Wednesday, July 24, 2013

Je, Walio-okoka Wanaweza Kwenda Jehanamu?

Kama Paulo anavyoandika, Mungu hutuadhibu “ili isitupase adhabu pamoja na dunia” (11:32). Dunia itahukumiwa kupotea milele. Basi, Mungu huwaadhibu waamini watendao dhambi ili wasiende jehanamu.


Hili linaleta maswali kadhaa ya muhimu. La kwanza ni hili: Je, kweli ipo hatari ya mwamini wa kweli kufika jehanamu?

Jibu ni NDIYO. Kama mwamini wa kweli atarudia kutenda zile “dhambi zinazotenganisha” – yaani, zile ambazo Maandiko yanasema zikitendwa, mtu hataweza kuingia katika ufalme wa Mungu (ona 1Wakor. 5:11; 6:9-10; Wagalatia 5:19-21; Waefeso 5:5, 6). Anapoteza uzima wa milele. Mungu hajaondoa hiari yetu, wala uwezo wetu wa kufanya dhambi. Kinyume na jinsi waalimu wengi wa siku hizi wanavyofundisha, Biblia inafundisha kwamba mwamini yeyote atakayefuata asili yake ya kale ya dhambi – au mwili – yuko katika hatari ya kufa kiroho. Paulo anasema hivi, anapowaandikia Wakristo:
Basi kama ni hivyo ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili. Kwa maana, kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanao-ongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu (Warumi 8:12-14. Maneno mepesi kutilia mkazo).
Inatubidi tuseme kwamba Paulo alikuwa anasema na waamini Wakristo walio hai kiroho, kwa sababu mbili.
Kwanza: Ona kwamba anawaita ndugu.
Pili: Walikuwa na uwezo wa kuyafisha matendo ya mwili kwa njia ya Roho. Hiki ni kitu ambacho waamini tu wanaweza kukifanya, ambao Roho wa Mungu anakaa ndani yao.
Ona sasa kwamba Paulo aliwaonya Wakristo Warumi kwamba, kama wangeishi kulingana na mwili, ni lazima wafe. Je, alikuwa anazungumza juu ya kifo cha kimwili au cha kiroho? Ni sahihi tukisema kwamba alikuwa anazungumzia juu ya kifo cha kiroho kwa sababu, kila mmoja – hata wale wenye “kuyafisha matendo ya mwili” – watakufa kimwili siku moja. Je, si kweli kwamba wale “wanaoishi kwa kuufuata mwili” mara nyingi huendelea kuishi katika mwili kwa muda mrefu tu?
Uamuzi tunaoweza kufikia kutokana na kweli hizi ni kwamba waamini Wakristo wanaweza kufa kiroho kwa “kuishi kwa kuufuata mwili”. Basi, zile orodha za “dhambi” za Paulo katika 1Wakor. 6:9-10; Wagalatia 5:19-21 na Waefeso 5:5-6 hazipaswi kufikiriwa kwamba zinawahusu wale tu wasiokiri kumwamini Kristo. Zinawahusu hata wale ambao wamekiri kumwamini Kristo. Ukweli ni kwamba, katika mantiki yake, zile dhambi ziliandikwa ili kuwa maonyo kwa waamini. NI wale wanao-ongozwa na Roho badala ya mwili ndiyo walio wana wa kweli wa Mungu, kama Paulo alivyosema waziwazi kabisa (ona Warumi 8:14).

Uthibitisho Zaidi Kwamba Walio-Okoka Wanaweza Kufa Kiroho

Paulo aliandika maneno kama hayo kwa Wakristo Wagalatia. Baada ya kuwaonya kwamba wale wanaojihusisha na “matendo ya mwili” hawataurithi ufalme wa Mungu, alisema hivi:
Msidanganyike. Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho (Wagalatia 6:7-9. Maneno mepesi kutilia mkazo).
Ona hapo kwamba watu wawili wanatofautishwa. Mmoja anapanda kwa mwili wake na mwingine kwa Roho. Wa kwanza anavuna uharibifu na wa pili anavuna uzima wa milele. Kama uharibifu ndicho kinyume cha uzima wa milele, basi bila shaka maana yake nyingine ni kifo cha kiroho. Ona hapa kwamba kuvuna uzima wa milele kunaahidiwa kwa wale tu wanaopanda kwa Roho, na wanaoendelea kupanda kwa Roho. Wale wanaopanda kwa mwili hawatavuna uzima wa milele bali uharibifu. Kama Paulo alivyotoa onyo, “Msidanganyike” kuhusu hilo! (Wagalatia 6:7). Lakini, wengi sana wamedanganyika siku hizi.
Kupanda kwa mwili ni kitu kilichomkera sana mtume Paulo, ambaye, kama Mkristo mwingine yeyote wa kweli, bado alikuwa na asili ya dhambi. Aliwaandikia Wakorintho kama ifuatavyo:
Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote. Basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika. Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa (1Wakor. 9:25-27. Maneno mepesi kutilia mkazo)
Sawa na wanariadha wa Olimpiki, sisi pia lazima tuwe na kiasi kama tunatazamia kupokea zawadi yetu isiyoharibika. Paulo anataja kwamba aliutesa mwili wake na kuufanya mtumwa wake, kwa sababu kama asingefanya hivyo, alikuwa katika hatari ya “kukataliwa”. Mtu anapokataliwa, hakuna tumaini kwamba atashinda. Mantiki ya maneno ya Paulo yanaweka wazi kwamba yeye hakuwa na wasiwasi juu ya kupoteza nafasi zingine za baadaye kufanya huduma, au thawabu za mbinguni, bali kupoteza kabisa wokovu wake. Katika mistari inayofuata (1Wakor. 10:1-4) Paulo aliwaonya Wakristo Wakorintho wasifuate mfano mbaya wa Waisraeli, ambao, ingawa hapo kwanza walikuwa wamebarikiwa sana na kuwa na fursa nyingi, waliangamia nyikani baadaye kwa sababu hawakuendelea katika utii wa imani. Tofauti na Waisraeli walioangamia, waamini wa Korintho waliambiwa wakimbie choyo, kuabudu sanamu, uchafu (ambazo ni dhambi alizotaja Paulo katika orodha yake ya 6:9-10), kumjaribu Mungu na kunung’unika. Pia aliongeza ushauri huu: “Kwa hiyo, anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke” (1Wakor. 10:12).

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW