa, Shetani na yeye alikuwa anateremsha aya zake kwa kupitia Jibril huyo huyo?
4. Kwanini Waislam wanakataa ukweli wa Mabinti wa Allah ambao Muhammad aliuukubali?
5. Kwanini Muhammad alishindwa kutofautisha maneno ya Allah na Shetani na kudhani ni mtu huyo huyo anasema?
MABINTI WA ALLAH
Uarabuni kabla ya Muhammad, kabila la Muhammad, Quaraysh, lilimwamini Mungu aitwaye Allah (au Al’Ilah) aliyekuwa na mabinti watatu walioitwa Al-Lat, Al-Uzza, na Manat.
" ‘Urwa alisema, ... kuhusiana na Ansar aliyezoea kumdhania Ihram kuwa anaabudu sanamu anayeitwa ‘Manat’ ambaye walizoea kumwabudu kwenye sehemu iliyoitwa Al-Mushallal..." Bukhari juzuu ya 2 kitabu cha 26 (Hija) sura ya 78 na.706 uk.413.
"Mstari huu ulifunuliwa kwa kuhusiana na Ansar aliyekuwa anamdhania Ihram kuwa sanamu Manat ambaye aliwekwa karibu na sehemu iliyoitwa Qudaid..."Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 27 (‘Hija ya Umra) sura ya 10 na.18 uk.11. Al-Lat, Al-Uzza wameelezewa Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 74 (Kitabu cha Kuomba Ruhusa ya Kuingia) sura ya 52 na.314 uk.209; juzuu ya 5 na.375 uk.259
Hakika Quran sio kitabu cha Mungu na kimejaa shaka kubwa kubwa.
Leo tumejifunza tena kuwa Quran sio kitabu cha Mungu, na zaidi ya hapo, Allah alikuwa na Mabainti watatu.
Mungu awabariki sana,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
For Max Shimba Ministries

BIBLIA INAKATAZA USHOGA

Image may contain: 1 person, beard
Je, Biblia inasema nini juu ya Ushoga?
Je, Ushoga ni dhambi?
Ndugu msomaji,
Leo, watu wengi kupitia viongozi fulani wa dini hawashutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja. Hata hivyo, Biblia iko wazi kuhusu jambo hilo. Inatuambia Mungu aliumba mwanamume na mwanamke na kwamba alikusudia ngono ifanywe kati ya mume na mke tu. (Mwanzo 1:27, 28; 2:24) Hivyo, haishangazi kwamba Biblia inashutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja.—Waroma 1:26, 27.
Waislam mara nyingi wamekuwa wakisema na kuwashutumu Wakristo, eti, Ukristo unaruhusu ushoga, huku ikifahamika kuwa, hakuna aya hata moja inayo ruhusu huu uchafu.
Walawi 18:22-23 "Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko".
Neno la Mungu kama lisemavyo kwenye Biblia linasisitiza kila mara kwamba ushoga na usagaji ni dhambi (Mwanzo 19:1-13; Mambo ya Walawi 18: 22; Warumi 1:26-27; Wakorintho wa kwanza 6:9). Warumi 1:26-27 inatufundisha ya kwamba ushoga ni njia mojawapo ya kumkana na kutomtii Mungu. Mtu anapodumu katika dhambi na kutokuamini biblia inatuambia ya kwamba “Mungu huwaachilia” kutenda maovu zaidi ili wapate kujua ubatili wa maisha bila Uwepo wa Mungu. Wakorintho wa kwanza 6:9 inasema kuwa mashoga hawataurithi ufalme wa Mungu.
Wanadamu wanajinenea kuwa wenye hekima na kupumbazika. Mtume Paulo ameeleza vizuri katika Waroma1:21-27.
Mungu amewaacha wafuate akili zao. Kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao ,Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.Waroma1:28
Watu wengine wanasema kwamba ushoga upo kwenye chembe za urithi. Wengine wanasema kwamba mtu hujifunza zoea hilo. Si kusudi la makala hii kujadili ikiwa zoea hilo ni la kurithiwa au ni la kujifunza. Kwa wazi, kusema kwamba ushoga unasababishwa na jambo fulani hususa haingekuwa kweli. Inaonekana kwamba kama ilivyo kwa mazoea mengine, ni vigumu kufahamu chanzo cha zoea hilo.
Hata chanzo kiwe nini, jambo muhimu ni kutambua kwamba Biblia inashutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja.
Mungu hakuumba mwanadamu mwenye tamaa ya ushoga.
Biblia inatuambia mtu huwa shoga kwa sababu ya dhambi. (Warumi 1:24-27), na pia kwa sababu ya uamuzi wake mwenyewe. Mtu anaweza kuzaliwa na msukumo juu ya ushoga kama vile watu pia huzaliwa na msukumo juu ya fujo na dhambi nyinginezo. Hili halihalalishi dhambi yoyote inayofanywa na wanadamu. Je, mtu akizaliwa na msukumo wa hasira mbaya, ni halali aendeleze hasira zake mbaya? La, hasha. Hata kwa ushoga pia si halali.
Hata hivyo Biblia haiitaji dhambi ya ushoga kuwa ndiyo kubwa zaidi. Kila dhambi ni chukizo kwa Mungu. Ushoga ni mojawapo ya mambo yaliyoorodheshwa katika wakorintho wa kwanza 6:9-10 yatakayozuia mtu asiingie katika ufalme wa Mungu. Kulingana na Biblia msamaha wa Mungu juu ya shoga upo sawa na wa mzinzi, muabudu sanamu, muuaji, mwizi na kadhalika. Mungu tena aahidi uwezo juu ya kushinda dhambi, pamoja na ushoga, kwa wale wote watakao mwaminiYesu kristo kwa wokovu wao (wakorintho wa kwanza 6:11; wakorintho wa pili 5:17).
JE, UNAWEZA KUISHINDA TAMAA HII YA USHOGA?
Unaweza kuepukaje kujihusisha na ngono ya watu wa jinsia moja?
 Kwanza Mtupie Mungu mahangaiko yako yote kupitia sala, ukiwa na uhakika kwamba ‘anakujali wewe.’ (1 Petro 5:7; Zaburi 55:22) Mungu anaweza kukuimarisha kwa kukupa amani “yenye ubora unaozidi fikira zote.” Amani hiyo ‘itaulinda moyo wako na nguvu zako za akili’ na kukupa “nguvu zinazopita zile za kawaida” ili usitende kulingana na tamaa zisizofaa. (Wafilipi 4:7; 2 Wakorintho 4:7) Sarah, ambaye alihofia kwamba anavutiwa na watu wa jinsia zote mbili, anasema: “Kila wakati ninapopatwa na hisia hizo, mimi husali; na Yehova hunitegemeza. Nisingeweza kukabiliana na tatizo hilo bila msaada wake. Sala ndiyo msaada wangu mkubwa!”—Zaburi 94:18, 19; Waefeso 3:20.
 Pili Jaza akili yako mambo ya kiroho yenye kujenga. (Wafilipi 4:8) Soma Biblia kila siku. Usidharau uwezo wake wa kuongoza akili na moyo wako daima. (Waebrania 4:12) Kijana mmoja anayeitwa Jason anasema: “Biblia—kutia ndani maandiko kama vile 1 Wakorintho 6:9, 10; na Waefeso 5:3—imenisaidia sana. Mimi husoma maandiko haya kila wakati tamaa mbaya zinaponijia.”
 Tatu Epuka ponografia, yaani picha au habari za kingono na propaganda za ngono kati ya watu wa jinsia moja ambazo zinaweza kuchochea mawazo yasiyofaa.* (Zaburi 119:37; Wakolosai 3:5, 6) Sinema na vipindi fulani vya televisheni pia huendeleza wazo la kwamba ngono kati ya watu wa jinsia moja ni mtindo mwingine tu wa maisha. “Maoni yaliyopotoka ya ulimwengu yaliathiri sana akili yangu, na kufanya nichanganyikiwe kuhusu hisia za kuvutiwa na watu wa jinsia yangu,” anasema Anna. “Sasa mimi huepuka kabisa kitu chochote au mtu yeyote ambaye anaunga mkono ngono kati ya watu wa jinsia moja.”—Methali 13:20.
 Nne Zungumza na mtu unayemwamini kuhusu hisia zako. (Methali 23:26; 31:26; 2 Timotheo 1:1, 2; 3:10)
MAMBO YA KUFIKIRIA
 Kwa nini Mungu hushutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja?
 Utafanya nini ikiwa unakabiliana na hisia za kuvutiwa kingono na mtu wa jinsia yako?
 Unaweza kuongea na nani ikiwa unahangaishwa na hisia za kufanya ngono na mtu wa jinsia yako?
Walawi 18:22-23 "Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko".
Ushoga ni dhambi na umekatazwa kwenye Biblia.
Mungu awabariki sana.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
For Max Shimba Ministries Org.

YESU ATABIRI KUWA MUHAMMAD NI MTUME NA NABII WA UONGO

Image may contain: meme and text
Ndugu msomaji,
Mara nyingi Waislam wamekuwa wakisema kuwa, eti, Yesu alitabiri kuja kwa Muhammad, pale alipo sema kuhusu Roho wa Kweli, la hasha.
Nabii ni mtu gani?
Nabii ni mtu aliyeteuliwa rasmi kwa vigezo vya Kiungu ili kuleta ujumbe wa Mungu kwa wanadamu, kwa maneno mengine nabii ni msemaji wa siri za Mungu.
Nabii: Ni mtu ambaye ni msemaji wa Mungu (a mouthpiece of God) .Husimama kati ya Mungu na binadamu, mwenye jukumu la kupeleka ujumbe wa Mungu kwa watu. Nabii anapokuwa msemaji wa Mungu, huvuviwa na Roho wa Mungu, bila ujumbe wake kuwa na makosa. Nabii hujizuia kabisa utashi wake, nafsi yake, na mawazo yake, anapokuwa anatoa ujumbe wa Kinabii toka kwa Mungu. Wakati mwingine Mungu mwenyewe hutia maneno yake vinywani mwao (Kum 18:18, Yer 1:9). Nabii ni mtumishi wa Mungu (Zekaria 1:6) na mjumbe wa Mungu 2 Nyak 36:15).
Ni kweli kuwa Yesu alitabiri kuja kwa manabii, lakini kamwe hakusema lolote kuhusu utume wa Muhammad zaidi ya kukiri kuwa watu wenye sifa kama za Muhammad ni Mitume na Manabii wa Uongo.
Miongoni mwa wanadamu wanaoitwa nabii na mtume, ni mtu aitwaye Muhammad s.a.w ibn Abdullah, ibn Abdu Mutallib, ambaye ni mtume na nabii katika dini ya Kiislamu.
Pengine wewe msomaji wa somo hili unaweza kushangaa ni kwa vipi sisi ambao si Waislamu bali Wakristo tuanze kuhoji habari za Muhammad s.a.w mtume wa Waislamu? Jibu lake ni kwamba kitabu cha Qur’an kinachotumiwa na Waislamu kimetutaja sisi Wakristo mara 62 kikitutaka kuupokea, kuuamini na hatimaye kuufuata ujumbe wa Muhammad s.a.w kwa madai ya kuwa yeye ni nabii na mtume wa mwisho hata kwetu Wakristo, aliyetumwa na Mungu.
YESU ATABIRI KUHUSU MTUME WA UONGO AMBAYE NI MUHAMMAD
Tahadhari ya Bwana Yesu: Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani alituonya kuhusu kuwatambua manabii na mitume wa uongo kabla Muhammad hajazaliwa (amezaliwa 570 B.K), wala kabla Uislamu haujaanzishwa na Muhammad mwaka 610 B.K, wala kabla ya kuwepo kitabu kinachoitwa Qur’an. Tunayasoma maonyo hayo ya Bwana Yesu katika
Mathayo 7:15-16 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali, mtawatambua kwa matunda yao”.
Mathayo 24:11-13 “Na manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi na kwasababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka”.
Yesu katika Ufunuo alisema kuwa watakuja Manabii na Mitume wa Uongo.
Ufunuo 2:2 Nayajua matendo yako na taabu yako, subira yako, na kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume nao sio, ukawaona kuwa waongo.
Je, Muhammad ni nabii wa Mungu?
Je, Muhammad anasifa za nabii wa Mungu?
Hebu endelea na somo hapa chini:
JINSI YA KUMFAHAMU NABII WA UONGO:
Kwa hivyo Muhammad ni miongoni mwa hao Mitume ambao ni waongo, ambao sisi kama Wakristo yatupasa kuutambua uwepo wao hapa Duniani, kwani tumeshapewa angalizo la kuwatambua hawa wanaojiita Mitume na Manabii, hali ya kuwa ni waongo
1 Yohana 4:1-3
1 Wapenzi msiamni kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu: kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea duniani. 2 Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; KILA ROHO IKIRIYO KWAMBA YESU KRISTO AMEKUJA KATIKA MWILI, YATOKANA NA MUNGU, 3 Na Kila roho isiyomkiri Yesu, haitokani na Mungu. Na HII NDIO ROHO YA MPINGA KRISTO ambayo mliskia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
Vigezo hivi tulivyopewa na Biblia Takatifu kuwajua manabii na mitume wa uongo ni muhimu sana tukavichunguza katika maisha ya wale wanaoitwa nabii au mtume
Kila nabii na mtume ambaye yeye hakubali kuwa Kristo alikuja katika mwili, kwa maana kuwa Mungu alidhihirishwa katika mwili, hiyo roho yaani huyo nabii si ambaye anatokana na Mungu, huyo ni Nabii anaetokana na shetani, kwa mujibu ya maandiko Matakatifu, Kristo alidhirishwa katika mwili.
1 Timotheo 3:16 Na Bila shaka siri ya utauwa ni kuu, Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulikana kuwa na haki katika roho,
Akaonekana na Malaika, akahubiriwa katika mataifa. akaaminiwa katika ulimwengu, akachukuliwa juu katika utukufu,
SASA KAMA MNATAKA KUAMINI KUWA KWELI Muhammad ni nabii na mtume wa uongo, waulizeni wafuasi wake,
SWALI LA KUPIMA UNABII WA MUHAMMAD:
Je! Kwa mujibu wa uislamu, Wanakubali kuwa Mungu alikuja kwa njia ya mwili wa kibinadamu na kuonekana?
Wakikubali, basi tambueni kuwa Muhammad ni mtume wa kweli, na wakikataa basi mjue kuwa Muhammad ni nabii na mtume wa Uongo.
SIFA ZA NABII WA KWELI:
Nabii wa kweli hupata ufunuo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu:- 2Petro 1:20-21.” Mkijua neno hili kwanza,ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu;bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu,wakiongozwa na Roho Mtakatifu”.
LAKINI MUHAMMAD YEYE ALIPATA UNABII KWA NJIA HII, SOMA
Katika kitabu kiitwacho “ Wakeze Mtume Wakubwa Na Wanawe” kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al Farsy uk.12 tunasoma maneno haya
“Basi Mtume akafanya hofu akarejea kwa mkewe akamhadithia; na pale pale homa kubwa kabisa ikampanda akataka afunikwe maguo. Mara akawa anatetemeka kwa nderema na anaweweseka na kusema “Najikhofia nafsi yangu kuchezewa na shetani na kuniharibu akili yangu na kunizuga”. Bibi Khadija palepale alimdakiza akamwambia; “ Wacha hayo; Siyo yatakayokuwa hayo. Wewe huwezi kuchezewa na mashetani. Shetani hawezi kumchezea mtu mwenye sifa zako. Wewe unatazama vyema jamaa zako, unachukuwa mizigo ya hata watu wasiokuwa wako, unawadhihirishia watu sifa zako nzuri ambazo hakuna mwenye nazo. Unafanya hivi na unafanya hivi. Furahi ndugu yangu. Tua moyo wako, Wallahi! Mimi naona umekwishakuwa mtume”.
Je, wapi katika Injili au Taurat au Zaburi tunasoma kuwa Manabii na Mitume katika Biblia walipata kwa njia ya homa na kukiri kuchezewa na mashetani kama Muhammad wa kwenye Quran?
1 Petro1:10-11 “Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta tafuta na kuchunguza chunguza ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. Wakatafuta ni wakati upi na wakati wa namna gani ulioonywa NA ROHO WA KRISTO ALIYEKUWA NDANI YAO ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo na utukufu utakaokuwako baada ya hayo…..” (maneno ya msisitizo kwa herufi kubwa ni ya mwandishi)
Ufunuo 19:10 “Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndiyo roho ya unabii”
Biblia Takatifu imetuonya kuwachunguza mitume na manabii. Katika kitabu cha Ufunuo 2:1-2 “ Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao siyo ukawaona kuwa waongo”
Kwa mujibu wa aya hizi Muhammad s.a.w hastahili kuitwa nabii na mtume wa Mungu wa Kweli, bali anaangukia katika kundi la manabii na mitume wa uongo.
Mungu awabarikisana, na tuendelee kujifunza kweli, na kweli itatuweka huru.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
For Max Shimba Ministries Org.

Sunday, June 18, 2017

YESU ALISEMA NINI KUHUSU ROHO MTAKATIFU NA MAREHEMU MUHAMMAD?

Image may contain: sky, cloud, ocean, nature, text and outdoor
1. Roho Mtakatifu atakuja kwa Jina lake.
2. Roho Mtakatifu anajua yote.
3. Roho Mtakatifu atakaa ndani yetu.
4. Roho Mtakatifu anamtukuza Yesu.
Neno la Mungu linasema kuwa, Roho Mtakatifu alikuja kwa Jina la Yesu.
1. ROHO MTAKATIFU ALIKUJA KWA JINA LA YESU:
UTHIBITISHO: - Yohana 14:26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
MUHAMMAD ALIPEWA UTUME NA MKEWE:
Kiitabu kiitwacho “ Wakeze Mtume Wakubwa Na Wanawe” kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al Farsy uk.12 tunasoma maneno haya
“Basi Mtume akafanya hofu akarejea kwa mkewe akamhadithia; na pale pale homa kubwa kabisa ikampanda akataka afunikwe maguo. Mara akawa anatetemeka kwa nderema na anaweweseka na kusema “Najikhofia nafsi yangu kuchezewa na shetani na kuniharibu akili yangu na kunizuga”. Bibi Khadija palepale alimdakiza akamwambia; “ Wacha hayo; Siyo yatakayokuwa hayo. Wewe huwezi kuchezewa na mashetani. Shetani hawezi kumchezea mtu mwenye sifa zako. Wewe unatazama vyema jamaa zako, unachukuwa mizigo ya hata watu wasiokuwa wako, unawadhihirishia watu sifa zako nzuri ambazo hakuna mwenye nazo. Unafanya hivi na unafanya hivi. Furahi ndugu yangu. Tua moyo wako, Wallahi! Mimi naona umekwishakuwa mtume”.
2. ROHO MTAKATIFU ANAJUA YOTE NA ATATUFUNDISHA KUHUSU YESU KRISTO:
Anafundisha yooote ambayo Yesu aliwaambia mitume wake.- Yohana 14:26
Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
MUHAMMAD HAKUJUA YOTE BALI ALIKIRI KUWA YEYE NI KIROJA.
Qur’an 46;9 (Surat Al-Ahqaf) Sema; mimi si kiroja (mpya) katika mitume wala sijui nitakavyofanywa, wala mtakavyofanywa ninyi, sifuati yaliyofunuliwa kwangu, sikuwa mie lolote, ila ni muonyaji tu ninayedhihirisha.
3. ROHO MTAKATIFU ALIKAA NDANI YA WANAFUNZI WA YESU
Yohana 14:17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
MUHAMMAD HAKUWEPO WAKATI WA YESU NA HAKUWA NA UWEZO WA KUKAA NDANI YETU KAMA ROHO MTAKATIFU.
4. ROHO MTAKATIFU ANAMTUKUZA YESU KRISTO:
Yohana 16:14 14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.
MUHAMMAD HAKUMTUKUZA YESU BALI ALLAH, HIVYO HAWEZI KUWA ROHO MTAKATIFU BALI ALIMKUFURU ROHO MTAKATIFU.
Walio mkufuru Roho Mtakatifu wote wataingia Jehannam.
5. YESU ANAWAPA ROHO MTAKATIFU WANAFUNZI WAKE
Yohana 20 aya ya 21 na 22 inasema: 21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. 22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.
AYA HAPO JUU IPO WAZI kabisa kuwa YESU ALIWAPA ROHO MTAKATIFU WANAFUNZI WAKE NA HAKUWAPA MUHAMMAD AMBAYE alikuwa bado HAJAZALIWA.
Nimevunja hoja dhaifu za Wakufuru Roho Mtakatifu kwa kutumia aya thabiti za Biblia Takatifu.
Shalom.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

YESU ALIWAPA ROHO MTAKATIFU WANAFUNZI WAKE MIAKA 630 KABLA YA KUZALIWA MUHAMMAD

Image may contain: bird and text
Yohana 20 aya ya 21 na 22 inasema: 21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. 22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.
AYA HAPO JUU IPO WAZI kabisa kuwa YESU ALIWAPA ROHO MTAKATIFU WANAFUNZI WAKE NA HAKUWAPA MUHAMMAD AMBAYE alikuwa bado HAJAZALIWA.
NI UONGO MKUBWA SANA KUOKA WAISLAM WANAPO DAI KUWA MUHAMMAD NI ROHO MTAKATIFU. HUKU NI KUKUFURU ROHO MTAKATIFU.

MAJINA KUMI NA MBILI YA ROHO MTAKATIFU

No automatic alt text available.
Katika kijarida hiki, tutajikumbusha majina kumi na mbili ya Roho Mtakatifu na kazi zake.
Haya ungana nami moja kwa moja na tujifunze kuhusu Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu anamajina mengi na wasifa mwingi, mengi yao kama sio yote yanaeleza kazi na huduma yake. Hapa chini ni baadhi ya majina na wasifa wake kama yalivyo semwa katika Biblia kuhusu Roho Mtakatifu.
1. MWANDISHI WA NENO (Author of Scripture)
2 Petro 1:21; 2 Timotheo 3:16. Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
Roho Mtakatifu ndie aliye weka pumzi katika vitabu vyote vya Biblia 66. Hivyo basi, waandishi wa Biblia walipewa nguvu/upako na Roho Mtakatifu na wakaandika Biblia bila ya makosa.
2. MSAIDIZI/WAKILI/MSHAURI WETU (Comforter / Counselor / Advocate)
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele.
Isaya 11:2; Yohana 14:16, 15:26; 16:7.
Maneno yote matatu yanatokana na neon la Kigiriki Parakletos, amabalo linatupa Paraclete. Jina linguine la Roho. Yesu alipo ondoka duniani, Wafuasi wake walijisikia vibaya sana kwasababu awalikosa mfariji. LAKINI Yesu aliwapa ahadi ya Roho ambaye atawafariji, Washauri, Wawakilisha na kuwa Msaidizi wao wale ambao wapo katika Kristo. Roho Mtakatifu vile vile yeye Ushuhudia roho zetu kuwa sisi ni watoto wa Mungu na utuhakikishia wokovu wetu.
KUMBE BASI, ROHO MTAKATIFU akama aya zinavyo sema atakuwa nasi MILELE.
3. MHAKIKISHI WA DHAMBI (Convictor of Sin)
Yohana 16: 7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.
8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;
10 kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena;
11 kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.
Roho Mtakatifu yeye ndio anakuonyesha au kufunulia UKWELI kuhusu Mungu katika akili zetu na roho zetu. Ukweli huu ndio utatuhumu kwa kuwa tutafahamu kuwa sisi ni watenda dhambi na hatuto weza pinga huo ukweli. Hufanya hivi kwa kuweka hatiani Moyo wako kwamba sisi ni watenda dhambi mbele ya Mungu Baba, na kwamba tunahitaji haki yake (righteousness) na kwamba kwahakika siku moja hukumu itakuja kwa watu wote. Wale ambao wanapinga ukweli huu, basi wanapinga ukweli wa Roho Mtakatifu.
4. AMANA/MHURI/BIDII (Deposit / Seal / Earnest)
2 Wakorintho 1:22; 5:5; Waefeso 1:13-14. Roho Mtakatifu ni Mhuri kwa watu wa Mungu. Yeye hutujali sisi kama watoto wake. Zawadi ya Roho Mtakatifu ni kama malipo ya amana kwetu sisi kwa urithi wa mbinguni, ambao Kristo alituahidi baada ya kazi ya pale Msalabani. Ni kwasababu ya Roho Mtakati ambaye ameweka Mhuri kwetu ndio maana tuna uhakika wa Wokovu. Hakuna mwenye uwezo wa kuvunja hii “SEAL” ya Mungu.
5. KIONGOZI (Guide)
Yohana 16:13. Kama ambavyo Roho alivyo waongoza waandishi wa Biblia katika kweli yote, vivyo hivyo ametuahidi kutuongoza wote tuaminio katika Kristo. Ukweli kuhusu Mungu ni jambao la mzaha kwa watu wa dunia na Makafiri, kwasababu hawana macho ya rohoni na hawamweli Roho Mtakatifu (1 Wakorintho 2:14) Wale walio katika Kristo ndani yao wana Roho Mtakatifu ambaye anatuongoza katika yote tunayo hitaji. Wale ambao hawana Roho Mtakati wao ni kama yatima, maana hawana kiongozi na hawata weza elewa maneno ya Mungu, wao baba yao ni Yule muovu, IBILISI.
6. ANAMAKAZI NDANI YA WAAMINIO (Indweller of Believers)
Warumi 8:9-11; Waefeso 2:21-22; 1 Wakorintho 6:19) Roho Mtakatifu anaishi katika mioyo ya waaminio/watu wa Mungu, na huku kuishi ndani ya kila mtu kwa wakati mmoja (omnipresence) ni sifa mojawapo pekee ya Mungu. Akiwa ndani ya Waaminio, huwaongoza, huwafundisha, kuwafariji, na ni mshawishi na zaidi ya hapo huzalisha matunda ya Roho (Wagalatia 5:22-23) Hutoa uhusiano wa karibu kati ya Mungu na Watoto wake “Intimate connection” Wakristo wote walio okoka wana Roho Mtakatifu ndani yao/katika mioyo yao.
7. MWOMBEZI (Intercessor)
Warumi 8:26 Kazi na au huduma moja ya muhimu sana ya Roho Mtakatifu kwa walio kombolewa na damu ya Yesu ni kuwaombea “interceding” Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
8. MFUNUAJI/ROHO WA KWELI (Revealer / Spirit of Truth)
Yohana 14:17; 16:13; 1 Wakorintho 2:12-16.
Yohana 14: 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.
Roho Mtakati yeye ndie anatufunulia yote ambayo Yesu aliyafanya na yote ambayo Yesu anataka tuyaelewa. Ndio maana watu ambao hawa Roho Mtakatifu wao huona mambo tunayo funiliwa si ya maana.
1 Wakorintho Mlango wa 2 :12 Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.
13 Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.
14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
15 Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.
16 Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.
. 9. ROHO YA MUNGU/BWANA/KRISTO (Spirit of God / the Lord / Christ)
Mathayo 3:16; 2 Wakorintho 3:17; 1 Petro 1:11 Katika vitabu hivyo tunahakikishiwa kuwa Hakika Roho Wa Mungu ni sehemu ya Utatu na Hakika yeye Ni Mungu kama alivyo Mungu Baba na Mungu Mwana. Alisemwa kwa mara ya kwanza wakati wa uumbaji, ikifuatiwa na Yesu ambaye aliumba kila kitu. Yohana 1:1-3. Tunaona Utatu huohuo katika Yesu wakati alipo kuwa anabatizwa, wakati Roho alipo shuka na tukasikia sauti ya Mungu Baba.
10. ROHO YA UZIMA (Spirit of Life)
Warumi 8:2 Neno Roho ya Uzima maana yake kuwa ni Roho Mtakatifu ambaye anatupa na au umba UZIMA, haimaanishi kuwa anasaidia wewe kuoka, bali anakufanya wewe kuwa umeokoka. Bila ya Roho Mtakatifu hakuna wokovu. HAPA VILE VILE tunaona Utatu katika Kazi ya Mungu. Tumeokolewa na Mungu Baba kupitia kazi ya Mwana wake Yesu, na wokovu unaedelezwa “sustained” na Roho Mtakatifu.
11. MWALIMU (Teacher)
Yohana 14:16; 1 Wakorintho 2:13. Yesu aliahidi kuwa Roho atawafundisha kila kitu na kuwakumbusha yote ambayo aliwafundisha wakati alipo kuwa nao. Waandishi wa Agano Jipya waliongozwa na Roho Mtakatifu ndio maana walikumbuka kila kitu ambacho Yesu alisema na kufanya.
Yohana 14: 26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
12. SHAHIDI (Witness)
Warumi 8:16; Waebrania 2:4; 10:15 Roho anaitwa SHAHIDI kwasababu YEYE anatuhakikishia na kutushuhudia kuwa sisi ni watoto wa Mungu, na kwamba Yesu na Wanafunzi wake walitumwa na Mungu Baba na kuwa Biblia ni Neno la Mungu. Zaidi ya hapo, Roho hutupa Zawadi ya Roho Mtakatifu, na utushuhudia sisi na dunia kuwa sisi tulio okolewa na Damu ya Yesu ni watoto wa Mungu.
Warumi Mlango wa 8:16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;
17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
Nakushauri uendelee kumwomba Mungu aliki aendelee kukufulia mambo makuu kupitia Roho Mtakatifu. Kumbu, bila ya Roho Mtakatifu, Wokovu wetu unakuwa wa mashaka. Ndio maana lazima tumfahamu huyu Roho Mtakatifu aliye ahidiwa kuja na Bwana wetu Yesu Kristo aliye kufa kwa ajili ya dhambi zetu.
Basi mpendwa, Mungu aendelee kukubariki.
Ni mimi, Mtumishi wake Max Shimba.
Katika huduma yake
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED

YESU KRISTO ALIUMBA HISABATI

Image may contain: 1 person, smiling
Najua unashangaa kivipi Yesu awe Mwana Mahesabu. Naam, katika somo hili tutajifunza Hisabati ambazo wana Hesabu wameshindwa kuziweka katika "practical" vitendo.
Sasa tuanze na aya tamu za Biblia: Yohana 6:1-14 au Soma Matayo 14:13-21. Nitaweka aya moja ya 17 katika Matayo: "tunayo Mikate Mitano na Samaki wawili"
Kwa akili za haraka haraka haiwezekani kwa Mikate Mitano na Samaki wawili kulisha watu zaidi ya Elfu tano.
Lakini kwa kutumia Hisabati za kawaida hesabu hiyo inawezekana, ila tunapo igeuza kuwa "VITENDO" haya mambo ni magumu sana. Je, Yesu aliwezaje kuwalisha watu elfu tano na zaidi kwa kutumia mikate mitano na samaki wawili?
Katika Hisabati kuna somo la "FACTORIAL NOTATION" hili somo ni la kuzidisha namba kinyume nyume mpaka namba ya chini kabisa ambayo ni moja.
Mfano:
1! = 1
2! = 2 × 1 = 2
3! = 3 × 2 × 1 = 6
4! = 4 × 3 × 2 × 1 = 24
5! = 5 × 4 × 3 × 2 × 1 = 120
Kimahesabu inawezekana lakini kivitendo kamwe hawa wana mahesabu hawata weza igeuza Mikate mitano na Samaki wawili kuwa "Factorial ya 7" na kuwalisha watu elfu tano.
Mikate Mitano (5) na Samaki wawili (2) ni sawa na vyakula Saba. Yaani kulikuwa na vipande saba vya vyakula ambavyo vinaweza kuliwa.
Bwana wetu Yesu ambaye ni Mungu Mkuu (Tito 2:13) anaweza kufanya atakalo na likawa.
Yesu katika aya ya 18 kwenye Matayo 14 alichukua hiyo Mikate Mitano na Samaki wawili akaangalia juu na kuvibariki. Akawagaia wanafuzi wake na kuwaambia, wapeni watu wale.
Kumbuka huyu ni Yesu aliye gauza maji ambayo yenye Chemical formula ya H2O na kuwa Divai yenye chemical formula ya C6H12O6 = 2CO2 + 2CH3CH2OH.
Je, kuna jambo lolote gumu ambalo Yesu hawezi kulifanya? Kwenye Yeremia 32:27 inakujibu kuwa, hakuna jambo gumu kwa Mungu wetu.
Sasa turudi kwenye somo la Mikate Mitano na Samaki 2. Kimahesabu ni sawa na kusema:
7! = 7 x 6 x 5 x 4 x 3 x 2 x 1 = 5040
Ngona nitumia formula ya Recursive:
Solved Example
Question: Simplify 10!6!
.
Solution:
10!6! inaweza kuandikwa kama 10×9×8×7×6!6!
=> 6! inaeza kukatwa with that in the denominator and the expression reduces to 10 × 9 × 8 × 7 = 5040.
=> 6! = 5040.
Recursive Definition of Factorial Notation
Back to Top
Recursive definition of factorial notation
(k + 1)! = (k + 1) . K!
Factorial notation has a place in both Permutation and combination formulas. Factorial notation comes into liberal play while evaluating Permutation and combination formula.
P(n,r) = n!(n−r)! na C(n,r) = n!(n−r)!r!
Naam, ndio maana mimi nampenda sana Yesu anayejua HESABU KUBWA KAMA HIZI, maana yeye aliziumba.
Wewe unaye mpinga Yesu, unaweza kunionyesha wapi mungu wako au mtume wako ameweza fanya Hisabati ngumu kama hizi?
Au wapi dini yako inaweza kutoa miujiza namna hii? Haya yote yanawezekana kwa Yesu Mungu Mkuu.
Shalom,
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo.

MUNGU ROHO MTAKATIFU ANAISHI NDANI YETU

Image may contain: one or more people and text
Ezekieli 36:27 “nami nitatia roho yangu ndani yenu na kuwaendesha katika sheria zangu nanyi mtazishika hukumu zangu na kuzitenda” maneno haya anayasema MUNGU kupitia kinywa cha nabii Ezekieli.
Ni Mungu aangaliae yote Zaburi 139:7 inasema “niende wapi njiepushe na Roho yako, Niende wapi niukimbie uso wako”
Ni maombi yangu Zaburi 51:11-12 inayosema “usinitenge na uso wako wala Roho Mtakatifu usiniondolee unirudishie furaha ya wokovu wako ,unitegemeze kwa Roho ya wepesi wako” yatimie kwako.
Katika Kumbukumbu la Torati anasema hivi Kumbukumbu la Torati 4:6 anasema “sikiza ee izraeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja” MUNGU ni mmoja anaposema nitatia roho yangu ndani yenu (yetu) maana yake Mungu kuja kukaa ndani yetu kupitia ROHO MTAKATIFU,
Biblia katika ule Waraka kwanza wa Yohana 4:8-9 anasema “kwa maana wako watatu washuhudiao[mbinguni Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu na hawa watatu ni umoja 9 kisha wako watatu washuhudiao duniani] Roho, na maji, na damu; na hawa hupatana kwa habari moja.tukipokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, amemshuhudia Mwanawe. Mungu mmoja aliye ziumba mbingu na nchi yeye Mungu na Roho Mtakatifu na Neno (Yesu) mbinguni ni umoja na duniani wako watatu wanaopatana kwa habari mmoja.
Watatu duniani Biblia inasema ni Roho Mtakatifu (Mungu pamoja nasi), Maji, na Damu. Kwa habari ya maji Biblia inasema hivi “Ezekieli 36:25 nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote” anaeleza habari ya utakaso. Damu ya YESU ndio ukombozi na upatanisho wetu ili tumwone Mungu.
ROHO MTAKATIFU ndiye aliyekuwa ndani ya Yesu akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake; Luka Mtakatifu anasema Luka 1:35 “Malaika kajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu MWANA WA MUNGU”
Maneno haya aliyasema Malaika Gabrieli alipokuwa akimweleza Mariamu juu ya kuzaliwa Yesu na matokeo yake ilikuwa hivi “Mathayo 1:18 “kabla hawajakaribiana alionekana ana mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu”.
Yesu ni Mungu na katika kitabu cha Waebrania anasema Waebrania 1:8 “lakini kwa habari ya mwana asema kiti chako cha enzi Mungu ni cha milele na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili”
Si wanadamu tu waliokili kuwa yesu ni mungu bali hata malaika waliotumwa na mungu walikiri kuwa yesu ni mungu “Luka 1:32-33 huyo atakuwa mkuu ataitwa mwana wa aliye juu, Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake, ataimiliki nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho” na tunajua ufalme wa mungu pekee ndio hauna mwisho na kupitia Yesu atamiliki nyumba ya Yakobo milele na milele. twaweza sema kwamba ufalme wake hauna mwisho kwa sababu yeye ni Mungu wa milele.
Matendo ya Mitume 1:8 Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa “mtapokea nguvu akiisha kuwajilia Roho Mtakatifu nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na katika uyahudi wote na Samaria na hata mwisho wan chi”
Tangu siku za yohana ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu tena nguvu za rohoni (nguvu za ROHO Mtakatifu) unapomwamini Yesu Roho Mtakatifu
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

Ancient Jewish Wedding Ceremony: “No man knows the day or hour, only the Father”

  The Ancient Jewish Marriage Rite: A Detailed Exposition of Betrothal, Preparation, and Consummation Dr. Maxwell Shimba Shimba Theological ...

TRENDING NOW