Friday, July 14, 2017

ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAPONYWA

Image may contain: one or more people and text


Nabii Yoeli alitabiri kuwa, “Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana. (Yoeli 2:32)
Mtume Paulo alitilia mkazo unabii huu aliposema,
“Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka” (Warumi 10:12-13).
Kila anayeliitia Jina la Bwana Yesu kwa imani anaponywa na, anaokoka kwa kuwa ndani ya jina hili la Yesu Kristo mna uponyaji na wokovu kwa kila amwaminiye Yesu Kristo.
Lakini mtume Paulo anauliza swali muhimu, ambalo ni muhimu kulitafakari, anasema, “Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?” (Warumi 10:14)
Hili jambo ni kweli. Huwezi kumwita mtu usiyemwamini. Hii ina maana ya kuwa ikiwa tunataka watu waliitie jina la Yesu Kristo ili waokoke na kuponywa madhaifu yao, inatubidi tufundishe na kuhubiri juu ya Yesu na jina lake.
Ndiyo maana Bwana Yesu Kristo alimwambia anania ya kuwa Paulo “ni chombo kiteule kwangu, ALICHUKUE JINA LANGU mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.” (Matendo ya mitume 9:15).
Biblia inasema pia kuwa, “Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, AKAWAHUBIRI KRISTO. Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia Kwa sauti kuu; Na watu wengi waliopooza, Na viwete, wakaponywa. Ikawa furaha kubwa katika mji ule” (Matendo 8:5-8)
Smith Wigglesworth aliyekuwa mhibiri wa inili nchini uiengereza miaka ya 1930 aliwahi kushuhudia katika mahubiri yake kuwa siku moja aliitwa kwenda kumuombea mgomjwa mmoja wa kifafaaliyekuwa amezidiwa hata kushindwa kuamka. Anasema watu wa eneno lile hata ndugu zake yule mgonjwa walikuwa wamekata tama. Waliona ndugu yao atakufa kwa ugonjwa huo, kwa hiyo ilimchukua muda Bwana Smith Wigglesworthkupata walio tayari kushirikiana naye katika kumwombea mgojwa yule.
Mwishowe alifanikiwa kuwapata na anasema walikizunguka kitanda cha yule mgonjwa na wakaanza kuliitia Jina La Yesu kwa pamoja wakisema “Yesu, Yesu, Yesu…” kwa kulirudia rudia jina hili. Baada ya kulitia jina la Yesu kwa muda hivi, anasema nguvu za Mungu zilishuka kitandani mwa yule mgonjwa, zikamtingisha mgonjwa na kitanda chake.
Yule mgonjwa akapona saa ile ile, akavaa nguo na kutoka nje. Kijiji kizima kilitaharuki na kushangaa kilipomuona mtu yule amepona. Smith Wigglesworth alipoona watu wamekusanyika hivyo wakishangaa, alichukua Biblia yake akahubiri, na watu wengi waliokoka na kutubu siku ile.
Ni muhimu ufahamu kuwa muujiza unaofanyika kwa Jina la Yesu Kristo unawavuta watu kwa Yesu Kristo, wamwamini na kumfuata. Ndiyo maana imeandikwa juu ya Yesu Kristo kuwa;
“Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizozifanya” (Yohana 2:23)
siku moja nilikuwa katika sehemu Fulani nikifundisha juu ya Jina La Yesu Kristo. Mwisho wa somo nilisema wanaotaka kujazwa na Roho Mtakatifu na wanene kwa lugha mpya pamoja na wagonjwa waje mbele. Watu wengi walikuja mbele.
Niliwaambia kuwa hatutaomba neno lolote zaidi ya kuliitia jina la Yesu kwa pamoja na kwa kulirudia rudia. Kwa pamoja tukaanza kuliitia jina la Yesu tukisema kwa sauti, “Yesu, Yesu, Yesu….”
Muda haukupia mwingi tukiwa bado tunaliitia Jina hili nikasikia toka upande wangu wa kushoto sauti ya mengi yakiporomoka. Nilijua hii ni ishara ya uwepo wa Roho Mtakatifukwani mahali tulipokuwa hakukuwa na mto wowote karibu, wala mvua ilikuw hainyeshi. Baadaye nilipowaeleza watu juu ya sauti hiyo ya maji mengi, kuna wengine waliosema kuwa pia waliisikia.
Tulipoendelea kuliitia Jina la Yesu Kristo, wagonjwa walipona, waliokuwa na mapepo walifunguliwa, na wengine walijazwa Roho mtakatifu na kuanza kuzungumza kwa lugha mpya! Ishara na miujiza mingi ilifanyika kwa Jina la Yesu Kristo!
Kumbuka Yesu Kristo alisema, “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya” (Marko 16:17-18).
Shalom,
Max Shimba mtuma wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW