Monday, December 14, 2015

YESU NI MUNGU NA ANATAKA KUKUOKOA

Watu wengi wanaelewa kuwa Yesu alikuwa mtu ambaye aliishi Israeli miaka 2000 iliyopita. Takribani kila dhehebu ulimwenguni lamchukulia Yesu kama mwalimu mwema/nabii. Huku hayo mambo yakiwa kweli kuhusu Yesu, hayaangazii kabisa Yesu kwa ni nani, ama kuelezea jinzi au kwa nini Yesu aokoa. Yesu ni Mungu katika mwili wa binadamu (Yohana 1:1,14). Yesu ni Mungu, alikuja ulimwenguni kama mwanadamu wa kweli (1Yohana 4:2). Mungu alikuja akawa mwanadamu katika Yesu ili atuokoe. Hiyo yaleta swali lifuatalo: Ni kwa nini tunaitaji kuokolewa?
Yesu anawaokoa wale wote wanaopokea tuzo lake la wokovu. Yesu anawaokoa wale wote wanaomwamini katika dhabihu yake pekee kama fidia ya dhambi (Yohana 3:16; Matendo 16:31). Huku Yesu kama dhabihu ilikuwa kamilifu na yatosha kulipia dhambi zote za binadamu, Yesu pekee ndiye aweza kuokoa wale pekee wanaoipokea zawadi yake (Yohana 1:12)
Kama sasa unaelewa yamaanisha nini Yesu aokoa, na unataka kuweka imani kwake kama mwokozi wa maisha yako, akikisha kwamba unaelewa na kuamini yafuatayo, na kama hatua ya imani, nena maneno yafuatayo,
SALA YA TOBA
Inawezekana kabisa ya kuwa wewe unayesoma ujumbe huu hujaokoka - yaani hujampokea Yesu Kristo ndani ya moyo wako kama Bwana na Mwokozi wako. Lakini sasa umeona umuhimu wa kumpokea Yesu Kristo katika maisha yako.
Naamini Roho Mtakatifu ameweka fursa hii mikononi mwako kwa mpango maalum wa Mungu ili ufike mahali pa kutubu na kuokoka. Inawezekana kabisa, pia ya kuwa hujawahi kuambiwa juu ya umuhimu wa wewe kuokoka. Lakini napenda kukuambia ya kuwa ni mpango wa Mungu uokoke. Soma Wakolosai 1:13,14 na Yohana 1:12-14 na 1 Timotheo 2:3-6 na Warumi 1:16,17 na Yohana 3:7. Ni vigumu kuona baraka za Damu ya Yesu bila ya kuokoka.
Kwa hiyo kama unataka kuokoka - tafuta mahali palipo na utulivu, na usome kwa sauti sala ifuatayo: (ukiweza unaweza kupiga magoti unapoomba sala hii)
“Ee Mungu wangu ulie Mtakatifu. Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu. Ninatubu kweli. Naomba damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi yangu na mwili wangu.
Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho wako – uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Ahsante kwa kunisamehe na kwa kuniokoa. Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina.
Ikiwa umesoma sala hii kwa kukusudia kabisa na kwa imani, basi wewe umeokoka na dhambi zako zimesamehewa na kusahauliwa na Mungu sawasawa na alivyoandika katika neno lake. Damu ya Yesu iko juu yako sasa.
Baada ya kuokoka
Unapoanza maisha haya mapya katika Yesu Kristo nakushauri mambo yafuatayo:
1.Zungumza na Mungu kwa maombi kila siku (Yohana 15:7)
2. Soma Neno la Mungu (Biblia) kila siku (Matendo ya Mitume 17:11)
3.Mruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-25; Warumi 8:14-17)
4.Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1Petro 5:7; Zekaria 4:6)
5.Usiache kukusanyika na kushirikiana na wengine waliompokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao kama wewe ili uimarike zaidi (Waebrania 10:25)
Ukipenda unaweza kuniandikia kwa anwani hii hapa chini juu ya uamuzi uliofikia leo wa kuokoka, ili tumshukuru Mungu pamoja, na tuzidi kukuombea; na pia, tukutumie maandiko mengine ya kukusaidia: maxshimbaministries@gmail.com
Max Shimba Ministries

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW