Friday, November 8, 2013

UTATA KATIKA UUMBAJI WA MAJINI

ALLAH: UTATA KATIKA UUMBAJI WA MAJINI
Je, Majini yaliumbwaje?

Leo hii tutajifunza UTATA wa Allah katika uumbaji wa Majini. Hebu tusome kwanza hii aya kutoka Koran iliyo shushwa na Jibril ambaye ni msaidizi wa Allah. 

Quran 15: 27. Na Majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto. ***

Katika aya hapo juu tumesoma kuwa Allah aliumba Majini kwa "MOTO" wa upepo Umoto. Hivyo ndivyo Majini yaliumbwa kutokana na Koran. Lakini nilipo soma kwa uzaidi na au undani Je, Allah aliumba vipi vitu vyote vyenye uhai, nilibakia nikishangaa kama Majini nayo yapo kwenye viumbe vyenye uhai. Hebu soma hii aya hapa chini.

Quran 21: 30. Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabandua? Na tukaumba kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini? ***

Katika aya tuliyo isoma ya 30. Allaha anasema kuwa aliumba kila kitu chenye uhai kupitia 'MAJI" Je, Majini ni viumbe vyenye uhai. Kama ni kweli, kwanini Koran inatuambia kuwa Majini yaliumbwa kupitia MOTO. 

Ndugu zanguni, leo, kwa mara nyingine tena Allah amesema UONGO. 

Kwanini tumfuate Allah mwenye kigeugeu namna hii?

Katika Huduma yake

Max Shimba Ministries Org.

No comments:

Mohammad’s Myths vs. Biblical and Scientific Reality: A Scholarly Debate on Laughter, Heart, and Divine Truth

By Dr. Maxwell Shimba, Shimba Theological Institute Introduction In evaluating the truth-claims of any religion, the alignment between i...

TRENDING NOW