Saturday, June 18, 2016

MAANA YA KUFUNGA KATIKA UKRISTO

Katika somo letu la "Maana ya kufunga katika Ukristo" tutajifunza maana ya neno "Kufunga na "Swaumu".
Nini maana ya KUFUNGA?
Neno “Kufunga“ linatokana na neno la Kiyunani “Nestevo“, ambalo ni muunganiko "consolidation" or "integral" wa maneno mawili ya Kiyunani “NE“ na “Esthio“. Neno “NE“ ikiwa na maana ya “bila“ au “hapana“, Kiingereza “no“ au “without“.
Neno “ESTHIO“ ikimaanisha “kula chakula au kunywa kinywaji“, Kiingereza “to eat solid food or drink liquid“. Neno “NESTEVO” sasa linaunga maneno hayo mawili ya Kiyunani ”NE” na “ESTHIO”, na lina maana “bila kula chakula au kinywaji chochote kile”. Hivyo maana ya kufunga, ni “bila ya kula chakuna na kinywaji chechote”.
Nini maana ya "SWAUMU"?
Neno Saumu katika lugha ya kiarabu maana yake ni 'Kujizuwia'. Yote sawa ikiwa kujizuwia na kula au kujizuwia na kusema, nk.
Bibi Maryam baada ya kumzaa Nabii Issa (Alayhas Salaam), alisema;
"Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa rehema ya kufunga, kwa hivyo leo sitasema na mtu".
Maryam - 26
Kwa hivyo hapa Bibi Maryam (Alayhas Salaam) ametumia neno 'Sauma' pale aliposema ((Inniy nadhartu lilrahmani 'Sauma')), si kwa maana ya kujizuwia na kula, bali kwa maana ya kujizuwia na kusema.
Anasema Abu Ubaidah (Radhiya Llahu anhu);
"Neno 'Saumu' katika lugha ya kiarabu, maana yake ni 'Kujizuwia na kula au kujizuwia na kusema au na kwenda".
SASA TUNAGALIE, BIBLIA INASEMA NINI KUHUSU KUFUNGA:
Nyakati za Biblia, watu walifunga kwa sababu mbalimbali zilizokubaliwa na Mungu. Baadhi yao walifunga kwa sababu ya huzuni au toba (1 Samweli 7:4-6), wengine walifunga ili kuomba mwongozo wa Mungu au ili wapate kukubaliwa naye (Waamuzi 20:26-28; Luka 2:36, 37), au ili kukaza fikira walipotafakari.—Mathayo 4:1, 2.
Bibilia inawazilisha kufunga kama kitu ambacho ni kizuri, cha muimu na cha manufaa. Kitabu cha Matendo Ya Mitume kimerekodi kuwa Wakristo walifunga kabla ya kufanya uamuzi wa maana (Matendo Ya Mitume 13:2, 14:23). Kufunga na maombi kila mara zimeambatanishwa pamoja (Luka 2:37; 5:33). Kila mara, angazo la kufunga ni kutokuwa na chakula. Badala ya lengo kuwa, kufunga ni kuyapeleka mawazo yako nche ya vitu vya dunia na kiukamilifu kumtazamia Mungu. Kufunga ni njia mojawapo ya kudhihirishia Mungu na sisi wenyewe kwamba hatutaki mchezo katika uhusiano wetu na yeye. Kufunga kunatuzaidia kupata mtazamo na kufanya upya tegemeo letu kwa Mungu.
Katika matukio kadhaa katika Agano la Kale, kufunga kunahusishwa na maombi ya kuombea. Daudi aliomba na kufunga juu ya mtoto wake mgonjwa (2 Samweli 12:16), akilia kwa bidii mbele za Bwana katika maombezi (vv. 21-22). Esta alimsihi Mordekai na Wayahudi kufunga kwa ajili yake alipokuwa akipanga mbele ya mumewe mfalme (Esta 4:16). Ni wazi, kufunga na kuomba sina uhusiano wa karibu.
Kwa kuchukua macho mbali na vitu vya dunia, tunaweza zaidi kuyaweka mawazo yetu kwa Kristo. Kufunga sio njia ya kumfanya Mungu atende vile tunavyotaka. Kufunga kunatubadilisha, sio kumbadilisha Mungu. Kufunga sio njia ya kuonekana mwokovu sana kuliko wengine. Kufunga kunastahili kufanyika kwa moyo wa unyenyekevu na nia ya furaha.
Mathayo 6:16-18 yasema, “Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamna; maana hujiimbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
1. Katika Ukristo hakuna kula daku wakati wa kufunga.
2. Yesu hakula daku wala futari wakati alipo funga kwa siku Arobaini.
3. Yesu hakujioneysha kwa wanafunzi wake kuwa alikuwa anafunga bali ilikuwa ni siri yake.
4. Hakuna Sheria ya kufunga katika Injili.
5. Hakusomi katika Taurat au Zaburi au Injili kuwa wakati wa Biblia watu wali kula daku na hakuna aya inayo ruhusu kula daku.
FAIDA YA KUFUNGA:
Katika Biblia, tunaona jinsi ambavyo mambo yalivyobadilika baada ya kufunga na kuomba. Angalia mifano michache hapa chini:-
A. Wana wa Israeli walipigwa mfululizo katika vita na wana wa Benyamini. Baada ya kushindwa mfululizo, wakaamua kufunga na kuomba (WAAMUZI 20:20-22, 24-26). Baada ya kufunga na kuomba matokeo yakabadilika, Benyamini wakapigwa sana, na wana wa Israeli wakashinda vita (WAAMUZI 20:34-35, 41-45, 48). Tunaweza kuitia moto miji yote ya Shetani tukiwa wafungaji, na siyo kinyume cha hapo;
B. Ezra hakumtegemea mfalme, bali alifunga, na matokeo ya kufunga yakawa kwamba mkono wa Mungu ulikuwa pamoja naye na yeye na wenzake wakaokolewa na mkono wa adui (EZRA 8:21-28, 31-33). Ikiwa Kanisa linahitaji kuokolewa kutoka katika mkono wa adui, ni lazima liwe na wafungaji.
Mpendwa msomaji, unaona faida ya kufunga? Usifunge kama wale wanao jionyesha kwa kukunja nyuso zao na kusema Swaumu kali bali funga kwa siri maana anaye fahamu kuwa unafunga ni Mungu na yeye anajua ya moyoni mwako.
Mungu akubariki sana,
Ni mimi Max Shimba, Mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW