Wednesday, February 21, 2018

KUVAA HIRIZI NI DHAMBI?

Image may contain: one or more people


Hirizi ni nini?
kitu cha kuvaa mwilini kama vile karatasi iliyo na maandishi maalumu, kipande cha mti au uganga uliofungwa kwenye nguo, ngozi, n.k. kinachoaminiwa kuwa ni dawa ya kujikinga na madhara.
Mungu anasemaje kuhusu hii ‘sayansi ya kiafrika’?
Naamini umeshasikia mara nyingi watu wakisema, “Jisaidie na Mungu naye atakusaidia.” Siwezi kukataa lakini kama ni Mungu huyu ninayekuambia habari zake hapa, Yeye anasema kinyume kabisa cha hayo. Imeandikwa: Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako. (Mithali 3:5-6).
Sasa watu wengi wanasema kuwa kwenda kwa waganga ni katika jitihada hizo za kujisaidia. Bwana wa majeshi anasema hivi: Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute, ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. (Mambo ya Walawi 19:31)
Na anaonya kwa ukali kabisa kuwa: Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake. (Mambo ya Walawi 20:6). Kuzini inaweza kumaanisha maana hii ya kawaida tunayoifahamu, lakini pia kibiblia, Mungu anaichukulia nchi kama mke. Nchi inapomwasi Bwana (yaani mume wake) na kwenda kwa miungu mingine, basi inakuwa inafanya uzinzi).
Pia Mungu anasema: Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA. (Kumb 18:10-12).

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW