Monday, December 14, 2015

JINSI YA KUTOA PEPO WABAYA/CHAFU

Maana ya neno pepo linamaanisha, pepo mbaya, shetani, mwovu, mharibifu na mwangamizi. Hao ni malaika waliomuasi Mungu wakatupwa duniani. “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na Yule joka (Shetani), Yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; Nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, Yule mkubwa, Yule wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Ufu 12:7-9.
1. Ili kutoa pepo, kuna mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa:
Ni lazima uwe na nguvu za Roho Mtakatifu.Tunaweza kujifunza kwa Yesu alivyoweza kutoa pepo kwa uwezo na nguvu za Roho. Imeandikwa, “…..awaaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.” Luka 4:36.
2. Kutoa pepo kwa jina la Yesu. Aliye na amri na mamlaka ya kutoa pepo ni mkristo ambaye amemwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake. “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo……” Math 16:17. Wale ambao bado hawajamwamini Yesu na kuokoka, Si vyema kujaribu kutoa Pepo kwa sababu hatatoka, vile vile wanaweza kushambuliwa na hao walio na Pepo, kama wale wana wa Skewa, Kuhani Mkuu.
“.....wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nakuapisha kwa Yesu, Yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, Kuhani Mkuu, walifanya hivyo..... na yule mtu aliye pagawa na pepo wachafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.” Mdo 19:13-16.
3. Kufanya maombi kila siku na wakati mwingine kufunga. Bila kufanya hivyo haiwezekani kwa neno lolote, ndio maana Yesu alisema “Lakini kwa namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.” Mat 17:21.
4. Kutoa pepo kwa imani. Unaweza kujifunza kwa wale wanafunzi wa Yesu waliposhindwa kumtoa pepo Yule kijana. Walishindwa kwa sababu ya upungufu wa imani. Wangekuwa na imani wangeweza kumtoa Yule pepo. “Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakisema, mbona sisi hatukuweza kumtoa? Yesu akawaambia kwa sababu ya upungufu wa imani yenu…..” Mat 17:19-20.
5. Kutoa pepo kwa amri na mamlaka. Unaamuru kwa jina la Yesu atoke naye hutoka. Tunaweza kujifunza kwa Mtume Paulo alivyomtoa pepo Yule kijakazi, akaamuru kwa kumwambia Yule pepo, “..…nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo mtoke huyu, Akamtoka saa ile ile.” Mdo 16:18.
6. Makosa yanayofanyika kwa wale ambao wanakemea pepo, kwa kuwaambia ninakuangamiza kwa damu ya Yesu, ninakuteketeza kwa moto, au ninakufunga. Kufanya hivyo ni kinyume na mamlaka ya Mungu aliyowapa watoto wake. Kwa sababu hiyo, Mungu hajatupa mamlaka ya kuwaangamiza, Kuwateketeza, wala kuwafunga. Bado pepo watakuwepo katika dunia hii kwa sababu wakati wao wakuhukumiwa na kuteswa haujafika. Ndio maana pepo walipomuona Yesu, “…..wakasema,Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?” Mat 8:23.
7.Wakati wa kumhudumia mwenye pepo si sahihi kuongea na mapepo na kuwaliza maswali wametoka wapi, nani akawatuma, ni kwa nini wanamtesa huyo mtu. Hatupaswi kumsikiliza shetani na mapepo yake kwa sababu wao ni waovu na waongo siku zote. “....Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewwe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo” Yn 8:44. Yesu Krsto hakufanya hivyo ambaye ndiye kielelezo chetu katika utumishi, ijapokuwa alimwona yule mtu aliyekuwa amepagawa na kuteseka siku nyingi alimuuliza swali akitaka kujua jina lake, si jina la pepo.Badala yake pepo waliokuwa wamemtawala yule mtu walijibu wao ni jeshi. “Yesu akamwuliza jina lako nani? Akasema jina langu ni jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia”. LK 8:30.
Pepo atolewapo hutaka kurudi.
Pepo anapotolewa ndani ya mtu aliyempagawa huondoka na baadae hurudi na kuangalia kama anaweza kuingia tena.Ikiwa mtu huyo anaishi maisha ya dhambi huona nyumba ni chafu na kuingia."Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, aspate. Halafu husema, nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. Mara huenda akachukua pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya". Mt12:43-45.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW