Wednesday, July 31, 2013

Sura Al-Baqara 2:109


Many of the People of the Book wish, through envy, to lead you back to unbelief, now that you have embraced the faith and the truth has been made plain to them. Forgive them and bear with them until Allah makes known His will. He has power over all things.

Hapa quran inaongelea watu wa kitabu (yaani Wakristo), na kusema:

Wengi wa watu wa kitabu, kutokana na wivu wao, wanatamani kuwarudisheni kwenye kutoamini baada ya kuwa mmeamini, pamoja na kwamba ukweli umeshadhihirishwa wazi mbele yao. Kwa hiyo wasameheni na kuwavumilia hadi Allah atakapowafunulia mapenzi yake. Yeye ana nguvu juu ya kila kitu. 

Quran pia inawaagiza Waislamu katika sura Al Imran 3:20  kwamba:

... if they give no heed, then your only duty is to warn them.

Yaani:

... kama wasipowasikiliza, basi ninyi kazi yenu pekee ni kuwaonya tu.

Kwa hiyo, kutokana na aya hizi mbili, yaani Al-Baqara 2:109 na Al Imran 3:20, tunaona mambo yafuatayo:

1.Ni wajibu wa Waislamu kuhubiri dini yao lakini si wajibu wao kuwalazimisha watu kuamini dini yao.
2.Allah kwa wakati wake atawafunulia wale wasioamini ukweli wa mambo.
3.Ni wajibu wa Waislamu kutoa maonyo tu kwa wale wanaowahubiria.

LAKINI, HEBU TAZAMA AYA ZIFUATAZO:

Al-Nisa 4:101

The unbelievers are your sworn enemies.

Yaani, 

Wale wasioamini ni maadui zenu wakubwa.

Vilevile inasema katika sura Al-Tawba 9:3

Proclaim a woeful punishment to the unbelievers.

Yaani:

Tangazeni mapigo makuu (ya ole) kwa wasioamini.

Pia quran inasema katika sura Al-Anfal 8:39

Make war on them until persecution is no more and Allah’s religion reigns supreme.

Yaani:

Fanyeni vita juu yao hadi kusiwepo na mateso tena na hadi pale dini ya Allah itakapokuwa imetawala.

Maswali:

1.    Je, aliyempa Muhammad maneno ya 2:109, 3:20 na yale ya 4:101, 9:3, 8:39 ni huyo huyo au ni wawili tofauti?
2.    Iweje aseme kuwa usiwalazimishe watu kuamini bali waonyeni na kuwavumilia tu, kisha anageuka sehemu nyingine na kusema walazimisheni, tena kwa vita?
3.    Je, hii si ishara ya tabia ya usahaulifu ambayo si tabia ya Mungu bali ni ya mwanadamu?
4. Kama ni huyo huyo, je, aya hizi zinafanana au zinapingana?
5.    Kama zinafanana, ni kwa vipi?
6.    Kama zinapingana, huu si ushahidi tayari kuwa quran haitoki kwa Mungu wa kweli kama ambavyo quran yenyewe imeweka kigezo cha kujua hilo? Maana Mungu wa kweli hawezi hata kidogo kusahau jambo alilolisema kabla halafu aje aseme kitu tofauti. Ni viumbe tu ndio wanaweza kusahau na kukosea.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW