Tuesday, August 13, 2013

JE, KUNATOFAUTI KATI YA KUPUNGA PEPO NA KUTOA PEPO?

Katika nyakati hizi za mwisho kumekuwa na roho nyingi zidanganyazo binadamu. Roho hizi za mpinga Kristo zinawadanganya wengi na kuwafanya wengi wajione kana kwamba wako na Mungu, kumbe Mungu hayupo kati yao na/au ndani ya maisha yao.

Katika soma hili, tutajifunza tofauti iliyopo kati ya Kupunga Pepo na Kutoa Pepo kwa ushaidi wa aya takatifu za Biblia.
( TIMOTHEO 4:1 ).
“Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza  roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”. Miongoni mwa mambo ya siku hizi za mwisho ni roho hizo kuwafanya watu wadanganyike na kufuata mafundisho ya uongo. Hao ni wale wanaoikataa ile kweli.
(2 TIMOTHEO 4:3-5 )
“Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo”.
(2 WATHESALONIKE 2:7-12 )
Watu ambao hawataki mafundisho ya utakatifu lakini wanataka kuona nguvu za Mungu maishani mwao, watadanganywa kwa ishara na ajabu za uongo.
Katika nyakati hizi tunaweza kuona jinsi watu wanavyofanyiwa maombezi kwa kuangushwa chini na hatimaye kusimama bila kupokea muujiza wa uponyaji. Utaweza kuona watu wamejazana madhabahuni wakigaagaa chini na baadaye husimama na kuondoka lakini wakati mwingine huchukua muda mrefu kwao kusimama na kuondoka. Jambo la kushangaza ni siku zote kuonekana watu haohao , mapepo yao hayatoki. Miujiza hii imeenea kote duniani, uatakuta watu wanapiga kelele lakini pepo hawawatoki watu hao. Miujiza ya kimungu huondoa pepo kabisa ndani ya mtu tena kwa mamlaka na kumwacha akiwa mzima. Watu hawa hawafanyi miujiza ya uponyaji bali wanapunga pepo. Ni muhimu kujua kuwa  hata wapagani wanaweza kupunga pepo na kuwafanya wapige kelele. Waganga wa kienyeji wanaweza kupunga pepo lakini hawawezi kuwatoa. Tunawaona wapunga pepo wakitaka kutoa pepo lakini wanashindwa  ( MATENDO 19:13-16 ). Watu hawa walikuwa wa kawaida lakini leo tungewaita walokole kwa kuwa walikuwa watu wa dini.
Jina jingine linalotumika kwa wapunga pepo ni” wapandisha pepo”. Mungu anasema kila anayepandisha pepo ni chukizo mbele zake ( KUMBUKUMBU LA TORATI 18:9-14 ). Waganga wa kienyeji ni wapandisha pepo au wapunga pepo. Kuna mazingira fulani  yanaandaliwa ili pepo wajidhihirishe kwao. Wanaimba na kuchezacheza ili nguvu hiyo ya shetani  iwe dhahiri kwa mfano  wetu tunavyofanya  katika kusifu au kuabudu ili nguvu ya Mungu ionekane  au idhihirike. Mfano Paulo na Sila gerezani walimsifu Mungu na nguvu za Mungu zikashuka milango ya gereza ikafunguka.
Kazi tuliyoitiwa  ni ya kutoa pepo na siyo kupunga au kupandisha pepo ( MARKO 16:17 ‘Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo”. MATHAYO 12:22-28 ). Kazi ya kupunga pepo ni ya shetani. Yesu aliuliza,” je, wana wenu huwatoa kwa nani?”. Swali hili la Yesu lilielekezwa kwa afarisayo walioishangazwa na mamlaka yake ya kuponya wagonjwa na kutoa pepo. Kimsingi hapo alikuwa akiuliza kuhusiana na wapunga pepo au wapandisha  pepo, kwamba wao wanatumia nguvu gain?
Kuna madaraja katika majeshi ya pepo. Katika kutoa kafara tofautitofauti kubwa au ndogo ndipo Mganga anapoweza  kupata pepo wa daraja la juu au la chini. Huyo anayelipa  leseni kubwa yaani kafara , anapewa uwezo mkubwa wa kipepo. Anakuwa na mamlaka makuu kama kamanda wa Jeshi hivyo anaweza kuwaamuru pepo kumwingia mtu na kunyamanzisha pepo wadogo waliomo ndani ya mtu lakini hatimaye hari ya huyo mtu baadaye inakuwa mbaya zaidi kwa sababu idadi yao ( pepo ) imeongezeka.

Wednesday, July 31, 2013

Islam offers HELL and that is all

Allah Promised hell for his followers:
 Sura 3:185, "Every soul shall have a taste of death: And only on the Day of Judgment shall you be paid your full recompense. Only he who is saved far from the Fire and admitted to the Garden will have attained the object (of Life): For the life of this world is but goods and chattels of deception."
This Suras from Quran very clearly says that after death everyone will go to hell fire then judgment.. When a person went to hell fire then how and why it is possible that he/she can come out from hell fire and go to paradise.. no way.. This verse does not say anything about eternal life. This verse very clearly says that every believer in Allah is tasting death means they did not get the life while Jesus promised eternal life and heaven as we read in
John 10:10 "The thief does not come except to steal, and to kill, and to destroy. I have come that they may have life, and that they may have it more abundantly.
And also every soul is going to hell fire till the day of judgment means they are not reaching heaven. So of course Allah promised hell fire for his believers.  There is no chance to go to heaven once you go to hell.  Jesus can save you when you are still in this world as He said in John 3:15 "that whoever believes in Him should not perish but have eternal life.

John 3:16 "For God so loved the world that He gave His only begotten Son, that whoever believes in Him should not perish but have everlasting life.

How a person can save himself/herself from hell fire when he/she is already in hell fire? And this verse says that they will be there till the time of Day of Judgment. Do you think a person who is already in hell  will get a seat in heaven after judgment? Judgment is a day when people get their sentence and verdict.. and there are no second chances to "make it to heaven" once you have been cast into hell.
And he claims all those who don't follow Islam are going to hell..so according to Muhammad, everyone is going to hell...
"If anyone desires a religion other than Islam (Submission to Allah), Never will it be accepted of him; and in the Hereafter he will be in the ranks of those who have lost."(Qur'an 3:85)

Sura Al-Nahl 16:28


The angels will say to those whom they cause to die in purity, ‘Peace be on you.’ Come into paradise for what you did.

Yaani:

[Kuhusu wale wanaoingia mbinguni] – Malaika watasema kwa wale ambao watawafanya wafe katika usafi (utakatifu), ‘Amani na iwe juu yenu. Ingieni paradiso kutokana na matendo yenu.’


LAKINI, QURAN HIYO HIYO INASEMA:


Sura Al-Hijr 15:45-47

Indeed, the righteous will be within gardens and springs, [Having been told], "Enter it in peace, safe [and secure]." And We will remove whatever is in their breasts of resentment, [so they will be] brothers, on thrones facing each other.

Yaani:

Wenye haki (watakatifu) watakaa kwenye bustani na chemchemi za maji, kwa amani na usalama wataingia humo. Nasi tutaondoa chuki yote ndani ya mioyo yao.

Maswali:

1.   Katika 16:28, inaonekana kwamba watakaiongia peponi ni watu walio safi kwa sababu malaika wamesababisha watu hao wafe wakiwa safi. Lakini 15:45-47 inaonyesha kuwa wataingia peponi wakiwa na chuki mioyoni mwao. Je, chuki ni sehemu ya usafi?
2.    Je, aya hizi zimetoka kwa mtoaji yule yule?
3. Kama chuki ni mbaya kiasi cha kuhitajika kuondolewa mioyoni mwa Waislamu wanaoingia peponi, iweje wakiwa duniani wanaagizwa kuwachukia wale wasio Waislamu (kama tulivyoona kwenye 4:101)?

Sura Al-Nisa 4:135


Believers, conduct yourselves with justice.

Yaani, 

Enyi mlioamini, enendeni kwa njia ya haki.

Hapa Allah anazungumzia juu ya haki.

LAKINI ALLAH HUYO HUYO ANASEMA:

Sura Al-Nisa 4:129

In no way you can treat your wives in a just manner even though you may wish to do that...

Yaani:

Haiwezekani kamwe kwa ninyi kuwatendea haki wake zenu hata kama mngependa kufanya hivyo ...

Maswali:

1.    Aya hizi zinafanana au zinapingana?
2.    Kama hazipingani ni kwa vipi?

Sura Al-Baqara 2:177


Righteousness is not that you turn your faces toward the east or the west, but [true] righteousness is [in] one who believes in Allah ...

Yaani:

Haki (mbele za Mungu) haitokani na mtu kugeukia mashariki au magharibi. Mtu mwenye haki ni yule anayemwamini Allah ...

LAKINI QURAN HIYO HIYO INASEMA:

Sura Al-Baqara 2:144

Indeed, we see you look repetedly towards heaven. We will make you turn towards a qiblah that will please you. So turn your face towards the sacred Mosque (qiblah). Wherever you are, turn your faces to it.

Yaani:

Tumekuona unavyoelekeza macho yako mbinguni tena na tena. Tutawafanya muigeukie qiblah itakayowafurahisha. Hivyo, geuzeni nyuso zenu kuelekea msikiti mtakatifu [japo quran zingine zinasema ‘towards al-Masjid al-Haram’ – najiuliza 'Haram' maana yake nini!!]

Maswali:

1.    Kama aliyesema aya hizi mbili ni yuleyule; na ni Mungu wa mbinguni, inakuwaje zinapingana?
2.  Kama zimetoka kwa Mungu wa mbinguni, si jambo la ajabu kuona kwamba hapendi watu waelekeze macho yake kule aliko badala yake waelekeze kwingineko? 
3. Kama wewe tunayekuabudu uko juu, kwa nini hautaki tuelekeza macho yetu huko? Huu si mkanganyiko?
4. Na kama wewe ni Mungu uliye mahali KOTE, kwa nini nielekeze macho yangu sehemu moja?

Sura Al-Kafirun 109:1-6


Say, "O unbelievers, I do not worship what you worship, nor do you worship what I worship. I shall never worship what you worship, nor will you worship what I worship. You have your own religion and I have mine."

Yaani,

Enyi msioamini, mimi siabudu mnachoabudu, wala ninyi hamuabudu ninachoabudu. Mimi kamwe sitaabudu kile mnachokiabudu, wala ninyi kuabudu kile ninachokiabudu. Ninyi mnayo dini yenu, nami nina yangu.

Pia, quran inasema katika sura Al-Baqara 2:256

There shall be no compulsion in religion.

Yaani:

Hakutakuwapo na kulazimishana katika dini.

LAKINI ALLAH HUYO HUYO ANASEMA:

Sura Al-Anfal 8:39

Make war on them until persecution is no more and Allah’s religion reigns supreme.

Yaani:

Fanyeni vita juu yao hadi kusiwepo na mateso tena na hadi pale dini ya Allah itakapokuwa imetawala.

Maswali:

1. Aliyemwambia Muhammad asiwalazimishe wasioamini kuamini Uislamu ndiye huyo huyo aliyemwambia afanye vita?
2. Aliyesema kuwa “ninyi msioamini hamtaabudu ninachoabudu” ndiye huyo huyo anayesema ni vita tu hadi dini ya Allah itawale?
3. Na je, aliyesema kuwa hakuna kulazimishana katika masuala ya dini ndiye huyo huyo anayesema watu wake wapigane vita?
4.    Huku si kujipinga mwenyewe?

Sura Al-Shura 42:40


Let evil be rewarded with like evil. But he that forgives and seeks reconcilement shall be rewarded by Allah.

Aya hii inamaanisha kuwa yule anayemwamini Allah akitendewa uovu basi anatakiwa alipe uovu, lakini akisamehe atapata thawabu!

Maswali:

1. Kama aliyetenda uovu anakuwa ametenda jambo baya ambalo halitakiwi na halikubaliki, iweje lile la mlipa kisasi litakiwe na kukubalika? Huku si kujikanganya?
2. Lakini hapo hapo, Allah anasema kuwa mwislamu anayesamehe na kusaka maelewano atapata thawabu kutoka kwa Allah. Unawezaje kukubali vitu viwili vinavyopingana? Kwa mfano, unawezaje kusema kuwa, mtu akikutukana, nawe ukimtukana ni sawa; na usipomtukana ni sawa!
3. Kikubwa kuliko chenzake ni kipi hapa sasa? Je, ni kulipa kisasi au kusamehe? Mbona mambo yenyewe hata hayafanani? Yanawezaje kwenda pamoja?

Sura Al-Ankabut 29:6

Quran inasema:

Allah does not need his creatures’ help.

Yaani,

Allah hahitaji kusaidiwa na viumbe wake. (bila shaka ni katika kutekeleza makusudi na mipango yake).

LAKINI QURAN HIYO HIYO INAWAAMBIA WAISLAMU:

Sura Muhammad 47:7

If you help Allah, He will help you and make you strong.

Yaani,

Kama mkimsaidia Allah, yeye naye atawasaidia na kuwafanya kuwa imara.

Maswali:

1.    Umesema huhitaji msaada, kisha unasema tena unahitaji msaada! Je, Mungu anaweza kufanya jambo kama hilo?
2.    Aya hizi zinafanana au zinapingana?
3. Je, hii si ishara kuwa aya hizi zilisemwa tu ili kukidhi mahitaji ya wakati fulani, lakini msemaji alipoona anahitaji kuwafanya watu watende kinyume chake, akajikuta amesema tofauti na alivyosema siku za nyuma?

Na tena quran inasema katika sura Al-Baqara 2:244

Fight for the cause of Allah and bear in mind that He hears all and knows all.

Yaani:

Fanyeni vita kwa ajili ya Allah na mkumbuke kwamba anaona yote na anajua yote.

Maswali:

1.    Kama kweli Allah hahitaji msaada wa viumbe wake; na kama kweli aliumba ulimwengu wote kwa NENO TU, iweje NENO hilo hilo lisiweze kuwabadilisha wanadamu hadi alazimike kuliingiza ndani yao kwa nguvu, kwa vitisho na kwa ukali namna hiyo?

(Ukristo unashinda na kufanikiwa kwa NENO tu. Maana sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu wetu. Yeye aliumba kwa Neno; na sisi watoto wake, tunaumba kwa Neno hilo hilo. Tunahubiri tu na watu wanaokolewa, wanaponywa, wanalindwa na kusimama na Mungu wa kweli. Huoni kwamba hii hasa ndiyo maana ya nguvu ya Mungu? Hatuhitaji kuchinja au kupiga watu ili wampende Mungu!! Unawezaje, hata tu wewe mwenyewe, kumfanya mwanao au mkeo akupende kwa njia ya vipigo na kulazimisha? yaani, ukitaka mwanao au mkeo akupende utamshikia rungu au panga au bunduki? Je, hiyo si ishara kwamba wewe huna nguvu ndiyo maana unalazimisha? je, huko si kujikanganya maana umetuambia kuwa wewe ni Mungu unayeweza yote?)
2.    Je, Allah anapotaka wanadamu wanaomwamini wafanye vita ili kuwalazimisha wasioamini wamwamini, huko si kutaka msaada kwa viumbe wake?

Sura Al-Baqara 2:109


Many of the People of the Book wish, through envy, to lead you back to unbelief, now that you have embraced the faith and the truth has been made plain to them. Forgive them and bear with them until Allah makes known His will. He has power over all things.

Hapa quran inaongelea watu wa kitabu (yaani Wakristo), na kusema:

Wengi wa watu wa kitabu, kutokana na wivu wao, wanatamani kuwarudisheni kwenye kutoamini baada ya kuwa mmeamini, pamoja na kwamba ukweli umeshadhihirishwa wazi mbele yao. Kwa hiyo wasameheni na kuwavumilia hadi Allah atakapowafunulia mapenzi yake. Yeye ana nguvu juu ya kila kitu. 

Quran pia inawaagiza Waislamu katika sura Al Imran 3:20  kwamba:

... if they give no heed, then your only duty is to warn them.

Yaani:

... kama wasipowasikiliza, basi ninyi kazi yenu pekee ni kuwaonya tu.

Kwa hiyo, kutokana na aya hizi mbili, yaani Al-Baqara 2:109 na Al Imran 3:20, tunaona mambo yafuatayo:

1.Ni wajibu wa Waislamu kuhubiri dini yao lakini si wajibu wao kuwalazimisha watu kuamini dini yao.
2.Allah kwa wakati wake atawafunulia wale wasioamini ukweli wa mambo.
3.Ni wajibu wa Waislamu kutoa maonyo tu kwa wale wanaowahubiria.

LAKINI, HEBU TAZAMA AYA ZIFUATAZO:

Al-Nisa 4:101

The unbelievers are your sworn enemies.

Yaani, 

Wale wasioamini ni maadui zenu wakubwa.

Vilevile inasema katika sura Al-Tawba 9:3

Proclaim a woeful punishment to the unbelievers.

Yaani:

Tangazeni mapigo makuu (ya ole) kwa wasioamini.

Pia quran inasema katika sura Al-Anfal 8:39

Make war on them until persecution is no more and Allah’s religion reigns supreme.

Yaani:

Fanyeni vita juu yao hadi kusiwepo na mateso tena na hadi pale dini ya Allah itakapokuwa imetawala.

Maswali:

1.    Je, aliyempa Muhammad maneno ya 2:109, 3:20 na yale ya 4:101, 9:3, 8:39 ni huyo huyo au ni wawili tofauti?
2.    Iweje aseme kuwa usiwalazimishe watu kuamini bali waonyeni na kuwavumilia tu, kisha anageuka sehemu nyingine na kusema walazimisheni, tena kwa vita?
3.    Je, hii si ishara ya tabia ya usahaulifu ambayo si tabia ya Mungu bali ni ya mwanadamu?
4. Kama ni huyo huyo, je, aya hizi zinafanana au zinapingana?
5.    Kama zinafanana, ni kwa vipi?
6.    Kama zinapingana, huu si ushahidi tayari kuwa quran haitoki kwa Mungu wa kweli kama ambavyo quran yenyewe imeweka kigezo cha kujua hilo? Maana Mungu wa kweli hawezi hata kidogo kusahau jambo alilolisema kabla halafu aje aseme kitu tofauti. Ni viumbe tu ndio wanaweza kusahau na kukosea.

Wednesday, July 24, 2013

Je, Walio-okoka Wanaweza Kwenda Jehanamu?

Kama Paulo anavyoandika, Mungu hutuadhibu “ili isitupase adhabu pamoja na dunia” (11:32). Dunia itahukumiwa kupotea milele. Basi, Mungu huwaadhibu waamini watendao dhambi ili wasiende jehanamu.


Hili linaleta maswali kadhaa ya muhimu. La kwanza ni hili: Je, kweli ipo hatari ya mwamini wa kweli kufika jehanamu?

Jibu ni NDIYO. Kama mwamini wa kweli atarudia kutenda zile “dhambi zinazotenganisha” – yaani, zile ambazo Maandiko yanasema zikitendwa, mtu hataweza kuingia katika ufalme wa Mungu (ona 1Wakor. 5:11; 6:9-10; Wagalatia 5:19-21; Waefeso 5:5, 6). Anapoteza uzima wa milele. Mungu hajaondoa hiari yetu, wala uwezo wetu wa kufanya dhambi. Kinyume na jinsi waalimu wengi wa siku hizi wanavyofundisha, Biblia inafundisha kwamba mwamini yeyote atakayefuata asili yake ya kale ya dhambi – au mwili – yuko katika hatari ya kufa kiroho. Paulo anasema hivi, anapowaandikia Wakristo:
Basi kama ni hivyo ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili. Kwa maana, kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanao-ongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu (Warumi 8:12-14. Maneno mepesi kutilia mkazo).
Inatubidi tuseme kwamba Paulo alikuwa anasema na waamini Wakristo walio hai kiroho, kwa sababu mbili.
Kwanza: Ona kwamba anawaita ndugu.
Pili: Walikuwa na uwezo wa kuyafisha matendo ya mwili kwa njia ya Roho. Hiki ni kitu ambacho waamini tu wanaweza kukifanya, ambao Roho wa Mungu anakaa ndani yao.
Ona sasa kwamba Paulo aliwaonya Wakristo Warumi kwamba, kama wangeishi kulingana na mwili, ni lazima wafe. Je, alikuwa anazungumza juu ya kifo cha kimwili au cha kiroho? Ni sahihi tukisema kwamba alikuwa anazungumzia juu ya kifo cha kiroho kwa sababu, kila mmoja – hata wale wenye “kuyafisha matendo ya mwili” – watakufa kimwili siku moja. Je, si kweli kwamba wale “wanaoishi kwa kuufuata mwili” mara nyingi huendelea kuishi katika mwili kwa muda mrefu tu?
Uamuzi tunaoweza kufikia kutokana na kweli hizi ni kwamba waamini Wakristo wanaweza kufa kiroho kwa “kuishi kwa kuufuata mwili”. Basi, zile orodha za “dhambi” za Paulo katika 1Wakor. 6:9-10; Wagalatia 5:19-21 na Waefeso 5:5-6 hazipaswi kufikiriwa kwamba zinawahusu wale tu wasiokiri kumwamini Kristo. Zinawahusu hata wale ambao wamekiri kumwamini Kristo. Ukweli ni kwamba, katika mantiki yake, zile dhambi ziliandikwa ili kuwa maonyo kwa waamini. NI wale wanao-ongozwa na Roho badala ya mwili ndiyo walio wana wa kweli wa Mungu, kama Paulo alivyosema waziwazi kabisa (ona Warumi 8:14).

Uthibitisho Zaidi Kwamba Walio-Okoka Wanaweza Kufa Kiroho

Paulo aliandika maneno kama hayo kwa Wakristo Wagalatia. Baada ya kuwaonya kwamba wale wanaojihusisha na “matendo ya mwili” hawataurithi ufalme wa Mungu, alisema hivi:

An Academic Critique of Internal Contradictions in the Quran with Reference to Eschatological Descriptions of Hell’s Sustenance

  Title: An Academic Critique of Internal Contradictions in the Quran with Reference to Eschatological Descriptions of Hell’s Sustenance Au...

TRENDING NOW