Tuesday, June 21, 2016

ALLAH ATEREMSHA AYA NA KUSEMA UISLAMU NI DINI YA WAARABU NA SIO WAAFRIKAKatika hii mada ninawaletea ushaidi kuwa Uislam ni dini ya Waarabu peke yao.
Waislamu bila kuchoka wamekuwa wakidai kuwa Uislamu utatawala dunia nzima. Katika kufanya hivyo, wao watakuwa wamekwenda kinyume na maneno ya Allaha kama yarivyo teremshwa kwenye Qur'an. Kwa hiyo, ni haki kwa kusema wao ni Makafiri.
Quran 10: 47. Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa.
Angalia hii aya pia
Quran 14: 4. Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Allah humuacha akapotea amtakaye, na akamwongoa amtakaye. Naye ni Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
Kama aya hizi ni kweli, basi Uislamu si kwa mashirika/mataifa/ummah yasiyo ya Waarabu. Quran inasema kwamba kila watu wamepokea ujumbe wao kutoka kwa Mungu katika lugha yao wenyewe ili waweze kuelewa na Qur'ani akaishuka kwa Waarabu ili Waarabu waweze kulewa nini Allah anasema.
Dhana hii ya Allah kushusha Kitabu kwa kila lugha ni muhimu sana kwasababu imejirudia mara nyingi na ndio msingi wa hili somo.
Quran 16: 36. Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa MwenyeziMungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha.
Quran 5: 48. Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo yenu nyote, na atakuja kuwaambieni yale mliyo kuwa mkikhitalifiana.
Quran 36: 5. Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. 6. Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa , basi wao wamekuwa wenye kughafilika.
Hizi aya zimekamilka na kueleza kiuwazi kuhusu kuja kwake kwa Waarabu pekee. Allah katika Koran anasema kwamba kila watu wamekuwa na Mtume wao wenyewe ambao aliwaonya katika lugha zao wenyewe, na kwamba amemtuma Muhammad kwa wale ambao bado hawajaanza mwongozo wowote, na ambao baba zao hawakuonywa, yaani Waarabu. Kwa njia hii watakuwa hawana udhuru wowote na hawezi kusema, lakini hatukuwai kupokea ujumbe wowote.
Endelea kusoma Koran hapa chini:
Quran 6: 156. Msije mkasema: Hakika mataifa mawili kabla yetu yameteremshiwa Kitabu; na sisi tulikuwa hatuna khabari ya waliyo kuwa wakiyasoma.
157. Au mkasema: Lau kuwa tumeteremshiwa sisi Kitabu tungeli kuwa waongofu zaidi kuliko wao. Basi imekufikieni bayana kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema. Basi nani aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye kanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo? Tutawalipa wanao jitenga na Ishara zetu adhabu kali kabisa kwa sababu ya kujitenga kwao.
Quran ni wazi ilitumwa kwa Waarabu. Wale ambao si Waarabu hawawezi kuielewa Koran, hayo ni maneno ya Allah. Waislamu wanasisitiza kuwa hakuna tafsiri ya Qur'ani inaweza kuwa sahihi. Hivyo, haiwezi kamwe kuwa wazi kwa mashirika yasiyo ya Waarabu na haikutumwa kwa mashirika/ummah yasiyo ya Waarabu.
Uthibitisho mwingine kuwa Qur'ani ilitumwa tu kwa ajili ya Waarabu ni katika mistari ifuatayo hapo chini:
Quran 26: 198. Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu, 199. Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini.
Kama ambavyo Waarabu wana haki ya kuto amini kitabu chechote kile kilichotumwa kwa lugha ambayo si yakwao, ikimaanisha Kiarabu, vivyo hivyo, mashirika yasiyo ya Waarabu nao wana haki ya kuto iamini Koran, kitabu kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu. Ndio kwasababu Koran inasema Allah atatuma mjumbe kwa kila lugha ili wao wenyewe kwa wenyewe waweze kuelewa.
Kuhakikisha hakuta kuwa na kutokuelewana, Allah anashusha hii aya 05:19 Quran: Enyi Watu wa Kitabu! Bila ya shaka amekujilieni Mtume wetu akikubainishieni katika wakati usio kuwa na Mitume, msije mkasema: Hakufika kwetu mbashiri wala mwonyaji. Basi amekujieni mbashiri na mwonyaji. Na Mwenyezi Mungu anao uweza wa kila kitu.
Kwa mujibu wa Qur'an watu wote wamepokea ufunuo. Aya ya hapo juu inasema Qur'ani ni kwa wale ambao kamwe hawakupokea ufunuo, iliwasije kusema, `kuwa sisi hatuja wai kutumiwa mbashiri na hakuna mjuonyaji aliye tumwa kwetu'.
Jambo hili ni wazi, lakini Allah anataka liwe wazi hata na kwa asiye na ufahamu wowote ule aelewe kuwa Koran ilitumwa kwa Waarabu pekee kwa kuzitaja sehemu halisi za kijiografia ambazo Muhammad alitumwa kama Mtume wa Allah.
Quran 6:92. Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa, chenye kuhakikisha yaliyo tangulia, na ili uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Na wenye kuamini Akhera wanakiamini hichi, nao wanazihifadhi Sala zao.
Leo, tumejifunza kuwa, Koran ilitumwa kwa Waarabu pekee na si kwa Mataifa yote. Sasa, nina uhakika baadhi ya Waislamu wanaweza kuleta aya nyingine zinazosema kwamba Uislamu ni kwa wanadamu wote. Kama Waislam watafanya hivyo, basi waelekuwa kwa kufanya hivyo ni kuthibitisha kwamba aya hapo juu ni za uongo.
Ama Quran ni pakiti ya uongo na utata au ni tu kwa Waarabu wa Makkah na jirani yake kama alivyo sema Allah ambaye ni mungu wa Waislamu.
Katika huduma yake,
Max Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW